Kusoma mambo mbalimbali na kufatilia vitu vipya ni chanzo kikuu cha Maarifa

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,861
Hapa duniani kuna madudu ya ajabu sana, tena sana, kuna maviumbe ambayo ukiyaona kwa mara ya kwanza utasema labda unaishi kwenye karne ya pili huko. Ili kwanza uyajue hayo yote, ndugu yangu jitahidi sana kutafuta maarifa.

Unajua sisi Waafrika tunashindwa sehemu ndogo sana, tunashikilia sana dini pasipo kufuatilia mambo kisomi. Waliotuletea hizi dini nao wanasoma sana, ila kwetu sisi, kwanza tunashikilia dini kuliko kusoma.

Mzazi wa kiafrika yupo radhi kumshinikiza mtoto wake aende madrasa ama kanisani kuliko shuleni kusoma, halafu baadaye ukimwambia masuala ya clonning, anakuona mchawi. Uzuri wa Wazungu ni mmoja, kila kitu wanachokifanya huwa wanaviweka kwenye filamu zao.

Mfano: Hiyo video hapo chini ni moja ya Tangazo la mwaka 2009 lililofanywa na kampuni ya HULU miaka mingi, na mtangazaji anazungumza kwa wazi kabisa kuna viumbe kazi yao ni ku-control Dunia katika vitu mbalimbali, na hakuna kitu mtafanya. Siku hizi hawafichi hata kidogo


View: https://youtu.be/TxBSPqJd2_Y?si=3hn4QOuqeWqDL7ZG

Pia nyingine unaweza kuziona hapa kwenye link 👉🏽 Alien on national TV ad

Hakuna siri kabisa, kila kitu kinawekwa wazi na kinafanyiwa kazi. Kuna mambo ambayo ukiyasikia kwanza utaziba masikio yako kwa sababu yanatisha. Kwenye kundi kule WhatsApp niliwahi kuwaambia kuhusu ugunduzi mkubwa mno mno mno uliowahi kufanyika miaka ya 80. Jamaa alibuni mashine inayoweza kuona kila kitu miaka ya nyuma kama mkanda wa video.

Baada ya kanisa Katoliki chini ya Papa kuona hilo jambo linaweza kuwa baya sana kwenye dunia hii, kanisa likachukua hicho kifaa, taarifa iliandikwa mpaka kwenye magazeti ya Italia, kifaa kipo wapi? Kwa nini kanisa limekichukua? Kanisa halikutaka kujibu chochote kile, likakaa kimya.

Kwa nini yule jamaa aliyeigiza kama Yesu alikuwa na sura ile? Je, ni kweli yesu alikuwa na sura ile? Kama ndiyo, walimuonaje? Bro! Hii dunia ina siri kubwa sana, kama hujakwenda darasani sana ama umeshikilia msaafu na biblia huwezi kuelewa kitu chochote kile, utaona kama unapigwa changa la macho.

Niliwaelezea mpaka mchizi aliyeitwa Michael Markam ambaye alitengeneza mashine ya Time Travel mwaka 1996, alipoulizwa angefanya nini endapo angerudi miaka ya nyuma, alisema angetamani sana kuwa na simu yake.

Mwaka 1997 mashine zake za Time Travel zikapotea, hakukuwa na mtu aliyejua zilipokuwa na watu walipofuatilia, miaka ya 1930 kulikuwa na habari iliyosema kuna mwili ulipatikana huko Calfornia ufukweni na ulipochunguzwa, ulikutwa ukiwa umeshika simu mkono mwake. Picha zilizoppigwa, zilionyesha alikuwa ni Mike. Unaweza kugoogle pia.

Hapa namaanisha nini? Hapa duniani kuna mambo makubwa sana yanafanyika na kama ukiyasikia utaziba masikio yako. Dini zimeletwa ili kututia hofu kufuatilia baadhi ya mambo, hatukutakiwa kusoma wala kujifunza, ili kutuzuia kwenye hilo, wakaleta dini zao.

Mwafrika hataki tena kujifunza. Mtu akisoma sana dini na akienda kuhiji Maka ama Israel tayari anajiona amemaliza kila kitu ingawa kichwani mwake anakuwa mtupu. Wayahudi wao wana sifa mbili kubwa, cha kwanza ni watu walisoma sana, wana akili mno na cha pili majamaa wana pesa balaa.

