Tiba asili tusizibeze sana, Mdudu aliekuwa ananisumbua kwenye kidole kaacha jeuri ndani ya masaa manne tu

Tiba asili tusizibeze sana, Mdudu aliekuwa ananisumbua kwenye kidole kaacha jeuri ndani ya masaa manne tu

watu kibao

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
466
Reaction score
1,645
Siku ya juzi na janausiku nilisumbuliwa na maumivu makali ya mdudu ndani ya kidole cha pete.

Huyu mdudu anakusubiri umalize mishe zako, vile umetulia au umelala yeye ndio anaanza kazi yake, ni tafrani.

Nimehangaika hospitalini, daktari kaniandikia dawa ila hakuna nafuu

Siku ya leo nikawa napiga story na mdau nikagusia shida niliyonayao akaniambia mbona dawa imetuzunguka.

Kuna miti mingi huwa naiona ina vinyanya kama vya njano, huwa vinaitwa ndura, kumbe ni dawa.

Nikaikata ndura na kuingiza kidole ila maumivu yakazidi hata mara 5 zaidi nahisi kidole kinadunda kama mapigo ya moyo, nikaambiwa nijikaze mdudu anaunguzwa na utomvu wa ndura amepandwa na hasira, hali itaisha baada ya masaa machache, kwa maumivu niliyoyapata sitakuja kushangaa mtu mzima akilia kama mtoto

Ni kweli ndani ya masaa manne maumivu yamepungua sana na mdudu simhisi tena akiwa ndani ya kidole

Update:

Siku inayofuata usaha umejikusanya nimeukamua
 
mimi nilichoma kidole kwenye moto ila sio kwa kugusa moto, nilikuwa nasogeza karibu na moto halafu natoa zaidi ya mara kumi mpaka kidole kiwe na ganzi, na wakati huo kidole nimekinyunyizia petrol

Asubuhi nilikuta uvimbe umepungua sanaaa na maumivu yakiwa yamekata

Hiyo yote ilikuwa ni hasira baada ya kutumia dawa zote zinagoma kuniponyesha, wazo likaja kichwani choma kidole kama ni mdudu atoke, ila sikuona kama ni mdudu niliona ni usaha tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom