Sura-ya-Kwanza
JF-Expert Member
- Nov 17, 2007
- 568
- 12
Lakini hebu tutafakari. Nitoe hapo mfano tu, unajua kwamba vijana 4,000 kila mmoja akichangia walau elfu 10 tu kwa mwenzi(ambayo ni kama dola 100 kwa mwaka) ifikapo 2010 tutakuwa na bilioni moja za kuwawezesha vijana kuchukua majimbo? Unajua kwamba jimbo moja- kama hutoi rushwa linahitaji kati ya milioni 10 na 20 kushinda? Kwa kiasi hicho unadhani vijana tukiamua kuchukua hii nchi tunashindwa? Mimi naamini, tunaweza. Bila kuwategemea mafisadi kutuchangia mabilioni, tunaweza kwa umoja wetu, fedha zetu za kiadilifu tukiamua kujikamua kidogo tu kwa ajili ya mabadiliko. Tunaweza kabisa, tukiamini- Maneno matupu hayavunji mfupa! Tunaweza kabisa! Tunaweza kupunguza hodhi ya chama kimoja bungeni. Tunaweza, ni kiasi cha kuchukua hatua.
Nimetoa mfano tu- kama unaamini ni mfano ambao unaweza kuwekwa kwenye matendo tuwasiliane tafadhali kupitia mnyika@yahoo.com au 0754694553 tubadilishane mawazo zaidi kuhusu FOCUS 2010
Sasa nini cha kufanya sasa hivi:
1) Ni lazima tuanze mara moja kuwaelimisha wananchi kwa sasa.
Na elimu yenyewe ilenge kwenye mapinduzi ya kuwakomboa wananchi.Ni lazima tuwafikie wapiga kura sasa hivi bila ya kusubiri eti mwaka au miezi kadhaa ndiyo tuanze.Halafu tuwaeleze kuwa Tanzania yenye neema inawezekana kabisa bila ya kusubiri ahadi za za uongo za CCM.Tutumie kila liwezekanalo kufikisha ujumbe huu.Kwa kupitia magazeti,radio binafsi,internet blogs,midahalo,fulana zenye kubeba ujumbe wa mapinduzi,kuongeza mikutano ya hadhara hasa vijijini na kadhalika!
2) Kufunua uozo ndani ya CCM.Wananchi siyo wajinga kama baadhi yetu wanavyofikiri.Zipo sehemu nyingi tu za Tanzania ambazo wananchi wake wameshaamka na huwezi kuenda na kuwapa ahadi za kusubiri ati 2010 mambo yatakuwa safi kama JK alivyosema huku wao wakifa sasa hivi.
Kwa hivyo tufanye kila namna kufichua uozo wote na vilevile kutoa solutions ya nini kingefanyika kama mbadala na siyo kulalamika tu kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo juu.
JJ...Nimetafakari, naamini ni mfano mzuri au ni ajenda nzuri ya kuanzia.
Mnyika,
Sikudhamiria hata kwa sekunde moja kuwa Chadema na Wapinzani watoboe mifuko yao kuanza kuendesha Taifa kwa niaba ya Serikali. Nafikiri hukunielewa.
Hazina kubwa ni mawazo na fikra zinazotekelezeka. Katika mada yangu ya Chadema must Reeform, nimekuuliza je mpo tayari kuweka nguvu zenu za kiutawala na utendaji katika kata, tarafa, wilaya na mikoa na si Kitaifa pekee? Ni yangu ni kuhakikisha kuwa msukumo wa maendeleo ambao utafanya wapinzani wauzike utaanzia kwenye mafungu madogo madog na mwishowe kutapakaa kama vilinge na kujenga umoja mkubwa. Jiulizeni CCM waliwezaje kuwa mashuhuru namna hiyo?
Wao walikuwa na ujamaa vijijini na siasa ya ujamaa na kujitegemea. Ndio mkono wa kiserikali ulitumika kuhakikisha njozi na fikra zinatumika.
Nikiuliza je msukumo wa Chadema ni nini kwa mtanzania wa kawaida, wengi hawajui na majibu mnayotoa ni njoo kwetu kwanza au nenda tembelea katiba na webusaiti!
