The road towards 2010 Elections

The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
kwani kutumikia chama lazima uwe kiongozi? Mbona sisi wengine tunatumikia chama bila kuwa viongozi? ina maana anataka kutuambia na sisi ni wafungwa ndani ya Chama? Huyu anaonesha kuwa lengo lake ni kuwa kiongozi, kwa mtaji huu anatakiwa kuwekewa viulizo.


Maana yake ni hii.
Ukiwa mwanCCM na unapenda kugombea nafasi fulani ya uongozi ni haki yako kufanya hivyo.
Ukiwa mwana CCM na huna mpango wa kugombea nafasi yeyote ya uongozi ni haki yako pia.

Yule mwenye nia ya kugombea nafasi fulani ndani ya CCM na hawezi kufanya hivyo kwa shinikizo la vijikamati, basi mtu huyo kweli ni mtumwa ndani ya CCM.Na ni mtumwa wa hiari kwa sababu chama si CCM tu.

Mtu unakuwa kiongozi kwa kuwa na lengo au malengo fulani, mazuri au mabaya bado ni malengo.
Kwa yule asiye na nia ya kuongoza na hana mpango wa kujitokeza kugombea nafasi fulani hana sababu ya kuwalalamiakia wale wanao wania uongozi Cats and Dogs kwa sababu ni haki yao ya msingi.

Kama mtu anatumikia cham kwa kuwa mwanachama wa kawaida hiyo nayo ni haki yake na pengine malengo yake yanaishia hapo.
 
--------------------------------------------------------------------------------

Akiona namna gani vipi ajiunge na CUF

TTTTEEEEHHHH MASATU UNATAKA KUMPELEKA KWENYE

SACCOS NDUGU YANGU!!!!!mhhhhhhhh mshauri chadiwema!!1
 
The way ninavyomjua huyu mkulu, nilitegemea kuwa by now angekua upinzani siku nyingi sana, nashangaa mpaka leo bado yupo CCM?


anatafuta maisha jamani!!!!!!
 
kwani kutumikia chama lazima uwe kiongozi? Mbona sisi wengine tunatumikia chama bila kuwa viongozi? ina maana anataka kutuambia na sisi ni wafungwa ndani ya Chama? Huyu anaonesha kuwa lengo lake ni kuwa kiongozi, kwa mtaji huu anatakiwa kuwekewa viulizo.

Mkuu wewe umezoea kutawaliwa lakini Shibuda kaliona hilo hataki.

Mimi naona Shibuda anaweza akawa mkombozi wa wanyonge ambao wapo wengi katika nchi hii.

Unajua ukiona mtu anapingwa vikali na viongozi waliopo madarakani ujue dhahili huyo mtu anafaa kuongoza binafsi naona Shibuda anafaa kwa hiyo amekuwa mwiba kwa watu wachache ambao wapo madarakani na baadhi wafuasi wachache kama akina Masatu,Bongolander na wengineo.......
 
Nina kijiswali kidogo, Shibuda siku hizi kaacha kale Ka-walwa konyagi? Na je ametoka au bado yumo UWT? Na ile tifu na jiraniye wa Bariadi bwana vijisenti imeeishia wapi? Otherwise people knows what is imminent!!! OR read as "Pita kwa uangalifu Matengenezo ya barabara yanaendelea"

Aache?!! Kiwanda kimefungwa? Sasa hivi anayemtia 'wazimu' si mwingine ila ni Amani Nzugile Jidulamabambasi! Tatizo ni lile lile aliloliona Mwalimu, '......... CCM ni Kokoro ..........'
 
Aache?!! Kiwanda kimefungwa? Sasa hivi anayemtia 'wazimu' si mwingine ila ni Amani Nzugile Jidulamabambasi! Tatizo ni lile lile aliloliona Mwalimu, '......... CCM ni Kokoro ..........'

Hahahaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!! Jidulamabambasi yupo mjini kumbe.
 
The way ninavyomjua huyu mkulu, nilitegemea kuwa by now angekua upinzani siku nyingi sana, nashangaa mpaka leo bado yupo CCM?

Labda nikuulize, mmeshamlipa? kwani nyie si mnakopa? unafikiri hatujui kama ccm mnakopa? Million 400 nalo ni deni, hapo sio chechi FMES. Nakushangaa na wewe kama unamshangaa Shibuda.
 