Kule unapokwenda kuhiji kwao, wenzako wamesoma sana, wenzako wana pesa sana, huyaoni haya, sijui kwa nini hutaki kusoma ndugu yangu. Unatengeneza ulimwengu wa giza pasipo kujua.

Liangalie kanisa kama Katoliki. Hawa jamaa huwa nawafagilia sana. Kwanza huwezi kuwa Padri kama huna PhD kichwani. Yaani padri yeyote utakayemtia machoni mwako, bro! Jua huyo jamaa ana PhD yake kichwani. Hujiulizi kwa nini Katoliki wanataka kila Padri awe msomi?

Wanakumbuka walivyopitwa sana na Wamisri miaka ya nyuma mpaka kuiba mavitabu katika maktaba pale Alexandria. Waliona kabisa ili uwe kiongozi bora ni lazima uwe na elimu kichwani.

Leo unasikia wazee wanaochotesha maji msikitini ama kanisani wanauana, yaani kuchotesha maji napo mauaji yanafanyika, yaani unasikia wale wazee wameshikilia dini lakini hawajasoma hata darasa la saba. Unadhani mtu kama huyu atazalisha kizazi cha aina gani? Atazalisha kile kizazi mtu akisikia mambo ya Clonning anaona kama umezungumzia jambo moja kubwa sana.

Siri ya dunia hii ipo kwenye vitabu, tafuta usome, tafuta uone dini yako ilitokea wapi, ilikuwaje huko nyuma. Leo nipo radhi kumpeleka mtoto wangu shule, akasome vizuri, ajifunze zaidi kuliko kumpeleka kanisani. Hii dunia ya sasa hivi ili usiteseke inahitaji uwe na elimu ya darasani, ili usionekane mjinga na kuutia aibu ukoo wako ni lazima usome kwanza.

Hujiulizi kwa nini mtu akiwa hajasoma halafu akapata utajiri ni lazima aingie darasani kusoma? Hujiulizi kwa nini tajiri akiwa hajasoma ni lazima awaajiri wasomi lakini si watu wa dini?

Asili ya Mwafrika hapendi kusoma, tumejengewa hivyo na wazazi wetu. Tumezaliwa katika familia ambazo zinaona dini ni bora sana kuliko elimu ya darasani. Unakuwa mkubwa, unajua sana masuala ya dini kuliko hata elimu ya dunia, mwisho wa siku ukikaa na kundi la watu unaonekana mjinga kuliko wote.

Tujitahidi sana kusoma. Kwenye simu yako, download App ya CNN, BBC, Aljazeera uwe unafuatilia habari za kimataifa, uwe unajua dunia imefikia wapi kwa sasa. Hapo ukiulizwa teknolojia gani ipo juu kwa mwaka huu, unaona kama unaonewa vile.

Mbali na kujua mengi kuhusu teknolojia, pia jifunze kujua mengi kuhusu tulipotokea, dunia imetoka wapi. Haupati pesa ila itaufanya ubongo wako kuwa na mambo mengi, hutoonekana kilaza hata kidogo.

Binadamu ana shepu ya kawaida, anakwenda hospitalini kuongezewa shepu. Yaani anapewa kitu ambacho hakuwanacho. Hapohapo ukimwambia mtu kwamba duniani kuna clonning, anakataa mpaka mishipa ya shingo inamsimama.

Hii dunia ni kama Mungu amemuachia shetani afanye anayotaka kuyafanya, na anayafanya kwa juhudi kubwa mno. Shetani ameleta teknolojia kubwa sana na amezipandikiza kwa watu na wanafanya mambo makubwa kupita kawaida.

Wale malaika walioshuka kutoka Mbinguni kipindi cha Nuhu ndiyo walisababisha haya yote, walileta elimu ambazo binadamu hakuwanazo hata kidogo, walileta uchawi, mambo ya biashara, elimu na mengine mengi.

