I wish you all the best of luck Prince! Leave no stone unturned in exposing these fisads. We look forward to hearing more from you. Great man! SAA YA UKOMBOZI NI SASA![/QUOTE]
Ili ukombozi upatikane tunahitaji kuwa na rais ambaye ni adui wa RA and the Co. Kwahiyo ndugu zangu, hasa sisi tuliotoka kule vijijini tufanye juu chini twende huko tukawaelimishe na kuwahamasisha ndugu zetu wasiendelee kuipigia CCM kura tena. YES WE CAN.
unajua unachokisema ni kikubwa mno kuliko unavyoashiria..
a. Inawezekana vipi kijana wa miaka 25 kutoka asikojulikana kuweza kugombea Ubunge na kushinda?
b. Akiwa na miaka 30 hivi kijana huyo huyo anakuwa mtu mwenye nguvu kabisa nchini kiasi cha kuitwa na jarida mojawapo kuwa ni "King Maker"?
c. Akiwa chini ya miaka 40 anaweza kuwafanya watu kama kina Ruhinda, Kingunge, Mkapa, Mwang'onda, n.k kuweza kukaa chini na kugwaya mbele zake?
d. Inakuwaje mtu huyo kuweza kupanga safu yake ya mashambulizi kuanzia Ikulu.. na hakuna mtu anayeweza kumnyoshea kidole hata gizani?
Asili ya nguvu zake ni nini? Watu wengi wanafikiri ni fedha yake... Hili si kweli kwani watu wenye fedha wamekuwepo wengi kabla yake kuna watu waliokuwa waitikise nchi hii kama wangetaka.. kina Rajpar (wengine hata hawamkumbuki huyu), kina Somaia (yule wa Tanga), na wengine wengi.
Mzee Mengi aliwahi kuuliza swali ambalo lina umuhimu kweli, "kiburi chake anatoa wapi"?
I have completed reading the radar thesis I will share with you the SFO findings in London, before Monday next week.
Yesterday I had a very good time her although it is very chilly to read the findings by SFO.
Anamiliki makampuni kama uyoga
Lakini jina lake halionekani popote
Na Saed Kubenea
MwanaHALISI
ROSTAM Aziz, mbunge wa Igunga, anamiliki makampuni mengi ambamo jina lake halionekani, MwanaHALISI limegundua.
Hata pale anapokiri hadharani kuwa anamiliki kampuni fulani, bado kampuni hiyo haina jina lake kamili la Rostam Abdulrasul Aziz kama linavyofahamika katika kumbukumbu za bunge.
Rostam anatajwa kumiliki makampuni 10 yaliyoanzishwa jijini Dar es Salaam kwa nyakati tofauti, lakini jina lake linaonekana katika kampuni moja tu, kwa mujibu wa fomu za Wakala wa Usajili wa makampuni na Leseni za Biashara (BRELA).
Kampuni ambako jina lake linatajwa ni African Trade Development (T) Limited (ATDL) ambako pia limeongezewa jina jingine Sakarri kwenye safu ya majina ya ukoo, ambalo hata hivyo halifahamiki kwa wengi.
Katika ATDL, orodha ya waanzilishi wenye hisa inaonyesha kuna Rostam watano (5) huku jina Rostam likiwa ama limekosewa au limebadilishwa herufi kadhaa au wahusika wakiwa na ubini tofauti.
Hata katika ununuzi wa magazeti ya Rai, Mtanzania, The African, Dimba, Bingwa na chuo cha uandishi wa habari MAMET, kutoka kampuni ya Habari Corporation Limited (HCL), hakuna jina lake.
MwanaHALISI linaweza kuripoti kuwa magazeti hayo yaliuzwa kwa kampuni inayoitwa Isenegeja Limited ya Dar es Salaam ambako jina la Rostam halionekani.
Aidha, ni Rostam Aziz aliyekiri mbele ya waandishi wa habari, 3 Mei mwaka huu katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski, kuwa anamiliki magazeti hayo kupitia kampuni ya New Habari Limited ambayo pia bado ni kitendawili.
