The Second Door (Tamthilia)

The Second Door (Tamthilia)

Ipigie kura simuizi hii

  • Nzuri Sana

    Votes: 9 56.3%
  • Inafaa Kusomwa

    Votes: 5 31.3%
  • Yakawaida

    Votes: 0 0.0%
  • Sijaisoma

    Votes: 2 12.5%

  • Total voters
    16
JamiiForum fursa hiyo upewe nini sasa

Baraaa! Lakinin beth nimemwambia Asubiri nikiiandika mpaka mwisho. nisije kushindwa kuimalizia halafu ikala kwake, then since wazo lake lilikua ni kuiondoa hii story hapa JF, mimi nitaingia uvivu kuiandika kwani hapa watu kama everlenk wananisaidia kuiboresha.
 
Hongera mwaya, story Inasisimua sana, can't wait for the next episode

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
ushauri mtunz nadhani ni nzur zaid ukianza new episode andika iv
Mfano:

THE SECOND DOOR -4
badala ya kuanza maelezo afu neno episode - 4 unalikuta ndan ndan ni ushsur tu other wise hadith ni tam sana
 
ushauri mtunz nadhani ni nzur zaid ukianza new episode andika iv
Mfano:

THE SECOND DOOR -4
badala ya kuanza maelezo afu neno episode - 4 unalikuta ndan ndan ni ushsur tu other wise hadith ni tam sana

Nashukuru sana kwa ushauri from next Episode Nitaufanyia kazi in a Beautiful Way. Enyoy the Story dada Anna.
 
MAPITIO YA TAMTHILIA; Kaeni mkao wa kula kwa ajili ya Episode No 6.

Kikosi cha Rweyemamu kinafanikiwa kujua mahali alipo Brenda na kujua kuwa Brenda hakuwa amepoteza maisha, sasa kinajipanga na kwenda kuvamia mahali alipokuwa mrembo huyo, What is next? watch Out for Episode No 6 jioni ya leo.

Jana after church nilikua invited na msomaji wangu mmoja anaishi tabata, niliinjoy sana kukuta familia nzima inafatilia Tamthilia hii, Lakini kikubwa zaidi the way walivyokuwa wakiizungumzia story hii ilinionesha jinsi wasomaji wangu wanavyo vutiwa na mtiririko wa matukio. Mwenyeji wangu hakutaka kunitajia ID yake ya hapa Jamvini hivyo nitashindwa kumtaja lakini Big up sana kwake.

Mwisho, naomba niwathibitishie kuwa Hii stori ndio kwanza inaanza, bado kabisa muda wa kusema theme ya hii story baadhi wanasema kuwa ni story ya Action na mapenzi kidogo, Trust me idea ya simulizi hii ni Action kidogo sana na Mapenzi mazito, utathibitisha hilo kadri tutakavyoendelea mbele na story hii. Ok nawatakia asubuhi njema na mafanikio kwenye shughuli zenu za kutwa nzima.

NAWAPENDA SANA.
 
Endelea na Episode 6, tafadhali
Simulizi ni nzuri sana

MAPITIO YA TAMTHILIA; Kaeni mkao wa kula kwa ajili ya Episode No 6.

Kikosi cha Rweyemamu kinafanikiwa kujua mahali alipo Brenda na kujua kuwa Brenda hakuwa amepoteza maisha, sasa kinajipanga na kwenda kuvamia mahali alipokuwa mrembo huyo, What is next? watch Out for Episode No 6 jioni ya leo.

Jana after church nilikua invited na msomaji wangu mmoja anaishi tabata, niliinjoy sana kukuta familia nzima inafatilia Tamthilia hii, Lakini kikubwa zaidi the way walivyokuwa wakiizungumzia story hii ilinionesha jinsi wasomaji wangu wanavyo vutiwa na mtiririko wa matukio. Mwenyeji wangu hakutaka kunitajia ID yake ya hapa Jamvini hivyo nitashindwa kumtaja lakini Big up sana kwake.