Ni nani ambaye atataka kwenda kukaa na kupukunyua kurasa kujifunza Chadema yafanya nini badala ya kufanya utafutaji?
Ndio upinzani hauna rasilimali za kifedha za kutosha. Lakini unazembea rasilimali za kimawazo ambazo ni nyingi kupita kiasi.
Tatizo la Watanzania ni njaa na umasikini na hii watu huona suluhisho lake ni pesa pekee au msaada wa hali na mali. Lakini msaada wa kimawazo ambao Mwalimu Nyerere aliujenga katika akili na mioyo yetu haupo tena. Kujituma bila kusukumwa au kutegemea kugawiwa na kusaidiwa kumekuwa ni mwiko kuanzia ngazi ya mtu binafsi mpaka Taifa. Tumekuwa tegemezi wa msaada na kushindwa kutumia fikra na mawazo yetu kwa urahisi na kuyafanya yatumike (bongo lala).
Mwiba katika hoja yake kumnadi Lipumba, anadai, umahiri wa kiuchumi wa Lipumba ni mkubwa sana kuwa hataweza kumsaidia mlima mchicha kujiendesha kwa ufanisi.
Sasa kama mawazo ya Wapinzani ni kuwa wao hawawezi kumfikia mtu wa kawaida in simple terms ili mtu huyu aimarike na wao (nyie) mnasubiri complex issues ndipo tuone utekelezaji wa Itikadi, falsafa na mipango mbinu yenu, basi kamwe hamtaweza kuwa na uwezo wa kuongoza nchi na kuleta mapinduzi.
Nafurahia ufasaha wako kujieleza hapa kwetu ukumbini, naamini wewe ni kijana mwenzangu ambaye katika safari yako ya kujifunza, pamoja na Kitila, mpo wazi kujielimisha kutokana na ubwabwaji wetu.
Je Elimu ya bure mnayoipata hapa natumikaje na vyama vyenu?
Je Vyama vyenu vina idara zilizoshiba ambazo zina wataalamu wa kila nyannja ambao wanaweza kujitolea kuelimisha umma jinsi ya kujitegemea na kuboresha maisha bila kutegemea msaada na kusukumwa na Serikali?
Jee Wapinzani wanafanya nini kuchukua tuzo ya Siasa ya Ujamaa(not communism like Russians but African Socialism) na Kujitegemea ambayo CCM imeacha kuinadi kwa nguvu za vitendo na kubakia kuwa maandishi katika makaratasi?
Tuendelee na shule!
Nafikiri focus ya vyama Tanzania inaweza kuwa sio sahihi kwa mawazo yangu kwa sababu yakutaka kwenda Ikulu mapema. Ikulu patawezekana tu wakati umeweka foundation nzuri. Swala liwe kupata wabunge wengi mengine yatafuata. Imagine kama tungekuwa na akina Zito, Slaa kama kumi tu katika bunge letu, ungeona moto unawaka bungeni. Iweje kiongozi anayevunja sheria alindwe na rais? (karamagi, Dito etc.)
Anyways 2010 inakuja tupo na tutaona jinsi tutakavyopelekana.
Nafurahi jinsi kijana Mnyika anavyojibu maswali anayoulizwa hapa; na kwa kiasi kikubwa nimegundua kwamba majibu mengi ya Mnyika na MAZURI kuliko maswali anayoulizwa. Wasioamini wazidi kuchunguza watatambua maana yangu.
Kikubwa ninachokiona hapa ni kwamba "wajuzi" wengi wanaojadili na "kuelimisha" wengine hapa hawajui siasa halisi. Mnyika anazungumza kutoka 'kazini' anasema anachofanya, watu wanaandika na kukejeli tu hapa kwa siasa za kompyuta, na bado wanataka Mnyika awaamini wao (ajifunze kwao) kuliko anavyojiamini yeye na wanasiasa wenzake mitaani.
Utawezaje kukejeli mchango wa mgombea urais katika kukusanya kura za wabunge wa chama chake? Hebu chunguza kinachoifanya kumshabikia Kibaki sasa - ndiye 'mgombea' wao wa urais, ingawa haitarajiwi KANU wapate wabunge wengi kuliko ODM.
