TICTS: The inside story

TICTS contract review out soon

2008-12-08 11:26:19
By Joyce Kisaka

The outcome of the review of the Tanzania International Container Services (TICTS) 25-year port services contract will be officially known this month, The Guardian has learnt.

However, it remains unclear whether the government will revoke the hotly dubious 15-years contract extension that was made before the original 10-year contract was over in 2010.

A government negotiating team comprising representatives of the ministary for Constitutional Affairs, Finance and Economic Affairs and Infrastructure Development has until the end of this month to complete its negotiations with TICTS officials.

The two parties have already agreed that the wharfage fees will now be directly collected by the Tanzania Ports Authority.

This will be a departure from the existing arrangement whereby TICTS collects the wharfage money then remits it to TPA.

The Guardian has been reliably informed that there are three sticking points which are still under hot discussion.

The Minister for Infrastructure Development, Dr Shukuru Kawambwa, in an exclusive interview with The Guardian, said the outcome of the discussions would determine whether the TICTS contract would be revoked or not .

He said the review seemed to be taking too long but the government had deliberately allowed a thorough review that would result into a beneficial contract.

`It is not secret that the contract has shortfalls. A lot of concentration is needed during the negotiations otherwise the government will end up as a loser,` he said.

The minister said that in January next year, the government would announce amendments on the TICTS contract.

Asked if the government would be ready to revoke the contract clause giving TICTS exclusive rights to handle cargo at Dar es Salaam port, the minister would not commit himself, but only said that a decision would be made after the contract review had been completed.

Dar es Salaam port cargo handling services were leased in 2000 by the government to the International Container Terminal Limited (ICTL) of Manila.

The ten year contract was to end in 2010, but government, in a questionable move, extended the contract for another 15 years.

The National Assembly has recommended the termination of the 2005 illegal contract extension.

The House recommendations were prompted by a public furore over a revelation made by the Comptroller and Auditor General that there was gross violation of the Public Procurement Act (PPA) of 2004 in the process of extending the TICTS contract from the initial 10 years to a whopping 25 years.

It has been alleged that the TICTS contract was illegally extended by former president Benjamin Mkapa towards the end of his second and final term in office in 2005.

According to the CAG`s report for the financial year that ended June 30, 2007, the dubious extension of the lease contract for the lucrative container terminal at the port of Dar es Salaam was unlawfully executed.

Prime Minister Mizengo Pinda, during direct discussions with editors on May 12, this year, revealed that the government had owned up to the fact that the TICTS contract was lopsided.

``The Government has already given notice to TICTS for terminating the contract in the year 2010 and the remaining two-year contract period would be pegged to performance,`` Pinda said.

He said the government had come to the conclusion that the 15-year extension of the TICTS contract after 2010 was wrong, and had notified TICTS to that effect.

``The government has rejected the 15-year TICTS contract extension. We have said no. We said we have to go back to the original terms of contract,`` said Pinda.

``The two parties to the contract (TICTS and the government) are now discussing the agreement,`` he added.

SOURCE: Guardian
 
source Mwananchi 4/30/2009
Habel Chidawali
HATIMAYE serikali sasa imeeleza bayana kuwa kampuni ya Ticts inayoendesha kitengo cha kupakua na kupakia makontena kwenye Bandari ya Dar es salaam imeshindwa kazi na sasa inapitia upya mkataba ulioipa kampuni hiyo haki peke.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema pia kuwa miongoni mwa mambo yanayofikiriwa ni kuufuta mkataba huo au kutafuta makampuni mengine na kuingia nayo mkataba wa kufanya kazi hiyo ili yaweke ushindani kwa Ticts na kuboresha huduma ya kitengo hicho kilichokuwa kiingizia Mamlaka ya Bandari (TPA) faida kubwa.

Waziri Pinda alitoa kauli hiyo jana Bungeni wakati akijibu swali la mbuge wa Tabora Mjini, Silaji Kaboyonga ambaye alitaka kujua serikali inafanya nini juu ya Ticts na kwanini isimalize mgogoro uliopo kwa manufaa ya taifa wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo.

