Thomas Nyimbo, ajitoa CHADEMA! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Thomas Nyimbo, ajitoa CHADEMA!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bhavick, Oct 27, 2012.

 1. B

  Bhavick JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimepigiwa simu na mkazi mmoja wa njombe,kuwa aliyekuwa mgombea wao wa ubunge mwaka 2010,amejitoa ndani ya Cdm!kama kuna mtu mwenye taarifa zaidi naomba atujuze!

  UPDATE:

  SUNDAY, OCTOBER 28, 2012

  MLEZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya, Thomas Nyimbo, ametangaza kujivua uanachama wa chama hicho kwa madai ya kuchoshwa na siasa za ‘Umangimeza’ ndani ya vyama vya siasa hapa nchini.  [TABLE="align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="align: center"]MLEZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya, Thomas Nyimbo, ametangaza kujivua uanachama wa chama hicho kwa madai ya kuchoshwa na siasa za ‘Umangimeza’ ndani ya vyama vya siasa hapa nchini.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="align: center"]-Awaasa vijana kuwa mabadiliko ndani ya Tanzania si kuiondoa CCM na kuiweka Chadema.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="align: center"]Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa mbeya na iringa wakimsikiliza mlezi Thomasi Nyimbo katika ukumbi wa hotel yake ya Maunt livingstone jijini mbeya[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="align: center"]Raymond wa Ebony FM Iringa na Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu wakiwa makini kumsikiliza mzee Nyimbo[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [TABLE]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]MLEZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya, Thomas Nyimbo, ametangaza kujivua uanachama wa chama hicho kwa madai ya kuchoshwa na siasa za ‘Umangimeza’ ndani ya vyama vya siasa hapa nchini.


  Nyimbo ambaye amewahi kuwa mbunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa miaka 10 katika Jimbo la Njombe Magharibi kabla ya kukimbilia Chadema mwaka 2010, amesema hivi sasa atabaki kuwa mwanasiasa huru asiyefungamana na vyama.

  Akitoa taarifa ya kuachana na siasa ndani ya vyama jana, Jijini hapa, huku akiwa ameambatana na mkewe Mary Mwenga, alisema amechukua uamuzi huo baada ya kuona siasa za kushabikia vyama hazina tija kwa watanzania walio wengi na badala yake zinawanufaisha viongozi wachahe wanaojineemesha wao wenyewe kwa kutumia jasho la wananchi.

  Akifafanua zaidi alisema alichojiuzulu ni siasa za vyama, lakini sio siasa, huku akitamba kuwa yeye alizaliwa akiwa ni mwanasiasa, kiongozi na mtu ambaye mawazo yake yanahitajika kwa ajili ya maendeleo ya nchi yake, hivyo atabaki kuwa mwanasiasa asiyekuwa na chama cha siasa.

  Katika taarifa hiyo aliyoitoa kwa vyombo vya habari mithiri ya Mhadhara, Nyimbo alitumia zaidi ya saa moja na nusu kuelezea mustakabali wa taifa na vijana kutokana na vyama vya siasa kuelekea kuwatumbukiza kwenye machafuko.

  “Nimeachana na Chadema baada ya kubaini kuwa siasa za vyama havina tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla na ni wakati huu sasa wa kuachana na dhana ya vyama vya siasa vituandalie sera na tunahitaji sasa itungwe sera ya kitaifa ambayo mgombe inabidi atueleze tukimchagua ataitekeleza vipi” alisema Nyimbo.

  Alisema hata nchi zenye wigo mpana wa Demokrasia kama Marekani ambao hivi sasa wapo kwenye mchakato wa uchaguzi Mkuu huwezi kuwasikia wagombea wake wakisifia vyama vyao, bali wanawaeleza wananchi wa Marekani watatekeleza vipi sera ya nchi yao .

  Alisema kuwa ikiwa katiba mpya inayoandaliwa hivi sasa itakuruhusu mgombea huru, atakuwa tayari kugombea ubunge tena kwenye jimbo lake la Njombe Magharibi, lakini kama katiba hiyo itazuia fursa hiyo hatogomea tena wadhifa huo maisha yake yote.

  Aliongeza kuwa baada ya kupatikana kwa katiba mpya, inabidi itungwe sera ya Taifa itakayolindwa kisheria, ambayo kila chama kitakachofanikiwa kuingia madarakani kilazimike kuifuata badala ya ilivyo sasa vyama vinaogelea hovyo.

  Alisema kuwa ndoto za kuwa mwanasiasa huru alikuwa nazo tangu zamani, na ndiyo sababu katika mabango yake ya kuhamasisha achaguliwe wakati akigombea ubunge kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, alikuwa na kauli mbiu ya ‘Mtu kwanza, chama baadaye.

  Alisema kuwa ikiwa katiba mpya inayoandaliwa hivi sasa itakuruhusu mgombea huru, atakuwa tayari kugombea ubunge tena kwenye jimbo lake la Njombe Magharibi, lakini kama katiba hiyo itazuia fursa hiyo hatogomea tena wadhifa huo maisha yake yote.

  “Nitapenda kushauriana na watanzania wanaopenda maendeleo ya taifa letu nje ya mlolongo wa vyama, hivyo hata kama naipenda vipi Chadema, nalazimika kuresighn (kujiuzulu) uanachama ili niweze kutimiza azma hiyo,” alisema Nyimbo.

  Kilichomkimbiza Chadema.

  Alisema ameamua kujiondoa ndani ya chama hicho baada ya kubaini kuwa kinaenda kinyume na malengo yake kama kinavyojipambanua mbele za watu.


