The Working Class, Savages in Suits

Teh teh teh....... nimecheka sana pale Ronny alipo jipeleka kwenye Corrola iliyochoka akaambiwa njoo huku kwenye Nissan.
 
Hamna bwana inategemea na mtu , au ndo samaki mmoja akioza?
Siyo kazini..........Kuna mkaka kuna siku nilimwomba anisindikize pale msasani mall ......kwenye duka la baby shop nikamchukulie dogo nguo.....eeh baada ya kuchagua nikamtania naomba ulipe akasema hana hela.....ila mie nilikiwa namtania .....nikatoa hela nikalipa......eeh kesho nasikia kazini nimemlazimisha alipe nguo za mtoto wangu nilimshangaa.......afu anavyoonekana mstaarabu nikasema nguo tu umetangaza je nikikupa papuchi itakuwaje........

Yani wanaume wa ofisini hawawezi kukaa na vitu moyoni uwa vinawawasha......nikajifunza hapo......
 
Sister ningekutafuta mimi wa mbali.
Tatizo tunafahamiana uraiani.
 
Dah! basi most of them bado wana akili za kivulana naona.

Sent from my TECNO-H3 using JamiiForums mobile app
 
masikini akajikosea papuchii hivihivi, mana yawezekana kunasiku ungempa
 
ha ha ha ha ha ha......savages in suits lara 1 hii stori inavutia sana maanake.......
Hahaha nimekutukana kimoyomoyo tayari. Ila on a serious note wanachokifanya sio utu, sio hata vitu vya kuimagine vimekukuta (hapa naongelea wale wa maofisini na hata babes wa kitaa wanaovujisha faragha za watu). Mwingine utamfanyia hivyo ataaibika atajikongoja vitaisha, wengine mioyo midogo ile fedheha wanashindwa kuihandle, mtu kabugia midonge amekufa. Wewe muhusika utakuwa na amani kweli?
Afu wewe unachekelea tu vibinti vya watu tunavyofanywa, wewe mbona hufanyi? Ila ni utoto haswa Kulikuta jitu zima linajisifia eti wale wote nishawagonga, sawa wao ni chupi mkononi, na wewe ni nini, kiboro dinda? Mwanaume ndo hutakiwi kujitunza? si vipotezee tu hivyo vi macho juu, em kueni huko, mnatuharibia tu decent girls wetu. (Mungu tuepushe watoto wako na mifisadi yote).
 
Hii stori ni tamu mno
 
dont hate the player hate the game....boys will be boys....make sure you can differentiate men from boys.
 
Our Biggest Issues Can Be Smallest Issues To Others.

Akarudi kwenye kibox chake, Mda wa kutoka Chieff akamfata kumwambia tunahitaji kumalizia yale maongezi. Linda akamwambia sawa. Akenda kumwambia Ronny naodoka na Chieff kuna mambo binafsi tunataka kuongea. Ronny akahisi foul! Akaanza kumkataza kwendaa, Linda akamwambia really i have to go talk to him. Ronny kakomaa aambiwe ni nini hayo maongezi yanahusu, akamwambia ni issue private, ila amuelewe. Ronny akawa pissed tu na whole idea, wana mipango yao mingine afu yeye analeta habari zingine, na kibaya ni huyo chieff kuhusikaaa. Akamuacha tu aende.

Wakaenda kukaa sehemu wanakunywaaa, Chieff akamwambia ulisema the son makes the mother sick why? Akamwambia tunimehisi coz mkeo ana mtoto mwingine wa kike, itakuwa ameanza kuumwa baada ya huyu mtoto kuanza kuleta shidaa. So as long as mtoto anaumwa, mkeo ataumwa lazimaa. Mtoto akiponaa au mkeo aki accept fate ya mtoto wake atapata recovery mpaka utashangaaa. Anachoumwa kikubwa ni rohooo, mwili unabeba side effects tu.

