This man is either a sadist or alimuua kibaka, akanywa bia kusherehekea?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,180
Wanabodi,
Siamini ninachokisikia hapa kwa kiongozi


Japo wote tunamasikio inawezekana sio wote tunaweza kusikiliza kitu tukasikia, hivyo kwa faida ya wengine naomba kusema kwa kifupi tuu mimi nilichosikia na kilicho nifanya nipandishe bandiko hili.

Kiongozi huyu anasema kibaka akiingia kwako hata kama ni kuiba chumvi, anakuwa ameomba mambo matatu.
1. Ameamua kuiba
2. Ameamua kuua
3. Ameamua kuuwawa

Amewaambia polisi wa mkoa wake kuwa kufuatia magereza kufurika, wayajibu maombi ya vibaka wote mkoani kwake kwa kuwapatia ombi lao la tatu yaani wauwawe!.

Kubwa kuliko ni akajitolea mfano yeye mwenyewe jinsi alivyomuua kibaka aliyevamia nyumbani kwake kwa kumpiga risasi mbili na kufa papo hapo, na yeye ili kukamilisha furaha yake kwa kufungua bia moja kunywa kwa kujipongeza!.

Kwa watu wanaojua kitu kinachoitwa psychoanalysis ya binaadamu, unaweza kumbaini a person of unsound mind kwa jinsi anavyoongea.

Kwa jinsi mtu huyu alivyoongelea hili tukio la kumuua kibaka na Kusherehekea kwa kunywa bia, I seriously doubt the soundness of his mind, this is a psychopath or a sadist!.

Naombeni sana msi question mamlaka yake ya uteuzi huwa inawaokota wapi watu kama hawa, kwa sababu huwa hakuna kipimo cha soundness of state of mind kabla ya uteuzi, hivyo nina amini kabisa alipoteuliwa, mteuzi hakujua state of mind ya mteuliwa huyu!.

Kwa vile state of mind is not static, ni dynamic, inawezekana kabisa wakati anateuliwa he was OK, akaja kubadilika mbele ya safari, kama hata baada ya kuyasema haya ataachwa aendelee, huu utakuwa ndio uthibitisho kuwa hali hii inafahamika vyema, hivyo mwacheni apige kazi.

Kitu nitakachowaomba wana jf wenzangu mfuatilie, ni kitu kinachoitwa Karma kinavyoshughulikia watu kama hawa, hivyo bandiko hili liwekeni pending kwenye kumbukumbu zenu, ili siku karma itakapo anza to take its toll kwa ma psychopath kama hawa kwa kumshungulikia, mkumbuke kuna watu humu tulisema kabla.

Psychoanalysis ya ma psychopath, na ma sadist, kwa kadri anavyofanya sadism na kuachwa, ndivyo blood thirsty inavyozidi, hivyo atafanya tukio kubwa zaidi na zaidi ndipo watu watashituka!.

It's only a matter of time.

Paskali
 
Duu..watendaji wa awamu hii,si mchezo! Kila mmoja anajaribu kumu impress Mheshimiwa Rais bila kujali namna ya kufikisha ujumbe. Sina hakika kama kuna chombo cha kuwachuja hawa mabwana kabla hawajapewa majukumu wanayopewa.Kwanini wasipelekwe Simiyu kwa Anthony Mtaka akawape somo la maadili ya uongozi?
 
Hawa ni watu ambao watakapoondolewa madarakani na kutupwa nje.. wataanza kuelezea kuwa "walipotea tu". Labda anafikiri kwa vile ni Mkuu wa Mkoa basi yuko juu ya sheria. Sasa polisi na mahakama zina kazi gani? Lengo zima la kuwa na sheria na vyombo vya dola ni kwa sababu jamii imeendelea na haitaki kila mtu kuwa mshtaki, jaji na mnyongaji! Huyu ni kiongozi mbovu. Ila asipoangalia anaweza kuishia kama Ditopile.
 
