figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 26,692
- 59,195
basi wekeni hapa huo mdahalo tuuone wenyewe manake mshaanza kutuchanganya. mia
Wana JF,
Leo alfajiri kulikuwa na mdahalo kati ya wagombea wenye nguvu kubwa katika siasa za Marekani, Mitt Romney wa Chama cha Republican na Barack Obama wa Chama cha Democrat. Mada kuu ilikuwa kuongelea sera zao za ndani ya nchi, hususani katika masuala ya Uchumi, Afya, Elimu, Nishati na Ulinzi. Katika mdahalo huo ulioanza mishale ya saa kumi na dakika tano na kuisha saa kumi na moja kasorobo alfajiri ya kuamkia leo, ni wazi kuwa mgombea urais kwa tiketi ya Republican Gavana Mitt Romney alionyesha kutulia huku akielezea sera za Chama chake kwa ufasaha na kujiamini zaidi na kujibu maswali yaliyoelekezwa kwake kwa weledi wa hali ya juu. Kwa upande mwingine, Rais anayetetea kiti hicho Barack Obama wa Democrat ameonyesha kutomudu vyema mdahalo huo huku akiongea kwa kutojiamini na kushindwa kumudu vyema maswali yaliyoelekezwa kwake kama ambavyo alivyokuwa mzungumzaji mzuri na mahiri wakati wa kampeni za Mwaka 2008. Kwa mdahalo huu wa leo, naamini hata kiwango cha kukubalika cha Mitt Romney kitaongezeka na hivyo kumpa wakati mgumu sana mtetezi wa kiti hicho Barack Obama.
Nini maoni yenu wadau?
Hata mimi naona Romney amefanya vizuri.. Wachambuzi wa BBC World News nao wanalitambua hilo. Wewe je?
Sasa sisi tusiojua kidhungu tumwamini nani? Mara Romney mara obama,kwa mama naomba Obama ashindwe mpaka kwenye uchaguzi,sizipendi sera zake kabisa hasa kwa africa na mashariki ya kati
Nimefurahi sana asubui ya leo maana Obama ni kilaza tu analeta maneno mengi wakati Romney anatoa data za uchumi.Obama alibaki anashangaaa tu.MAREKANI INAMUITAZI MTUU KAMA ROMNEY.Kwanza asilimia 70% ya wamarekani wanaamini huyu jamaa ni muislum
Mkuu nakushauri pia ufuatilie na wachambuzi wa kimataifa wanasemaje kuhusu huo mdahalo.
wachambuzi wengi wanasema Obama alimudu vema kuliko mpinzani wake.
Na mpaka sasa kwa mdahalo ule Obama ana 48% na Romney ana 46%
sasa nani hapo amegalagazwa?
Umeona jamaa alivyochukua ushindi kiulaini!
Wana JF,
Leo alfajiri kulikuwa na mdahalo kati ya wagombea wenye nguvu kubwa katika siasa za Marekani, Mitt Romney wa Chama cha Republican na Barack Obama wa Chama cha Democrat. Mada kuu ilikuwa kuongelea sera zao za ndani ya nchi, hususani katika masuala ya Uchumi, Afya, Elimu, Nishati na Ulinzi. Katika mdahalo huo ulioanza mishale ya saa kumi na dakika tano na kuisha saa kumi na moja kasorobo alfajiri ya kuamkia leo, ni wazi kuwa mgombea urais kwa tiketi ya Republican Gavana Mitt Romney alionyesha kutulia huku akielezea sera za Chama chake kwa ufasaha na kujiamini zaidi na kujibu maswali yaliyoelekezwa kwake kwa weledi wa hali ya juu. Kwa upande mwingine, Rais anayetetea kiti hicho Barack Obama wa Democrat ameonyesha kutomudu vyema mdahalo huo huku akiongea kwa kutojiamini na kushindwa kumudu vyema maswali yaliyoelekezwa kwake kama ambavyo alivyokuwa mzungumzaji mzuri na mahiri wakati wa kampeni za Mwaka 2008. Kwa mdahalo huu wa leo, naamini hata kiwango cha kukubalika cha Mitt Romney kitaongezeka na hivyo kumpa wakati mgumu sana mtetezi wa kiti hicho Barack Obama.
Nini maoni yenu wadau?
Nimefurahi sana asubui ya leo maana Obama ni kilaza tu analeta maneno mengi wakati Romney anatoa data za uchumi.Obama alibaki anashangaaa tu.MAREKANI INAMUITAZI MTUU KAMA ROMNEY.Kwanza asilimia 70% ya wamarekani wanaamini huyu jamaa ni muislum
Yaani obama alivyoanza mambo yako ya fare shot or Donald trump duh yaani obama amechemsha mnoooHata mimi naona Romney amefanya vizuri.
kuna kipindi Obama alikuwa na kigugumizi kama JK.
Hata baada ya mjadala mke wa Obama, Michele alionekana dhahiri kuwa amekuwa very disapointed wakati mke wa Romney alionekana kufurahia.
Libya libyadah, ngoja tusubiri debate nyingine tarehe 16 oct, hii nafikiri itakuwa ya international policies.
Nafasi ya obama kujipanga upya KUVUNJIKA MWIKO SI MWISHO WA UHUNZI,,!
Obama naye alitusahau sana africa, wakati wengi tulikuwa na matarajio ya mtelemko kutokana na yeye kutokea asili ya africa. hiki kipigo ni kama laana kwake!
Unazijua sera za Romney kwa hayo maeneo uliyayataja?
Kwa hiyo tatizo la Marekani ni Uislam?