....CCM ni umaskini na kujirudisha nyuma tuu!
Wakuu kinachowauma nini haswa.. yaani hawa wazee hawana haki ya kumteua mtu wanayempenda?.. jamani semeni nanyi chaguo lenu kisha pinganeni na usemi huo wa wazee hao na kuzipanga sababu zenu lakini mnaposema Kikwete hafai aondolewe hali hamna mtu mwingne inachekesha...
Mada hii mefikia kurasa zaidi ya nne na hakuna hata mmoja wenu amediriki kumtaja mgombea dhidi ya Kikwewe kwa tiketi ya chama..
Na nimeliweka swali hilo makusudi kwa sababu naelewa fika kwamba CCM bila Kikwete haiwezi kwenda popote. hakuna na narudia kusema hakuna kiongozi CCM anayeweza kuwa mbora kuliko Kikwete ktk kiti cha Ikulu.. chama kizima Muflisi, kimeshikwa na mafisadi.. Sii Mwandosya, magufuli wala mjomba wake anayeweza kuinua hata kidole against kundi hilo..
Wanaojiweza kidogo ni Mwakyembe, Sitta, Mama Kilango, na Malecela.. hawa wote ni watu wa Kikwete na wanampendekeza Kikwete kwa sababu hawawezi kupita hata Ubunge 2010 kama sio nguvu ya Kikwete..haya tukiondoa hawa huko CCM kabakia nani?..nani anaweza kumkemea Rostam au Lowassa! nani anaweza kusimama na hawa jamaa na kuwatazama usoni akawaambia wanakwenda lupango!..hakuna...
Hakuna rais hata mmoja anayeweza kuendesha nchi peke yake bila nguvu ya chama nyuma yake -hakuna..Sii Tanzania wala Afrika nzima!
Kinachouma wengi hapa (pamoja na mimi) niWakuu kinachowauma nini haswa.. yaani hawa wazee hawana haki ya kumteua mtu wanayempenda?.. jamani semeni nanyi chaguo lenu kisha pinganeni na usemi huo wa wazee hao na kuzipanga sababu zenu lakini mnaposema Kikwete hafai aondolewe hali hamna mtu mwingne inachekesha...
Mada hii mefikia kurasa zaidi ya nne na hakuna hata mmoja wenu amediriki kumtaja mgombea dhidi ya Kikwewe kwa tiketi ya chama..
Na nimeliweka swali hilo makusudi kwa sababu naelewa fika kwamba CCM bila Kikwete haiwezi kwenda popote. hakuna na narudia kusema hakuna kiongozi CCM anayeweza kuwa mbora kuliko Kikwete ktk kiti cha Ikulu.. chama kizima Muflisi, kimeshikwa na mafisadi.. Sii Mwandosya, magufuli wala mjomba wake anayeweza kuinua hata kidole against kundi hilo..
Wanaojiweza kidogo ni Mwakyembe, Sitta, Mama Kilango, na Malecela.. hawa wote ni watu wa Kikwete na wanampendekeza Kikwete kwa sababu hawawezi kupita hata Ubunge 2010 kama sio nguvu ya Kikwete..haya tukiondoa hawa huko CCM kabakia nani?..nani anaweza kumkemea Rostam au Lowassa! nani anaweza kusimama na hawa jamaa na kuwatazama usoni akawaambia wanakwenda lupango!..hakuna...
Hakuna rais hata mmoja anayeweza kuendesha nchi peke yake bila nguvu ya chama nyuma yake -hakuna..Sii Tanzania wala Afrika nzima!
maneno mazito haya Bob... ni ukweli unaouma sana hasa kutokana na udhaifu/kutokukubalika kwa upinzani. Mungu ibariki Tanzania.
14 December 2005 Matokeo ya Uchaguzi wa Rais TanzaniaKuraChama Cha Mapinduzi9,123,952 80.28Civic United Front1,327,125 11.68Chama cha Demokrasia na Maendeleo668,756 5.88
Semilong,
Mkuu wangu weee hivi kweli umeshindwa kuliona kosa bali unavumbua kosa kwa mtindo wa Vasco Dagama..