Pinda alisema kuwa anakerwa na huduma hiyo ambayo alisema kuwa

ni mbovu na haileti tija kwa Watanzania, ukilinganisha na huduma kama hiyo ambayo inatolewa katika nchi ya Ireland alikotembelea hivi karibuni.

“Unajua laizma tukubaliane kuwa tuliingia katika mkataba mbovu kabisa na watu Ticts ambao wanaonekana kuwa wameshindwa kabisa kutimiza majukumu yao kama tulivyotarajia hivyo mheshimiwa spika nalitaarifu bunge lako tukufu kuwa mkataba huo unapitiwa upya hivi sasa,” alisema Pinda.

Alisema kuwa bandarini kwa sasa hakuna ushindani kabisa ukilinganisha na bandari za nchi ningine ambazo zinakuwa na makumpuni zaidi ya tisa na kutoa mfano wa bandari ya Dublin iliyo nchini Ireland ambako alisema kuna makapuni mengi ambayo yanashindana kutoa huduma hiyo na hivyo kuongeza ufanisi.

Alisema katika kuangalia upya mkataba huo, ikionekana kuwa kuna umuhimu ni lazima kampuni hiyo ipelekwe mahakamani.

“Hapa suala halihitaji kuwa mwanasheria. Unaweza kuona kuwa kilichofanyika si sahihi hawa jamaa wamekiuka kanuni za mkataba hivyo naamini kuwa hata tukiwapeleka mahakamani bado serikali inaweza kushinda bila ya wasiwasi,” alisema Pinda.

Kiongozi huyo wa shughuli serikali bungeni alisema kuwa kama wataalamu wataona kuwa inafaa kuiachia kampuni hiyo iendelee na kazi yake kwa kipindi cha miaka 15 ijayo itakuwa ni vema, lakini akatahadharisha kuwa ni laizma kutakuwa na hasara kubwa mno.

Pamoja na kuupitia mkataba huo, Pinda pia alitaka miundombinu ya bandarini iboreshwe na kuweka mazingira kwa makampuni mengi zaidi ya kufanya kazi hiyo badala ya kutegemea kampuni moja ambayo inaonekana

kushindwa kufanya kazi yake.

Katika taarifa yake, mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Kabwe Zuberi Zitto alipendekeza kuangaliwa upya kwa mkataba huo na Waziri Pinda aliipongeza kamati hiyo kwa ufanisi mzuri katika kazi hiyo.

Ticts (Tanzania International Container Terminal Services), ambayo inamilikiwa kwa asilimia 75 na kampuni ya nje ya ICTS huku asilimia 25 zikimilikiwa na kampuni ya Vertex ya Tanzania, ilianzishwa baada ya ICTS kushinda zabuni ya mkataba wa miaka 10 wa kutoa huduma hiyo kwenye Bandari ya Dar es salaam mwaka 2000.

Ilikuwa ni miezi michache baada ya Ticts kuundwa Aprili mwaka 2000 kabla ya kushinda zabuni hiyo, na miaka mitano baada ya kufanya kazi hiyo, Ticts iliongezwa na kuwa wa miaka 25 kwa madai kuwa maagizo hayo yalitoka Ikulu.

Hata hivyo, Aprili 25 mwaka jana, Bunge lilipitisha uamuzi wa kuitaka serikali isitishe mkataba huo wa nyongeza ya miaka 15 katika mkataba wa awali wa miaka 10, kwa maelezo kuwa kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa Sheria ya Manunuzi ya Umma wakati wa uongezaji wa mkataba huo, jambo lililotafsiriwa kuwa kulikuwa na mazingira ya rushwa.

Pia ilidaiwa kuwa mkataba huo uliongezwa wakati hali ya utendaji wa Ticts ikizidi kuwa mbovu na hivyo kudhihirisha kuwa kulikuwa na mazingira ya rushwa.

Kwa wakati wote huduma katika kitengo hicho cha upakuaji na upakiaji makontena kwenye Bandari ya Dar es salaam zimekuwa zikilalamikiwa sana licha ya hatua kadhaa kuchukuliwa kujaribu kurekebisha hali hiyo.
 
Say what you want about Pinda, when he wants to keep it plain he can do that.Problem is everybody is soo slow to act to the point of making everything said appear to be said for effect only.
 
