Sasa chukulieni gari hili la CCM limekwama, nanyi mnataka kubadilisha dereva kwa sababu gari limekwama... hii kweli inaingia akilini jamani..Shukeni, tatizo sio dereva kuna gari jingine pembeni linasubiri abiria tena bureee hakuna gharama zaidi...Sambamba na kukiri kulindana, Msekwa pia alikiri kuwa rushwa imetawala katika uchaguzi ndani ya chama hicho na kubainisha kwamba CCM haikumbatii rushwa ila utekelezaji na usimamizi wa sera ya chama hicho kupambana na rushwa umekwama.
kusema kweli sioni kiongozi bora ndani ya CCM ambaye ataweza kutimiza yale nayoyataka..Wengi ambao ningefikiria pengine wanaweza kuleta mabadiliko wameondoka ktk kurupushani za siasa..Waliobakia wote wanaogopa Mtandao kama anavyoogopa Kikwete mwenyewe!
Tuna watu kama Dr. Slaa akienda sambamba na Mafisadi, akichukua kila kitu hatua kwa hatua lakini ameshindwa kwenda mbele kwa sababu hana ubavu..Now, just imagine mtu huyu anakuwa Rais au Waziri Mkuu wa Tanzania!..Matatizo yetu yote yamekwisha!
Kwa nini bado mnafikiria CCM!
Nani huyo mwenye uwezo?..hawezii aachie ngazi aone wenzake wenye uwezo....yeye hawezii.,
Mkuu wangu wakuambie mara ngapi?.. wamesema sifa zote za Kikwete sasa kama wewe hukubaliani na sifa hizo, sii kura yako unayo mkononi?.. Unachotaka wewe wafanye kipi..wao ndio chaguo lao au wataka wamruhusu Rostam agombee na kwa sifa zipi?kilichotakiwa kwa wao ni kutufafanulia kwanin jmk anafaa kuendelea. na hilo lisifanywe kijuu juu. kwamba ccm wana kawaida ya kuachiana miaka kumi kumi si hoja
.............. kwa Rais Kikwete, haoni kitakachowafanya wampinge kutokana na uwajibikaji wake kwa taifa na mapambano dhidi ya rushwa.
...............Utamaduni wetu ndani ya chama unafahamika, Mwinyi tulimpa miaka kumi, Mkapa naye vile vile
...............amekuwa mvumilivu wa kukosolewa, msikivu na ni mtu anayeipenda nchi yake kwa moyo wote na si kiongozi wa visasi.
...............tunaamini kwamba usalama na amani ya nchi yetu upo salama leo na kesho chini ya uongozi wake.
Kwa maana hiyo, nasi tunaungana na wale wengine kumuunga mkono kwa kipindi cha pili cha urais," alisema.
Pilipili usioila inakuwashia nini? Sikujua kama CCM imekukaa namna hiyo!Mwaka jana kwenye kampeni za uchaguzi wa Raisi Marekani tulishuhudia mchango wa kizazi kipya katika kuchochea mabadiliko katika siasa ya nchi. Tulishuhudia vijana wakitofautiana wazi wazi na wazazi wao katika misimamo yao mpaka kutishia kukata mawasiliano nao. Vijana wa Marekani walidhihirisha kuwa kweli wao ni taifa la leo na siyo kesho kama vijana wetu hapa wanavyodanganyika kirahisi siku zote.
Nikiangalia hapa nyumbani Tanzania nashuhudia vijana wanavyopigana vikumbo kufuata nyayo za wazazi wao ambao ni wazi wamepitwa na wakati. Baada ya tamko la wazee wastaafu wa CCM, nilitegemea vijana wa CCM kujitokeza na kupinga kwa nguvu kauli zao. Lakini kinyume chake nasikitika kusema vijana hawa kama kawaida yao wanafanya maandamano kuunga mkono hizi kauli mfu - ama yawezekana nilikuwa naota tu !
Wako wapi akina Nape, Januari, Ridhwani, Masauni, Beno n.k. au tayari mmejipanga kurithi na hamtaki kutia mchanga vitumbua vyenu ? Je, mnakubaliana na kauli kama hizi zisizoendana na wakati na zinazoturudisha kwenye zile tawala za kiimla ? Hamuoni kuwa hapa hamuwi tena tegemeo la taifa bali sasa mnabakia tu kama mafisadi-in-waiting mkisubiri muda wenu muafaka muendeleze yale yale ya baba zenu ?
