Thread ya watu waaminifu kwa wapenzi wao

Thread ya watu waaminifu kwa wapenzi wao

Kwamtoro acha kutunga story zako ,hapa unasema una mke halafu kwingine unampenzi unataka kulipwa na mchumba wake, ACHA.
 
Kwa hiyo sasa, uzi huu una dedicate kwa wote wanaume kwa wanawake mafaithfulness. Kujumuika pamoja hapa kubadilishana mawazo katika safari yetu ya kubaki waaminifu kwa wapenzi wetu tuwapendao katika maisha yetu.

Jamani na mimi nilyeamua kwa dhati wiki tatu zilizopita kuachana kabisa na nyumba ndogo naruhusiwa kuchangia????? Au mtaniona sina cha kujumuika nanyi??????
 
sijui kama ntakuja kuwa mwaminifu. najifikiria sana
 
Kwamtoro acha kutunga story zako ,hapa unasema una mke halafu kwingine unampenzi unataka kulipwa na mchumba wake, ACHA.
Asakuta same ndugu yangu. Kuna mengine ni ya kwangu na mengine navaa uhusika kwa maswahibu yanayo ikuta jamii yangu na marafiki zangu ambao awana uwezo wa kushare na sisi. Naweka bandiko ambalo kwa dhati kabisa nitaona inamanufaa kwa sisi wana MMU.
Kuna ubaya gani kwa sisi kuwa waaminifu? Uoni kwamba nawarudisha ambao awapo kundini.
 
Kwa kipindi hichi, dunia inaishi na watu siyo waaminifu. Kwa asilimia kubwa wanaume kwa wanawake wanakuwa na mipango ya kando. Pamoja na yote naamini kwamba kuna watu kama mimi (sijisifu) ambao wamefanikiwa kuishi kwa uaminifu kwa wapenzi wao. Wameshinda vishawishi na majaribu mbalimbali kutokana na nia yao madhubuti ya kuwa waaminifu.

Binafsi nipo na mke wangu kwa miaka 4 sasa, toka niwe naye sijawai kulala na mwanamke mwingine yeyote mpaka leo. Kipindi mke wangu akiwa just a girlfriend, watu walikuwa wakisema she is cheating on me. Sikujali sababu I have made commitment to stay faithful kwake yeye sababu she special to me. Naamini kuna watu wengi wanaume kwa wanawake both singles & married who’ve stayed faithful to their partners no matter what the world has turned into today.

Kwa hiyo sasa, uzi huu una dedicate kwa wote wanaume kwa wanawake mafaithfulness. Kujumuika pamoja hapa kubadilishana mawazo katika safari yetu ya kubaki waaminifu kwa wapenzi wetu tuwapendao katika maisha yetu.

Karibuni sana

Miaka 4. tu? mapema mno kijidai na kujinadi hivyo kha.Ngoja long run ije mkeo kawa mnene kama kiboko,kakuzoea anakujibu kama nyau wake,azeeke kwa speed arafu we bado unadai,umfumanie hayo machache tu na mengineyo wenzangu watanisaidia
NB;SI KILA ANAECHEAT CHANZO NI YEYE KUNA VILAZIMISHI VINGI MNO KAKA NA UTAVIONA AS DAYS GO ON.
 
Its not Cheating so long as you are not Caught
 
Inatia moyo hii thread, kwa maana niekua muaminifu kwa mpenz wangu,tena ukizingatia tunaish mikoa tofauti...lakini katu sijawah vunja uaminifu
 
Asakuta same ndugu yangu. Kuna mengine ni ya kwangu na mengine navaa uhusika kwa maswahibu yanayo ikuta jamii yangu na marafiki zangu ambao awana uwezo wa kushare na sisi. Naweka bandiko ambalo kwa dhati kabisa nitaona inamanufaa kwa sisi wana MMU.
Kuna ubaya gani kwa sisi kuwa waaminifu? Uoni kwamba nawarudisha ambao awapo kundini.

nimekuelewa , hakuna ubaya......ila ili kuonyesha uhalisia kwa hadhira uwe unaelezea uhusika halisi ndugu na kutanabaisha kuwa hiyo ni kwa niaba ya mtu mwingine mkuu!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom