Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Akizungumzia suala hilo leo April 11, 2025 Mratibu THRDC Kitaifa, Wakili Onesmo Olengurumwa amesema kwamba mazingira na utaratibu uliotumika kumkamata Tundu Lissu haukuzingatia usalama wake, usalama wa raia waliokuwa kwenye Mkutano pamoja na usalama wa Polisi.
Olengurumwa amesema nguvu iliyotumika ni kubwa na yenye kuleta hofu kubwa kwa Wananchi kushiriki michakato ya uchaguzi. Ameeleza kuwa Jeshi la Polisi kama walijua kuna tuhuma dhidi ya Lissu wangemwita kwa wito au kumchukua kwa utaratibu rafiki wa kisheria nje ya eneo la Mkutano halali.
Aidha Mtandao umesema kuwa, hata maneno anayotuhumiwa kuyatamka hayana uzito mkubwa wa kufikia kuandikiwa kosa la uhaini.
"Uhaini ni kosa kubwa hapa nchini lisilokuwa dhamana na lenye adhabu ya kifo au maisha. Ni kosa ambalo kwa miaka mingi sasa hapa nchini halijawahi kutumika pengine kutokana na uzito wake."amesema Olengurumwa
Amesisitiza kwamba katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi ni dhahiri kuwa lazima kutakuwa na kauli mbalimbali kutoka kwa wanasiasa na wananchi, ambazo zinaweza zisiwapendezeshe makundi mengine au Serikali.
Amehasa kuwa katika mazingira hayo inahitaji watu kuwa na uvumilivu wa hali ya juu ili kuepuka kuvunja amani ya Nchi.