Mwananchi 4/30/2009
Habel Chidawali

Ilikuwa ni miezi michache baada ya Ticts kuundwa Aprili mwaka 2000 kabla ya kushinda zabuni hiyo, na miaka mitano baada ya kufanya kazi hiyo, Ticts iliongezwa na kuwa wa miaka 25 kwa madai kuwa maagizo hayo yalitoka Ikulu.
Hapo wanataka kusema kwamba ni Mkapa ndio ali order hili dili la Karamagi. Okay, Mkapa ni fisadi anajulikana, lakini hapa kwa kweli ni cabinet nzima ya Mkapa liliidhinisha hili dili:
Karamagi aitosa serikali

2008-07-09 09:21:44
Na Jackson Kalindimya, Dodoma

Uamuzi wa kuongeza muda wa mkataba wa Kampuni ya Tanzania International Container Terminal Services (TICTS) kwa miaka 15 zaidi kufanya kazi ya kupakua mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam, ulifanywa na Baraza la Mawaziri, Bunge limeelezwa.

Spika wa Bunge, Bw. Samuel Sitta, amekiambia kikao cha Bunge kinachoendelea mjini hapa jana, kuwa amepokea ushahidi toka serikalini unaothibitisha kwamba uamuzi wa kuongeza muda wa mkataba wa TICTS ulifuata taratibu za maamuzi ya serikali.

Bw. Sitta aliliambia Bunge kuwa Bw. Nazir Karamagi, aliwasilisha barua yenye kumbukumbu na TYC/A/400/386 ya Oktoba 25, 2005 iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Peniel Lyimo kwenda kwa Ofisa Mtendaji wa TICTS, ambayo pamoja na mambo mengine ilithibitisha kuwa, serikali ilikubali kuongeza muda wa kufanya kazi kwa miaka 15 hadi mwaka 2025.

Alisema pamoja na barua hiyo, Ofisi ya Spika pia ilipokea barua nyingine ya Juni 18, mwaka 2008 kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Bw. Gray Mgonja, yenye kichwa cha habari `Ushahidi wa kuwa Mkataba wa TICTS ulijadiliwa na Baraza la Mawaziri`.

Barua hiyo inanukuliwa kuandikwa ``Naandika kuthibitisha kwamba, uamuzi wa kuongeza muda wa mkataba wa kampuni ya TICTS ulifuata taratibu za maamuzi Serikali``.

Bw. Sitta aliliambia Bunge kuwa, baada ya kutafakari maudhui ya maelezo yaliyomo kwenye barua hizo mbili, ameridhika kwamba ushahidi uliotolewa na Bw. Karamagi umekidhi matakwa na masharti ya Kanuni ya 63(6) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, toleo la 2007 yaliyomtaka kuthibitisha ukweli wa maelezo yake aliyoyatoa Bungeni kwa kiwango cha kuliridhisha Bunge.

Ufafanuzi huo unamnusuru Mbunge wa Bukoba Vijijini (CCM) Bw. Karamagi, kuchukuliwa hatua kwa kuzingatia kanuni kuhusiana na kulidanganya Bunge kufuatia matamshi aliyoyatoa Aprili 25, mwaka huu, wakati akichangia hoja binafsi ya Bw. Geofrey Zambi, kuhusu utendaji usioridhisha wa kampuni ya TICTS ambapo alidai kuwa mkataba wa kampuni hiyo uliokuwa wa miaka 10 uliongezwa muda wake kwa miaka 15 zaidi kabla ya kuisha kwa muda wake na Baraza la Mawaziri.

Kufuatia matamshi hayo, Mbunge Anna Abdallah (CCM- Viti Maalum), aliomba mwongozo wa Spika kwa kuzingatia kanuni ya 68(7) kumtaka Bw. Karamagi taarifa aliyozungumza kama kweli iliamuliwa na Baraza la Mawaziri.

Spika Sitta alimtaka Mbunge Karamagi aseme na kudhihirisha kama ana ushahidi wa Baraza la Mawaziri vingineyo arekebishe taarifa yake.