Mwisho, naomba niwathibitishie kuwa Hii stori ndio kwanza inaanza, bado kabisa muda wa kusema theme ya hii story baadhi wanasema kuwa ni story ya Action na mapenzi kidogo, Trust me idea ya simulizi hii ni Action kidogo sana na Mapenzi mazito, utathibitisha hilo kadri tutakavyoendelea mbele na story hii. Ok nawatakia asubuhi njema na mafanikio kwenye shughuli zenu za kutwa nzima.

NAWAPENDA SANA.
 
mapitio ya tamthilia; kaeni mkao wa kula kwa ajili ya episode no 6.

kikosi cha rweyemamu kinafanikiwa kujua mahali alipo brenda na kujua kuwa brenda hakuwa amepoteza maisha, sasa kinajipanga na kwenda kuvamia mahali alipokuwa mrembo huyo, what is next? Watch out for episode no 6 jioni ya leo.

Jana after church nilikua invited na msomaji wangu mmoja anaishi tabata, niliinjoy sana kukuta familia nzima inafatilia tamthilia hii, lakini kikubwa zaidi the way walivyokuwa wakiizungumzia story hii ilinionesha jinsi wasomaji wangu wanavyo vutiwa na mtiririko wa matukio. Mwenyeji wangu hakutaka kunitajia id yake ya hapa jamvini hivyo nitashindwa kumtaja lakini big up sana kwake.

Mwisho, naomba niwathibitishie kuwa hii stori ndio kwanza inaanza, bado kabisa muda wa kusema theme ya hii story baadhi wanasema kuwa ni story ya action na mapenzi kidogo, trust me idea ya simulizi hii ni action kidogo sana na mapenzi mazito, utathibitisha hilo kadri tutakavyoendelea mbele na story hii. Ok nawatakia asubuhi njema na mafanikio kwenye shughuli zenu za kutwa nzima.

Nawapenda sana.

i like it am your follower , ila mi napenda upate chochote kwenye haya maandishi yako andaa kitabu utuuzie tutanunua kwa fujo, fulsa zenyewe ndo hizi,

talents pays more than proffessional bwanaaaaaaaa
 
i like it am your follower , ila mi napenda upate chochote kwenye haya maandishi yako andaa kitabu utuuzie tutanunua kwa fujo, fulsa zenyewe ndo hizi,

talents pays more than proffessional bwanaaaaaaaa

Prospa thankyu sana, I promise nitalifanyia kazi any how
 
MAPITIO YA TAMTHILIA; Kaeni mkao wa kula kwa ajili ya Episode No 6.

Kikosi cha Rweyemamu kinafanikiwa kujua mahali alipo Brenda na kujua kuwa Brenda hakuwa amepoteza maisha, sasa kinajipanga na kwenda kuvamia mahali alipokuwa mrembo huyo, What is next? watch Out for Episode No 6 jioni ya leo.

Jana after church nilikua invited na msomaji wangu mmoja anaishi tabata, niliinjoy sana kukuta familia nzima inafatilia Tamthilia hii, Lakini kikubwa zaidi the way walivyokuwa wakiizungumzia story hii ilinionesha jinsi wasomaji wangu wanavyo vutiwa na mtiririko wa matukio. Mwenyeji wangu hakutaka kunitajia ID yake ya hapa Jamvini hivyo nitashindwa kumtaja lakini Big up sana kwake.

Mwisho, naomba niwathibitishie kuwa Hii stori ndio kwanza inaanza, bado kabisa muda wa kusema theme ya hii story baadhi wanasema kuwa ni story ya Action na mapenzi kidogo, Trust me idea ya simulizi hii ni Action kidogo sana na Mapenzi mazito, utathibitisha hilo kadri tutakavyoendelea mbele na story hii. Ok nawatakia asubuhi njema na mafanikio kwenye shughuli zenu za kutwa nzima.

NAWAPENDA SANA.

Vizuri sana JamiiForum nadhani utaanza kuamini maneno yangu,big up!!! Ufaidi na mengine mengi mazuri,hiyo ni lulu itunze usiikalie ifanye pesa ikutunze,nasubiri kwa hamu zote episode 6.
 