Pilipili usioila inakuwashia nini? Sikujua kama CCM imekukaa namna hiyo!
Mbu,
Mkuu wangu nakusikia sasa hoja yangu inaambatana na matakwa yako..
Wewe na wengineo mnasema Kikwete ameshindwa ku deliver.. kitu gani mlichotaka?..
Je, ni kukomesha Ufisadi?... huyo Selelli na Mwakyembe wataweza vipi? hawa hata kukemea tu wameshindwa tena basi Mtu kama Mwakyembe ali vote against kuwajibisha viongozi..Ni wapi amesimama kuhusiana na swala lolote na Ufisadi toka Mkapa/Lowassa na Rostam..hana hata ubavu wa kuzungumza na Rostam uso kwa uso..
Ni type ya viongozi ambao kwa uzalendo wao hata akipigwa kofi hujibu namwachia Mungu atalipa..Mwinyi kind of..
He is too soft for CCM chairman acha mbali President wa nchi..
Hakuna Mtanzania yoyote aliyekatazwa na CCM kugombea urais. Bandiko hili umelibandika mwenyewe lakini naona hujalifahamu.Duh!!! Hili siyo swala la CCM tu, kama mnataka kutumia utamaduni wenu wa kuachiana ndani ya chama chenu hakuna atakayewaingilia, lakini inapokuja kwenye uongozi wa Taifa hilo ni swala la Watanzania wote.
Kwa hiyo kwa akili yako Watanzania hatuna haki ya kujadili jambo hili ambalo linatuathiri Watanzania wote with exception ya mafisadi, huku ni kuendekeza udikteta!!!!? Kazi kweli kweli!!!!
Hakuna Mtanzania yoyote aliyekatazwa na CCM kugombea urais. Bandiko hili umelibandika mwenyewe lakini naona hujalifahamu.
Kwani kuna vyama vingapi hapo TZ, mpaka mfanye issue kubwa kwa mambo ya ndani ya CCM?
Kwa ufupi wengi humu ni visebu sebu na viroho vi papo!
"Kwa kifupi ni kwamba hatuna wazee!! Hao ndio washauri? Haishangazi tupo hapa tulipo."
*************************
Mpigafilimbi: Correct kabisa, hatuna wazee, waliishia enzi yaJKN. Nakumbuka mapema miaka ya 90 wakati Mwinyi ananadi sera ya kuchangia eklimu ya juu, ktk mkutanio mmoja wa ndani na wazee wa Mbeya, alikuwa anakatizwa kwa kupigiwa makofi na vigelegele ktk hotuba yake ya kuwataka wazazi wachangie.
Hivi sasa wazee hao wanajisikia vipi watoto wao wanatimuliwa hovyo Vyuo Vikuu kwa kukosa hela za kuchangia ada! Wazee wetu siku hizi hawana maana yoyote, hawa wa CCM waliotoa tamko juzi wanaganga njaa tu, na bila shaka utakuta wamehongwa na mafisadi ili kusema.
Kwa mtindo huu tutasikia mengi siku zijazo na wengi kujitokeza ktk kampeni ya kunadi "JK TENA": Viongiozi wa walemavu, vijana, wanawake wanawake, machinga, vijana, wanafunzi etc watapewa hela na mafisadi ili waende ukumbi wa maelezo kutoa matamko ya kiajabuajabu!
Hadi sasa sijamsikia mzee yoyote wa CCM akisimama jukwaani na bila kigugumizi kuwashambulia mafisadi. Hakuna! labda Warioba na Butiku, lakini angalia jinsi mafisadi wanavyojaribu kuwageuzia vibao!
Hakuna Mtanzania yoyote aliyekatazwa na CCM kugombea urais. Bandiko hili umelibandika mwenyewe lakini naona hujalifahamu.
Kwani kuna vyama vingapi hapo TZ, mpaka mfanye issue kubwa kwa mambo ya ndani ya CCM?
Kwa ufupi wengi humu ni visebu sebu na viroho vi papo!