Kosa ni kuwachagua Mwinyi na Mkapa kuwa marais...hakuna hata siku moja miaka ikawa sababu ya makosa ya uchaguzi bali ni uchaguzi wa mtu wenyewe ndio una makosa..
sasa unaposema makosa Kumchagua Kikwete ni vizuri sana ukafikiria kuchagua nje ya Kikwete na wagombea watakuwepo.. That's the ONLY solution uliyokuwa nayo. Usitake kulazimisha bus linalokwenda Mbeya lisimame kwa sababu Ulitegemea kwamba hao madereva hupokeza njiani..Umeshaambiwa utaratibu wao sio hivyo bado hutaki, kama hutaki safari ya CCM shuka wewe acha wengine waendelee na safari..
kumchagua tena kikwete itamaanisha kwamba watanzania tuko tayari kuchagua uzembe kwa mara nyingine na hao wazee unaowaona wote ni wa pambe na njaa zao.
ukiniuliza nani apewe nakuambia MAGUFULI.
na magufuli nae asipofanya kazi miaka 5 tu mwisho.
mkandara unaabisha JF kuona kwamba ushakubali ya ishe, watu regular wa JF kama nyie mnakubali ya ishe inaonekana hamtaki CHANGE.
Wajumbe wa Kamati Kuu, waliochaguliwa ni Dk Maua Daftari, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Bw. Muhammed Seif Khatibu, Bw. Omar Yusufu Mzee na Bi. Fatma Said Ali.
Wengine ni Bw. Yusuf Hamad Yusuf, Samia Suluhu Hassan, Bw. Rostam Aziz, Bw. Andrew Chenge, Bi. Pindi Chana, Dk. Abdallah Kigoda, Bw. Abdulrahman Kinana na Bi. Anna Makinda.
kumchagua tena kikwete itamaanisha kwamba watanzania tuko tayari kuchagua uzembe kwa mara nyingine na hao wazee unaowaona wote ni wa pambe na njaa zao.
ukiniuliza nani apewe nakuambia MAGUFULI. hata wizara ya minofu anafanya kazi na kama kawaida inaonekana kuna nguvu zinamsimamisha baada ya kuchukua hatua. hata alivyokuwa wizara za nyuma alikuwa anafanya kazi lakini bosi wake alikuwa anamsimamishwa, kama ilivyo bosi wa sasa hivi. kumpeleka magufuli minofu ni kumnyima media attention ili kuua nguvu yake kisiasa.
putin aliwekwa kwenye urais na oligarchs na alivyokuwa rais akawachukulia wote atua na kuhakikisha utajiri wa rusia unatumika kuinua uchumi wa russia na sio familia chache.
magufuli akichaguliwa atapambana na kina rostam kwa ajili yeye ndio mwenye nguvu zote.
kikwete sio kama hawezi kuwachukulia hatua bali hataki.
na magufuli nae asipofanya kazi miaka 5 tu mwisho.
mkandara unaabisha JF kuona kwamba ushakubali ya ishe, watu regular wa JF kama nyie mnakubali ya ishe inaonekana hamtaki CHANGE.
mabadiliko yanatakiwa kila miaka mitano mpaka viongozi waanze kufanya vizuri.
MKANDARA WEWE HUNA TOFAUTI NA HAO WAZEE SIJUI NA WEWE NI MZEE.
YOU ARE RESISTANCE TO CHANGE, IT IS TIME FOR YOU TO START SUPPORTING THE CHANGE MOVEMENT.
HII INAONYESHA WEWE NI MKAZI WA DAR NA SIO WA TARIME.
Babu ataka kusema,
Mkuu kitu kimoja tu Kikwete hakufanya kulingana na wanaCCM nacho ni kumwacha Apson, Mahita, Lowassa, Karamagi, Meghji, na baraza zima la mawaziri . Kikwete katengua katiba ya chama kuwaondoa viongozi wote wanaotaka kufanya biashara wakiwa mawaziri. Utawala wa Kikwete umewafikisha Yona na Mpamba mahakamani.
Pungufu moja kubwa kwa wananchi ni mtu mmoja tu Lowassa..jambo ambalo hakuna kiongozi hata mmoja Tanzania ambaye angeweza hata kumsimamisha madaraka kwa sababu madhambi ya Chimwaga na uchaguzi mkuu waliyafanya wote ndani ya chama.
