TICTS: The inside story

Muda mfupi uliopita, nimemsikia Spika wa Bunge, Samuel Sitta, akisema,

"Katika Mkutano wa Bunge uliopita, Mheshimiwa Anna Abdalah alisimama na kumuomba NAzir karamagi athibitishe kuhusu TICS kua ilijadiliwa na BAraza la MAwaziri. Yeye aliniletea barua ambazo hazikutosheleza sana. Niliagiza ofisi yangu iwasiliane na Ikulu, Jibu, Mkataba wa TICS ulifuata taratibu zote za kiserikali, ni dhahiri kwamba utaratibu ulihusika… Natoa uamuzi kwamba Karamagi hakusema uongo."

Hii maana yake nini? Maana kuna uamuzi wa Bunge kwamba Mkataba wa TICS wa nyongeza haukufuata taratibu na serikali ifuate utaratibu wa kuufuta. Sasa hii ya sasa ina maana gani?
 
Ina maana kwamba hakuna mtu yeyote atakayechukuliwa hatua za kisheria katika ufisadi wowote unaofanyika katika taifa letu, hakuna hata mmoja anayethubutu kumnyooshea mwenzake kidole na kumwambia hapa ulikosa. Wote ni kitu kile kile wanashirikiana kuimaliza hii nchi.
 
Ina maana kwamba hakuna mtu yeyote atakayechukuliwa hatua za kisheria katika ufisadi wowote unaofanyika katika taifa letu, hakuna hata mmoja anayethubutu kumnyooshea mwenzake kidole na kumwambia hapa ulikosa. Wote ni kitu kile kile wanashirikiana kuimaliza hii nchi.


Mipango ambao ni Rahisi kuufanya ni kujiunga nao tu na unatokeoa huko huko na kuwaumbua,ila ukiwa mbali nao si rahisi kuwasema sababu sasa hivi hakuna msimamo wa mmoja mmjoa wameamua kuwa na collective responsibility,
 
Hiii si hatari jamani? kweli utafika? hapa serikali yetu inatutania, ina maana hata Spika kasalimu amri? sawa .... kumbe haya yote ya ufisadi nayo hayatashughulikiwa,,,,,, hapa iko kazi, EEEEmungu tuasaidie sisi maskini wa taifa hili
 
sitta hakuwa na jinsi ila kumhukumu karamagi kwa kulidanganya bunge....lakini kwa vile hii ni serikali inayoongozwa na mafisadi, basi tu wakapitisha ufisadi wao na kwa kutumia jina la ikulu, wame khiari kusema kuwa taratibu zote makini zilifuatwa.

na iwapo taratibu hizo zilifuatwa, inamaana na extension ya miaka mengine 10 inaendelea au?
 
kwani hamfahamu hata RICHMOND ilifuata sheria zote za serikali? ikiwamo kujadiliwa na kuafikiwa na baraza la waziri! Nadhani kuna haja ya kuwa na kamati ya bunge katika hili, ili kuachana na rongo rongo za taasisi za serikali (km TAKUKURU)!
 
Muda mfupi uliopita, nimemsikia Spika wa Bunge, Samuel Sitta, akisema,

"Katika Mkutano wa Bunge uliopita, Mheshimiwa Anna Abdalah alisimama na kumuomba NAzir karamagi athibitishe kuhusu TICS kua ilijadiliwa na BAraza la MAwaziri. Yeye aliniletea barua ambazo hazikutosheleza sana. Niliagiza ofisi yangu iwasiliane na Ikulu, Jibu, Mkataba wa TICS ulifuata taratibu zote za kiserikali, ni dhahiri kwamba utaratibu ulihusika… Natoa uamuzi kwamba Karamagi hakusema uongo."

Hii maana yake nini? Maana kuna uamuzi wa Bunge kwamba Mkataba wa TICS wa nyongeza haukufuata taratibu na serikali ifuate utaratibu wa kuufuta. Sasa hii ya sasa ina maana gani?

Hapo maana yake ni kwamba huo UFISADI tuliouimba kwa muda mrefu ngoma yenyewe inachezwa hivyo.
 