Chieff akamuuliza unanishaurije sasamdogo wangu what should i do? Niachane na hizi habari za Maombi na bwana Yesu hazisaidii eeeh? Linda akamwambia Yesu anasaidia sanaa when you are in the right direction. Kama ukimpeleka kwenye kituo, ukawa unamwomba Mungu wako, tatizo litagunduliwa haraka, atapewa matibabu sahihi, Yesu wako huyo huyo ndo ataongoza jahazi la uponyaji, Yesu mwenyewe alisema jisaidie na mimi nikusaidie. And most of all Yesu atakujibu harakaa coz unakuwa na roho safiii, na unamuachia yeye kweli. Zile hisia hisia na kutia watu ubaya wasiokuwa nao Yesu pia hapendi, mnavoshika watu uchawi wa uongo inaondoa kabisaa upako. You never know inaweza ikawa unazidi kumcheleweshea tiba wakati ungewahi angepona zaidi atakapopona. Tusipoteze mda jmosi tumpeleke kile kituo bao kiko.

Chieff akawa anawaza what if they say my bod is retarded? Can i handle it? Yaani sijui. Linda akamwambia once ukimtia mtoto kwnye gari kumpeleka Moro you will be ready, mambo mengi yatafunguka huko huko. Retard ziko za aina mbili, akili kushindwa kudevelop, au akili kuwa kubwa sanaa. Huenda ikawa issue nyingine tu ndogo ya dawa tu, ukarudi zigo lote umelitua.

Mimi Linda baba yangu mkubwa alikuwa naanguka ghafla tu anapoteza fahamu afu baadae zinarudi. Kapimwa pressure, hanaa, kahangaika hospital baadae kwa waganga ndo ikawa nyumbani kwakwe. Mtajie mganga atakwambia alipo. Mshahara woote wanamalizia kwa waganga, kunua ngombe, mbuzi na kuku anapata nafuuu baadae yale yale. Kila mganga baba mkubwa yuko Tanesco kitengo kizuri, wenzie sio watu wazuri wanataka kumuua wachukue cheo. Akawa anaishi maisha ya wogaa, anafanya makafaraa, hirizi kila sehemu. Akianguka tu utasikia jini maiti, jini Ashura, Jini Zainushi, Jini makata wa makata wametumwa kuja kumtoa roho bora alivowahi kwa huyo mganga.

Kaishi hivo hivo karibia miaka mi 3 sijui, ofisini akawa kisirani anakosana na wenzieee, mnatakaa kuniua mchukue hiki cheo, na sifi nawaambia mtakufa nyie. Kashfa kashfaaa. Watu wakaanza kumuogopa sasa. Siku hio kaanguka kapelekwa hospitali ya mkoa, kufika pale akakuta kuna Dr. casuality sio wa pale katoka Gabon kapata ajali Msamvu ikawa ndo kaenda pale kujiuguzaa. Alivoletwa ikawa hauna Dr, in duty si mnajua hizi hospital za gvt, ikabidi manesi wamuite yule mgabon amuhudumie, baadae fahamu zikamrudi.

Dr akamwambia wewe tatizo lako UNENE TU, body frame yako ndogo so mafuta yamezidi yanabana mishipa ya fahamu kichwani huko ndo maana unaanguka na kukatika fahamu. Ukindekeza bia na michemsho utakuja kuanguka kimojaaa. On the mean time nunua hii dawa pharamarcy itakupunguzia tatizo ila unene upunguzee, uslie wanga na uanze mazoezi mara moja. Akapewa discharge akapita darajani kwa wahindi akawapa ile prescription. Akaambiwa dawa hii 6000! Akastukaa tu? Akaambiwa eeh. Akainunua akawa anaimezaa. Kichwa kilichokuwa kinamuuma mfululizo afu ndo ananguka kikaacha kabisaa, kabisaa. Akaanza na diet mpaka kesho mzimaaa.

Mpaka kesho mzimaaa wa afyaaa, hajaanguka zaidi ya miaka. Siku hizi hata akikuta paka kafa nje kwake anazoa mwenyewe na kwenda kumtupaaa. Akikuta hirizi anaitia kibiriti mwenyewee. Ilimuuma mnoo mnoo kupoteza mihela na mihela alafu kuja kuponea dawa ya sh 6000! Manina zao waganga wooote.