Na nakuhakikihsia Kitendo cha Kikwete kuwatema Lowassa na mtandao ni ushindi kwa wananchi na wana CCM kwa sababu hakuna mtu ndani ya chama hicho angeweza kufanya hivyo..na leo hii hakuna kiongozi yeyote anayeweza kufanya unayoyataka wewe.kwa sababu sifa unazotafuta hazipo ktk uongozi bora wa CCM isipokuwa nje ya chama.
Huo ndio UNAFIKI kupiga kelele nyuma ya pazia..na bado tu mkuu unakazania JK wakati sijakusikia ukitaja mtu anayefaa!.. sasa Unataka JK ongembee na UKUTA.. yaani turudishe zile picha za uchaguzi wa Nyerere na Ukuta mkuu wangu!
Recta,
Mkuu wangu nakusikia sana na kilio cha Watanzania.. sii wewe peke yako ila tupo wengi sana. Tofauti yangu na wewe ni ktk imani.. Wewe unaamini atakayetupeleka peponi ni mtu lakini sii Kikwete..Wakati mimi hapa naamini kinachokupeleka peponi sii mtu ila ni imani nzima ya dini (kile alichotufundisha) na sisi tukafuata.
Ikiwa sera za chama CCM zina mapungufu na toka tupate Uhuru hatujaweza piga hatua wakati kuna marais watatu wamepokezana, then something is very wrong na utawala huu (imani ya dini hiyo) haijalishi nani kiongozi na wala sii swala la uchaguzi wa nani akuongoze kwani sisi sio kundi la kondoo..hakunamtume huko CCM anayefahamu pepo inapatikana vipi..
So the only thing kwangu mimi siwezi kumkataa Yesu kwa sababu tu nina imani zaidi na Mohammad... hapana mkuu wangu, tofauti zetu ni ktk mafundisho na sii watu..
Hata kama Recta ndiye angekuja na ujumbe sawa na Koran ningemfuata yeye na sii Mohammad kwani bado ningekuwa Muislaam. Uislaam unajengwa kwa imani ya dini na sio jina la mwakilishi wa Ujumbe..tofauti zetu zinatokana na kitabu (ujumbe na sii uzawa na makeke ya kiongozi)..
Ikiwa kuna mtu CCM ambaye wewe unafikiria ni mbora mtaje mkuu wangu mbona swali dogo sana!
TZ needs a new direction 2010, they need to mbeki-nize him and choose a new leader
- Wakishamtoa rais wa sasa, ni nani anayefaa kushika nchi naona hili swali halijibiwi, vipi?
William.
- Wakishamtoa rais wa sasa, ni nani anayefaa kushika nchi naona hili swali halijibiwi, vipi?
William.
Katiba iachwe ifuate mkondo wake, siyo lazima atakayemreplace Kikwete awe na jina kubwa, anaweza kabisa kuwa si mtu ambaye anajulikana sana ndani ya CCM au hata Tanzania. Kumbuka Obama hakuna mtu aliyemtabiria kuwa angeibuka kuwa mgombea wa Democrats na hatimaye kuwa Rais wa Marekani. Hovyo basi nasi tunaweza kabisa kumpata Obama wetu, mtu ambaye hana jina kubwa, si maarufu sana ndani ya CCM au Tanzania lakini kutokana na sera zake atakazomwaga basi wengi ndani ya CCM wanaweza kabisa kuamua kumsupport na hatimaye kuibuka kama mgombea wa CCM.
Ni lazima tuachane na dhana kwamba Rais wa Tanzania ni lazima awe na jina kubwa lenye umaarufu kwa siku nyingi katika anga za siasa za nchi yetu.
Suala si anayefaa, wao tayari wanaye mtu wao wa kushika nafasi. Kwamba anafaa hilo ni suala jingine ambalo Watanzania watalazimika kujifunza kwa kutumia uhalisia.
Lakini pia kwao sasa hivi suala la nani atachukua nafasi si relevanty, vita yao kwa sasa ni kuondoa huyu aliyepo
- In your opinion nani anaweza kufaa na kumshinda rais wa sasa?