Siku tatu kabla ya kauli yake kwamba anamiliki kampuni hiyo, gazeti lake la Rai liliripoti kuwa inasadikika kwamba Rai linamilikiwa na Rostam.
Kwa mujibu wa barua ya Katibu wa Bodi ya Wakurugenzi ya HCL, Shaaban Kanuwa ya 30 Aprili mwaka huu, bado wamiliki wa sasa wa magazeti hayo hawajayalipia.
Barua hiyo inayoandikwa kwa Isenegeja Company Limited, kupitia New Habari (2006) Limited (NHL), ambayo Rostam Aziz anadai kumiliki, inasema MAMET na magazeti ya Dimba na Bingwa, bado hayajalipiwa.
Kanuwa anasema katika barua hiyo, kwamba wakurugenzi wa HCL wanapendekeza zilipwe mara moja Sh. 100 milioni ambazo walikubaliana wakati wa ununuzi wa kampuni hiyo.
Wakati huohuo, Kanuwa anaelekeza kuwa iwapo Isenegeja haijawa tayari au imeshindwa kulipia magazeti mawili ya Dimba na Bingwa na MAMET, basi iache kuvitumia, kwa maana ya kuyachapisha na kuendesha chuo.
Habari Corporation iliuzwa miaka mitatu iliyopita. Haijafahamika magazeti ya Rai, Mtanzania na The African yaliuzwa kwa kiasi gani.
Lakini barua ya bodi ya HCL inasema gharama ya magazeti ambayo hayajalipiwa ilikuwa kama ifuatavyo: Dimba Sh.40 milioni, Bingwa Sh. 30 milioni na chuo Sh. 10 milioni na ilitaka kiasi hicho kilipwe ifikapo 29 Mei mwaka huu.
MwanaHALISI haikuweza kufahamu majengo ya HCL yaliuzwa kwa kiasi gani. Kanuwa alipoulizwa iwapo Isenegeja wamekwishawalipa, alisema swali hilo aulizwe mwenyekiti wa bodi, Jenerali Ulimwengu ambaye imefahamika yuko nje ya nchi na hakuweza kufikiwa.
Uchunguzi wa gazeti hili haukuweza kubaini faili la NHL ambako ulitegemea kukuta jina la Rostam Aziz aliyesema anamiliki kampuni hiyo na magazeti yake.
Lakini miezi miwili iliyopita, kulikuwa na andishi kwenye mtandao wa jamiiforum.com lililokuwa linaenda kwa Rostam Aziz kumtahadharisha kuwa alikuwa anaendesha kampuni ya NHL bila kusajiliwa na bila mwelekeo wowote.
Andishi lililosainiwa kwa jina moja la Salva, halikujulikana iwapo lilikuwa linatoka kwa mmoja wa wakurugenzi wa HCL na ambaye hivi sasa ni mkurugenzi wa mawasiliano ikulu, Salva Rweyemamu.
Mwandishi alikuwa anaonya juu ya kutozingatia sheria za nchi, kushindwa kuendesha kampuni kwa misingi bora ya menejimenti ambako kulikuwa kunaelekea kuua kampuni.
Haijafahamika pia uhusiano wa NHL na Isenegeja, na uhusiano wa Rostam na makampuni yote mawili NHL na Isenegeja. Waanzilishi na wamiliki wa Isenegeja ni Hassani Haidari na Gulam Abdulrasul wote wa anwani za Dar es Salaam.
Katika umiliki wa kampuni ya African Trade Development (T) Limited (ATDL) ndiko kuna vimbwanga vya majina yanayohusiana na Rostam.
Majina yaliyotumika kusajili kampuni hiyo ni Rostom A. Sakarri, Rostam Sakarri, Rustom Aziz Sakarri, Rustam Sakarri na Rustam Sakaari.
Wanahisa wengine wa kampuni hii waliojiandikisha BRELA, ni Gulam Abdulrasul Chakaar, Bahram Abdulrasul Chakaar na Abdulkadir Mehrab.