  Alisema licha ya kuwaaminisha wananchi, hususani vijana kuwa ndio chama chenye kuleta mabadiliko ya kweli,lakini viongozi wake wa daraja la juu akiwataja Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dk. Wilbroad Slaa wamekuwa wakijinufaisha binafsi.


  Alisema viongozi hao pia wamekuwa si watu wa kushaurika ndani ya chama hicho, lakini kibaya zaidi ni kuendesha siasa katika mfumo mbaya wa kushawishi na kuaminisha bila kuwa na suluhisho (Mob Politics).


  Alisema siasa za namna hiyo ni hatari kwa taifa kwa kuwa baada ya kuungwa mkono kwa kiwango cha juu na kundi la vijana kwa imani ya kukombolewa pale watakapofanikiwa kuingia madarakani na kushindwa kuwatimizia kutazua vurugu.

  Kuhusu CCM.

  Nyimbo alidai kuwa chama hicho kinajimaliza chenyewe kutokana na kuacha suala la rushwa kwenye chaguzi zake za ndani kuwa ndio kigezo muhimu cha kuwapata viongozi wake.

  Hata hivyo alisema ili tatizo hilo limalizike ni wananchi wenyewe kuamua kuikataa rushwa kwa kupokea rushwa isiyoleta matunda kwani wakifanya hivyo watakuwa wamemaliza tatizo hilo .

  “Mfano wewe ukipokea rushwa na kuamua kufanya tofauti na aliyekuhonga kwa kuwa baadaye atakuwa hajapata kile alichotaka kukinunua toka kwako, unafikiri kesho atarudia”.

  Vijana.

  Amewataka vijana nchini kupigania maslahi yao kwa mtazamo hasi wenye kuleta mstakabali mzuri wa Taifa, badala ya kufikiri kuwa mabadiliko ni kuiondoa CCM madarakani na kuiweka Chadema.

  Alisema kuna mambo mengi ya msingi ambayo kama vinana wanapaswa kuwahoji viongozi waliowachagua kama wameyatekeleeza , ikiwemo kupigania katiba mpya kuwa na sera ya inayoweza kuruhusu mgombea binafsi kwa kuwa huko wanaweza kupata viongozi bora.

  Kujiengua kwa Nyimbo linaweza kuwa ni pigo kubwa kwa Chadema, kwani baada ya kujiunga na chama hicho mwaka 2010, alikuwa ni mlezi wa Chadema kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, huku pia akiwa ni miongoni mwa wanasiasa wenye mvuto na wahamasishaji wazuri wa Chadema katika mkoa mpya wa Njombe.

  Habari kwa hisani ya Moses Ng’wat,Mbeya. picha na Mbeya yetu
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mkuu kwa kuwa wewe ndiyo mtoa habari kwa nini utupe habari nusunusu?kama ni kweli amejitoa atakuwa anasumbuliwa na njaa,huyu ni mchumia tumbo!
   
 3. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  I doubt it!
   
 4. commited

  commited JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  ngoja waje wathibitishe kama kuna ukweli au ni urojo.
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hili jimbo linawakilishwa na Anna Makinda?
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Huyu ni mtaka vyeo. Amepiga darubini akaona kuwa hata ramani za 2015 hazisomi, akaamua kukubali yaishe.
  Kwa umri wake hawezi kuiweza kasi ya vijana.

  Amefanya uamuzi mzuri mapemaa kabla ya aibu za ukubwani.
   
 7. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,744
  Likes Received: 12,822
  Trophy Points: 280
  Kwani lazima kuandika habari?
  Yan habari ulete mwenyewe alaf uanze kutuuliza!
  Hii inaonesha jinsi usivyo makini.
   
 8. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Kakosa cheo huyo.
   
 9. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Sosi??
   
 10. ipogolo

  ipogolo JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2012
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 4,062
  Likes Received: 2,941
  Trophy Points: 280
  jimbo la jah pipo
   
 11. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ni vyema arudi alikotoka maana CDM siyo chama cha kugawana madaraka!
   
 12. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hizi ni tetesi za kijinga unawezaje kuleta habari ya ajabu hii bila utafiti hata ule mdogo tu kabla hujaleta habari hii hapa
   
 13. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Ameona chadema ni chama cha fujo.kusini hawapendi kabisa fujo
   
 14. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  yea,ndio mana ukitangaza nia ya kugombea urais kama hutoki kaskazini lazima uonekane msaliti
   
 15. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Juzi juzi walikua wanamsifia humu sasa ngoja tukae mkao wa kusoma matusi atakayopokea toka kwa wanazi wa chadema humu
   
 16. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  tumia akili japo kidogo,amekwambia amepigiwa simu,unataka sosi ya nini tena au kwa kuwa gwanda limeraruka unaanza kuweweseka
   
 17. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280

  Join Date : 3rd October 2011
  Posts : 3,029
  Rep Power : 0

  Likes Received
  130
  Likes Given5


  Mmmm:clap2:
   
 18. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #18
  Oct 27, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  mkuu mbona nilichosema akiendani na ulichoandika?kwa ni wewe unatoka kanda ipi?wasalimie milembe!
   
 19. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #19
  Oct 27, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,347
  Trophy Points: 280
  Biashara zake zimeathiriwa sana kwa kujiunga na CDM.
   
 20. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  mkuu mwendo mdundo,jf ina kila aina ya watu,usipoteze muda wako kushangaa watu!
   
Loading...