Chieff akasema jumamosi twende Moro, nampeleka mtoto nishaamua. Ngoja kwanza nikampange mama yake huko mpaka kieleweke. Na HOM nitatumia mbinu zooote akupe hio kazi. Hilo niachie mimi, wewe fanya mipango huko Moro, mimi nafanya makarateka kwa HOM. Linda akamwambia asante sanaa, wakaagana kila mtu akarudi kwao

Ronny ikawa kasusa flani kwanini Linda alimsecong kwa CFO, wakati wana mambo yao mazito ya kumalizia???? Akawa anampotezea kibingwaaa. Linda akawa anaendelea tu na maisha. CFO akashindwa kumvua gamba HOM. Interview ikafanyika bila Linda, ila Joy alifnyaaa. Linda akamwambia Jmosi mpango wa Morogo upo pale pale sina nachofanya nitakupeleka.

Kati kati hapo akawa kakaa na Da Asha Linda akamshauri afanye CIMA au CFA sio lazima ACCA. Hizo rahisi atapata harakaa afu zote uzito wake ni sawa. Dada Asha akawa kafurahi, nitafanya CIMA. Jmosi wakaenda Moro na CFO na mkewe ndo akamuona huyo mtoto mgonjwa, wla haoneshiii, hatemi udenda hataaa, akasema ngoja ake kimya, akakaona a kale ka kike, kapo kimyaaaa, akajua tu side effect za kuuguza mda mrefu.

Wakafika wakalipia, Sista akamwambia inabidi huyu mtoto akae hapa tumchunguze kumpima juu juu tuta over look matatizo. Muacheni tutakupigieni simu observation ikikamilika. CFO akageuza Dar na mkewe na yule wa kike, Linda akabakia Morogoro anakula bata tuuu.

Jtatu akarudi kazini, CFO hatulii kila saa anangalia simu, isije kuwa sister kapiga hajaiona au labda vipi. Simu haikupigwaa mpaka ijumaa.CFO hatulii sehemu moja. Joy akawa katokewa rushes mwili mzima hakuja kazini. Akamwambia Linda njoo unione pleaseee! Akawa anamwambia mwenzio naogopaaa, nitakufa mimi. Linda anamtia moyo bwana hujajua kama ndivooo. Inaweza kuwa allergy tu. Wakaenda hospital akakutwa na allarge. Akapewa dawa within 3 days ikaishaaa.

Sasa alivokuwa kwa kina Joy, mama yake Joy anamuuliza hivi huyu Joy hajawahi kukwambia kama ana mchumba labda? Au anataka kuolewa hiviii, manake simuelewi kabisaaa kajibweteka ka relax kabisaaa. Linda akamwambia hajaniambia kitu chochote kuhusu hilo swala. Mama anakomaa wewe si shoga yake humjui bwana yake yoyote labda, unemuona ni potential? Dada zake wote nimewaoza huyu simuelewi.

Linda akamwambia simjui kwa kweli. Mama analalamika hizo ni dalili mbaya kwa kweliiii, dalili mbaya sanaa. You should go out more offen, msijifungie tu ndani, kazini, ndani, kazini ndani, go out have fun. Meet people. Basi mama anamwambia akiwa na mtu unitonye mwanangu sawa eeeh. Si unajua cha kudeka wangu huyu last born. Akasema sawa mama. Moyoni akajisemea laiti ungejua hali halisi ungebakia kma mshumaaa.

Huku CFO akapigiwa simu kati kati ya wiki akaenda Moro mwenyewe kumfata mtoto. Kurudi akamwambia nashukuru sana Linda, huwezi amini imegundulika hana tatizo kubwa zaidi tu kuwa kapoteza uwezo wake wa kusikiaaa na ndo maana haongeiii. Ila Akili yake iko vizui kabisaa. Na tena ningewahi angeweza kuwekewa vifaa akasiki tena. Sema ndo mabo ya kuhangaika sehemu sizooo.