Ukweli ni kwamba kwa mkakati wa sasa wa opposition Bongo, lazima awepo mgombea urais wa opposition kama uniting force, hata kama anajua atashindwa! Bila hiyo hata wabunge hapati. Kama Mbowe, Cheyo, Lipumba na Mrema watagombea ubunge watapata, lakini bado wanahitaji wabunge wengi zaidi ya hao wanne au watano, na nguvu ya kuwapata itatokana na hamasa itakayowekwa na mgombea urais, wapatikane hao 4, a mmoja wao akose kwa kugombea urais lakini aunganishe nguvu zao kitaifa. Kishoka hulioni hili? AU unadhani vyama vya upinzani vilipolisema vilikosea sasa wewe ukilirudia hapa ndipo linakuwa na maana?
Kumbuka pia kuwa ushindi unategemea factors nyingi, hasa unapopambana na chama kikongwe kilichojaa mafisadi...kinachopambana na watu wenye raslimali limited, na ambao wangpaswa kuungwa mkono na jamii lakini inaogopa kuonekana nao...hata hapa kwenye mtandao tunawaona watu wanabehave hivyo.
Mtu makini hawezi kuwalaumu wapinzani kwa kuanika ufisadi wa CCM, na hawezi kusema "I am pissed of" wakati kazi ndo imeanza na inapaswa ishinikizwe hadi mwisho! ndio hizo siasa za kompyuta...anataka walete jingine hilo waliache pale Jangwani au Mwembe Yanga! Lakini hatazami impact ya suala hilo kwa sasa kitaifa.
Ushauri kwa MNYIKA:
Mnyika umekuwa mkweli na muungwana sana hapa JF, lakini bahati mbaya unaozungumza nao huwajui, huwaoni... na wanatumia fursa hiyo kukuchokoza na kukuchota...Kama wanataka siasa kweli waingie, WATAJIFUNZA tofausti kati ya siasa za kweli na porojo za kwenye kompyuta.
Unapomwaga mikakati yenu hapa kwa MIZIMU ambayo huijui (mingine ni ya CCM) na ni mioga ya kufanya siasa, naamini kwamba huwatendei haki wapinzani wenzako wanaokaa kuweka mikakati hiyo na hawadhamirii kuianika hadharani kabla ya wakati wake. Ukitaka ku-argue, waambie wakutafute mfahamiane na mpeane hoja, la sivyo unaumia sana kujadili mambo haya na MASKS za watu waoga kama hawa ninaowaona hapa JF...
Kichwamaji
Nashukuru kwa ushauri wako. Ila niliwahi kusema, na narudia tena- tunaweza kujifunza toka kwa yoyote wakati wowote popote- unaweza kujifunza mazuri na mabaya. Cha msingi ni kufanya maamuzi sahihi. Kwa kweli, yahitaji ukomavu na stahamala kuweza kufanya mjadala mahala kama hapa, lakini najua kabisa kwamba muda haupotei bure. Hata kwa wanaouliza kwa nia iliyojificha, majibu yangu najua yanasomwa na watu wengi- najua wapo ambao yanawasaidia kuwafanya maamuzi sahihi na kama tayari wamashaamua basi kuwa na msimamo thabiti katika yale waliyoamua.
Lakini jambo moja siwezi kufanya, nalo ni kuanika mikakati yetu ya ndani- maadili ya uongozi na uwajibikaji wa pamoja hauruhusu hilo. Ndio maana kuna mengine nasema kabisa kwamba hilo siwezi kuanika. Hata ukinitafuta pembeni, bado siwezi kukupa mambo kwa kina kwa kweli- imani hujengwa kwa muda na hutegemea ngazi na kazi.
Cha msingi tu, ulewa kwamba kila nisimecho hapa ni kile ambacho najua mtu yoyote akifanya jitihada kidogo tu angeweza kukipata. Chama cha siasa ni mali ya umma, hivyo mawasiliano na umma kujulisha na kujua kinachoendelea ni nyanja muhimu ya kuongeza ushirikiano na ni daraja la msingi la kutaka kuungwa mkono au kukabalika.
