THRDC: Licha ya kuongezeka kwa Uhuru wa Kujieleza Nchini, bado Serikali haijabadili baadhi ya Sheria kandamizi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,815
11,992
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini (THRDC) umesema hali ya Uhuru wa Kujieleza nchini imebadilika na kuongezeka kwa Uhuru tofauti na miaka 6 ya utalawa wa Hayati Rais Magufuli. Lakini pamoja kuwepo kwa Uhuru huo bado Serikali haijazifanyia marekebisho Sheria zinazokinzana na Uhuru wa Kujieleza, Kupata na Kutoa Habari, zikiwemo Sheria ya Vyombo vya Habari, Sheria ya Mitandao na Sheria za Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA).

Akizungumza kutoka kwenye Mkutano wa Mashauriano na Uthibitishaji kuhusu Ukuzaji wa Mkakati wa Utetezi wa Uhuru wa Kujieleza (FOE), Wakili, Paul Kisabo ambaye ni Protection Officer wa THRDC amesema kuendelea kuwepo kwa Sheria hizo bado kunatafsiri Uhuru uliominywa na kuendeshwa kwa utashi wa Mamlaka.

Kati ya maeneo yanayopigiwa kelele katika Sheria hizo ni pamoja na kifungu cha 7(2b) kinachosema Mpokeaji wa Ujumbe anaweza kushtakiwa kwa kosa la kupokea ujumbe ambao sheria imeufanya kuwa jinai. “Mfano mtu akikutumia ujumbe aliotumiwa na wewe ukaupokea na wewe uliyeupokea utakuwa umefanya kosa la jinai”alisema Soko.

Maeneo mengine ni kifungu cha 21(1), ambacho ameeleza kinamuweka katika mazingira ambayo si salama mtumiaji wa vituo vya mtandao kutokana na kifungu hiki kumtaka mtoa huduma za mtandao kutoa habari zake pale serikali itakapozihitaji.

Aidha, kifungu cha 8 kinaongeza mbinyo wa uhuru wa habari kutokana na kumtaka mtumiaji wa taarifa kutotoa taarifa zenye tafsiri ya usiri kwa umma hata kama ni nyaraka za kusaidia nchi kwa ujumla, sheria inawabinya wananchi kutoa taarifa zenye maslahi kwa umma. “Kifungu hiki kinazuia mtu kutoa taarifa hata kama ni za matumizi mabaya ya mali za umma ikiwa serikali itasema hizo ni taarifa za siri,”

Rejea adhabu ya ibara mbalimbali, sheria hii kila kosa linaweza fanya mtu afungwe kifungo hadi maisha na kulipa pesa hadi zisizohesabika kwani hakijaweka kikomo cha juu cha adhabu bali kikomo cha chini tu kwa kiingereza not less than”

Tafsiri ya taarifa ya ukweli na uhakiki wa taarifa ya mtandaoni

Kuhusu ukweli wa taarifa, kifungu cha 22 kinazidisha mbinyo kutokana na kuainisha kuwa ukiweka ujumbe katika mitandao ya kijamii na ukaufuta au kuuboresha kama ujumbe ukikutwa na kosa, mashataka yataongezewa kosa lingine la kuuboresha ujumbe ama kuufuta.

Kwenye upande wa utekelezwaji wa sheria ya Mitandao, imeonekana kuzidisha hofu kwa watumiaji wa mitandao kutokana na uwepo wa vifungu vya 31 mpaka 35 na 39 mpaka 45 ambavyo vinaelekeza kuwa mmiliki wa mtandao wa kijamii u mtoa huduma, pale anapobaini kosa na akalitoa na akawa kwenye mkakati wa kuitaarifu mamlaka husika, askari nae anaweza kwa wakai huo huo akaamuru kumkagua na hata kuchukua vifaa vya mwandishi wa mtandaoni ama mmiliki wa kituo cha utoaji wa habari ili kufanya ukaguzi bila amri ya Mahakama.
 
Back
Top Bottom