Shetani kupitia wanachama wake ndiyo wanatupangia nini cha kufanya. Yaani wewe nenda kanisani, msikitini lakini jua maisha yako unapangiwa na wanachama wa shetani, yaani wao ndiyo wanaokupangia nini cha kufanya, yaani wao ndiyo wanakutengenezea simu zako, mitandao yako ya kijamii, yaani wao ndiyo wanakulipa pesa unapofanya biashara za mitandaoni, yaani wao ndiyo wanakusimamia na kukukataza nini cha kufanya na nini si cha kufanya.

Wao ndiyo wamekutengenezea Apps za Kurani na Biblia na kukuwekea kwenye simu yako kwa makusudi yao hapo baadaye. Yaani wao ndiyo wanakulazimisha sana uupende mpira , kubeti kuliko hata kwenda nyumba za ibada.

Yaani wao wanakulazimisha ufanye kitu chochote kile wanachokitaka. Wao wanakuingizia chuki, wanakuingizia kisirani, wao wanakuingizia roho za ajabu, na ndiyo maana ni rahisi kumchukia mtu wa mtandaoni ambaye hujawahi hata kumuona, kwa nini, tayari washakupandikizia chuki moyoni mwako.

Kuna teknolojia kubwa sana zipo mbioni kuja, hizo ni teknolojia ambazo endapo utabaki hai wakati zinatambulishwa, ndugu yangu utakuja kushangaa! Achana na ile ya Urusi ambayo unaiambia mashine unataka chakula gani na inakuandalia muda huohuo, kuna teknolojia kubwa sana zinakuja, nikikwambia, utafumba masikio yako usisikie tena.

Miaka ya tisini, kama ungekuwa unawaambia watu kutakuwa na televisheni za ukutani, magari ya umeme wangekushangaa sana. Bill Gates alipomwambia mwandishi wa habari kwamba angeleta kitu kiitwacho internet, ambapo humo watu watasikiliza hadi redio, mtangazaji alishangaa, halafu akakataa kwamba haiwezekani, leo tupo wapi?

Wazungu wanagundua mambo makubwa kwa sababu ya kusoma. Yaani wale wanasoma sana ndugu zangu, hebu jiulize, mara yako ya mwisho kusoma ilikuwa lini? Je, ni kweli unatengeneza kizazi cha usomaji ama?

Usiposoma sana, mwisho wa siku unakuja na misemo ya ajabu kwamba bahati mafungu saba......ndugu zangu sometime mnanichekesha sana. Kwa hiyo wewe sasa hivi ushapata fungu la ngapi?

Tusomeni na tuijue dunia ili tusitawaliwe kifikra.
 
Maarifa ya kweli yanaletwa na uzoefu katika utekelezaji wa mambo kwa vitendo na sio kuishia kusoma vitu vipya kila siku. Kutekeleza ideas ndio dhahabu.

Kujifunza bila utekelezaji. Uwo ni ujuaji usio na faida.
 
Maarifa ya kweli yanaletwa na uzoefu katika utekelezaji wa mambo kwa vitendo na sio kuishia kusoma vitu vipya kila siku. Kutekeleza ideas ndio dhahabu.

Kujifunza bila utekelezaji. Uwo ni ujuaji usio na faida.
Hata kama hausomi ila ukiwa ni mtu wa kutafakuri sana,na ukiwa mtu wa kutokuchukulia udogo vitu ambavyo ni vidogo basi utakuja kuona unavumbua vitu ambavyo huwezi amini.

Naamini sana hii kitu
 
Hata kama hausomi ila ukiwa ni mtu wa kutafakuri sana,na ukiwa mtu wa kutokuchukulia udogo vitu ambavyo ni vidogo basi utakuja kuona unavumbua vitu ambavyo huwezi amini.

Naamini sana hii kitu
You can say that again.
 
Hata kuishi Tanzania kuyaona majitu kama Lucas mwashambwa ni kujifunza tosha... Baada ya kumjua Lucas mwashambwa nimegundua hii dunia ina maviumbe ya kisenge sana, yaani matakataka kummae kabisa.
 
Udadisi ndio akili.

Siku hizi maarifa ni mengi sana. Ni wewe tu kuchagua kujua ama kubakia mbumbumbu.

