Hata mimi sielewi ndugu yangu, inasikitisha kwa kweli halafu Kikwete mwenyewe pamoja na vitisho hivi yeye kakaa kimya kabisa kama kawaida yake!!!!
Hawa unaowasikia wanampinga Karume ,maana Karume anatayarishwa kuchukua nafasi ya Kikwete ,ikiwa Kikwete ataamua kuachia ngazi ,ila wapo katika kutoa ishara kuwa hakuna sababu ya Kikwete kuachia ngazi, kama unakumbuka Mwinyi alipomaliza kuwa Raisi wa Zanzibar alipewa wa Tanzania na ndio hivyo hivyo ,kama unavyofahamu taratibu za CCM ,ili kujificha na ile dhana kuwa Zanzibar haipewi uongozi wa Tanzania ,ndio inaonekana kuwa Karume apishwe katika kipindi hiki au hata Kikwete akimaliza miaka kumi yake kama akiipata apewe Karume.Ni utaratibu wanaosema wamejipangia au wameamua kuurudisha ili kudumisha muungano.
Wewe Mwiba, nani kakuambia Karume anasifa za kuwa rais wa Tanzania? Unaacha kuangalia watu wenye uwezo na mtizamo? huyo sana sana labda kuwa mkuu wa mkoa tu.
Bubu Ataka Kusema,
Mkuu swali langu rahisi sana.. kama yeye hafai nani anafaa?.. ambaye wewe una hakika atayaleta yale unayoyataka.. mwenye kutimiza ahadi zake maanake nijuavyo Mimi sii Mwinyi wala Mkapa walitimiza lolote..
Ukishindwa hilo bila shaka ni kutokana na uvivu wa kufikiri..Unapinga kitu ukiwa na solution mkononi, kama huna wewe pia mvivu vile vile, ndio nachosema mimi..
Wako wengi tu ambao kwa kujua udhaifu utakaomfanya Kikwete asikae madarakani kwa awamu ya pili, wao watayafanya yale ambayo Kikwete alikuwa anayaogopa kuyafanya kwa kuwa ni Kiongozi dhaifu na hao anaowaogopa kama akina Rostam, Karamagi na wengineo wengi ambao wana tuhuma nzito za kifisadi watachukuliwa hatua za kisheria bila woga wowote. Kwanini tunyooshe mikono juu eti Kikwete aendelee tu kwa sababu hakuna mwingine? Kwenye Urais huwezi kuwa na solution maana hakuna yoyote aliyewahi kushika nafasi hiyo zaidi ya Nyerere ambaye ni marehemu, Mkapa na Mwinyi ambao wamemaliza muda wao na hawaruhusiwi tena kurudi madarakani. Nchi ya watu 40 millioni kweli tushindwe kupata Kiongozi mzuri kuliko Kikwete!!!!! 😕 Haya kwangu ya kung'ang'ania Kikwete aendelee ni maajabu ya hali ya juu. Kuwe na sababu za kiutendaji ambazo zimeturidhisha Watanzania na hivyo kumuona anastahili kuendelea na miaka mitano mingine, lakini hili la 'utamaduni wa kuachiana' eti Mwinyi tulimuachia miaka mitano mingine na Mkapa tukamuachia miaka mitano basi na Kikwete tumuachie miaka mitano mingine kamwe siafikiani nalo!!!!
Ama kweli bubu ataka kusema...duh..Nauliza tena ni kina nani hao?..Wako wengi tu ambao kwa kujua udhaifu utakaomfanya Kikwete asikae madarakani kwa awamu ya pili, wao watayafanya yale ambayo Kikwete alikuwa anayaogopa kuyafanya kwa kuwa ni Kiongozi dhaifu na hao anaowaogopa kama akina Rostam, Karamagi na wengineo wengi ambao wana tuhuma nzito za kifisadi watachukuliwa hatua za kisheria bila woga wowote
MKUU BUBU kwanini hutaki kutusikia nasi wenzio. Tumeshakusikia kuwa JK aasirudi tena kwenye madaraka lakinimbona hutaki kulisaidia Taifa katika mchakato wa kumtafuta mbadala wa JK?
Unatwambia kuwa tusikate tamaa bali tutampata mbadala tu tena kutoka CCM hiii hii tunayoijuwa. Sijui kiasi gani wewe mwenyewe unaamini hili lakini wengi wetu tunaona kuwa mbadala huyo kutoka CCM kama hayupo.
Hoja yako ya kumuondowa Jk na kumpata mbadala wake mpaka sasa umeijenga katika ufisadi tu,tu. Tunashindwa kumpata mpiganaji halisi wa Ufisadi kutoka CCM kwani Ufisadi ndio uliowaweka madarakani Wabunge wote wa CCM. Kama walipandia ngazi hiyo wana nguvu gani kuipiga mateke?