Labda nikuulize, mmeshamlipa? kwani nyie si mnakopa? unafikiri hatujui kama ccm mnakopa? Million 400 nalo ni deni, hapo sio chechi FMES. Nakushangaa na wewe kama unamshangaa Shibuda.

Hapa the ishu ni Shibuda, kama unataka mimi anzisha thread inayonihusu, ya CCM kukopa kwanza siyajui na sielewi yanauhusiano gani na hii topic? au?

Vipi mkuu mbona kwa kawaida huwa tunaheshimiana?
 
Hapa the ishu ni Shibuda, kama unataka mimi anzisha thread inayonihusu, ya CCM kukopa kwanza siyajui na sielewi yanauhusiano gani na hii topic? au?

Vipi mkuu mbona kwa kawaida huwa tunaheshimiana?

FMES

Nakuheshimu sana sana na sana kabisa kama mimi ninavyopenda kuheshimiwa.


Tatizo ambalo nimeshindwa kukuelewa ni jini gani ambavyo ulikuwa unamtetea bwaba Tanil na mamilion yake huko kwenu UVCCM. Halafu kabisa unamshangaa mwanawane Shibuda

FMES pamoja na kuheshimiana kwetu na pamoja na umaskini wetu tusikubali tu kutoa wala kupokea misaada kabisa inatufanya tunakuwa watumwa yaani haina tija. Kufa na njaa yako, mbona Mkwawa alikubali kufa? kwani alishindwa kukubaliana na wakoloni? siamini kama watu wanafanya maamuzi yao kutokana na matakwa yao ila kuna makosa yaliwapelekea au mazuri wanayofkiri kuamua hivyo.

Hivi leo nina harusi ya gharama ya milioni tano, wewe kunijua mimi, kuheshimiana na ulafi wangu ukaamua kunipa milion nne kugharamia harusi. Hivi kesho ukiniambia inataka kumkiss wetly mke wangu nitabishaaa. Pinda na Hosea wamesema kuwa mafisadi watayumbisha nchi, si kunanihiii kabisa utawala wa sheria na kukosa confidence? what the source?

Urafiki wa kweli katika ya mtu na mtu na kadhalika is always based on interest. wote wavuta bangi, walevi, malaya, mafisadi nk. haiwezakni mlevi simply bia akawa rafiki na muuza bangi, au mjasiriamali na fisadi. mifano hai USA na Osama, JK and his team, mimi niliosoma nao pr,ms,un ninao wapi? Look at you self, ni watu wangapi leo are you are best friends? count from Pr, sec, col.Na unaokutana nao hapa kazini au unapojitolea? wale nilionao since then ni wale tu ambao we have common interest.

Hoja ya Shibuda na CCM, my understanding kama wewe hujaelewa ni hivi.....

I do trust you, na unaelewa bila shaka kuwa watu wengi wapo huko CCM sio kwa kupenda ila kulinda maslahi yao. Wapo wanaotaka kutoka but wakifikiria ugali wao na maharage yao since then yanatoka CCM. sasa leo umwambie atoke?!!!!! Hivi leo Tanil ametoa mil 400 kachapisha yeye hizo noti?. JK alisema ametangaza kibiashara sasa leo mambo yanaenda kombo atatoka? si wale waliomshawishi watamwambia bosi, mzee, nk subiri tunafanya viitu? kwani anatengeneza faida ya mil 400 kwa saa? Shibuda anapingwa wilayani, mkoani sina hakika na taifa, je hajawahi kutoa mchango kama (sio kiasi, alipoweza) wa Tanil? kwani ccm ni Chechi au msikitini kuwa ametoa sadaka atalipwa ahera au paradiso? Je, kama mafisadi wengine wakipelekwa mahakamani nchi itayumba, je Shibuda nae hayumo? kama ana siri fulani kuhusu epa na kladhalika hakuna wa kumzuia asitoke kulinda hadhi ya chama na serikali?

FMES, hivi haya umejiuliza na kujijibu? mana nahisi unajua vema CCM kuliko mimi sasa nashangaa tena kumshangaa Shibuda.

Asante
 
Shibuda: Mwaka 2010 nitakuwa Obama wa Tanzania

Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Maswa (CCM), Bw. John Shibuda, ametamba kuwa anataka kuwa Obama wa Tanzania mwaka 2010 kwa kugombea uraisi na kusisitiza kuwa misukosuko inayoendelea kujitokeza nchini ni kielelezo kuwa kuna matatizo ya uwajibikaji.