Last edited by a moderator:
........mtunzi, kuna suala la kuchanganya majina na kama si mfuatiliaji mzuri wa tamthilia hii anaweza jikanganya. Utunzi mzuri na unaovutia, kila muda naangalia kifuatacho ni nini
 
........mtunzi, kuna suala la kuchanganya majina na kama si mfuatiliaji mzuri wa tamthilia hii anaweza jikanganya. Utunzi mzuri na unaovutia, kila muda naangalia kifuatacho ni nini

Kweli kaka, najitahidi sana kwa kulifanyia kazi hilo, nitajitahidi zaidi niondoe kabisa hilo tatizo
 
Nmesoma zote 2day na nimekukubali mkuuu ,keep it up Ninja ,ni mpenzi wa hadith n mtunz kiaina, ktk story nying nilizosoma wengi huwa ni fupi mno bt urz unajitahid ni ndefu kiasi mtu anarizka kabisa na unasikiliza sana ushauri wa wasomaji wako humu jf tofauti na watunzi wengine wanao post story zao humu ,kwa hili nakupa hongera sana na km siku moja utamua ku make bussiness utapata mafanikio cuz watu wengi wamekupenda seemz. Big up ninja JamiiForum

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:

The Second Door Episode-6

Habari gani mpenzi msomaji, ni matumaini yangu kuwa umzima buheri wa afya. Leo tunaenda kuendelea na Episode ya 6 kwenye Tamthilia yako uipendayo ya The Second Door, na moja kwa moja tunaenda kuanzia kwenye familia ya Brenda. Mama yake mzazi na Brenda, baada ya kuona ni zaidi ya siku 2 sasa zimepita, bila kuwa na mawasiliano yoyote na mziwanda wake. Anaamua kumfata nyumbani kwake, Baada ya kufika kwa Brenda anakuta nyumba hiyo ikiwa imefungawa na mazingira yote yakiwa kimya. Mama huyo ambae alikuwa anampenda sana mwanae anapata hasira kwa kuhisi pengine binti yake inawezekana akawa amesafiri nje ya nchi bila kumwambia, na aliweza kuwaza hivyo kutokana na namba zote za Brenda kuwa hazipatikani, aliamini kuwa endapo angekuwa nchini basi lazima angewasiliana nae kwenye simu.

Profesa Rweyemamu naye, akiwa ametoka kuvurugwa na Ustadh, anaamua kutomwamini, kwani katika fikra za kawaida,yeye alishagundua kuwa mwenzake ambaye Ustadh alimzungumzia na kusema ndio nuru alikuwa ni Frank, na Rweyemamu licha ya kwamba alikuwa akifahamu, na kukubaliana na ukweli kuwa Frank alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kufikiria, yeye aliamini kuwa uwezo wa kimadaraka, na kiuchumi alio nao unaweza kumuweka juu endapo ushindani wowote utatokea baina yake na Frank, mambo yote haya ambayo Rweyemamu aliendelea kutafakari akiwa ofisini kwake, yalidhihirisha ni jinsi gani Proffessa huyu alivyokuwa akimhofia Frank.
Akiwa anaendelea kutafakari mawili matatu, mara Watu wake wanaingia. Wanasalimiana kisha wanaanza kumpa ripoti ya kazi ya kumtafuta Brenda. mmoja kati yao ambae alikua akifahamika kwa jina la Bosko anasema. "Bosi, Tumefanikiwa kufahamu mahali alipo Brenda, lakini habari zenye uhakika kabisa ni kwamba Brender ni mzima wa afya", Kauli hiyo inamstua Profesa, ana uliza kwa mshangao, "What! Mnauhakika nyinyi?" Bosko anajibu kwa kijiamini, "Tunauhakika Bosi, na kama ulivyosema jana kwenye kikao, kuna mtu ambae amemficha". Kimya kifupi kinatanda, Rweyemamu anaonekana akifikiria jambo kwa nguvu, muda huu anaanza kuunganisha matukio Tangu asikie taarifa za kuwepo kwa mtu alietaka kukata rufaa kwenye hukumu ya Tariki, anaoanisha kutoweka ghafla kwa Brenda mara tu wao walipo toka eneo lile, kwa haraka haraka pia anafikiria ujio wa Frank ofisini kwake na kauli alizozitoa. Wakati wote wakiwa wanamtizama profesa wakati anatafakari jambo. Ghafla mmoja wao ambae alikuwa anaitwa Lugano, anaonesha mstuko mkubwa na kutanua mikono huku akiashiria wote wakae kimya kwani kunajambo tata linaendelea, mpenzi msomaji kama unavyofahamu, Frank alikuwa ameweka kile kifaa cha DMR pale kwenye meza ya Rweyemamu, na muda huo frank akiwa kwenye chumba alichopanga hotelini, alikuwa akiendelea kufatilia kwa makini mazungumzo yote yaliyokuwa yakiendelea ofini kwa Rweyemamu. Na kilichotokea muda huo na kusababisha Lugano kuwastua wenzake ni alarm nyembamba sana ambayo kifaa hicho huwa kinatoa kila baada ya kutuma taarifa zenye ujazo Fulani. Alarm hiyo ni nyembamba kiasi kwamba mtu anaeweza kuisikia ni mtu ambae anakifahamu vizuri kifaa hicho na jinsi kinavyofanya kazi.

