This man is either a sadist or alimuua kibaka, akanywa bia kusherehekea?

Hawa ni watu ambao watakapoondolewa madarakani na kutupwa nje.. wataanza kuelezea kuwa "walipotea tu". Labda anafikiri kwa vile ni Mkuu wa Mkoa basi yuko juu ya sheria. Sasa polisi na mahakama zina kazi gani? Lengo zima la kuwa na sheria na vyombo vya dola ni kwa sababu jamii imeendelea na haitaki kila mtu kuwa mshtaki, jaji na mnyongaji! Huyu ni kiongozi mbovu. Ila asipoangalia anaweza kuishia kama Ditopile.
Magu ndo anapenda viongozi wa namna iyo, ukiwa msimamia haki au mtetezi wa wananchi we kwake ni sawa na mpinzani na atatengua uteuzi wako kama kina NAPE
 
Naombeni sana msi question mamlaka yake ya uteuzi huwa inawaokota wapi watu kama hawa, kwa sababu huwa hakuna kipimo cha soundness of state of mind kabla ya uteuzi hi nina amini kabisa alipoteuliwa, mteua hakujua state of mind ya mteuliwa huyu!.
Ni kipi kinachokuzuia kuamini kuwa anayeteua anavutiwa na vigezo na sifa hizo alizonazo mteuliwa ambazo wewe unazoziona kuwa hazifai?

Hizi njia zako za 'deduction' siku hizi hazina ushawishi wa kuaminisha tena.
 
Wanabodi,
Siamini ninachokisikia hapa kwa kiongozi

Japo wote tunamasikio inawezekana sio wote tunaweza kusikiliza kitu tukasikia, hivyo kwa faida ya wengine naomba kusema kwa kifupi tuu mimi nilichosikia na kilicho nifanya nipandishe bandiko hili.

Kiongozi huyu anasema kibaka akiingia kwako hata kama ni kuiba chumvi, anakuwa ameomba mambo matatu.
1. Ameamua kuiba
2. Ameamua kuua
3. Ameamua kuuwawa

Amewaambia polisi wa mkoa wake kuwa kufuatia magereza kufurika, wayajibu maombi ya vibaka wote mkoani kwake kwa kuwapatia ombi lao la tatu yaani wauwawe!.

Kubwa kuliko ni akajitolea mfano yeye mwenyewe jinsi alivyomuua kibaka aliyevamia nyumbani kwake kwa kumpiga risasi mbili na kufa papo hapo, na yeye ili kukamilisha furaha yake kwa kufungua bia moja kunywa kwa kujipongeza!.

Kwa watu wanaojua kitu kinachoitwa psychoanalysis ya binaadamu, unaweza kumbaini a person of unsound mind kwa jinsi anavyoongea.

Kwa jinsi mtu huyu alivyoongelea hili tukio la kumuua kibaka na Kusherehekea kwa kunywa bia, I seriously doubt the soundness of his mind, this is a sadist!.

Naombeni sana msi question mamlaka yake ya uteuzi huwa inawaokota wapi watu kama hawa, kwa sababu huwa hakuna kipimo cha soundness of state of mind kabla ya uteuzi hi nina amini kabisa alipoteuliwa, mteua hakujua state of mind ya mteuliwa huyu!.

Kwa vile state of mind is not static, ni dynamic, inawezekana kabisa wakati anateuliwa he was OK, akaja kubadilika mbele ya safari, kama hata baada ya kuyasema haya ataachwa aendelee, huu utakuwa ndio uthibitisho kuwa hali hii inafahamika vyema, hivyo mwacheni apige kazi.

Kitu nitakachowaomba wana jf wenzangu mfuatilie, ni kitu kinachoitwa Karma kinavyoshughulikia watu kama hawa, hivyo bandiko hili liwekeni pending kwenye kumbukumbu zenu, ili siku karma itakapo a
Huyu ni psycopath Pascal.Ila sishangai viongozi wetu wengi wana tabia zinazofanana na hiyo.It is actually a demonic behaviour.View the following:




Image result for psychopath

Image result for psychopath

Image result for psychopath

Image result for psychopath

Image result for psychopath

View all

Psychopathy is traditionally a personality disorder characterized by persistent antisocial behavior, impaired empathy and remorse, and bold, disinhibited, and egotistical traits.
 
Msishangae hao mnaowaona hawastahili kuwa viongozi wakiendelea kudunda. Kosa moja linalofanyika mitandaoni ni kuwajadili hao watu lengo la kuonyesha jinsi wasivyofaa. Mamlaka yao ya uteuzi ilishasema wazi kuwa mnapojaribu kushinikiza waondolewe ndiyo hawataondolewa!
 
Kuna mambo mawili either ni addicted wa vilevi vikali/moshi au aliathilika katika malezi yake ya utotoni.
Kuondolewa au kutokuondolewa kwao sio funzo kwa wengine maana tabia ni kama ngozi.
 
Mkuu Pascal Mayalla huyu Mtu hajaanza leo na kauli zake za ajabu ajabu..

Mimi wanaonishangaza ni hao Wanaccm wanaomshangilia kwa vigelegele.

Mwenyekiti wao alishawahi kutoa kauli "Wafungwa wafanyishwe kazi ikibidi wapigwe na Mateke "

Huyu anaendeleza tu.
Nilifikiri pia unge refer ile aliyosema "wanyang'anywe silaha harakaharaka"
 
Mkuu Pascal, upo vizuri mno ktk analytical skills, you are an exemplary contributor, Indeed it is one of many other issues you always share and in turn the forum could start focusing on it. Hii hoja yako naomba nijipange vizuri niipe shavu zaidi.
 
Wanabodi, This man is either a sadist or alimuua kibaka, akanywa bia kusherehekea? Siamini ninachokisikia hapa kwa kiongozi
Tatizo letu Watanzania ni unafiki na mimi sipendi unafiki kwani naamini hakuna adui hatari kama mnafiki. Pascal Mayalla, bila shaka umeshuhudia jinsi huyo unayemwita sadist anavyoshangiliwa kila akitamka hayo ambayo huamini unayasikia kutoka kwake. Lakini kwa upande wangu nimepigwa butwaa na huko kutokuaimini kwako? Huko kutoamini kwako kumenishtua zaidi kuliko yanayotamkwa na huyo kiongozi. Kwa sasa nitaachia hapo!
 
pascal pascal kwa heshima naomba ujibu comment yangu tafadhari!

ni swali yule mkurugenzi aliye ua mtu kanisan kafanywa nini? kumbuka ww ni mwandishi wa habari za kiuchunguz japo siku hizi umeacha umeamua kuunga juhudi kimya kimya naomba hili tuu unijibu kiufasaha!

tuliambiwa yupo jera! lakn cheo chake ameenda nacho, means anayeendelea kulipwa.

sasa kwa matukio haya mwenye matatizo ni nani kati ya watendaji wauaji na mwajiri wao??

PASCAL TAFADHARI NJOO UNIJIBU!
 
Tatizo kubwa ktk jamvi letu, mtu anaweza kujenga hoja zake, tena vizuri tu. Lakini ona maoni ya wachangiaji, tena kwa maneno machache tu. Mimi nafikiri tuwe na constructive criticisms pale mtu anapohisi kutokukubaliana na mtoa hoja. Hili ni jukwaa lenye hadhi kubwa ktk kuelimishana, kutokukubaliana kimsimamo na kuhabarishana. Sentiments zipo lkn ni kwa kutokupania ama kuudhi wengine kwa makusudi.
 
Back
Top Bottom