"Yanayotokea sasa ni kielelezo kuwa kuna uwajibikaji wenye machukizo kwa wananchi," alisisitiza na kutolea mfano migomo inayojitokeza nchini ikiwa ni pamoja na walimu kushindwa kulipwa malimbikizo yao.

Alisema hayo jana alipofika katika ofisi za gazeti hili Dar es Salaam, kutoa salamu zake za rambirambi kutokana na kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi wa Kampuni za Business Group na Mbunge wa Mbeya Vijijini, Bw. Richard Nyaulawa.

Bw. Shibuda ambaye alijiita Obama wa Tanzania mwaka 2010, alisema CCM na Serikali yake wanahitaji kung'arishwa kwa kuondoa watu wenye machukizo kwa jamii bila kuwaonea aibu, kazi ambayo aliahidi kuifanya pindi akichaguliwa kuwa Rais mwaka 2010.

Aliongeza kuwa wakati umefika sasa dhana ya uongozi isiwe ya kiburi cha umangimeza kwa kukataa kuvuna mawazo kutoka kwa watu wenye vipaji ambao hawana madaraka ya uongozi.

Huku akizungumza kwa kujiamini, Bw. Shibuda amesema unatakiwa uongozi wa kujenga mshikamano ndani ya CCM na kuondokana na tabia ya kubebana ambayo imekithiri kwa dhana ya fulani ni mwenzetu.

Akizungumzia sakata la ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), Bw. Shibuda alionekana kusikitishwa na baadhi ya watuhumiwa kusamehewa kutokana na kurejesha fedha walizotuhumiwa kuiba.

Source: Majira
 
•
Urais CCM 2010 moto,'Sumu' ya Shibuda yaenea kwa kasi,Wagombea 2005 nao sasa waguswa

Similar Stories
• Shibuda ajitangaza 'Obama' 2010 12.11.2008 [More]
• Shibuda amtolea uvivu waziri Mathayo 02.07.2008 [More]
• UWT Dar kujadili wagombea leo 11.09.2008 [More]

* 'Sumu' ya Shibuda yaenea kwa kasi
* Wagombea 2005 nao sasa waguswa

Na Mwandishi Wetu, Jijini

HATUA ya Mbunge wa Maswa, John Shibuda (CCM) kutangaza kujitosa kwenye kinyang'anyiro cha mchakato wa kutafuta mgombea urais kwa tiketi CCM mwaka 2010 imewasha moto na kuibua hisia mbalimbali miongoni mwa wanachama wa chama hicho huku wengine wakihamasisha wagombea zaidi kujitokeza bila kuwekewa mizengwe.

Wakizungumza na gazeti hili wanachama hao, wamesema uamuzi wa Shibuda ni ujasiri na anapaswa kuungwa mkono na wanachama wengine kwani alichofanya ni kielelezo kuimarisha demokrasia ndani ya chama hicho kikongwe nchini.

Wanachama hao walisema tofauti na utaratibu wa sasa ambao si rasmi, ambapo rais aliyepo madarakani amekuwa akipitishwa bila kupingwa kugombea ili kumalizia ngwe yake ya pili, kujitokeza wanachama zaidi kugombea, kutaongeza changamoto zaidi ndani chama.

"Si kosa kwa wanaotaka kugombea kujitokeza mapema kama Shibuda hii ni haki ya kidemokrasia ndani ya chama na kama tunataka kujenga chama imara lazima, tugongane sisi wenyewe wakati wa uchaguzi, hapo tutapata wagombea makini," alisema msomaji mmoja aliyepiga simu na kujitambulisha kuwa ni kada wa CCM kutoka mkoani Morogoro na kuomba kutoandikwa jina gazetini.

Aliendelea kusema "Tuwe kama Marekani, Rais akimaliza miaka minne anarudi tena kwenye chama chake iwe Democrats au Republican, anapata changamoto ya upinzani,kama alifanya vizuri wanachama wanamchagua, kama amevurunda anaachwa."

Msomaji mwingine mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mwingira Majura, alisema hatua ya Shibuda kutangaza kugombea imefungua njia kwa wanaCCM wengine na kuwataka wote waliogombea mwaka 2005 kujitokeza tena kuomba nafasi hiyo mwaka 2010.