Rostam hakupatikana kuthibitisha iwapo Rustam, Rustom, Rostom na Rostam Sakarri yalikuwa majina yake, kulikuwa na jina lake au yalikuwa ya ndugu zake wa karibu. Simu yake ilijibu wakati wote kuwa haipatikani.
Kwenye muhutasari wa kikao cha kampuni ya ATDL cha 17 Machi 1993, kuna saini mbili za Rustam Chakaari (mkurugenzi) na Bahram A Chakaar (mwenyekiti).
Kubadilikabadilika kwa tahajia (spelling) za jina Rostam na mwingiliano wa majina ya ukoo, ni mambo yanayoacha kitendawili kigumu kutegua.
Kwa mfano, siyo rahisi kujua iwapo majina haya yameparanganyishwa kwa makusudi: Rustam Sakarri na Rustam Sakaari.
Mwanasheria aliyezungumza na MwanaHALISI kuhusu utata huu, amesema ni vigumu kumhusisha Rostam na majina hayo matano iwapo kunazuka matatizo ya kisheria kwenye kampuni hizo.
Amesema akihusishwa ataweza kuruka kihunzi na kudai hahusiki kwa kuwa nchi nzima, na labda vyeti vyake, kama anavyo, vinaonyesha anafahamika kwa jina la Rostam Abdulrasul Aziz.
Mwanasheria huyo alisema labda mtu wa aina hiyo anaweza kunaswa kwa kutumia ushahidi wa mazingira.
Makampuni ambayo yanatajwa kumilikiwa na Rostam, lakini jina lake halionekani BRELA, ni pamoja na Africa Tanneries Limited, Tanzania Leather Industries Limited na Wembere Hunting Safaris Limited.
Mengine ambako jina lake halionekani ni Tanzania Packages Manufacturers Limited na Caspian Construction Limited ambayo anwani zake zilikuwa zinatumiwa na kampuni tata ya kufua umeme ya Dowans.
Gazeti hili lina orodha ya makampuni ambayo yanadaiwa kuwa ya Rostam, wale wote waliotajwa kuwa waanzilishi na baadhi ya ofisi za makampuni haya ambako inadaiwa alikuwa anakwenda binafsi kuhimiza utendaji au kufuatilia malipo.
Madai ya Rostam kumiliki kampuni zisizo na majina yake yalianza kujitokeza lilipozuka sakata la yeye kuhusishwa na kampuni kadhaa zenye kashfa, zikiwamo Dowans na Kagoda.
Rostam mweyewe alikiri kuwa na uhusiano na Dowans, lakini akadai hamiliki kampuni hiyo isipokuwa anuani na barua pepe za kampuni yake ya Caspian Construction zilikuwa zinatumiwa na kampuni hiyo ya Dowans.
Jina la Rostam linatajwa katika umiliki wa kampuni tata ya Kagoda. Wakili wa Mahakama Kuu, Byidinka Michael Sanze amenukuliwa katika hati yake ya kiapo, akisema kwamba Rostam ndiye aliyemtaka kushuhudia hati za mikataba ya Kagoda.
Kampuni ya Kagoda ilichota zaidi ya Sh. 40 bilioni katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Lakini miezi miwili iliyopita, kulikuwa na andishi kwenye mtandao wa jamiiforum.com lililokuwa linaenda kwa Rostam Aziz kumtahadharisha kuwa alikuwa anaendesha kampuni ya NHL bila kusajiliwa na bila mwelekeo wowote.
Silence in issue we ought to speak against, means agreement, participation or both.Tatizo la most Tanzanians ni hiyo tabia ya uoga and unnecessary silence.huyu hajakoma sio, tindikali haikumtosha, safari hii watakuua.
Sijui kwa habari hiyo hapo juu kuna ubaya gani kisheria. Labda kama directors/shareholders hawa-exist, au less than 18 years old. To register a company you need an address and the names of shareholders and directors (living). Kwa shughuli alizonazo Rostam sitashangaa kama ana kampuni hata mia. THis is a guy who have been also playing offshore, especially Cyprus, Isles Man etc he must be having more companies there.
huyu hajakoma sio, tindikali haikumtosha, safari hii watakuua.