Tuendelee na mjadala- FOCUS 2010
JJ
Unapomwaga mikakati yenu hapa kwa MIZIMU ambayo huijui (mingine ni ya CCM) na ni mioga ya kufanya siasa,
Ukitaka ku-argue, waambie wakutafute mfahamiane na mpeane hoja, la sivyo unaumia sana kujadili mambo haya na MASKS za watu waoga kama hawa ninaowaona hapa JF...
Kichwamaji,
Ni mimi ambaye unaniandikia hasira yako na hitimisho lako ni kutamka maneno niliyosema "I am pissed off"! Sasa kama wafikiri nampotezea wakati Mnyika, unapotoka!
Mrema na Mtikila, walitumia "tabloid" politics 1995, 2000 na 2005, je Watanzania walichiukua hatua gani? Nothing they made CCM to be the party of choice.
Sijakataa kuanika mafisadi, lakini kutumia kutafuta uchafu na kuanika uozo wa CCM kama turufu ya kushinda uchaguzi si nja ya makini kushinda uchaguzi. Ndio maana nimesema kwa sisis tunaoelewa Siasa za Kitanganyika na uelewa wa Siasa kwenye Demokrasia ya kweli, political smear campaign inaachwa kwenye vijiwe na opposition kuweka nguvu zao katika mkondo wa kisheria unaofanya kazi (Bunge hata Mahakama).
Je ni wangapi wamejiunga na Mtikila katika kesi zake anazopeleka Mahakamani ambazo ni za msingi kabisa kuhusiana na Katiba na Utendaji (Wagombea Huru) ili kuonekana kuna mshikamano? Hakuna, sana sana tunamuona Mtikila ni taahira fulani wakati anayofanya, ndiyo yanayopaswa kufanywa na Wapinzani wote kwa pamja ili kuonyesha mshikamano wa kudai mambo ya msingi ingawa kila chama kina sera zake!
Suala la Muafaka Zanzibar, BOT, Madini, Kiwira, Richmond na ufisadi mwingine hata kama umepita mfano IPTL, Radar, Ndege na kadhalika ni masuala ambayo ni nyeti kuishia katika mikutano ya waandishi wa habari pekee!
Mambo kama haya yanapaswa yashinikizwe Bungeni na wapinzani kwa kupitia kanuni na sheria zilizopo. Kuwasilishwa kwa hoja za kudai kuundiwa kwa kamati za bunge za kuchunguza niliyoyataja hapo juu, ndiyo nja sahihi ya kujenga imani kwa watu, hata kama CCM na Bunge lao la kiimla watapinga (mfano wa Zitto na Karamagi)!
Suala la Zitto kuhusu Karamagi, lilipotea njia awali kutokana na udhaifu wa hoja na ushahidi kuwakilishwa Bungeni ambako kungeshinikiza uchunguzi wa Suala la Buzwagi ufanywe na Bunge na si kuundia Kamati Kibogoyo ya Rais ambayo haitakaa kamwe kutoa suluhisho na tathmini ya maana ambayo itapelekea watuhumiwa kushitakiwa.
Sawasawa na uchunguzi wa BOT, badala ya kushinikiza kuundwa kwa kamati ya Bunge au kuipa madaraka Kamati ya Fedha ya Bunge kupeleleza na kuchunguza ubadhirifu huu kwa kutumia mamlaka yake kisheria (Bunge), kazi imepewa kwa kampuni binafsi na matokeo yake yanaenda kwa Waziri na Ikulu kwanza, yafanyiwe uhariri ndipo Taifa lipewe nakala ambayo imechujwa!
Ndio maana, nimesema " I am pissed off" with technics ambazo zinatumika na wapinzani kuelimisha umma kutumia habari ambazo zinaonekana kuwa ni za udaku na si za kweli!
Solution ni kuongeza uwakilishi wa vyama hivi katika Bunge ili miswaada ya kuchunguza ishu ikifika, basi kura zao zitafanya kazi!
