Thomas Nyimbo, ajitoa CHADEMA!

Wasomaji,

Kuna wakati mambo yanapotokea yanatupa wakati mzuri wa kujifunza. Napata kujifunza kuwa Mzee wangu nyimbo hana msimamo na wala kusema kuwa yeye amezaliwa kuwa kiongozi silioni hilo kwake. Ningefurahi sana kusikia jitihada zake alizo zifanya kuona kama kweli kuna matatizo ndani ya CDM kayatatua, mtu anayependa kuwepo sehemu kwa kuwa tu mambo yanakwenda vizuri sidhani kama anapaswa kuwa kiongozi wetu, ningetarajia kuwa atuonyeshe njia na hasa tukitambua kuwa amekuwepo kwenye siasa kwa muda mrefu sasa, uzoefu wake ulipaswa kuonekana katika kuleta madaliko. Sasa mtiu mzima ambaye amakuwepo kwenye mfumo kwa muda mrefu kubakia kulalamika tu haisaidii.

Ningetamani sana kwenye hii mitandao ya kijamii tuyachambue mambo kuelimishana kulikoni tukawa tunashabikia tu haitatufikisha mbali.
 
Tena bora ameondoka, watu walioingia chadema kutaka vyeo na wajifanye kutetemekewa utawajua tu. . .ali-loose interest alivyoona watu wanampuuzia.Sisi tunaongozwa na nguvu ya umma bhana.
Kwaheri kunguru nyimbo. . .njiwa tumebaki bandani.
 
Tatizo si M4C wala CDM wala Wabunge wake kutembea Nchi Nzima Kuhamasisha Maendeleo na Mabadiliko Ambayo CCM imeshindwa kuwaletea Watanzania kwa miaka mingi ,Ona Ufisadi Ulio Kidhiri,Rushwa ya Kutisha,Umaskini wa Kutupa NA Zaidi Njaa, Jamani hivi ndo Vitu Vinavyo Hamasisha Uvunjifu wa Amani Tanzania Kwani Njaa na Amani wapi na wapi Ninawachukia CCM toka ROHONI.
 
Jiweke sawa usije ukapatwa na ugonjwa wa moyo utakaposikia Dr. Silaa kajitoa CDM. Sijui utamfuata atakakokwenda Au vipi ila najua utaanza na maneno hayo hayo I doubt it!

Siwezi kupatwa na ugonjwa wa moyo kwa mtu yeyote kujitoa CHADEMA, maana CHADEMA is bigger than any person!
 
Views 3077 Replies 172

Walioiona hii thread Ni 3077 lakini waliojibu Ni 172! Kuna Jambo hapa nadhani CDM wengi wamezimia wako Kwenye ambulance wanakimbizwa Hospitali. Mwingine Karibu Maneno Mawili tu. "I doubt" naye kaishia. Mtaishia wengi siku mtakayosikia dr. Bunduki naye kaanza.

Kumbe wewe unatafuta attention tu?
-Huyu aondoke tu kwani wasaliti hawakosi sababu na katika safari hii ni lazima wawepo na wengine watakuja
-By the way anaogopa kasi ya vijana,political liability.Mbona kuna wazee ambao ni tishio na wanaenda sambamba na kasi ya vijana kama akina Victor Kimesera,Marando,prof.Baregu? Wazee hawa ni asset
 
kesho najiunga mimi kwa upelelezi maalum, lazima CDM ife kwa Njama zake za kutuibia,bora CCM wanang'ata na kupuliza..kwa barabara zinajengwa,huduma mbalimbali zinaboreshwa
 
Tunamtakia mafanikio.hayo ni maamuzi yake.asijichanganye akawanenea watu uwongo huwa unagharimu.
 
Nimepigiwa simu na mkazi mmoja wa njombe,kuwa aliyekuwa mgombea wao wa ubunge mwaka 2010,amejitoa ndani ya Cdm!kama kuna mtu mwenye taarifa zaidi naomba atujuze!

UPDATE:

SUNDAY, OCTOBER 28, 2012

MLEZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya, Thomas Nyimbo, ametangaza kujivua uanachama wa chama hicho kwa madai ya kuchoshwa na siasa za ‘Umangimeza’ ndani ya vyama vya siasa hapa nchini.



DSC00710.JPG

MLEZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya, Thomas Nyimbo, ametangaza kujivua uanachama wa chama hicho kwa madai ya kuchoshwa na siasa za ‘Umangimeza’ ndani ya vyama vya siasa hapa nchini.

DSC00804.JPG

-Awaasa vijana kuwa mabadiliko ndani ya Tanzania si kuiondoa CCM na kuiweka Chadema.

DSC00711.JPG

Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa mbeya na iringa wakimsikiliza mlezi Thomasi Nyimbo katika ukumbi wa hotel yake ya Maunt livingstone jijini mbeya

DSC00795.JPG

Raymond wa Ebony FM Iringa na Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu wakiwa makini kumsikiliza mzee Nyimbo

DSC00705.JPG


DSC00707.JPG

DSC00704.JPG

MLEZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya, Thomas Nyimbo, ametangaza kujivua uanachama wa chama hicho kwa madai ya kuchoshwa na siasa za ‘Umangimeza’ ndani ya vyama vya siasa hapa nchini.