Mara baada ya lugano kuwastua wote Rweyemamu anauliza,"vipi! Nini kwani?", Lugano anajibu, "Kunamtu amepandikiza DMR humu ofisini". Neno DMR linaonekana kuwa msamiati kwa kila mmoja mle ndani, Mmoja wao anajitoa muhanga na kuuliza, "Ndio kitu gani hicho?". Lugano huku akifahamu wazi kuwa kitendo cha kuendelea kuzungumza chochote ni kuendelea kufanikisha malengo ya jasusi ambae alikuwa amepandikiza kifaa hicho humo ndani, hivyo kwa kufahamu hilo, Lugano badala ya kujibu swali aliloulizwa anasema, "Wait! " kisha anaanza kupapasa maeneo ya chini kuzunguka ile meza inakuwa sio kazi nyepesi kwa Lugano kufahamu kifaa hicho kilitoa sauti kutokea wapi kwani kwa jinsi sauti ya kifaa hicho inavyotoka hatakama imelia kwenye mfuko wa shati huwezi kugundua. Kwa sekunde kazaa Rweyemamu anaweza kukumbuka vitendo vya Frank kipindi alichokuwana amekaa mle ofisini kisha ananyanyuka kwenda kupekua kiti alichokuwa amekalia Frank. Rweyemamu anakagua kwa ustadi mkubwa kile kiti, wakati akiwa anaendelea kukagua kiti anaona kidude kidogo kikiwa kimenasia chini ya meza, anakitoa na kumuonesha Lugano. Lugano anakichukua na kukiminya kisha kina jizima.

Frank pale alipokuwa anapata hofu kubwa, kwanza ilitokana na kifaa kilichokuwa kikimpa taarifa kuzimwa, lakini pia kifaa hicho kinazimwa wakati kundi la Rweyemamu likidai kufahamu alipokuwa Brenda, Frank alitegemea kile kiDMR kingemsaidia kusikia sehemu ambayo wangeitaja ili imsaidie kufahamu kama ni kweli walikuwa wamegundua Brenda alipo, lakini pia angeweza kusikia ni kasi gani watakayotumia kwenda kuvamia pale alipo. Hayo yote yanamfanya Frank akune kichwa na kuwazua cha kufanya haraka haraka.

Huku ofisini Kwa Rweyemamu, baada ya kufanikisha kutambua uwepo wa siri wa ile DMR na kuizima, Lugano anasema, "Hiki ni kifaa cha kurekodia sauti, kunamtu amekipandikiza humu ndani". Rweyemamu anataka kuzungumza kitu lakini kabla hajasema simu yake inaita, Rweyemamu anapokea simu hiyo ambayo inampa taarifa za kutakiwa kusafiri na waziri wa katiba na sheria kwenda Dodoma, Baada ya kupokea simu hiyo, Rweyemamu anauliza, "Mmepangaje kuhusu Brenda?" swali hilo linafanya wote wanatizamana, kana kwamba walikua wakitegeana kujibu kulijibu, lakini kutizamana huko ulikua ni mshangao kuona jinsi ambavyo bosi wao anapuuzia kugundulika kwa ile DMR, wao hawakujua kuwa bosi wao alikua ameshajua mtu ambae alikuwa ameipandikiza mle ofisini. Lakini pia Rweyemamu hakutaka kusimulia chochote kinachoendelea baina yake na Frank.

