The SGR, War, MAGUFUGAME Kidedea, MUSEVENYATTA Mikono Juu Kukubali Matokeo!, Magufuli Shujaa, Apiga Bao Kupiga Tanchi!. Hongera JPM Kwa Kuona Mbali!.

Magufuli mwana wa Africa

Anashambulia km Barcelona

Tuna Rais bwana

Kweli wajinga ndio waliwao, hii post ya Paskali kwa asiyejua anaweza dhania anasifia kumbe anasanifu. Treni ya Kenya Ina afadhali maana wangalau inatembea, hii ya kwetu hata Morogoro haijaanza kwenda, na haifahamiki kama itavuka Morogoro itakapoanza. Rejea hapo anaposema huenda hizo ndege zikaleta faida ya ajabu huko mbele, ina maana mpaka saa ni hola.
 

Reli ya Tanga imefufuliwa au unauziwa maneno na wanasiasa na ww unakubali? Nenda kaangalie reli ya Tanga-Arusha kisha uje ulete mrejesho hapa jukwaani. Toka nje ya box unaingizwa mjini boss.
 
Reli ya Tanga imefufuliwa au unauziwa maneno na wanasiasa na ww unakubali? Nenda kaangalie reli ya Tanga-Arusha kisha uje ulete mrejesho hapa jukwaani. Toka nje ya box unaingizwa mjini boss.
Reli iliyofufuliwa ni ile kutoka Tanga - Moshi.

Moshi - Arusha bado kwa kuwa inabidi ifumuliwe yote na kuwekwa reli mpya yenye kubeba mzigo mzito.
 

Hizi ni sifa za kijinga, ana uthubutu hilo ni kweli lakini hajui madhara ya uthubutu wake. Hana mpango wa kujipendekeza au huko kwa kujipendekeza hawakubaliani na uchezeaji wake wa demokrasia? Hao wazungu hawatoi msaada kwa mwizi wa kura.

Ni kweli mambo yanaenda, lakini unajua deni la taifa mpaka sasa limekua kwa kiasi gani? Hiyo miradi ina uhakika wa kulipa hilo deni, unajua terms za ulipaji wa hayo madeni?
 
Reli iliyofufuliwa ni ile kutoka Tanga - Moshi.

Moshi - Arusha bado kwa kuwa inabidi ifumuliwe yote na kuwekwa reli mpya yenye kubeba mzigo mzito.

Niliposema Tanga+Arusha nimemaanisha ni pamoja na Tanga- mpaka moshi nakuendelea. Ndio maana na kuambia nitajie lini kuna treni ya Tanga- moshi nikapakie mzigo wangu. Narudia tena, toka nje ya box unaingizwa mjini na wanasiasa wasaka kiki, hakuna kinachoendelea kwenye hiyo reli.
 

Sio sofa za kijinga. Waafrika wengi hatuna hata confidence ya kufanya yale ambayo tuna utaalamu nayo sababu ya kuogopa wazungu wanasemaje au wananionaje.
JPM sets a new tone. Hata kama wengi hawakubaliani naye.
One thing for sure, we needed this pill to cure us from our illness. Ipo siku tutakaa sawa na kufanya tofauti. Tumezubaa sana
 
Pascal punguza njaa ndugu yangu maana wote tuna njaa lkn tunaridhika na hali zetu kwani umasikini siyo kilema
 
Pascal kweli kuna mambo ya msingi yanampoteza.

1:Ukabila

2:Hali ya kiuchumi aliyo nayo inamlazimisha kuwa hivyo anavyofanya ili alazimishe kakake ampatie angalau ukuu wa wilaya.

3:Umri unazidi kumtupa mkono sana wakati familia inayo mtegemea bado ni kubwa
 
Akikujibu naomba unitag
 
Ngada
 

Hatusemi kuogopa wazungu, bali wazungu hawakwepeki. Sina tatizo na uthubutu wake, je huo uthubutu wake una mtiririko mzuri? Mfano kwa sasa anajenga miradi miwili kwa wakati mmoja inayozidi 13t+, ni dhahiri hawezi kutekeleza miradi hiyo kwa fedha za ndani bila mikopo. Je unajua mikopo anayochukua inasemaje?

Uzoefu unaonyesha viongozi wa kiafrika wana tabia ya kukopa fedha ili kufanya miradi ya kusaka political millage. Je kuna mpaka mpango mzuri wa kulipa hizo pesa? Je kwa mfano huo mradi wa reli, ni dhahiri kutokana na raslimali muda sioni kama anaweza kumaliza hiyo reli kabla ya muda wake kuisha, huenda ikaishia Dodoma, je atakayeingia ataweza kuiendeleza? Ikiishia Dodoma italipa kiwango cha kuweza kulipa deni?
 
Hapa sasa iv tunavoongea sgr ya kenya ipo naivasha maana yake inaweza fanya kazi tokea mombasa hadi naivasha km 579.

Lakin hadi sasa sie watanzania sgr yetu haijaanza kufanya kazi dar to moro 200 km, then wewe pasco unakuja kusifia hata hueleweki
 

Kuna mtu ka-hack account ya huyu bwana!

Matamahuluku haya!
 

Ni hivi, ww ni baadhi ya watanzania mnaolishwa propaganda mfu na kuamini utapeli wa wanasiasa. Hivi ninavyozungumza niko hapa Tanga, nina mzigo ninataka kuupeleka moshi, nitajie kesho, jumamosi au jumapili kuna treni ya saa ngapi nikapakie huo mzigo? Toka nje ya box unaingizwa mjini na wanasiasa wasaka kiki. Nilijua tu unaongea jambo usilolijua ndio maana unasema treni ya Tanga-moshi inafanya kazi. Kama jambo hulijui kaa kimya maana utachekesha walionuna.
 
Mbona hiyo habari aliyoileta sijaona siasa wala mwana siasa, nimeona Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement Mkoani Tanga Bw.Reinhardt Swart. Akiongea na waandiahi wa habari.

wewe utakuwa na chuki binafsi na wala hiyo habari hujaisoma.

ulitumbuliwa wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…