Ufisadi si kila kitu katika maendeleo ya nchi yetu hivyo ubora wa kiongozi hautapimwa kwa ufisadi peke yake bali kuna mambo mengine chungu nzima pengine JK amewashinda wengine. Halafu uozo huu mbona ulishakuwepo toka kiongozi wa mwanzo iweje sasa kumshikia bango huyu mmoja tu ambae angalau anachukua hatuwa.
Bubu utakuwa umetusaidia kama utatowa hadharani wateule wako na wala usiogope kuwa watachambuliwa, kwani angalau tutakuwa tumepiga hatuwa moja katika kulitekeleza hili la kumzuia JK asigombee tena.
mwinyi katulaghai tume mmpa miaka kumi....
mkapa katulaghai tume mmpa miaka kumi...
kosa si kosa bali kosa ni kurudia kosa , mwinyi na mkapa inatosha
kikwete katulaghai sasa hivi kwa hiyo inatakiwa miaka mitano mwisho na wengine wote watakaofuata watajua atutaki mchezo.
Bubu ataka kusema,
Ama kweli bubu ataka kusema...duh..Nauliza tena ni kina nani hao?..
Mkuu wangu weee hivi kweli umeshindwa kuliona kosa bali unavumbua kosa kwa mtindo wa Vasco Dagama..mwinyi katulaghai tume mmpa miaka kumi....
mkapa katulaghai tume mmpa miaka kumi...
kosa si kosa bali kosa ni kurudia kosa , mwinyi na mkapa inatosha
kikwete katulaghai sasa hivi kwa hiyo inatakiwa miaka mitano mwisho na wengine wote watakaofuata watajua atutaki mchezo.
Semilong,
Mkuu wangu weee hivi kweli umeshindwa kuliona kosa bali unavumbua kosa kwa mtindo wa Vasco Dagama..
Kosa ni kuwachagua Mwinyi na Mkapa kuwa marais...hakuna hata siku moja miaka ikawa sababu ya makosa ya uchaguzi bali ni uchaguzi wa mtu wenyewe ndio una makosa..
sasa unaposema makosa Kumchagua Kikwete ni vizuri sana ukafikiria kuchagua nje ya Kikwete na wagombea watakuwepo.. That's the ONLY solution uliyokuwa nayo. Usitake kulazimisha bus linalokwenda Mbeya lisimame kwa sababu Ulitegemea kwamba hao madereva hupokeza njiani..Umeshaambiwa utaratibu wao sio hivyo bado hutaki, kama hutaki safari ya CCM shuka wewe acha wengine waendelee na safari..
Mkuu, kwanza ningeomba mada hii iunganishwe na zile nyingine tunajaza ukumbi tu...Wakizungumza Dar es Salaam jana na Majira kwa masharti ya kutotajwa majina, makada hao walidai dhamira ya kweli ya Rais Kikwete kupambana na mafisadi itaonekana pale tu atakapowaengua haraka ndani ya chama watuhumiwa wote wa ufisadi.
Bubu ataka Kusema,
Mkuu, kwanza ningeomba mada hii iunganishwe na zile nyingine tunajaza ukumbi tu...
hata hivyo, haya madudu ndio nayazungumza - hakuna mtu CCM, sasa kama wewe unataka kupinga hoja kwa nini unajigubika na blanketi usionekane!.. Ndo unafiki huo, wajitokeze hadharani waseme ukweli wananchi wawasikie na wafahamu kwamba wapo watu wanaweza kusimama na Rostam/Lowassa na Mkapa ktk ufisadi..
Kumbuka mkuu wangu labda unasahau nguvu ya Mtandao, kumbuka Mzee Es alituambia nini wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2005 ndani ya chama CCM.. Mkapa, Kawawa na Mwinyi walifungwa midomo...Malecela alitupwa nje kama mbwa na hakuna mtu aliyesimama kuettea, leo unambie ati kuna watu CCM wanataka mafisadi washughulikiwe..
Ikiwa bungeni tu wameshindwa kunyoosha vidole vyao kupendekeza mafisadi wakidai Usalama wa nchi utapotea, leo unambie ati kuna watu wanataka JK asisimame.. Hawa wote ni Wanafiki wametumwa na Rostam/Lowassa, sio habari ya awamu mbili kwa sababu KJK kashindwa kazi.. nakwambia hakuna kati yao, hakuna hata mmoja angeweza kuwa ondoa madaraka hata watu wa usalama kina Apson au Mahita - Hakuna... that is the fact..