Bosko anajibu swali ambalo liliulizwa na Rweyemamu, kwa kusema "tumepanga kufanya mawasiliano na wenzetu wa polisi ili tuongeze nguvu ya kwenda eneo la tukio" kusikia kauli hiyo Rweyemamu anasema,"Hapana, hakuna sababu ya kuwashirikisha polisi" baada ya kusema hivyo kimya cha sekunde kadhaa kinatanda, kisha Rweyemamu anasema, "Namjua mtu aliemtorosha siku ile, ni mshenzi mmoja anajifanya anaakili sana anaitwa Samba, kuweni makini sana na swala hili " Kauli hiyo inajibiwa na lugano kwa kujiamini anasema, "Bosi! Aliyemtorosha Brenda ni Mwanamke sio mwanaume", huku taarifa hiyo ikimfanya apigwe na Butwaa Rweyemamu anauliza kwa mshangao, "Kweli!" kisha Bosco anamjibu kwa kumwambia,"tunauhakika na hilo bosi, tena mwanamke huyo alimbeba Brenda mgongoni wakati anaondoka nae, hii inaonesha pia nae ni Bint mdogo tu" Rweyemamu anaonekana kutoridhishwa na maelezo hayo kisha anasema, "Wasiwasi wangu ni kwamba msije mkatumia akili na nguvu zisizokuwa sahihi, kwasababu kama ni Samba ninaewaeleza mimi, itawapashida, anakitabia ka kujifanya mwerevu sana, hivyo hakikisheni msije mkafanya makosa ya kutumia nyavu za pelage kuvulia papa. Ila kama ni binti tu, kama jinsi mnavyodai naamini itakuwa kazi nyepesi". Kauli hiyo ilikuwa inawapa taadhali kuwa wasije wakajiloga kutumia nguvu na akili kidogo kwenda kumchukua Brenda endapo yupo mikononi mwa Frank.

Mpenzi msomaji, Maficho ambayo Brenda alikua amehifadhiwa kwa ajili ya kupata matibabu ilikua ni kwenye Hosteli ya kanisa ambayo ilikuwa nje kidogo ya mji, kutokana na ukubwa wa hosteli hiyo ilikuwa inachukua hata wafanyabiashara na wasafiri waliokuwa wakifika Jijini Dar es Salaam na kuhitaji mahali pa kupumzika penye utulivu na ustaarabu.

Tukirudi kwa Frank, yeye mara baada ya kuona ishara kuwa kundi la Rweyemamu linaweza kufika pale hosteli muda wowote, anaamua kutafuta kambi nyingine ya kumhamishia Brenda. wakati akiwa anaendelea kuzunguka kwenye mitaa mbali mbali pembezoni mwa jiji, kikosi cha Rweyemamu kilikuwa tayari kimeshajisuka kwaajili ya kwenda kumchukua Brenda, Lakini mbali na hayo Rweyemamu alikuwa amewaagiza kukamata watu wote watakao kutwa nae na kuwafungulia mashtaka, ya utekaji nyara na kuhatarisha maisha ya mtu, na mashtaka haya yalileta maana zaidi kwakuwa Brenda alitoweka akiwa na hali mbaya sana, hivyo basi kitendo cha kumchukua na kumuweka mafichoni badala ya kumpeleka hospitali ni kuhatarisha uhai wake. Kikosi hiki kikiwa kinajiandaa kuelekea hosteli, Rweyemamu anaingia kwenye msafara wa Waziri kuelekea Bungeni mjini Dodoma, safari ambayo aliwaahidi watu wake kuwa anaweza kurudi kesho yake au siku inayofata.

Baada ya kuhangaika kwa muda, Safari hii Frank anapata chumba kikubwa kwenye gest ya mgahawa wa wahindi iliyopo kati kati ya jiji. Frank anaiamini gest hiyo kwakuwa, ni gest ambayo imezoeleka kuwa wanaofika hapo huwa ni wahindi pekee, hata chakula kinachopatikana mahali hapo ni aina ya chakula ambacho huwa kinatumiwa na mabaniani, hivyo isingekuwa rahisi Kundi la rweyemamu kuhisi kuwa Brenda anaweza kuwa hapo.