Muda mfupi uliopita, nimemsikia Spika wa Bunge, Samuel Sitta, akisema,

"Katika Mkutano wa Bunge uliopita, Mheshimiwa Anna Abdalah alisimama na kumuomba NAzir karamagi athibitishe kuhusu TICS kua ilijadiliwa na BAraza la MAwaziri. Yeye aliniletea barua ambazo hazikutosheleza sana. Niliagiza ofisi yangu iwasiliane na Ikulu, Jibu, Mkataba wa TICS ulifuata taratibu zote za kiserikali, ni dhahiri kwamba utaratibu ulihusika… Natoa uamuzi kwamba Karamagi hakusema uongo."

Hii maana yake nini? Maana kuna uamuzi wa Bunge kwamba Mkataba wa TICS wa nyongeza haukufuata taratibu na serikali ifuate utaratibu wa kuufuta. Sasa hii ya sasa ina maana gani?

Ikulu wakati huo chini ya Ndugu Ben ndio ilitoa amri kwa maandishi kuwa mkataba uongezwe na inawezekana ikawa kweli baraza la mwaziri lilipitisha amri toka kwa bwana mkubwa kama 'formalities'.Pia ikulu hiyo leo imeombwa kuthibitisha.Waliopo ikulu leo yawezekana wameangalia kumbukumbu za ikulu na kweli kuna barua ya Rais alitoa agizo.Kwa hiyo jibu likaenda kwa Spika kwamba ni kweli,Kara yuko sahihi.Lakini pia ikumbukwe hivi karibuni kuna nyaraka zimeongezwa au kubadilishwa kwenye kumbukumbu za baadhi ya viongozi kuhusiana na mali walizotangaza wanamiliki.Kwa hiyo hata kuhusu hili lolote lawezekana
 
Maana yake maamuzi yao ya Dodoma katika NEC yao na Wabunge wote walitaka kila mtu asafishwe wajipange kwa vituko tena mwaka 2010
 
Hiii si hatari jamani? kweli utafika? hapa serikali yetu inatutania, ina maana hata Spika kasalimu amri? sawa .... kumbe haya yote ya ufisadi nayo hayatashughulikiwa,,,,,, hapa iko kazi, EEEEmungu tuasaidie sisi maskini wa taifa hili

Mpango kamili ni kuyapiga faini mabenki pamoja na BOT!
Na wanataka kuwasafisha MAFISADI KWA VIGEZO KUWA SYSTEM NI MBOVU!
Na sisi ujumbe wetu ni kuwa SYSTEM PAMOJA NA VIONGOZI NDIYO WABOVU!
N sheria ichukuwe MKONDO WAKE!
Hizo institutions zinasimamiwa na watu na viongozi waliopewa madaraka ili wailinde katiba,uhuru na haki ya mtanzania...Wameshindwa kufanya hivyo na sheria ndiyo haki itakayoamuwa nani ni nani na alifanya nini kwa manufaa ya nani!
 
Kama WORK ETHICS ZILIKUWA VIOLATED TO THIS EXTENT...THEN HAKUNA CHA KUJIUZULU PEKE YAKE...BALI ACCOUNTABILITY MAHAKAMANI!
 
Tusitegemee chochote kipya toka serikali hii ya kifisadi katika kuivunja mikataba iliyopitishwa kifisadi.

Date::7/8/2008
Serikali yajikoroga kuhusu mkataba TICTS

*Ikulu yasema ulipitishwa na Baraza la Mawaziri
*Yadai ulifuata taratibu zote za kiserikali

*Zambi asema Baraza lilikiuka sheria ya manunuzi

*Cheyo adai haamini kauli ya Ikulu

Na Muhibu Said, Dodoma
Mwananchi

WAKATI Spika wa Bunge, Samuel Sitta, akimsafisha Mbunge wa Bukoba Vijijini, Nazir Karamagi (CCM), kuhusu kauli yake kwamba uamuzi wa kuongewa muda wa mkataba kati ya serikali na Kitengo cha Upakiaji na Upakuaji Makontena Bandarini (TICTS) unaopingwa na Bunge, ulitolewa na Baraza la Mawaziri, Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi (CCM), amesema uamuzi huo wa Baraza hilo ulikiuka sheria.