" Mimi nadhani wana CCM tuna woga wala na si kwamba tunafungwa na kanuni, Shibuda ni jasiri, sasa wenzake waliogombea mwaka mwaka 2005, wajitokeze kwani kufanya hivyo si kosa wala si kukigawa chama bali ni kuleta changamoto ya demokrasi ya kweli ndani ya chama na Taifa kwa jumla," alisema na kuongeza;

"Kwa mfano akina Malecela (John Malecela), Mwandosya (Prof. Mark Mwandosya), Sumaye ( Frederick Sumaye), Idd Simba, Salim ( Dkt. Salim Ahmed Salim), Kigoda (Dkt. Abdallah Kigoda) na wengine walikuwa na wanachama waliowaunga mkono wakati huo, hivyo wana haki kujaribu tena kwani mazingira ya mwaka 2005 si yale yaliyokuwepo 2005, wanaweza kuchaguliwa," alisema Majura.

Wana CCM wengine walijitokeza kwenye mchakati huo ni pamoja na Balozi Ali Karume,Dkt. William Shija, Balozi Patrick Chokala

Aliwashambulia wanasiasa na kudai kuwa mara nyingi wamekuwa wakiwakwaza washabiki na wapiga debe wao kwa kufuata taratibu ambazo zinarudisha nyuma demokrasia na kuwataka waige mfano wa Shibuda wa kuwa wazi kujitokeza kugombea.

Alisema Shibuda ameonesha kuwa ni mwanachama wa kweli anayekipenda chama chake na muumini wa kweli wa demokrasia mwenye nia njema na mustakabali wa nchi kwa kuwa muwazi na kueleza dhamira yake bila woga wala unafiki.

"Shibuda ni muumini wa kweli wa demokrasia, anakipenda chama chake, hivyo hakuna sababu ya kuogopa wala kutishwa, CCM nayo inapaswa kufungua milango zaidi ya demokrasia kwa kuwapa nafasi wanachama wake kujitokeza kugombea bila woga," alisema .

Mwanachama mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Vivian Swai alisema umefika wakati kwa wana CCM kuacha woga kama Shibuda na kuwataka viongozi wa chama hicho kukubali changamoto na kuachana na dhana ya kuona anayesimama kumpinga mtu fulani amekiuka taratibu za chama.

Vivian amekitaka pia chama hicho kuiga utaratibu unaotumiwa nchini Marekani wa kuwazungusha wanachama wake wanaogombea urais nchi nzima kuhojiwa katika midahalo mbalimbali ili kuwapa fursa wanachama kupima uwezo wao.

"Watu wajitokeze kugombea uchaguzi unapofika wala viongozi wasiwaone wanaofanya hivyo kuwa wamekiuka taratibu na vikao vya chama viwapitishe, tukiwa na wagombea wengi tutakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi kupata kiongozi bora," alisema na kuongeza;

" Nchi Marekani Obama ( Barack Obama- Rais mteule), alichuana ndani ya chama chake( Democrats) na vigogo akina Hillary Clinton, John Edward na wengine, haikuwa kazi ndogo, walifanya midahalo mikali wakavutana sana, ndio maana alipowashinda wenzake, alipokwenda kwenye urais alishinda kwa kishindo kwasababu alishaonesha ubora ,"alisema mwanachama huyo.

Akizungumza na gazeti hili leo asubuhi, Shibuda amesema amepokea simu nyingi za wanachama wa chama hicho wakimpongeza kwa hatua yake ya kuwa muwazi na kutangaza kupambana na Rais Kikwete kwenye uchaguzi mkuu ujao ndani ya CCM na kusisitiza kuwa jambo hilo si dhambi na ni haki ya msingi kwa kila mwanachama.

Aliwata wanachama wengine kujitokeza na kutangaza mapema nia yao ya kugombea wasisemee pembeni kwani alisema hiyo ndiyo namna bora ya kumuenzi Baba wa Taifa marehemu Mwalimu Julius Nyerere aliyewahi kutamka kwamba anayetaka kugombea urais wa nchi yetu ajitokeze mapema ili wananchi wamjadili.

Shibuda alisema jambo muhimu katika Tanzania ya sasa ni kujenga ustawi wa jamii, uchumi wa kaya, uwajibikaji makini na maendeleo kwa mustakabali wa mazingira nchi.

Shibuda alisema uongozi bora wa kutojenga matabaka ndani ya jamii ambayo huzaa mafarakano kama ilivyozaa neno 'mtandao' na kaulimbiu ya 'uanamtandao.'

