The Truth behind aliens

Jack HD

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
851
1,166
Habari wanajukwaa?
Naona kichwa cha habari kitakuwa kimekuvutia na wewe pia.
Hata mimi natamani kufahamu ukweli uliojificha juu ya viumbe hivi kutoka sayari nyingine. Nilishapataga kusikia sana hususani nikiwa bado kijana mdogo kuwa viumbe hivi vilikuja duniani na kufanikiwa kutua sehemu za US. walikimbizwa na majasusi wa kimarekani lakini vyombo vyao vilikuwa na kasi kubwa na vilikuwa na uwezo wa kukata kona ya nyuzi tisini.

Sina uhakika wa habari hizi ama ni hadithi za mwalimu wa fizikia, tafadhali mwenye ujuzi zaidi hebu atujuze!!

Wasalaam!!
 
nashindwa kulijadili hili kwasababu ya kukosa "uthibitisho" kwanza sijui kama kweli wapo au hawapo! endapo mazingira yanasharabu uwepo wa viumbe wengine either wanafanana nasi au hawafanani.
hata leo angani unaweza kuona chombo usichokielewa au ni kipya kbs hiyo haimaanishi umeona alien!
hata ukiona kiumbe anaefanana na picha zinazochorwa kama alien haimaanishi umeona alien!.. hapa namaanisha kuwa kuna uongo wa aina nyingi,maneno mpk vitendo!

kwenye hili jambo kuna kuchotwa(kudanganywa) ama kuambiwa ukweli,be careful with your mind!
 
Ukiliangalia Eneo la Area 51 ambalo linahusishwa na hawa viumbe wa ajabu waishio angani wa Aliens. Eneo hili lipo katika Jimbo la Nevada nchini Marekani ambapo kama ilivyokuwa kwa Bermuda Triangle, nalo limejaa mauzauza ya kila aina. Japo ni siri kubwa lakini inaaminika kuwa wapo Aliens wanaoishi eneo hilo ambalo lina ngome kubwa ya kijeshi ambayo mlango wake wa kuingilia umetengenezwa kamba pyramid (pembetatu) na ambao umechongwa kwa alama ya jicho moja. Kuhusu uwepo wa hawa Aliens eneo hili ndipo yanapoibuka maswali mengi hasa njia ya mawasiliano wanayotumia kwa maana ya lugha au ishara. Katika eneo hili mambo mengi ya kiteknolojia yamekuwa yakishuhudiwa na watu waishio jirani na eneo hilo.
 
Katika kufanya utafiti inaelezwa kwamba wanasayansi waligundua kuwa kuna maisha nje ya Sayari ya Dunia katika Sayari ya Mars. Inaaminika kwamba kuna viumbe wanaishi katika sayari hiyo. Inatajwa kuwa, viumbe wanaoishi katika Sayari ya Mars wameendelea sana kiteknolojia kuliko binadamu. Ufahamu wao ni mkubwa mara nyingi zaidi ya ule wa wanadamu.

Serikali ya Marekani kwa kushirikiana na kituo cha anga cha NASA wanadaiwa kwamba wanafahamu ukweli wa jambo hilo lakini wanauficha kwa binadamu kwa sababu wanazijua wao wenyewe.

Kabla ya jambo hilo, kwa muda mrefu wanasayansi wamekuwa wakitafuta uwezekano wa maisha katika sayari nyingine mbali na dunia.

Kuna imani kuwa kwenye sayari hizo, huenda kuna rasilimali nyingi kwa urahisi kuliko duniani ambako binadamu wameishi maelfu ya miaka hadi sasa.

Wataalam hao wa anga wamekuwa wakifanya utafiti huo kwa muda sasa na moja ya mambo muhimu ambayo wamekuwa wakiyaangalia ni upatikanaji wa maji. Popote maji yanapopatikana, wanaamini maisha yanawezekana. Moja ya sayari ambazo wamekuwa wakiichunguza kwa miaka mingi sasa ni Sayari ya Mars ambayo ni ya nne kutoka kwenye jua. Dunia ni ya tatu.

Inaelezwa kwamba sababu kuu za kuichagua sayari hiyo tofauti na zingine ni kwamba, hali ya hewa inatofautiana kidogo sana na ya dunia.Sayari nyingine kama Mercury na Venus, zipo karibu zaidi na jua na hali ya joto iko juu kiasi kwamba hali ya maisha inaweza kuwa tabu.

Sayari ya Mars ambayo wanasayansi wanaipa jina la Sayari Nyekundu ipo karibu na dunia, hivyo ni rahisi kufika iwapo wanasayansi watathibitisha iwapo maisha yanawezekana huko.

Wanaiita sayari nyekundu kwa sababu eneo kubwa la uso wake ni wa rangi nyekundu, tofauti na nyingine zilizomo kwenye mfumo wetu wa sayari.

Hakuna mwanasayansi ambaye amethubutu kusafiri hadi kwenye sayari hiyo kutokana na ugumu wa kupata vyombo vya kuaminika, vinavyoweza kusafirisha watu kutoka duniani hadi Mars na kurudi salama.

Hata hivyo, hilo siyo tatizo kwa sababu wakibaini mazingira mazuri, utengenezaji wa vyombo hivyo hauwezi kuwapa tabu.Kazi ya uchunguzi imekuwa ikifanywa kwa vyombo maalum ambavyo havina watu lakini vina uwezo wa kuleta mawasiliano duniani.