Zambi alisema hayo katika mahojiano maalum na Mwananchi nje ya ukumbi wa Bunge mjini

hapa jana, muda mfupi baada ya Sitta kutamka kwamba, Karamagi hakusema uongo kuhusu kauli yake hiyo kwa vile Ikulu imethibitisha suala hilo.

Karamagi ambaye alijiuzulu Uwaziri wa Nishati na Madini kutokana na kashfa ya Richmond, ni mmiliki wa Kampuni ya Harbours Investment Limited (HIL) inayomiliki asilimia 30 ya hisa katika TICTS, huku Kampuni ya Hutchison Port Holdings (HPH) ya Hong Kong, China, ikimiliki asilimia 70 ya hisa katika TICTS.

Zambi ambaye Aprili 24, mwaka huu, aliwasilisha bungeni hoja binafsi kuhusu utendaji usioridhisha wa TICTS na kutaka mkataba huo usitishwe na Bunge kupitisha azimio kuhusu hoja hiyo, alisema kauli ya Spika juu ya kauli ya Karamagi haimaanishi kwamba Baraza la Mawaziri halifayi makosa.

Alisema kama kweli Baraza hilo liliamua kuhusu mkataba huo, basi lilikiuka Sheria ya Manunuzi Serikalini namba 21 ya mwaka 2004.

''Kauli ya Spika si kwamba, Baraza la Mawaziri halifanyi makosa. Lilikiuka Sheria ya Manunuzi Serikalini,'' alisema Zambi.

Alisema hata Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali katika taarifa yake ya ukaguzi ulioishia Juni 30, mwaka 2007, ilitaja kukiukwa kwa Sheria ya Manunuzi serikalini katika mkataba wa TICTS.

''Hivyo, hoja yangu bado iko valid (ina maana) na maamuzi ya Bunge hayafutwi na kauli ya Spika kwani ni mali ya Bunge,'' alisema Zambi.

Naye Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo, alisema hawezi kulumbana na Spika katika jambo ambalo amekwishalitolea maamuzi, lakini akasema hakuna anayeweza kuyathibitisha majibu hayo ya Ikulu.

Awali, akitoa uamuzi kuhusu ushahidi uliowasilishwa na Karamagi ofisini kwake kuthibitisha kauli hiyo, Spika Sitta alisema baada ya kuwasiliana na Ikulu, iliwasilisha majibu ofisini kwake yanayoeleza kuwa mkataba wa TICTS ulifuata taratibu zote za kiserikali.

''Mheshimiwa Karamagi alileta barua, lakini hazikutosheleza sana, hivyo, nikawasiliana na Ikulu. Majibu yaliyokuja ni kwamba mkataba wa TICTS ulifuata taratibu zote za kiserikali. Kwa hiyo, Mheshimiwa Karamagi hakusema uongo, bali alisema ukweli,'' alisema Spika Sitta.

Karamagi alilazimika kuwasilisha ushahidi huo baada ya kutakiwa na Spika Sitta kufanya hivyo kutokana na kauli kwamba, mkataba huo wa TICTS uliongezwa kwa kufuata sheria na kwamba, uliamuliwa na Baraza la Mawaziri kutokana na ufanisi mzuri wa kitengo hicho. Alitoa kauli hiyo katika Mkutano wa 11 wa Bunge, Aprili 24, mwaka huu.

Baada ya kutoa kauli hiyo, Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Anna Abdallah, aliomba mwongozo wa Spika na kumtaka Karamagi athibitishe kama mkataba huo uliamuliwa na Baraza la Mawaziri kwa vile anavyoelewa yeye (Anna) wakati huo Karamagi hakuwa waziri.

Hata hivyo, Anna Abdallah alipoulizwa na Mwananchi nje ya ukumbi wa Bunge jana, alisema ameridhika na majibu ya Ikulu kwa vile taratibu za kiserikali ni nyingi na kwamba hakukuwa na ulazima majibu yatolewe kama alivyofikiria yeye.

''Mimi nilichohitaji ni ushahidi kama kweli Baraza la Mawaziri liliamua kuhusu mkataba ule. Sasa kama Ikulu imesema mkataba ule ulifuata taratibu zote, full stop (mwisho).Taratibu ziko nyingi, nimeridhika na majibu hayo na siyo lazima iwe kama nilivyofikiria,'' alisema Anna.

