hansrashid
Senior Member
- Nov 26, 2018
- 143
- 111
Hakuna uhai kwenye sayari ya Mirihi (Mars). Hii imani ilianza wakati watu waliona mistari kwenye darubini usoni mwa Mirihi kwenye karne ya 19. Waliamini kumbe ni mefereji ya umwagiliaji.
Tangu kupata darubini nzuri zaidi na tangu kutembelea sayari kwa vipimaanga inajulikana hakuna mistari wala mifereji wala uhai wowote.
Kuna dalili kwamba Mirihi -ambayo leo hii ni jangwa tupu- ilikuwa na maji na mito miaka milioni iliyopita. Sasa kuna mpango kuwa Marsrover (gari lenye vifaa vya uchunguzi) inayoandaliwa sasa kutumwa Mirihi itachimba shimo na kufanya utafiti wa udongo kama kuna dalili za bakteria za zamani.
Picha kama hizi zimeleta hoja kuwa maumbo yanyaoonekana ni ya delta, yaani mdomo wa mto unapoishia katika ziwa au bahari. Hapa asili ya imani Mirihi ilikuwa na maji ya kutiririka kwenye uso wake, miaka milioni iliyopita.