Unategemea nini kama anatoa kauli za kutishia uhai wa watu halafu Raisi anamuacha ofisini?
Ingekuwa kwenye nchi zinazojali haki za raia zake huyo mtu angekuwa ameshalazimishwa na mamlaka zilizomteua ajiuzulu!
Lakini hili huwezi kuliona Bongo. Maadamu mtu akiongea kila baada ya sentensi mbili mtu anasifu yaani anamfagilia raisi, basi haina neno, huyo mtu hawezi "kutupwa"
 
Duu..watendaji wa awamu hii,si mchezo! Kila mmoja anajaribu kumu impress Mheshimiwa Rais bila kujali namna ya kufikisha ujumbe. Sina hakika kama kuna chombo cha kuwachuja hawa mabwana kabla hawajapewa majukumu wanayopewa.Kwanini wasipelekwe Simiyu kwa Anthony Mtaka akawape somo la maadili ya uongozi?
Tuache unafiki!

Mkulu mwenyewe aliwahi toa kauli/agizo gani kwa Polisi?

Je,si Mkulu aliagiza majambazi watangulizwe?

Pascal Mayalla haya ni maokeo ya mtu ambae nyie mko humu kutwa kumtetea hivyo kubalini bwana yule na watu wake wote hawafai vinginevyo kaeni kimya.
 
Mkuu Pascal Mayalla huyu Mtu hajaanza leo na kauli zake za ajabu ajabu..

Mimi wanaonishangaza ni hao Wanaccm wanaomshangilia kwa vigelegele.

Mwenyekiti wao alishawahi kutoa kauli "Wafungwa wafanyishwe kazi ikibidi wapigwe na Mateke "

Huyu anaendeleza tu.
Acha ujinga, sasa mfungwa kulala siku nzima unaona sawa, yaani afanye uhalifu halafu kodi zetu zimlishe, duniani kote wafungwa hufsnyishwa kazi sana tu, wengine mnawaona wanatujengea mabrabara
 
Wanabodi,
Siamini ninachokisikia hapa kwa kiongozi huyu!.



P

t nchi yetu inako elekea sio kuzuri nyinyi mnaiba mabilioni ya kodi za wananchi halafu mnalipwa mishahara mkubwa. na mnapewa magari makubwa yaliyo nunuliwa na kodi zetu, mafuta mnajaziwa na dreva mnapewa bado mnaiba kodi mnapokea rushwa mbona hamuuwawi ? ila mnataka mwananchi mliye mfilisi mpaka akashindwaa kulisha familia yake, akajikuta kwenye hali yakudokoa kuku, mnataka auwawe. jee nyinyi manao iba mabilioni au manao sababisha hasara za mabilioni kama wale walio taifisha shamba la mkulima bila kufuwata sheria na kupelekea kutumia kodi zetu kumlipa mabilioni na bado ndege yetu ikakamatwa tuwafanye nini?
 
Acha ujinga, sasa mfungwa kulala siku nzima unaona sawa, yaani afanye uhalifu halafu kodi zetu zimlishe, duniani kote wafungwa hufsnyishwa kazi sana tu, wengine mnawaona wanatujengea mabrabara
Dunia ipi unayozungumzia wewe!..
Wanayopiga wafungwa mateke..
 
Acha ujinga, sasa mfungwa kulala siku nzima unaona sawa, yaani afanye uhalifu halafu kodi zetu zimlishe, duniani kote wafungwa hufsnyishwa kazi sana tu, wengine mnawaona wanatujengea mabrabara
Hukuelewa Chochote,labda wewe ni mke wa Chalamila ama mwanaye...kauli ya kuua mtuhumiwa ikichukuliwa serious nawe siku moja utajikuta ahera kwa kosa ambalo kama sheria ingefuatwa ungepaswa kulipa fine isiyozidi shilingi elfu moja!
 
77 Reactions
Reply
Back
Top Bottom