Aprili 25, mwaka huu Bunge lilipitisha azimio la kuitaka serikali isitishe mara moja nyongeza ya mkataba wa miaka 15 uliofikiwa kati yake na TICTS kwa maelezo kwamba ulikiuka sheria.

Mkataba huo uliongezwa na serikali Desemba 30, mwaka 2005 na kufikia miaka 25 badala ya miaka 10 ambao ulikuwa unaisha mwaka 2010.

Azimio hilo lilipitishwa na karibu wabunge wote isipokuwa Karamagi, aliyetoa sauti bungeni ya 'siyo' baada ya Spika kuhoji wabunge wanaoafiki na wasioafiki azimio hilo lipite.

Azimio hilo lilipitishwa na Bunge baada ya Zambi kuwasilisha bungeni hoja binafsi kuhusu utendaji usioridhisha wa TICTS.

Katika maelezo kuhusu hoja yake, Zambi alisema mkataba huo uliongezwa kinyume cha sheria kwa kuwa tayari utendaji wa TICTS ulikwishashuka na kushindwa kufikia malengo yaliyoainishwa kwenye mkataba huo.


Pia alisema ripoti ya CAG), ambayo iliweka bayana kuwa mkataba huo ulikuwa batili.


''Mheshimiwa Spika, katika taarifa yake ya ukaguzi wa Hesabu za Mashirika ya Umma kwa mwaka ulioishia 30/06/2007, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG) pia amebaini upungufu mkubwa sana kwa upande wa TICTS. Ametaja pia kukiukwa kwa Sheria ya Manunuzi serikalini, kukiukwa kwa mkataba wenyewe wa TICTS na serikali. Kwa ujumla amesema nyongeza hiyo ya mkataba ni mbaya na haifai. Kwa ujumla ni kwamba

mkataba hauna nguvu kisheria,'' alikaririwa Zambi akisema.

Alisema kwa mfano, nyongeza ya mkataba kwa miaka 15, ilifanywa kupitia barua Na. TYC/R/160/32 ya Septemba, 2005, iliyoandikwa na kutiwa saini na aliyekuwa Waziri wa Fedha wakati huo, Basil Mramba, ambayo pamoja na mambo mengine, ilimtaka Kamishna wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ahakikishe muda wa mkataba unaongezwa kuwa wa miaka 25.

Zambi alisema miongoni mwa mambo ambayo hayakutekelezwa kama mkataba ulivyotaka, ni pamoja na TICTS kuongeza ufanisi, matengenezo ya vifaa na malipo ya mrahaba.

Alisema msongamano wa makontena katika bandari ya Dar es Salaam uliongezeka kwa kiwango kikubwa na hivyo, kufanya baadhi ya meli kuacha kuja nchini.

Alitoa mfano kuwa mwaka jana msongamano uliongezeka na kufikia asilimia 88.7 ikilinganishwa na kiwango cha kimataifa cha asilimia kati ya 50 na 60.

''Mheshimiwa Spika, kimsingi mambo yote hapo juu yanaonyesha upungufu mkubwa uliopo serikalini na hususan katika suala hili. Hivyo, ni wajibu wa Bunge lako tukufu kuisimamia serikali kikamilifu ili isiendelee kuvunja kwa makusudi sheria, kanuni na taratibu mbalimbali ambazo zipo kwa mujibu wa sheria,'' alisema Zambi.

Kutokana na hali hiyo, aliliomba Bunge kupitisha azimio la kusitisha mkataba wa TICTS ili upitiwe upya kwa maslahi ya taifa.
 
Ikulu yamwokoa Karamagi

na Tamali Vullu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

OFISI ya Rais, Ikulu imethibitisha kauli iliyotolewa na Mbunge wa Bukoba Vijijini, Nazir Karamagi (CCM), kwamba uamuzi wa kuongezwa kwa mkataba wa Kampuni ya kupakua makontena katika Bandari ya Dar es Salaam (TICTS) ulifuata taratibu zote za kiserikali.

Tamko hilo la Ikulu ambalo limemuepusha Karamagi katika uwezekano wa kuadhibiwa na Bunge iwapo ingethibitika kwamba alisema uongo, lilisomwa bungeni jana na Spika, Samuel Sitta, baada ya kipindi cha maswali na majibu.