Nyimbo ambaye amewahi kuwa mbunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa miaka 10 katika Jimbo la Njombe Magharibi kabla ya kukimbilia Chadema mwaka 2010, amesema hivi sasa atabaki kuwa mwanasiasa huru asiyefungamana na vyama.

Akitoa taarifa ya kuachana na siasa ndani ya vyama jana, Jijini hapa, huku akiwa ameambatana na mkewe Mary Mwenga, alisema amechukua uamuzi huo baada ya kuona siasa za kushabikia vyama hazina tija kwa watanzania walio wengi na badala yake zinawanufaisha viongozi wachahe wanaojineemesha wao wenyewe kwa kutumia jasho la wananchi.

Akifafanua zaidi alisema alichojiuzulu ni siasa za vyama, lakini sio siasa, huku akitamba kuwa yeye alizaliwa akiwa ni mwanasiasa, kiongozi na mtu ambaye mawazo yake yanahitajika kwa ajili ya maendeleo ya nchi yake, hivyo atabaki kuwa mwanasiasa asiyekuwa na chama cha siasa.

Katika taarifa hiyo aliyoitoa kwa vyombo vya habari mithiri ya Mhadhara, Nyimbo alitumia zaidi ya saa moja na nusu kuelezea mustakabali wa taifa na vijana kutokana na vyama vya siasa kuelekea kuwatumbukiza kwenye machafuko.

“Nimeachana na Chadema baada ya kubaini kuwa siasa za vyama havina tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla na ni wakati huu sasa wa kuachana na dhana ya vyama vya siasa vituandalie sera na tunahitaji sasa itungwe sera ya kitaifa ambayo mgombe inabidi atueleze tukimchagua ataitekeleza vipi” alisema Nyimbo.

Alisema hata nchi zenye wigo mpana wa Demokrasia kama Marekani ambao hivi sasa wapo kwenye mchakato wa uchaguzi Mkuu huwezi kuwasikia wagombea wake wakisifia vyama vyao, bali wanawaeleza wananchi wa Marekani watatekeleza vipi sera ya nchi yao .

Alisema kuwa ikiwa katiba mpya inayoandaliwa hivi sasa itakuruhusu mgombea huru, atakuwa tayari kugombea ubunge tena kwenye jimbo lake la Njombe Magharibi, lakini kama katiba hiyo itazuia fursa hiyo hatogomea tena wadhifa huo maisha yake yote.

Aliongeza kuwa baada ya kupatikana kwa katiba mpya, inabidi itungwe sera ya Taifa itakayolindwa kisheria, ambayo kila chama kitakachofanikiwa kuingia madarakani kilazimike kuifuata badala ya ilivyo sasa vyama vinaogelea hovyo.

Alisema kuwa ndoto za kuwa mwanasiasa huru alikuwa nazo tangu zamani, na ndiyo sababu katika mabango yake ya kuhamasisha achaguliwe wakati akigombea ubunge kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, alikuwa na kauli mbiu ya ‘Mtu kwanza, chama baadaye.

Alisema kuwa ikiwa katiba mpya inayoandaliwa hivi sasa itakuruhusu mgombea huru, atakuwa tayari kugombea ubunge tena kwenye jimbo lake la Njombe Magharibi, lakini kama katiba hiyo itazuia fursa hiyo hatogomea tena wadhifa huo maisha yake yote.

“Nitapenda kushauriana na watanzania wanaopenda maendeleo ya taifa letu nje ya mlolongo wa vyama, hivyo hata kama naipenda vipi Chadema, nalazimika kuresighn (kujiuzulu) uanachama ili niweze kutimiza azma hiyo,” alisema Nyimbo.

Kilichomkimbiza Chadema.

Alisema ameamua kujiondoa ndani ya chama hicho baada ya kubaini kuwa kinaenda kinyume na malengo yake kama kinavyojipambanua mbele za watu.


Alisema licha ya kuwaaminisha wananchi, hususani vijana kuwa ndio chama chenye kuleta mabadiliko ya kweli,lakini viongozi wake wa daraja la juu akiwataja Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dk. Wilbroad Slaa wamekuwa wakijinufaisha binafsi.


Alisema viongozi hao pia wamekuwa si watu wa kushaurika ndani ya chama hicho, lakini kibaya zaidi ni kuendesha siasa katika mfumo mbaya wa kushawishi na kuaminisha bila kuwa na suluhisho (Mob Politics).


Alisema siasa za namna hiyo ni hatari kwa taifa kwa kuwa baada ya kuungwa mkono kwa kiwango cha juu na kundi la vijana kwa imani ya kukombolewa pale watakapofanikiwa kuingia madarakani na kushindwa kuwatimizia kutazua vurugu.