Bw. Karamagi alikataa kufuta usemi wake na kuliambia Bunge kuwa ana ushahidi wa waraka toka Baraza la Mawaziri alioupata wakati yakifanyika majadiliano na Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC).

Spika Sitta, alimpa muda wa siku moja awasilishe ushahidi huo ambao hadi muda aliopewa ulipofika hakuwa amewasilisha na badala yake, akaongezewa muda wa wiki moja zaidi ili awasilishe ushahidi na hatimaye akafanya hivyo.
 
Kama kampuni hii imeshindwa kazi hatua gani zimechukuliwa kuleta marekebisho. Ningependa kuona matendo zaidi kuliko maneno
 
Sasa kama kuna ushahidi wa kutosha kwamba TICTS imeshindwa kazi kwanini mkataba huo usivunjwe!? Bunge si liliidhisha tangu mwaka jana kwamba mkataba wa TICTS uvunjwe? Au Kikwete anaogopa hisani alizofanyiwa na Karamagi za kumchangia mabulungutu ili achaguliwe kama mgombea wa CCM!?
 
Kuna mkataba gani viongozi waliopo na waliopita ambao waliupitisha wenye tija na faida kwa WANANCHI?

Kuna kiongozi yeyote anayeweza kujibu hilo swali?
 
Karamagibado anadai chake alichochangia ccm wakati wa kampeni ali cover kanda yote ya ziwa.....kwa pesa yake.
 
Time for execution, no more plan..... Tumeshapanga sana, mkataba uliingiwa kifisadi fisadi.
 
source Mwananchi 4/30/2009
Habel Chidawali
HATIMAYE serikali sasa imeeleza bayana kuwa kampuni ya Ticts inayoendesha kitengo cha kupakua na kupakia makontena kwenye Bandari ya Dar es salaam imeshindwa kazi na sasa inapitia upya mkataba ulioipa kampuni hiyo haki peke.

Hapo kwenye reddish nyekundu boldish hapo ndo usanii wenyewe ulipo. Serikali inawezaje kusema inapitia mkataba ambao awali iliuidhinisha? Ina maana waliusaini huku wakiwa wamefumba macho..sasa wameona kila mtu anajua hasara inayopatikana kutokana na ufisadi wao ndo wanaanza sarakasi sasa..lol..
 
Kwa maelezo ambayo JK, PM na wakuu wengine wamekuwa wakiyatoa wanapotembelea bandari ilitosha kutoa muelekeo wa Mkataba mpya kama sio kutafuta njia mbadala za kuongeza ufanisi. Kutokana na hilo nashawishika kuona kuwa mkataba wa TICKS unamizizi mikubwa yenye ugumu tosha wa kuing'oa na hili litakuwa ndani ya ufisadi.
 
He! Mazingaombwe ya TICTS yanataka kuanzishwa tena? Mbona nilishaanza kusahau. Pinda naye, haya mambo si tushayasahau sasa anataka nini tena? Au na yeye anautaka urais?
 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema pia kuwa miongoni mwa mambo yanayofikiriwa ni kuufuta mkataba huo au kutafuta makampuni mengine na kuingia nayo mkataba wa kufanya kazi hiyo ili yaweke ushindani kwa Ticts na kuboresha huduma ya kitengo hicho kilichokuwa kiingizia Mamlaka ya Bandari (TPA) faida kubwa.

Waziri Pinda alitoa kauli hiyo jana Bungeni wakati akijibu swali la mbuge wa Tabora Mjini, Silaji Kaboyonga ambaye alitaka kujua serikali inafanya nini juu ya Ticts na kwanini isimalize mgogoro uliopo kwa manufaa ya taifa wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo.

" mkataba huo unapitiwa upya hivi sasa," alisema Pinda.

"Hapa suala halihitaji kuwa mwanasheria. Unaweza kuona kuwa kilichofanyika si sahihi hawa jamaa wamekiuka kanuni za mkataba hivyo naamini kuwa hata tukiwapeleka mahakamani bado serikali inaweza kushinda bila ya wasiwasi," alisema Pinda.