Kundi la Rweyemamu linaingia Hosteli, na ndani ya muda huu Frank ndio alikuwa anatoka kufanya makubaliano na wahindi na kulipia chumba. Japokuwa frank alihisi kwamba muda wowote polisi wangeweza kuingia eneo la hosteli na kumkamata Dokta roby kisha kumchukua Brenda, Hakufikiria kabisa kuwa muda huu askari hao watakuwa tayari wamefika Pale hosteli, hosteli ambayo ilikuwa umbali wa zaidi ya Dakika 45 kutoka kwenye mgahawa wa wahindi alikokuwa frank, na hii ni endapo ukitumia usafiri binafsi na njiani kukawa hakuna foleni, ila kutokana na tatizo la foleni zisizotabilika, inaweza kuchukua mpaka masaa2. Kabla hajapanda gari kuelekea hosteli frank anampigia simu Dokta Roby na kumtaarifu kuwa ajiandae anaenda kuwachukua wabadilishe makazi, baada ya kumpa taarifa hiyo, frank anaingia supermarket na kutizama chochote aweke tumboni kwani muda huo tumbo lilianza kumfurukuta kwa njaa.
Pale hosteli Wanaonekana Jamaa wawili kati ya lile kundi la Rweyemamu wakifanya Doria isiyokuwa Rasmi, wanajaribu kutizama huku na kule huku wakiyasoma mazingira. Kumbuka jamaa hawa walikuwa wanajua mpaka namba ya chumba ambacho Dokta Roby na Brenda walikuwa wanakitumia.
Mpenzi msomaji, Frank yupo super market na kundi zima la vibaraka wa Mh Profesa Rweyemamu, Limesha anza kuwasili eneo la tukio, ndani ya kipindi hicho Dokta roby anaamua kumtundikia dripu moja mgonjwa wake kabla ya kuanza safari ya kuelekea kwenya eneo jipya, Je ni kitu gani Kitaendelea kwenye hosteli wakati Frank na Dokta wakiwa hawana hata Moja?

Great!..... Acha mimi niishie Hapa Katika Episode Hii ya 6. Mpaka wakati mwingine tutakapoendelea kwenye Episode Namba 7, kama imekuvutia Episode Hii ya 6, Fanya vitu viwili tu ili nijue bonyeza like, au toa comment. Pia wahariri wangu wa kujitolea kabisa nawashukuru sana kwa kuendelea kupendekeza maboresho tofauti tofauti mungu awape nguvu tuendelee kuwa pamoja.
SHUKRANI


[TABLE="class: outer_border, width: 800, align: center"]
[TR]
[TD][TABLE="class: grid, width: 750, align: center"]
[TR]
[TD]View attachment 159324[/TD]
[TD]................................
View attachment 159325

View attachment 159327
[/TD]
[TD]View attachment 159326[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="width: 800, align: center"]
[TR]
[TD="align: left"]
magicHand Community

friends, sasa unachaguzi
nyingi zaidi za kuamua ni jinsi gani usome
au usikilize Riwaya hii ya The Second
Door. magicHand ni jumuia ya Wasomaji
wa simulizi hii kutoka JamiiForum,
FACEBOOK reverbNation pamoja na
WATTPAD , Na ili kuweka wepesi kufatilia
Tamthilia hii nimeamua kutumia wattpad
pamoja na kutengeneza Android App
watpadd ni kwa ajili ya wale wanaotumia
simu kusoma simulizi hii, na Android app
ambayo nimeitengeneza kwa msaada wa
reverbNation Platform ni kwaajili ya
kukuwezesha kusikiliza simulizi hii kwenye
simu yako ya android.
[/TD]
[TD] Soma kupitia Wattpad