Angalizo tu kwa wenye kubagua na kubakia na vimaarifa vichache tu vya aina fulani au kitabu fulani. Maana tazama imeandikwa: Ole wao wale wayakataaao maarifa, maana hata katika ufalme wa mbinguni watakataliwa. Hawafai kabisa popote.

Tunapaswa kuyaelewa maarifa, kuielewa dunia, maana hasira hukaa vifuani mwa wapumbavu pia.
 
Mwaka 2004 nilipata kusoma mfululizo wa riwaya za A Song of Ice and Fire kwa hakika nilipokuja kukutana na filamu za lords of the Rings nikatabua kuwa kusoma vitu vingi kunaongeza sana ufahamu.
nilianza kukusanya vitabu magetoni kwangu na mwezi wa Saba nilipata kutabu cha Timeof Contempt kutoka kwa Bwana Mkubwa Andrzej Sapkowski.
Maarifa yapo kwenye vitabu jamani, ila kuna kitabu cha The Truth About Magic: Poems, naomba Mshana Jr unisaidie mkuu :D
 
Hata kama hausomi ila ukiwa ni mtu wa kutafakuri sana,na ukiwa mtu wa kutokuchukulia udogo vitu ambavyo ni vidogo basi utakuja kuona unavumbua vitu ambavyo huwezi amini.

Naamini sana hii kitu
Mkuu, hivyo vitu vidogo vidogo ni vingi mno,ukiamua kuvichunguza sijui utaanza na lipi na kumalizia na lipi! Binafsi napenda sana kujifunza, lakini hii Hali pia inaitaji uwe na utulivu wa akili,yahani familia yako iwe stable..,kazini usiwe na contradictions zozote..,kiufupi usiwe na mambo ya kukuboa kichwani hapo ndio unaweza kukaa na kufukunyua angalau bahadhi ya mambo!

Sasa jiulize,ni sisi hambao bahadhi yetu tunapata stress kwa nauli za daladala kupanda kwa shilling 100 unafikiri tunaweza kweli kupata utulivu unaoitajika Ili uweze kujifunza?


Kitu hambacho naendelea kujutia maishani mwangu ni kutojifunza mambo mengi wakati nilipokuwa mtoto, kabla sijaingia kwenye majukumu ya kifamilia na majukumu ya kikazi,changamoto za kazini na za kifamilia zinapunguza uwezo wa kujifunza asikwambie mtu!

Lakini pia nimeitumia changamoto hii kama Fursa maana nimejipanga kwamba mwanangu wa kwanza atakapoanza kuwa na akili za kujifunza,nitahakikisha ninamjaza nondo kichwani kadri niwezavyo, maana hii elmu yangu ya form 4 itatosha kuwasukuma wanangu angalau wamalize elimu ya msingi

Kujifunza ni kitu kizuri mno, lakini je utulivu unaoitajika Ili uweze kujifunza ni wangapi tunao?

Binafsi naweza kupata angalau miezi miwili au mitatu ya kuwa stress free, baada ya mambo yatajitokeza na kuharibu kabisa uwezo wa kukoncetrate!
 
Mkuu, hivyo vitu vidogo vidogo ni vingi mno,ukiamua kuvichunguza sijui utaanza na lipi na kumalizia na lipi!
Unakimbilia wapi mkuu mpaka uanze kuwaza uwingi wake 😀😀?

Hakuna kwa kuwahi mkuu,utaratibu wa kufikiria unatumia muda sana hakuna haja ya kuwaza kwamba Mambo ni mengi no no no.




,kiufupi usiwe na mambo ya kukuboa kichwani hapo ndio unaweza kukaa na kufukunyua angalau bahadhi ya mambo!
Mkuu kama kutafakari ni hobby yako basi hautaweza kuwa destructed na mambo ya kawaida kama kukosa nauli n.k

Mimi binafsi nina stress kibao za maisha lakini kwa kuwa mijadala ndio hobby basi hata iwe vipi nikikuta mjadala mtaani wenye tafakuri nitasahau shida zote na kuanza kuchangia hapo.

So changamoto sio kigezo cha kwamba mtu asiwe mtafakariji,bali ksma ni hobby yake hawezi kukwamishwa na changamoto hizo.
 
Back
Top Bottom