Alilalamika na kudai kuwa mtandao umezaa utamaduni wa kubaguana ndani ya chama hicho na kusisitiza chama hicho kinapaswa kuzingatia lengo kuu la uhuru wa nchi yetu ambalo ni umoja na maendeleo.

Alisema dira ya Watanzania ni kujenga mshikamano na kupiga vita vishawishi vyote vya kutugawa nakuleta mpasuko ndani ya jamii.

Naye Samweli Mwanga kutoka Maswa anaripoti kuwa kauli ya Shibuda kutangazakugombea urais kupitia CCM imepokelewa kwa hisia tofauti na wakazi wa jimbo hilo .

Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti mjiniMaswa baadhi ya wakazi hao walisema uamuzi huo ni mzuri huku wengine wakidai kuwa ni mapema mno kutangaza nia yake hiyo.

Bi Vivian Kombo mkazi wa mjini Maswa alipongeza uamuzi huo kwa kueleza kuwa Bw. Shibuda ametumia uhuru wake kama mwanachama kikatiba wakugombea nafasi yoyote ndani ya CCM hivyo asionekane kama msaliti.

"Mimi naona uamuzi wa Mbunge Shibuda kutangaza nia yake ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu kupitia CCM ni mzuri kwani ametumia uhuru wake kama mwanachama hivyo asionekane kama msaliti,"alisema.

Alisema kuwa kwa sasa ndani ya CCM inaonekana wazi mwanachama yoyote anayeonekana kutaka kumpinga Rais Kikwete katika uchaguzi mkuu ujao ndani ya chama anaonekana kama msaliti jambo ambalo linatishia uhuru wa demokrasia .

Aliongeza kwa kueleza kuwa kwa sasa utawala wa Rais Kikwete umeyumba hivyo katika kipindi kingine tunahitaji kuwa na Rais mbadala ambaye ataweza kutatua kero za Watanzania ambazo kila kukicha zimekuwa zikiongezeka.

Naye Juma Masanja alisema kuwa uamuzi aliouchukua Shibuda ni mfano wa kuigwa wa ujasiri hali hiyo imetokana na makundi yaliyojitokeza ndani ya CCM huku Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Rais Kikwete akiyatazama.

"Shibuda ni jasiri na hawa ndiyo viongozi tunaowahitaji wanaothubutu kuweka bayana nia zao za kuwania nafasi mbalimbali na haya yote yanatokana na makundi ndani ya CCM ambayo Rais Kikwete kila siku amekuwa akiyatazama bila kuchukua hatua zozote,"alidai.

Alisema kuwa Mbunge huyo tangu amechaguliwa amekuwa akikabiliwa na misukosuko mingi ndani ya chama hicho huku jina lake likikatwa mara kwa mara katika vikao vya juu vya chama hicho katika nafasi mbalimbali anazoomba ndani ya chama hata kufikia hatua ya kuitwa mfungwa wa kisiasa ndani ya CCM

Baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo walisema kitendo cha Mbunge huyo kutangaza kumpinga Rais Kikwete katika uchaguzi huo si kizuri na kinaoneesha wazi ndani ya chama hicho kuwepo kwa mgawanyiko mkubwa hali ambayo isipodhibitiwa inaweza kukigharimu cha hicho.

"Mimikauli ya Shibuda sikubaliani nayo ya kumpinga Rais Kikwete kwani hali hii inadhihirisha wazi kuwa hali si swari ndani ya CCM hali hii isipodhibitiwa mapema huenda ikakigharimu chama hicho katika uchaguzi mkuu mwaka 2010,"alisema Johson George.

Alisemakuwa licha ya kuwa hakuma mwanachama wa CCM mwenye hatimiliki na chama hicho nivizuri utaratibu ukafuatwa uliozoeleka wa kila Rais kutawalakatika vipindi viwili kuliko kuanza kumpinga mapema.

Naye Esteria Mkama alisemakuwa muda wa Bw Shibuda kuwania Urais haujafika kwani bado wakazi wa Wilaya ya Maswa wanamhitaji kuwatumikia katika kipindi kingine ili aweze kukamisha mipango yake aliyoaanza kuifanya.
 
