unajua unachokisema ni kikubwa mno kuliko unavyoashiria..
a. Inawezekana vipi kijana wa miaka 25 kutoka asikojulikana kuweza kugombea Ubunge na kushinda?
b. Akiwa na miaka 30 hivi kijana huyo huyo anakuwa mtu mwenye nguvu kabisa nchini kiasi cha kuitwa na jarida mojawapo kuwa ni "King Maker"?
c. Akiwa chini ya miaka 40 anaweza kuwafanya watu kama kina Ruhinda, Kingunge, Mkapa, Mwang'onda, n.k kuweza kukaa chini na kugwaya mbele zake?
d. Inakuwaje mtu huyo kuweza kupanga safu yake ya mashambulizi kuanzia Ikulu.. na hakuna mtu anayeweza kumnyoshea kidole hata gizani?
Asili ya nguvu zake ni nini? Watu wengi wanafikiri ni fedha yake... Hili si kweli kwani watu wenye fedha wamekuwepo wengi kabla yake kuna watu waliokuwa waitikise nchi hii kama wangetaka.. kina Rajpar (wengine hata hawamkumbuki huyu), kina Somaia (yule wa Tanga), na wengine wengi.
Mzee Mengi aliwahi kuuliza swali ambalo lina umuhimu kweli, "kiburi chake anatoa wapi"?