Ki scenario kwa kuwa Mheshimiwa Mbowe Freeman alikuwa ziarani katika mikoa hiyo, maelezo yako yanaonekana kuwa ya kweli kwa asilimia kubwa ingawa kwa kweli yanahitaji ushahidi usio wa mashaka lakini pia yanakosa mantiki ya kisiasa ndani yake na kubwa zaidi yanaibua tatizo la collectivity katika uongozi wa CDM.
Kama kweli Mzee Thomas Nyimbo alikuwa mlezi wa Chama katika mikoa ya kusini na nyanda za juu inawezekanaje Mwenyekiti wa Chama taifa apite katika eneo lake bila yeye kushirikishwa wala kupewa taarifa? Hoja ya Dkt. Slaa kwamba ratiba ilikuwa imebanana ni sawa lakini Je Mzee Nyimbo asingeweza kushiriki hata katika baadhi ya mikutano? Hili ni tatizo kubwa.
Ieleweke kwamba appreciation ni moja ya sifa ya kiongozi. Sasa kama viongozi wa CDM wanaona appreciation ni kumkweza Mzee Nyimbo hili ni tatizo lingine pia. Kuwa na viongozi wa chini katika chama maana yake ni kuwatambua na kuwapa hadhi stahiki. Ni lazima kuwa motivate na kuwapa courage ya kupambana zaidi. Hauhitaji kuwapa fedha lakini kupitia kuwashirikisha na kutambua uwepo wao wanarizika.
Watu wamekuwa wakipiga kelele juu ya haja ya viongozi wa CDM kuanza ku rehearsal na kubehave kama viongozi wenye uwezo wa kuongoza dola lakini halionekani kufanyiwa kazi. Hivi Mbowe angekuwa Rais kwa mfano angeweza kufunga ziara katika mikoa hiyo bila kuwataarifu viongozi wa maeneo husika hasa mlezi wa kanda mbili za utawala?
Lakini pia kuna hili. Kama huoneshi appreciation kwa viongozi wa chini kama walezi wa vyama utawezaje kujenga mtandao wa chama kuanzia chini? Sisemi ni tabia ya uongozi wa CDM kutokutambua viongozi wa chini lakini kumekuwa na malalamiko ya wapenda mageuzi wengi kwamba CDM bila uongozi wa juu ni sawa na haipo hivyo ijikite katika kujenga mtandao na makada wengi iwezekanavyo huko mikoani.
Let us be realistic na fair kwa Mzee Nyimbo. Amekuwa akitumia fedha zake nyingi kufungua matawi ya chama na hata kugharamia mikutano mingi tu labda viongozi wa CDM wanaweza kuja kukanusha hili lakini ni wazi tumekuwa tukipata taarifa zake kupitia humu jamvini. Anaweza kuwa na matatizo yake lakini si katika kujitoa.
Kunaweza kuwa na makapi kweli yanayotoka CCM kuingia CDM lakini Nyimbo anaonekana si wa aina hiyo labda kama tutashawishiwa vinginevyo. Leo Kamanda Mawazo na James Millya kwa mfano kila mtu anawasifia kwa utendaji wao lakini kesho wakichoka na mwenendo wa masuala fulanifulani wakaachia ngazi tutawatukana na kuwapaka hivihivi.
Ingawa Mzee Nyimbo alipaswa kuwa mvumilivu na msikivu (kama kweli alielezwa na Dkt. Slaa juu ya kilichotokea) maana ni sifa nyingine ya kiongozi lakini katika hili uongozi wa CDM umeteleza. Haukumtendea haki.
WOWOWO. Heshima kwa ko kwa observation yenye muono wa mizani inayojitosheleza.
Kulewa madaraka si katika maneno tu bali hata vitenda. Viongozi wa CDM wameshaanza kulewa hata kabla madaraka makubwa hayajawapata.
Nina mfano mzuri wa kujinyenyekeza kwa viongozi , kwa waliochini yao.
Miaka ya mwishoni mwa ' 60 , baba yangu aliyekuwa afisa wa jeshi tulienda naye mess ya NS Mgulani(National Service), baada ya kutoka kwenye halaiki ya kitaifa Uwanja wa Taifa.
Ndani ya mess tulikuwa na mana yangu mzazi aliyekuwa akimnyonyesha mdogo wagu wa mwaka mmoja.
Ghafla walinzi waliingia ndani ya mess na kututaka tuondoke, wakati tunafikiri kinachoendelea akaingia Mwalimu Nyerere akiwa na tabasamu kubwa usoni.
Aliniuliza kama nilikuwo pale uwanjani nami nikamjibu kuwa nilikuwepo kwenye halaiki ile.
Halafu akamsalimia mama yangu SHIKAMOO MAMA!!!
Baada ya hapo akaendele na shughuli zake na kutokomea na walinzi wake wengi.
Tukio zima lilinipumbaza kwa muda. Nilikuwa nimeongea na R ais!!
Sikuelewa mantiki ya somo lenyewe mpaka nilipoingia sekondari na kufikiria kwa makini tukio lile.
Nikaja kugundua kuwa Mwalimu alikuwa na umri mkubwa kuliko mama yangu kwa wakati ule, lakini alimuamkia shikamoo mama!
Hii ni hekima ya hali ya juu, kwa kiongozi wa kitaifa kujishusha na kujinyenyekeza mbele ya watu wake,na wala hakujipunguzia wadhifa wake.
Leo viongozi wengi wanaenda kwa kujikweza sana na hivyo kutoona kuwa wanawakwaza hata wananchi wao.
Kwa Mbowe kukimbilia kufung u matawi Mbeya na kumwacha Mzee Nyimbo, kwanza its a snub, dharau.
Mtu akidharaulika mbele ya kadamnasi kwa kiongozi wake kukosa unyenyekevu, options kwa watu kama Nyimbo ni chache, hatakiwi CDM.