Shibuda you are a man!! Kindly stay in CCM make sure you convince other CCM members to be like you! when times come please, just do as Mrema did in 90s.

cheers
 
1.
FMES

Nakuheshimu sana sana na sana kabisa kama mimi ninavyopenda kuheshimiwa.
Tatizo ambalo nimeshindwa kukuelewa ni jini gani ambavyo ulikuwa unamtetea bwaba Tanil na mamilion yake huko kwenu UVCCM. Halafu kabisa unamshangaa mwanawane Shibuda

Sawa sawa nimekusikia mkuu, naomba kuweka sawa kama ifuatavyo:-

1. Suala la Somaiya kutoa sh. Mill 400, kwangu sijaliona kua ni tatizo kwa sababu so far Tanzania hatuna sheria ya kukataza misaada ya wananchi kwa vyama vyetu vya siasa, nijuavyo mimi ni kwamba vyama vyetu vyote kuanzia upinzani mpaka CCM hupokea misaada mbali mbali toka nje na ndani ya nchi yetu, Mrema for the record alipewa hela nyingi sana na Scandnavians, pamoja na chama kimoja cha South Africa, hakukuwa na ubaya wowote, nitakuwa na tatizo kama tungekua na sheria, lakini ya kupewa misaada inafanyika kila siku na tunajua sana ila haisemwi tu hadharani na hatusemi kwa sababu haivunjwi sheria ya jamhuri na hiyo misaada.

- Mimi sikumtetea mtoaji wa msaada, siwezi kumtetea mtu ambaye sifahamu vizuri habari zake, sidhani kama kuna asiyeelewa hilo lakini siwezi kukataa msaaada wa mwananchi bila sababu ya msingi kama sheria inaruhusu, sasa labda wewe uniambie kosa la huyu mwananchi aliyetoa msaada ni lipi kwa sababu siamini kwamba kuwa Mhindi ukatoa msaada kwa chama cha siasa ni kosa.


2.
FMES pamoja na kuheshimiana kwetu na pamoja na umaskini wetu tusikubali tu kutoa wala kupokea misaada kabisa inatufanya tunakuwa watumwa yaani haina tija. Kufa na njaa yako, mbona Mkwawa alikubali kufa? kwani alishindwa kukubaliana na wakoloni? siamini kama watu wanafanya maamuzi yao kutokana na matakwa yao ila kuna makosa yaliwapelekea au mazuri wanayofkiri kuamua hivyo.

- Kupokea msaada kwangu sio kuwa mtumwa, tatizo ni kama ni mtumwa siku zote, maana msaada wa siku moja hauwezi kukugeuza ukawa mtumwa mwananchi ambaye hujawahi kuwa mtumwa. Obama ameshinda kwa kusaidiwa sana na misaaada sasa unasema kwamba atakuwa mtumwa kwa waliompa misaaada? Unafikiri FBI itamuacha? Hapana bro hapa tatizo hakuna kabisa ila tunajaribu kulazimisha kwa sababu hatuaminiani, na tatizo ni kwamba hatuna sheria na hata kama ingekuwepo haifuatwi, sasa hilo lisiwazuie wananchi kutoa misaada kwa sekta muhimu za taifa zinazohitaji misaada. Mimi siwezi kukataa msaada kama nina shida, ila sitakubali masharti ya msaada maana ni afadhali nikachukue mkopo if that is the case, lakini mifano ya njaaa za binafsi haiwezi kuhusishwa na siasa za taifa.

- Mimi ningeelewa kwamba huyu Mhindi ni proven fisadi, au ana kesi tayari, lakini the man is clean as mwananchi, sasa what is the beef? Unless kuna something hamukisemi!

- Ndugu yangu Mkwawa has nothing to do na this, hivi unajua kuwa akifufuka leo atajiua tena kukuta wananchi weusi wameoa wazungu, licha ya hayo unayoyasema?


3.
Hivi leo nina harusi ya gharama ya milioni tano, wewe kunijua mimi, kuheshimiana na ulafi wangu ukaamua kunipa milion nne kugharamia harusi. Hivi kesho ukiniambia inataka kumkiss wetly mke wangu nitabishaaa. Pinda na Hosea wamesema kuwa mafisadi watayumbisha nchi, si kunanihiii kabisa utawala wa sheria na kukosa confidence? what the source?

- Hapa sijakuelewa kabisa, una maana watu wanaotoa michango mikubwa kwenye harusi za wengine basi ni haki yao kuwaomba wake wa harusi? Is that so? Hivi unajua Mengi hutoa hela nyingi sana kusaidia harusi za wananchi, sasa unasema nini exactly?