Kuhusu CCM.

Nyimbo alidai kuwa chama hicho kinajimaliza chenyewe kutokana na kuacha suala la rushwa kwenye chaguzi zake za ndani kuwa ndio kigezo muhimu cha kuwapata viongozi wake.

Hata hivyo alisema ili tatizo hilo limalizike ni wananchi wenyewe kuamua kuikataa rushwa kwa kupokea rushwa isiyoleta matunda kwani wakifanya hivyo watakuwa wamemaliza tatizo hilo .

“Mfano wewe ukipokea rushwa na kuamua kufanya tofauti na aliyekuhonga kwa kuwa baadaye atakuwa hajapata kile alichotaka kukinunua toka kwako, unafikiri kesho atarudia”.

Vijana.

Amewataka vijana nchini kupigania maslahi yao kwa mtazamo hasi wenye kuleta mstakabali mzuri wa Taifa, badala ya kufikiri kuwa mabadiliko ni kuiondoa CCM madarakani na kuiweka Chadema.

Alisema kuna mambo mengi ya msingi ambayo kama vinana wanapaswa kuwahoji viongozi waliowachagua kama wameyatekeleeza , ikiwemo kupigania katiba mpya kuwa na sera ya inayoweza kuruhusu mgombea binafsi kwa kuwa huko wanaweza kupata viongozi bora.

Kujiengua kwa Nyimbo linaweza kuwa ni pigo kubwa kwa Chadema, kwani baada ya kujiunga na chama hicho mwaka 2010, alikuwa ni mlezi wa Chadema kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, huku pia akiwa ni miongoni mwa wanasiasa wenye mvuto na wahamasishaji wazuri wa Chadema katika mkoa mpya wa Njombe.

Habari kwa hisani ya Moses Ng’wat,Mbeya. picha na Mbeya yetu




Aende tu huko aendako kwa sababu hana athari zozote kwa CDM. Kwanza mi ndo namskia leo,he is a noboby.Apumzike tu kwa amani na waachie vijana wafanye siasa. Nadhani itakuwa amekosa cheo alichokuwa anakitaka.
 
“Nasema bila ya kubabaika na nina uhakika na ninachokisema ni kwamba kwa asilimia 50, mauaji ya mwanangu ambaye pia alikuwa ni rafiki yangu Mwangosi, yalisababishwa na Chadema kwa kutotii amri ya Jeshi la Polisi na kupanga kwenda kuzindua tawi la chama ambalo mimi (Nyimbo) nikuwa tayari nimekwishalizindua miezi mitatu iliyopita kabla ya tukio lile,” alisema Nyimbo.( MWANANCHI-29/10/2012)
 
“Nasema bila ya kubabaika na nina uhakika na ninachokisema ni kwamba kwa asilimia 50, mauaji ya mwanangu ambaye pia alikuwa ni rafiki yangu Mwangosi, yalisababishwa na Chadema kwa kutotii amri ya Jeshi la Polisi na kupanga kwenda kuzindua tawi la chama ambalo mimi (Nyimbo) nikuwa tayari nimekwishalizindua miezi mitatu iliyopita kabla ya tukio lile,” alisema Nyimbo.( MWANANCHI-29/10/2012)

...kwa hiyo Kamhanda angeenda nyumbani kwake na kutoa amri ya kumgeuza angegeuka? Si kila amri ni halali.
 
"Nasema bila ya kubabaika na nina uhakika na ninachokisema ni kwamba kwa asilimia 50, mauaji ya mwanangu ambaye pia alikuwa ni rafiki yangu Mwangosi, yalisababishwa na Chadema kwa kutotii amri ya Jeshi la Polisi na kupanga kwenda kuzindua tawi la chama ambalo mimi (Nyimbo) nikuwa tayari nimekwishalizindua miezi mitatu iliyopita kabla ya tukio lile," alisema Nyimbo.( MWANANCHI-29/10/2012)

Hilp ni onyo kwa wanahabari kutotumika kama alivyo uwawa Mwangosi, wakati CDM na Polisi wanatunishiana misuli.
 
Kumbe wewe unatafuta attention tu?
-Huyu aondoke tu kwani wasaliti hawakosi sababu na katika safari hii ni lazima wawepo na wengine watakuja
-By the way anaogopa kasi ya vijana,political liability.Mbona kuna wazee ambao ni tishio na wanaenda sambamba na kasi ya vijana kama akina Victor Kimesera,Marando,prof.Baregu? Wazee hawa ni asset
kubenea huyu kijana yuko wapi? sisi kama UVCCM wapenda DEMOCRACY tunaombeni vikao vyenu huko DODOMA vije na majibu
 
hivi hii Hoteli yake aliirudisha? napita pale imekuwa Gofu japo inaiulinzi... pia nakumbuka alipata presha siku aliyo angushwa na Lwenge mpaka kuzimia kwaajili ya hiyo hoteli
 
Back
Top Bottom