Mimi sijui wakubwa wa nchi hii mipango yao wanaiiga kutoka taifa gani dhaifu. Huwezi kuwa na uwanja wa kuhudumia watu milioni sita wakati kasi ya uwekezaji inatisha. Miaka miwili baadaye watabomoa! Kuna mahali tumemkosea Mungu.
Umenena mkuu.
Na huu ni ugonjwa upo in all sectors of our economy and government.
Wataalam ndio hao hao waliobuni miundombinu ya ajabu ya afya, elimu, ardhi etc etc.... Kila sehemu ni majanga matupu.
Kiwanja cha ndege sio majengo tu. Kuna runway/s ambazo ndio muhimu zaidi. Kwa nafasi iliyopo JKNIA hakuna nafasi ya kuongeza urefu wa runway iliyopo au kujenga mpya kabisa. Kuna reli ya Tazara imeizingira airport kwa upande upande Jet club na Kitunda.
Runway iliyopo ni fupi mno. Ndege kubwa za masafa marefu haziwezi kuruka na maximum load bila kupitia mji mwingine kuongeza mafuta.
Kuna mapungufu mengi mno ya waziwazi kabisa. Wataalam mburura wa UPE ndio wenye maamuzi haya ya ajabu ajabu.
Wakoloni waliona haja ya kujenga Dar Airport kwenye miaka ya 50s. Walihamisha kutoka eneo la mwanzo...
KUNA ANAEJUA AIRPORT YA KWANZA DAR ILIKUWA WAPI???
Jibu kesho!