Kama wewe umekuwa mpenzi wa simulizi
Hii kwa njia ya usomaji, njia bora kabisa ya
kusoma simulizi kupitia simu, ni kwa kutumia
application ya wattpad. Application
ambayo inawatumiaji zaidi ya
billioni moja Duniani, hivyo
kama kweli wewe
ni mpenzi wa kusoma simulizi ungana na
wasomaji wengine kwa kuanza leo
kutumia Application hii kusoma
simulizi yako uipendayo ya
THE SECOND DOOR.
ili kuanza kusoma the second door
kupitia wattpad kwenye simu yako
bonyeza picha ya wattpad hapo juu
[/TD]
[TD] Android Application

magicHand ni
Android application maalum
kabisa inayokuwezesha
kusikiliza simulizi za
riwaya za kiswahili,
sikiliza Tamthilia upendayo
kama unasikiliza kipindi
kizuri cha redio, moja kwa
moja kwenye simu yako.
mimi ninashauri sana
ufatilie simulizi zangu kwa
kupitia application hii.
ili uweze download
MagicHand Android App
bonyeza oicha hapo juu.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]








 
da nimesikiliza you have a nice voice ina mvuto wa kuisikiliza kama ilivyo story yenyewe ,

lakini kwanini usiwauzie hata bongo movi these ideas nilimsikia JB wa bongo movi anasema bongo movi hawana waandishi wa stories sasa nadhan wewe ni suluhisho jaribu kumtafuta akupe dili.
 
da nimesikiliza you have a nice voice ina mvuto wa kuisikiliza kama ilivyo story yenyewe ,

lakini kwanini usiwauzie hata bongo movi these ideas nilimsikia JB wa bongo movi anasema bongo movi hawana waandishi wa stories sasa nadhan wewe ni suluhisho jaribu kumtafuta akupe dili.

Prospa umenikuna sana kunitajia huyo mtu, namheshimu huyo jamaa kupita maelezo let me tell you this, JB ni kati ya watu ambao walinielekeza jinsi ya kufanya uandishi wa story kwa kukaa kitako na mimi zaidi ya lisaa limoja. tena nikiwa simjui wala hanijui, ofcoz hakuwa star sana kipindi kile, ila kwa moyo ambao alinionesha that day naamini jamaa hawezi kuwa amebadilika hata kama amekuwa top star. Anamuheshimu kila mmoja bila kitizama wapi ametokea, anaumrigani, rangi, yupoje nk. leo kesho akinipa nafasi nimuandikie filam au Tamthilia, prospa kutokana na wema alionifanyia nakuahidi mungu atanipa nguvu nitafanya kitu ambacho hakijawahi kufanywa kwenye makaratasi yoyote hapa tz.

nakumbuka nilipomaliza shule nilimuandikiaga story nzuri sana ya comed lakini kwakuwa nilipoteza namba yake nilishindwa kupata na nilimtafuta bila mafanikio

sasa acha hili liwe tangazo rasmi kwamba, Kama kunamtu yoyote anamfahamu JB, amwambie mwanafunzi wa sekondary ambae aliwahi kunifundisha jinsi ya kuandika story tukiwa ndani ya duka la madawa ubungo Liverside. anamtafuta ampe zawadi.

White heart Jacob Steven. Mungu ampe maisha marefu na yenye mafanikio zaidi.

Bongo movie ni kweli story zetu zina shida prospa. na mtu yoyote akitaka kuthibitisha hilo ajaribu kutizama hata tamthilia moja ya kifilipino au ya kikorea, pengine unaweza kuwa mwisho wako wa kutizama filamu za kibongo. watu wanaandika, capital wanaonesha Iljimae sasa hivi nilipoiona hii tamthilia first time nilisema afadhari niliacha kuandika story kwani nikajiona sijui hata kuandika mkasa mmoja kwenye story.

Hata hivyo natamani sana siku nifanye kazi naa Bongo movie.
 
  • Thanks
Reactions: ram
Uko juu kijana
Ngoja tuone kama watatoka salama hapo hostel
 
View attachment 159648

Jana Nimezindua FaceBook Fan Page. Kama Wewe ni Mpenzi Wa FaceBook Ungana na Wenzio huko.
Enjoy(ili kutembelea Page hii Bonyeza Picha).

Note: Kesho mapema sana Episode No 7
inaendelea ili tuweze kufahamu nini
kulijiri mara baada Frank, Dokta Roby na
mgonjwa wao kufumwa pale Hosteli.
 
Back
Top Bottom