Tiba mbadala ya chumvi: Sehemu ya tatu

Tiba mbadala ya chumvi: Sehemu ya tatu

Samahani naomba kuuliza nimeanza kutumia chumvi kwenye maji ili kuoga kuanzia juzi Sasa jana baada ya kuoga nimelala vzur kufika saa tisa nmeshtuka baada ya kusikia sauti za bundi zaidi ya wawili zinashindana kuimba karibu na dirisha langu.
Je niendelee kutumia chumvi .
Naomba ushauri
 
Samahani naomba kuuliza nimeanza kutumia chumvi kwenye maji ili kuoga kuanzia juzi Sasa jana baada ya kuoga nimelala vzur kufika saa tisa nmeshtuka baada ya kusikia sauti za bundi zaidi ya wawili zinashindana kuimba karibu na dirisha langu.
Je niendelee kutumia chumvi .
Naomba ushauri
Endelea usiache tafadhi nakusihi mno
 
Mshana Jr, naomba ujibu hili swali, kama inatibu ni namna gan ya kuitumia kwa mtu anaetaabika kwa tatizo Hilo?
Tiba ni tiba njema kwa kinga lakini pia kwa mtu aliyekwisha athirika na ishu za shirki ina nguvu pia na ni msaada mkubwa sana
 
Mkuu, nimejaribu kutafuta part 1,2 sijaziona,
Kama hutojali nitumie part 1-3, somo kuhusu chumvi, pm yangu ipo wazi
 
Mkuu, nimejaribu kutafuta part 1,2 sijaziona,
Kama hutojali nitumie part 1-3, somo kuhusu chumvi, pm yangu ipo wazi
 
 
Nipende kwanza kujivunia kwa mada ya tiba mbadala ya chumvi ... Sijivunii kwa wingi wa wachangiaji la hasha bali kwa mada husika kuwa msaada mkubwa kwa wengi mno... Tiba ile imewasaidia hasa kwenye
Kutopatwa na mauzauza tena
Kuota ndoto mbaya na za kuogofya
Kupata usingizi mororo
Kukingwa na nguvu hasi za kiroho
Kusafisha nyota zilizofifia
Kutakasa miili iliyokuwa imechafuliwa
Kuboost CD4 za kiroho
Kuleta mvuto
Kuondoa uchovu na kuleta uchangamfu, furaha na amani mioyoni

Baada ya hapo ilifuatia mada ya mrejesho : yatokanayo na tiba mbadala ya chumvi hii ilikuwa maalum kwa ajili ya ufafanuzi namna ya kuitumia chumvi vizuri kwa matokeo bora zaidi... Lakini vilevile kwa wale wenye shuhuda mbalimbali ambao wangependa kushare na wengine....

Hii ni sehemu ya tatu na ya mwisho kuhusiana na hii tiba mbadala ya chumvi... Kwa usahihi zaidi chumvi ya mabonge... Hivyo mwenye swali la ziada, hoja ama maoni bado anakaribishwa kuhusiana na kile nitakachoandika hapa ama kwenye mada zilizotangulia...

Wengi wetu wamekuwa wakidhani kuwa tiba mbadala ya chumvi ina dozi maalum hivyo kutamani kujua kwa hakika wanaweza kutumiaje, kwa kiasi gani na hata kwa muda gani....

Kwenye mada zilizotangulia nilishauri matumizi yawe kati ya wiki moja mpaka mwezi mmoja.... Lakini ningependa kusema hivi... IFANYE CHUMVI SEHEMU YAKO YA KUDUMU...

Kama hujawahi kuitumia chumvi basi kwa mara ya kwanza ni kiwiko kimoja cha mkono kwenye ndoo ya maji ya lita 20... Huhitaji kuikoroga bali utaoga na sabuni maji ya juu kisha yale ya mwisho yenye chumvi ndio utatumia kujisuuzia huku ukiyanenea na kunuia utakayo.

Kama ni nyumbani ama ofisini basi nyunyiza ama mwagia kuzunguka eneo husika.. Na kwa kuogea unaweza kufanya hivyo kwa mwezi mzima bila kukosa.

Baada ya hapo ifanye chumvi sehemu yako ya maisha kama ilivyo simu yako, sabuni yako, lotion yako nknk.. Hakikisha chumvi haikosekani na unapoitumia kuogea si lazima uweke kiwiko kizima la hasha bali hata punje mbili tatu zinatosha kabisa.. Usiache kuwa nayo nyumbani, chumbani, ofisini kwenye gari na hata kwenye mkoba..

Chumvi ya mabonge ni tiba rahisi isiyo na miiko, isiyo na maagano isiyo na masharti, nafuu ya bei na rahisi kuitumia.... Usiipuuze wala kuidharau... Imewafaa wengi na haina uhusiano na ushirikina wala uchawi...

ANGALIZO muhimu: Ukiona kwako haijafanya kazi tarajiwa usiichukulie haifai bali nayo ni tiba kama tiba nyingine.... Inaweza kumsaidia mmoja na mwingine isimsaidie... Japo naamini asilimia 95 inafanya vizuri

View attachment 1186647

Soma

Sehemu ya KWANZA
MREJESHO
Mkuu naomba Link ya Sehemu ya Pili pls. Maana naona sehemu ya kwanza na tatu tu
 
Mkuu naomba Link ya Sehemu ya Pili pls. Maana naona sehemu ya kwanza na tatu tu
 
nina ufugaji wa kuku naona sijui nimepigwa zongo ama nini kuku hawatagi inavyotakiwa yaani, je chumvi itasaidiia???
Hili jambo hata mimi huwa linanisumbua sana, huwa nafuga Kuku, Sungura hadi Njiwa lakini sijawhi kupata faida ya ufugaji zaidi ya hasara. Kuna wakati hadi najiuliza au ndo sina mkono wa ufugaji au kuna Walozi wanafanya mambo yao?
 
Tumia makata ni kiboko ya zongo
Habari Mkuu Mshana Jr . Kwanza natanguliza shukrani [emoji120], Mimi ni mtu ninayesumbuliwa sana na kusisimkwa sana ubavu wangu wa upande wa kushoto hadi kichwani, midomo kucheza, nimeshahangaika sana kwenye swala la tiba bila mafanikio. Mganga anatibu baada ya wiki au siku 4 tatizo linarudi. Nimefatilia kuogea chumvi ya mawe nimeona imerudisha mvuto, kusisimkwa kunaenda kunapungua japo kwa taratibu, inabakia tu kama nimebandikwa kitu kizito kwenye kifua.
Nahisi hii niliyopigwa ni zongo. Nimeona hapo umezungumzia tena kuhusu dawa ya makata. Pengine hiyo inaweza kunitatulia tatizo langu. Samahani, naomba formula jinsi ya kuitumia hii makata na utaratibu wake.
 
Back
Top Bottom