Pia wanatumia viona mbali katika mchakato huo kuchunguza hali ilivyo kwenye sayari hiyo ambayo kumekuwapo na hisia kwamba huenda waliwahi kuishi viumbe hai mamilioni ya miaka iliyopita lakini baadaye mazingira yakabadilika na kuwa mabaya.

Uchunguzi unaonesha kuwa, Sayari ya Mars ina mabonde mengi ambayo yana kila dalili kuwa awali yalikuwa yanatiririsha maji kama ilivyo mito ya hapa duniani.

Kwa muda mrefu, wanasayansi wamekuwa wakiichukulia sayari hiyo kuwa na mazingira ya jangwa yanayotokana na ukame wa muda mrefu.

Hata hivyo, tafiti za hivi karibuni zilikuja na maelezo kwamba sayari hiyo ina kiwango kikubwa cha maji na mengi yapo mita chache kutoka uso wake.

Mmoja wa wanasayansi wanaochunguza sayari hiyo ni Profesa Jay Melosh wa Chuo Kikuu cha Purdue nchini Marekani. Yeye anasema uchunguzi huo umewapa imani siyo tu kwamba Mars ina maji bali kuna viumbe ambao siyo binadamu na bakteria ambao wanaendelea kuishi humo hadi leo hii.

Ni uchunguzi ambao wanaamini una matumaini tofauti na taarifa za uchunguzi uliopita na kizuri zaidi pia ni kubaini kuwa maji yapo kwa wingi zaidi.
Kwa sababu hiyo, wanaamini kwamba maisha yakianza kwenye Sayari ya Mars, kuna uwezekano pia binadamu wakahamia huko.

Taarifa za uwepo wa maji kwenye sayari hiyo zilitolewa kwenye mkutano wa wanasayansi wanaochunguza anga za mbali, uliofanyika nchini Australia, Juni, mwaka huu.

Moja ya dalili za uwepo wa maji ni vimondo ambavyo vimekuwa vikianguka kwa wingi kwenye uso wa sayari hiyo.

Mtaalam wa Uhandisi na Mambo ya Anga, Profesa Kathleen Howell anasema picha walizopiga maeneo ambayo vimondo vimegonga uso wa Mars, zilionesha dalili kama za mtu aliyetupa jiwe kwenye eneo lenye tope.
 
Eiyer mkuu naomba utufafanulie please hope unajua...
Mkuu

Kuhusu nijuacho ambacho pia inawezekana kikawa hakiko sahihi kwa asilimia 100 ni kwamba ninaamini Aliens wapo,labda swali la msingi ni kwamba wapo wapi....

Kwa utafiti wangu ni kwamba wapo hapa hapa duniani japokuwa kumekuwepo na dhana kuwa wanatokea nje dunia yetu hii lakini kwa ushahidi mwingi tu inaonekana wapo hapa hapa duniani....

Uwepo wa viumbe ambao wana uwezo zaidi ya binadamu siyo suala la kubishana maana kwa wale ambao wanafanya utafiti juu ya historia ya dunia hii na yale yote yaliyowahi kutokea ataweza kuyaona haya kwa urahisi kabisa....

Kundi dogo la binadamu limekuwa likipata msaada kutoka kwa viumbe ambao ni superior kwao na kusababisha maendeleo chanya na hasi kwa maelfu ya miaka....

Aliens wanaweza kusafiri kwenda maeneo tofauti huko angani na kurudi lakini pia wanaweza kukaa huko kwa muda mrefu lakini hilo halimaanishi wanatoka nje ya dunia hii....
 
Habari wanajukwaa?
Naona kichwa cha habari kitakuwa kimekuvutia na wewe pia.
Hata mimi natamani kufahamu ukweli uliojificha juu ya viumbe hivi kutoka sayari nyingine. Nilishapataga kusikia sana hususani nikiwa bado kijana mdogo kuwa viumbe hivi vilikuja duniani na kufanikiwa kutua sehemu za US. walikimbizwa na majasusi wa kimarekani lakini vyombo vyao vilikuwa na kasi kubwa na vilikuwa na uwezo wa kukata kona ya nyuzi tisini.

Sina uhakika wa habari hizi ama ni hadithi za mwalimu wa fizikia, tafadhali mwenye ujuzi zaidi hebu atujuze!!

Wasalaam!!

hakuna aliens wala hakuna sayari zenye uwezo wa kuishi viumbe,sayari zote ni nyota tu wala hazina udongo wala maji,hii dunia sio sayari,hairuki angani wala haina motion ya aina yeyote badala ya tetemeko la ardhi na iko peke yake na inawezekana kuwa ukubwa wake hauna mwisho inaendelea milele na milele wala sio duara na bahari pia ni milele.

kama kuna viumbe wanaishi basi watakuwa juu ya ardhi hii ambako sisi hatuwezi kufika na wao hawawezi kuja huku kwetu ,na hao viumbe hawatakuwa kama eliens tuaoonyeshwa kwenye movies inawezekana wakawa kama sisi tulivyo
 
Mmmmhhh Hii ni kiboko yao!!
 
Hahahahaha
 
magreat thinker katika ubora wao

Back
Top Bottom