Mimi sijui wakubwa wa nchi hii mipango yao wanaiiga kutoka taifa gani dhaifu. Huwezi kuwa na uwanja wa kuhudumia watu milioni sita wakati kasi ya uwekezaji inatisha. Miaka miwili baadaye watabomoa! Kuna mahali tumemkosea Mungu.
mkada, kwanini unataka nijinyonge?Heathrow ya TZ mkuu,,,kwani Arusha si ni Geneva ya Afrika,,,hutaki jinyonge mkuu.
Yes, hata mimi nilikuja gundua kosa langu baadae kabisa - kumbe nilikuwa na angalia bird's eye view na sio jengo kwa uhalisia wake - thanks 4 the photo - naona ulipiga terminal 5. Je, ukupata tatizo na watu wa usalama!! Tukirudi kuhusu design ya third terminal ya uwanja wetu wa ndege, Mkuu bado nasisitiza kwamba design ya jengo la mwanzo yaani ndege zinapo park ukiangalia nyuma ya jengo hilo linaonekana limejengwa ki-godown/workshop regardless ya kama unaliangalia ukiwa angani au ukiwa aridhini unless kama sehemu ya chini ya jengo hilo imekuwa designed spefically kuhifadhi CARGO kubwa kubwa na sio baggages, kama ni hivyo hapo naweza kuhafikiana nao. Jengo la pili yake hilo kidogo limekuwa designed vizuri lakini not 2 my liking, nisijue wenzangu wanalionaje? Mkuu juzi juzi hapa Waziri Mkuu alikuwa Uchina na akakutana na Viongozi wa Kampuni kubwa ya kusafirisha abiria kwa ndege, kampuni hiyo hiyo inadesign na kujenga Terminals za Airport nchini mwao mpaka nchi za nje - mfano Merikani, sasa hawa jamaa wa Civil Aviation kwa nini awalinganishi design za hawa wa Holanzi/ma Brit na design za kampuni hii ya Kichina inayo sifika Duniani kote. Kama Waingereza wameona umuhimu wa kuomba Wachina waje kwao ku-redesign na Kujenga yard ya London Dock sisi tunashindwa nini kuwa-emulate i.e tujenge majengo yanayo vutia. Mimi ndio maoni yangu mkuu, ila naipa pongezi Serikali kwa dhamila yake nzuri ya kutaka kulifanya Taifa letu linonekana la ki-leo.Mkuu Bukyanagandi.Ni kweli unachosema lakini hata hiyo Heathrow, ilianza na third terminal mwaka 2008 wakaongeza Terminal 5, hata London ukituwa unaona kama Gowdown kwa juu hebu angalia hapa chini uwanja wa Heathrow.
Mbona sehemu ipo kubwa tu, Airport ya mkoloni ilikuwa Ferry pale karibu na Kanisa la St Joseph mwaka 1954 ndiyo wakaamia Ukonga.
Usiige kunya kwa tembo.
Huo unatutosha kutokana na uwezo wetu, tukitaka tujenge kama cha Cape town international airport, tutakula majani humu kama ilivyokua kwenye ununuzi wa ndege ya Rais
Huu uwanja wa Jomo Kenyatta ndiyo wakuutolea mifano wakati mweingine tuwe makini wanaukumbi hebu angalieni huu uwanja hapa chini amabao Mwita Maranya anautolea mifano kila kikicha.
Kila kitu na wakati wake, sasa ndio mkataba umeshakamilishwa.
Ni kasi ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM from 1.2 mil to 6 mil.
Big Results NOW...
Yaani FaizaFoxy kukamilika kwa mkataba kumechukua miaka zaidi ya mitano!!!!
Ujenzi utachukua muda gani???
Kwa serikali yetu!!!..Afadhali tungeshughulika na Matatizo ya Umeme ...Ambao unagusa jamii kubwa zaidi...
Go Tanzania Go,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,Love you Tanzania.Kitu kama Heathrow Airport
Mh!kama solution ya muda planning yake inachukua miaka 7 na utekelezaji bila shaka utachukua miaka si chini ya saba...basi hizo solutions za muda mrefu tutasubiri mpaka Yesu atakaporudi.Umeme tayari umeshashughulikiwa na implementation za miradi mbali mbali ya umeme zimeshaanza, tembelea tovuti ya TANESCO ujionee.
Hii inayoongezwa ni terminal tu, kulikuwa kuna mambo mengi ya msingi, Airport zinazokuja Tanzania ni nyingi kuliko unavyofikiria. Hii ni solution ya muda wakati Airport tatu mpya za Kimataifa zikiwa kwenye pipeline.
Mbona sehemu ipo kubwa tu, Airport ya mkoloni ilikuwa Ferry pale karibu na Kanisa la St Joseph mwaka 1954 ndiyo wakaamia Ukonga.
Mh!kama solution ya muda planning yake inachukua miaka 7 na utekelezaji bila shaka utachukua miaka si chini ya saba...basi hizo solutions za muda mrefu tutasubiri mpaka Yesu atakaporudi.
Haya twambie hizo airports mpya ni zipi?
Serikali yetu ina matatizo mengi...likiwemo kutopenda kusikia ushauri wa wataalam na kuweka siasa mbele..ona mbeya(songwe) airport..hadi fastjet ilkuwa imeshindwa kutua pale mpaka walifanya marekebisho ya ziada.unafikiri hiyo itaweza kupewa hadhi ya kimataifa.wakati tuliambiwa inajengwa international aiport!
Hivi unafikiri Rome ilijengwa siku moja?
Ndo tunavyopeana hopes kwa kutumia misemo kama hiyo!rome haikujengwa siku moja lakini bila shaka hiyo miaka 1000 ilipangwa! Sisi tunaangalia miaka 5 mbele..hatujamaliza planning tiyari mahitaji yameishaongezeka.hili linajidhihilisha hata katika maelezo yako katika post ya mwanzo!
Sasa fikiria 1,000 na Katanzania ketu, ndio kwanza kana miaka 49.
Halafu tuoneshe maendeleo ya Roma ya miaka 50 ya mwanzo tulinganishe.