Kumbe aliacha kuongea sio sababu ya majini wala ukichaa but sababu ya kutokusikia, na mtu akipoteza uwezo wa kusikia anapoteza na uwezo wa kuongeaa vizuri matamshi kwa umri wake huyuu. Na ile kusema mtoto kiburiii, mtoto tahira halielewi kumbe sababu hasikii maskini mwanangu. Ileukimsemesha mda mwingine hakujibu, wanasema majini, kumbe ukimsemesha mnaangaliana anajibu sababu anakuona midomo yako na ishara ila akiwa kakupa mgongo hasikii. Mimi nikafocus kumpima akili, na nilivoambiwa akili ziko vizuri nika conclude kalogwa maskinii au mambo ya kishirikinaaa

Sista kasema nimtafutie tu shule zao za viziwi, na kanishauri Patandi Arusha patamfaa sanaa, na kanihakikishia atakuwa vizuriii, atafanya kazi za viziwi vizuriii tu, na ana IQ kubwa tuu. Wamempa kifaa cha kusikilizia, n toka nimrudishe jana, nona anaenda sawa na mama yake. Na mama mtu anakaa sebuleni, anamfata mwanae kila mahali, nafuu naiona. Asipotaka nae kwenda Arusha kuishi nae sijuiii. Sina cha kukupa ila nashukuru.

Ronny akaanza kurudi kwa kasi sanaa, akawa anashangaa, baadae akamuomba msamaha kwa kumhisi vibaya, CFO alimwambia asimhisi vibaya alimsindikiza hospitali mwanae alikuwa anaumwa, na akiwaona wote ni hayo hayo mambo ya ugonjwaa, yeye kama mwanaume mwenzie anamhakikishia hamna cha ziada.

Wakawa wamerudiana, sasa Ronny anakomalia anatengeneza mazingira ya mechi, Linda ana punch kumbe lengo lake akapime kwanzaaa. Manaake siku zinavozidi kwenda anazidi kumuelewa kijana Ronny. Siku hio akamkokota Joyce mpaka ANGAZA, wakataka waingie wote kupima, Joy akamwambia acha mimi nipime kwanza afu nitakusindikiza ukapime na wewe tusipime wotee walau mmoja amsindikize mwenzie home.

Akaingia Joy ndani, Huku Linda kakaaa, kakaaa, nje moja haikai, mbili haisimamiiii. Akatoka baadae sanaa. Akawa ile wameonana akamuona halii akajua mambo safi tuuu. Wacha aanze kipiga vigelegele. Bsi anajisemesha unaoanaaa, hata sio ishu kubwaaa. Joy anacheka tu. Jmosi ijayo mimi. Wkafanya ratiba zao za kila siku,akamrudisha kwao Joy yeye akarudi kwao.

Kufika, Joy akamtext upo nyumbani? Linda akaona kawaida tu akamjibu nipo home, una mtoko kwani? Joy akamtext mwenziomajibu yameonesha ni HIV + kwa hio i guess NIMEATHIRIKA. Didnt want tll you then cause ungepanic na mimi nisha panic so ingekuwa sio. If you dont want to be my friend anymore i will understand.

Linda akawa anaona lile neno moja tu HIV+ tu, akaondoa gari mpaka kwa Ronny, akawalipa mateja hela ya kulinda akakumbuka chochoro zotee, kufika akazama ndani bila kugonga. Akajibwaga kitandani. Ronny anamuuliza vipi? Jasho linamtoka tu. Neno moja tu kichwani HIV + ndo lilimkaa. Simu ya Linda ikaitaaa kungalia nani anapiga MCHEPUKO WA MBWA akashangaa yuledem wa Bae wa Moro anamtafutia nini siku kama ya leo?

ITAENDELEA KESHO SAA 5.
 
dont hate the player hate the game....boys will be boys....make sure you can differentiate men from boys.
Me sio kama nawalaumu bana, yakinikuta (God forbid), ntajibebesha tu zigo langu mwenyewe mwee. me nilitaka kusema tu "there is no reward for being a bad boy", hakuna jipya
 
Hii stori ni nzuri sana. Naisubiri saa tano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…