William.
Wote wanaotaka kugombea toka CCM kama ni akima Mwandosya na wengineo wote waruhusiwe kuchukua form na kuwe na mjadala kati yao na atakayeonekana anafaaa kuliko mwingine basi apitishwe. Hili la kutoa jina kwamba fulani anafaa mimi siliafiki maana nakumbuka Mwalimu (RIP) alisema Mkapa ndiye aliyemuona anafaa kuwa Rais 1995 yalitokea baada ya hapo wote tunayajua.
Vigezo gani mlivyotumia kufikia conclusion kwamba ndani ya CCM hakuna mbadala wa Kikwete? Hata wanaotaka kugombea hawajapewa nafasi ya kufanya hivyo, tayari nyie mmeshaona kwamba hakuna mwingine ila Kikwete!!! Je mmeenda kwa Sheikh Yahya au kwa Toboa tobo kuweza kufikia conclusion yenu!?
Kikwete kashindwa kupambana na mafisadi ndiyo maana wahusika wote wa ufisadi akina Chenge, Rostam, Idissa Rashid na wengine wengi bado wanapeta uraiani. Huoni Rais ambaye anashindwa kutetea sheria za nchi na kuweka maslahi ya nchi mbele kwamba hafai kuiongoza nchi hiyo maana sheria za nchi zinazidi kukiukwa kila kukicha bila athari yoyote kwa wale wanaokiuka sheria hizo? Wakati umefika wa kutafuta mtu atakayeisafisha CCM na Tanzania kwa ujumla
Kwako wewe ufisadi si kila kitu katika maendeleo lakini inapotokea watu wanaifisadi nchi karibu shilingi Trilioni ($1 billion approximately)moja katika kipindi kifupi na kama ukaguzi wa EPA ungefanywa kuanzia 1995 mpaka 2006 badala ya 2005/2006 basi si ajabu pesa iliyoibwa ingefika hata shilingi Trilioni 2 ($2 billion approximately) , hili ni tatizo kubwa sana kwa nchi yoyote ile inayotaka kupata maendeleo kwa wananchi wake wote, kama wewe unaliona hili ni dogo hiyo ni juu yako. Inapotokea Rais anashindwa kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha wageni badala ya wananchi wake pamoja na kuwa aliahidi kulishughulikia tatizo hilo hii ni dalili nyingine ya kiongozi dhaifu ambaye hastahili tena kurudi madarakani. Je ni akina nani hao uliowasema hapo juu walioshindwa na Kikwete!? Na wameshindwa katika mambo gani!? Na hiyo tathmini iliyomuonyesha Kikwete kawashinda hao ilifanyika lini na wapi!?[/B]
Narudia tena, ndani ya CCM kuna wengi ambao wanaona wana uwezo wa kuiongoza Tanzania vizuri zaidi ukilinganisha na Kikwete. Katiba ya CCM na ya nchi pia zinawaruhusu kugombea nafasi hiyo bila vitisho wala mizengwe toka kwa Malecela, Chiligati, Msekwa au Wazee wa CCM. Hakuna haja ya mimi kutamka kwamba fulani ndiye anayefaa kuwa Rais 2010. Wote wanaotaka kugombea ndani ya CCM waachwe wafanye hivyo na kama baada ya taratibu zote ndani ya CCM kufuatwa na bado ikaonekana Kikwete ndiye anayefaa kuwa mgombea wa CCM basi hapo taratibu za CCM zitakuwa zimefuatwa bila upendeleo wala vitisho dhidi ya wagombea wengine, lakini huu udikteta wa "watakaompinga Kikwete watakiona" na "Wasitumie ufisadi kutaka umaarufu wa kisiasa' Kamwe hilo mimi silikubali. Mambo ya kulinda viongozi dhaifu na mafisadi ni lazima tuyapige vita kwa nguvu zetu zote maana hawa ndiyo tatizo kubwa la nchi yetu kutokuwa na maendeleo ya kuridhisha pamoja na misaada na mikopo chungu nzima tunayopata toka nchi mbali mbali za wafadhili na mashirika ya kimataifa pamoja na rasilimali nyingi tulizojaaliwa na Mungu.