Sitta alikuwa akijibu hoja iliyotolewa bungeni na Mbunge wa Viti Maalum, Anna Abdallah Aprili mwaka huu, ambaye alimtaka Karamagi athibitishe kauli aliyoitoa bungeni wakati huo kwamba, uamuzi wa kuingozea TICTS mkataba mwaka 2005 ambao umezua maneno mengi, ulipata baraka za Baraza la Mawaziri.

Kutokana na ombi hilo la Abdallah, Spika Sitta alimpa Karamagi hadi siku inayofuata awe ameleta uthibitisho wa kauli yake hiyo, uamuzi ambao aliuahirisha na kumpatia muda wa nyongeza wa wiki moja.

Sitta alichukua uamuzi huo wa kuongeza muda wa utetezi, baada ya kueleza bayana kutoridhishwa na maelezo ya utetezi yaliyotolewa bungeni na mbunge huyo, ambaye Februari mwaka huu alilazimika kujiuzulu uwaziri baada ya jina lake kutajwa katika Kashfa ya Richmond.

Spika alisema iwapo Karamagi angeshindwa kuthibitisha kauli yake hiyo, angeliwasilisha suala lake katika Kamati ya Maadili ya Bunge inayoongozwa na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango ambayo ina uwezo wa kikanuni kumuadhibu kwa kulidanganya Bunge.

Karamagi alitoa maelezo hayo juu ya Baraza la Mawaziri bungeni wakati akichangia hoja binafsi ya Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi (CCM).

Kwa mujibu wa maelezo aliyotatoa Karamagi wakati huo, nyongeza hiyo ya mkataba kutoka miaka 10 ya awali na kufikia 25, haikuwa batili na ililenga zaidi kuinufaisha nchi na si watu binafsi kama baadhi ya wabunge na watu wengine wanavyofikiri.

Baada ya kutoa kauli hiyo, Abdallah ambaye mwaka 2002 alikuwa Waziri katika Serikali ya Awamu ya Tatu, alisimama na kutaka mwongozo wa Spika, akihoji Karamagi alizipata wapi habari hizo, kwa sababu wakati mkataba huo unaongezwa hakuwa katika Baraza la Mawaziri.

Katika maelezo yake ya awali kwa Spika ambayo yalikataliwa, Karamagi aliandika barua kuwa hakuweza kupata waraka huo wa Baraza la Mawaziri, kwa kuwa maamuzi ya chombo hicho ni siri na hayapaswi kutolewa labda kwa kunukuu vifungu vilivyomo, na akaliomba Bunge limpe muda mpaka mkutano ujao alete ushahidi.

Karamagi ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Harbours Investment Ltd yenye hisa asilimia 30 katika TICTS na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TICTS, alilazimika kutoa utetezi kutokana na shinikizo la baadhi ya wabunge kutaka mkataba wa TCTS uvunjwe baada ya serikali kukiri kuwapo tatizo katika utendaji wa kitengo hicho.

Katika utetezi wake, Karamagi alisema, alifahamu kuhusu suala hilo wakati wa vikao kati ya TICTS na maofisa wa Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC) ambao ndiyo waliokuwa wakisoma waraka wenye maelekezo hayo kutoka katika Baraza la Mawaziri.

Akichanganua utetezi huo wa maandishi wa Karamagi wakati huo (Aprili), Spika Sitta alisema katika maelekezo yake ya awali hakumtaka mbunge huyo kuwasilisha waraka wa Baraza la Mawaziri kwani, uzoefu wake wa kuwa waziri kwa miaka 14 ulikuwa ukimfanya ajue maana ya usiri wa vikao hivyo.

"Mimi nimeshika nafasi ya uwaziri kwa muda usiopungua miaka 14 na najua taratibu zake na wala sikutaka ulete waraka huo, bali ni ushahidi ambao unapatikana kirahisi kwa katibu pale Ikulu," alisema Sitta muda mfupi baada ya kusoma kumbukumbu za Bunge (hansards) za mjadala wa siku moja iliyopita ambao ndiyo uliofikia uamuzi wa kumtaka Karamagi awasilishe ushahidi.