Kuhusiana na urais, nimeuliza, kwa nini wasitafute mtu mmoja mahiri na popular awawakilishe wapinzani wote? Jibu ni kuwa kila mmoja wao anautaka Urais na zaidi, wengine wao ni makuwadi wa CCM. Tayari kuna mgawanyiko katika upinzani ambao unaonyesha wazi kuwa kamwe ufa wao hautaweza kuzibika.
Ni kwa nini kina Shayo, Mtikila na Makaidi wamekimbilia mbali, Cheyo yupo pekee halafu Mbowe, Lipumba, Mrema na Marando upande mmoja?
Will this work?
My passion and opinions are for the sake of Taifa and I am not a stooge who is trying to figure the upinzani best next move. I learn by observation and reading simple details and analyze them and try to provide alternatives that can work on the best interest of opoosition to make sure that the Political Dominance and Un-Accountability of CCM comes to an end!
Hivyo basi kama waona nampotezea wakati Mnyika, huo ni uhuru wa maoni yako, na mtazamo wako na nitauheshimu kwa maana weye na mimi hatujuani!
Mnyika,
Unakata tamaa hivyo mapema mdogo wangu at your age?
Muhimu message imefika-sasa ndo kutangaza kususa? Kwa faida ya nani?
Adult human beings are rational beings in making decisions!
Tambua pia audience unayowasiliana nayo- na upeo waliokuwa nao!
Tusonge tu mbele!
Rev. Kishoka
umesoma ripoti ya usalama wa taifa ikimshauri Waziri Mkuu Lowasa ahakikishe Kashfa ya BOT kama alivyoiandika Dr Slaa haiingii bungeni?
Kuhusu BOT, mkondo wa bunge ulijaribiwa na Dr Slaa alishaandika Hoja Binafsi lakini dalili zilionyesha wazi kabisa kwamba walitaka kuifanyia mizegwe isiingie, umesoma ripoti ya usalama wa taifa ikimshauri Waziri Mkuu Lowasa ahakikishe Kashfa ya BOT kama alivyoiandika Dr Slaa haiingii bungeni? Katika mazingira hayo, unaweza kumlaumu vipi Dr Slaa kuichomoa hoja yake na kuiwasilisha kwenye mahakama ya wananchi ama bunge la umma? Dr Slaa ni mbunge, kama angeiwasilisha ile hoja mule, kuna baadhi ya mambo angebanwa na kanuni za bunge(naomba niseseme kwa nini ingawa najua kwaninini). Kwa hiyo, alifanya uamuzi wa busara kabisa. Kuhusu EPA, hili ni tone dogo sana kati ya bahari ya yanayohitaji kuchunguzwa kuhusu BOT na kwa maoni yangu mimi limefanyika ili watu waghilibike kwamba uchunguzi umeshafanyika.
It is very disappointing kuona sio tu kwamba "Usalama wa Taifa" (note the quotes) wanaingilia katika mambo ya siasa kiasi cha kumpangia priorities Waziri Mkuu on a purely tyrannical basis, but also kuona upinzani unajua hilo lakini they do not make that an issue.Mnaogopa usalama wa taifa? This is sheer cowardice na ndiyo maana hatuendelei kwa sababu kwa jinsi nchi yetu ilivyooza tunahitaji revolutionaries walio tayari kujitoa mhanga maisha yao na sio calculating politicians.
Sasa tumefikia point hata kuongelea technicalities zinazowafunga kusema ukweli bungeni wanaogopa, either they are too cowardice to be effective or they have awkward skeletons in their own closet.
Both options are dangerous indeed.
What happenned to "kumkoma nyani giladi"?
Mnyika,
Unakata tamaa hivyo mapema mdogo wangu at your age?
Muhimu message imefika-sasa ndo kutangaza kususa? Kwa faida ya nani?
Adult human beings are rational beings in making decisions!
Tambua pia audience unayowasiliana nayo- na upeo waliokuwa nao!
Tusonge tu mbele!
Ni mategemeo ndani ya jamvi hili, kama wanauelewa mpana. Hivyo inashangaza baadhi ya wachangiaji wanavyoleta hoja nyepesi kwa masuala mazito.Mimi kwa sasa hivi niko kijijini lupaso-Kyela nathibitisha watu wanavyoitikia mwito wa kuchunguza masuala ya madini na masuala ya utawala bora.