Kiongozi huyo wa shughuli serikali bungeni alisema kuwa kama wataalamu wataona kuwa inafaa kuiachia kampuni hiyo iendelee na kazi yake kwa kipindi cha miaka 15 ijayo itakuwa ni vema, lakini akatahadharisha kuwa ni laizma kutakuwa na hasara kubwa mno.

Ilikuwa ni miezi michache baada ya Ticts kuundwa Aprili mwaka 2000 kabla ya kushinda zabuni hiyo, na miaka mitano baada ya kufanya kazi hiyo, Ticts iliongezwa na kuwa wa miaka 25 kwa madai kuwa maagizo hayo yalitoka Ikulu.

Hata hivyo, Aprili 25 mwaka jana, Bunge lilipitisha uamuzi wa kuitaka serikali isitishe mkataba huo wa nyongeza ya miaka 15 katika mkataba wa awali wa miaka 10, kwa maelezo kuwa kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa Sheria ya Manunuzi ya Umma wakati wa uongezaji wa mkataba huo, jambo lililotafsiriwa kuwa kulikuwa na mazingira ya rushwa.
Taarifa za kibongo na statement za viongozi nikisoma huwa sizielewi.

Hapa wanasema Bunge lilipitisha uamuzi wa kuitaka serikali isitishe mkataba. Lakini kumbe inaonekana serikali bado ina discretion ya kufanya inavyotaka kutekeleza au kutofata azimio la Bunge. Hata sielewi utaratibu hapa.

Halafu Pinda anavyosema wasipofuta mkataba wataleta washindani wengine zaidi ya hawa, kwa model ya huko Dublin port. Utawekaje makampuni mengine wakati ushatoa contract kwa kampuni ambayo inayolipwa kufanya kazi yote? Haiingii akilini hii, ndio uzembe huu unaotufanya tuwe fukara kila siku.

Halafu Pinda anasema wakiona kuna umuhimu wataenda mahakamani. Mahakamani kufanya nini, kudai chao au kufuta mkataba? Kumbe ni lazima mikataba ifutwe na mahakama sio? Maana mara nyingi utasikia oooh, serikali ifute mikata, serikali ifute mikataba. As if ina nguvu ya kujifutia futia mikataba kirahisi rahisi nje ya mahakama kama inavyoongelewa bungeni na mitaani.

Unasema mtafuta mkataba "kama kuna umuhimu" wakati hapo hapo unasema tukiendelea na mkataba kutakuwa na "hasara kubwa mno." Sasa whichi is which? Mawasiliano ya Kibongo hata siyaelewi.
 
Hakuna lolote, wanadhani wakiibua hayo ya TICS tutsahau kukaba makoromeo ya mafisadi papa!

Huku ni kutaka kuhamisha mjadala, bunge lilisha sema mkataba huo ulikuwa bomu, haufai.. pinda anakuja na bla bla upitiwe upya? wanasheira wakiona uendelee kwa miaka 15 itakuwa hasara? which is which?

Cant he put it short and clear, tunavunja ama tunatangaza zije kampuni shindani and thats it!
 
Koba,
Mombasa kwa sasa sii swari- mawaziri 4 wa M7 wapo leo kutafuta namna bidhaa zao zinaweza kupitia Dar!

Hivi kwa nini bandari za Tanga na Mt zisitumike kupitisha bidhaa zetu- ili kungumguza msongamano Dar?

Kuna urasimu gani?

Kwasababu wenye meno hawajafikia uamuzi wa jinsi ya kuzinajisi bandari hizo!
 
Ukipitia mjadala huu wote na wachangiaji wake tangu 2008 basi utagundua ni kwa kiasi gani nchi yetu TANZANIA ilimuhitaji sana Rais mwenye kariba ya MAGUFULI.
Bahati mbaya awamu zilizopita ziliponzwa sana na mtandao/makundi yaliyowaingiza madarakani pamoja viongozi hao kukosa uthubutu na uzalendo wa dhati katika mioyo yao.

Mungu kasikia kilio chetu, leo tumempata JPM mwenye uthubutu, asiye na chembe ya uoga, mwenye uzalendo ndani ya moyo wake.

RAIS JPM wengi tunakuelewa kwa kazi ngumu unayoifanya, wachache wasiokuelewa leo watakuelewa kesho!!!
 
Back
Top Bottom