Kutokana na kutoridhika huko, alimpa wiki moja zaidi mbunge huyo wa Bukoba Vijijini kuwasilisha ushahidi huo la sivyo rungu la kanuni za kulidanganya Bunge lingemkumba.

"Muda unaotaka mpaka wa mkutano ujao ni mrefu sana, mimi nakupa wiki moja mpaka Ijumaa ijayo uwe umeniletea ushahidi huo, la sivyo nitalifikisha suala hili katika Kamati ya Maadili ya Bunge," alisema Sitta.

Awali, wakati akiwasilisha hoja yake, Zambi alitoa barua iliyokuwa imeandikwa na aliyekuwa Waziri wa Fedha wa wakati huo, Basil Mramba, iliyokuwa ikionyesha kuwa, rais ndiye aliyeidhinisha kuongezwa kwa mkataba wa TICTS.

"Kwa mujibu wa barua hii, Mramba anasema Rais (Benjamin Mkapa) ametoa maagizo ya kuongezwa kwa mkataba wa TICTS kwa muda wa miaka 25, hivyo TRA, na vitengo vingine watoe ushirikiano," alikariri Zambi wakati huo katika hoja ambayo iliungwa mkono na serikali.

Nia ya serikali ya kuvunja mkataba huo, ilipata kuelezwa bungeni na aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Miundombinu, Dk. Milton Mahanga aliyeunga mkono hoja ya kutaka kuvunja mkataba na TICTS, iliyotolewa na Zambi, aliyetaka serikali isimamishe nyongeza ya mkataba wa kitengo hicho na kufanya mapitio ya mkataba wa awali ili vifungu visivyo na manufaa kwa taifa virekebishwe. Mkataba huo umeongezwa kwa miaka 20 hadi mwaka 2025.

Dk. Mahanga alisema serikali inachukua hatua dhidi ya kitengo hicho na majadiliano yangeanza mapema kati ya serikali na TICTS kuangalia namna bora ya kusimamisha mkataba.

Alikiri kuwa kuna matatizo na mkataba wa TICTS na kwamba hivi sasa, majadiliano yanaendelea kutafuta namna ya kuusimamisha. Hata hivyo, alisema kwa kuwa ni suala la mkataba ambalo kitengo hicho kina saini ya serikali, ni vigumu kuchukua uamuzi wa haraka. Badala yake, alisema mchakato uliopo ni wa kuangalia athari za baadaye kisheria, za kusimamisha mkataba huo.

Katika hoja hiyo iliyoungwa mkono na wabunge wote waliochangia isipokuwa Karamagi, Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa (CHADEMA), alieleza kushangazwa kwake na barua iliyoambatanishwa katika nyaraka zilizowasilishwa bungeni, ikionyesha kuwa uamuzi wa kuiongezea TICTS muda wa mkataba ulifanywa kutokana na maelekezo ya Ikulu kwenda kwa Waziri wa Fedha.
 
Serikali imekuwa hodari sana kwenye ku-flip flop. Mwanzo tulisikia kuwa fedha za EPA ni mali ya umma na tulioibiwa na wananchi, baadaye serikali hiyo hiyo ikaja kusema fedha za EPA si mali ya umma bali ni za wafanyabiashara fulani. Na baadaye serikali hiyo hiyo ikarudi na kusema tena fedha za EPA ni za umma. Same story kuhusu Richmond, leo inasema hili kesho inasema lile, same story kuhusu, TISCAN leo hili kesho lile. Ni uchwara mtupu, tuna serikali ya jabu sana ambayo hata haijui mali ya wananchi wake ni ipi, leave alone kuilinda.
Soon tunaweza kusikia kuwa serikali ya Tanzania sio ya Tanzania ila inaongozwa na watanzania. Teh the the!
 
Wajameniii!!!

Mtu mzima akikosea sio lazima aseme amekosea... hii tayari hata wao wenyewe wakikaa kwenye vikao vyao watakuwa makini zaidi!
 
Hawa wahuni sana wanafikiri kila mtanzania bado amelala usingizi. Hapa six anajaribu kufisha uchafu wa mkapa na mramba, naona ameamua kuwaunga mkono au ndo ibara ya 15:1
 
Back
Top Bottom