- Pinda na Hosea wanaweza kusema anything they want, sisi tutawahukumu kwa matendo yao, kwenye ufisadi Hosea hana credibility kabisa, angalau kidogo Pinda hatujamsikia, lakini na yeye ni muoga, anawaogopa mafisadi, sasa what this has to do na Somaiya kutoa msaada kwa CCM?


4.
Urafiki wa kweli katika ya mtu na mtu na kadhalika is always based on interest. wote wavuta bangi, walevi, malaya, mafisadi nk. haiwezakni mlevi simply bia akawa rafiki na muuza bangi, au mjasiriamali na fisadi. mifano hai USA na Osama, JK and his team, mimi niliosoma nao pr,ms,un ninao wapi? Look at you self, ni watu wangapi leo are you are best friends? count from Pr, sec, col.Na unaokutana nao hapa kazini au unapojitolea? wale nilionao since then ni wale tu ambao we have common interest.

- Hii point ingekua na nguvu sana kama Somaiya ni proven mwizi au jambazi, lakini huyu amehojiwa na wazungu hawakumshitaki lakini wamemshitaki patner wake, I mean ninaelewa kwamba kuna some hisia, sasa in absence of sheria ya kubana hii misaada as a nation tunafanya nini? Hatuwezi kushambulia chama cha siasa kwa kupokea msaada legally na pia hatuwezi kumshambulia mtoa msaada eti kwa sababu ni Mhindi!

- I mean with all due respect na mifano ya binafsi, lakini haina uhusiano wowote na national politics zetu, ni kwamba kuna ishu moja wengi hamtaki kuiona hapa ni kwamba Tanzania hatuna sheria inayokataza wananchi kutoa misaada kwa vyama vyetu vya siasa, na hakuna sheria inayokataza vyama kupokea msaada, na hii misaada inapokewa na vyama vyote nchini,

Kwa hiyo kwangu tatizo ni sheria, kwa sababu sio siri kwamba Mtandao walipewa hela na Iran za kampeni, lakini still bado hawakuvunja sheria zetu kwa kupokea misaada hiyo, katiba mbovu ndiyo inayotuletea matatizo, maana in the absence of respect kwa rule of law ndio hivi sasa tunashitukiana, na hatuaminiani sasa badala ya kugusa panapotakiwa tunalaumu kila mtu bila sababu, tatizo mkuu wangu ni kwamba hatuna sheria ya kubana misaada!


Kumtetea fisadi hata siku moja, lakini pia siwezi kumchukia mwananchi bila ya sababu, au kwa sababu ana hela nyingi za kutoa msaaada hapana, lakini pia ninakuelewa sana, ingawa sikubaliani na mawazo yako ambayo ninayaona ni model ya kuhisi na kuhukumu, bila sababu ya msingi.
 
Hoja ya Shibuda na CCM, my understanding kama wewe hujaelewa ni hivi.....
I do trust you, na unaelewa bila shaka kuwa watu wengi wapo huko CCM sio kwa kupenda ila kulinda maslahi yao. Wapo wanaotaka kutoka but wakifikiria ugali wao na maharage yao since then yanatoka CCM. sasa leo umwambie atoke?!!!!! Hivi leo Tanil ametoa mil 400 kachapisha yeye hizo noti?. JK alisema ametangaza kibiashara sasa leo mambo yanaenda kombo atatoka? si wale waliomshawishi watamwambia bosi, mzee, nk subiri tunafanya viitu? kwani anatengeneza faida ya mil 400 kwa saa? Shibuda anapingwa wilayani, mkoani sina hakika na taifa, je hajawahi kutoa mchango kama (sio kiasi, alipoweza) wa Tanil? kwani ccm ni Chechi au msikitini kuwa ametoa sadaka atalipwa ahera au paradiso? Je, kama mafisadi wengine wakipelekwa mahakamani nchi itayumba, je Shibuda nae hayumo? kama ana siri fulani kuhusu epa na kladhalika hakuna wa kumzuia asitoke kulinda hadhi ya chama na serikali? FMES, hivi haya umejiuliza na kujijibu? mana nahisi unajua vema CCM kuliko mimi sasa nashangaa tena kumshangaa Shibuda.

Asante

Ninataka kuamini kwamba nimekuelewa, Shibuda nimesema he is a good man kwa sababu ninamfahamu sana binafsi, lakini kwenye uongozi sina uhakika naye kwa sababu simuelewi kabisaa what he stands for,

Kwa taarifa yako ni kwamba leo nimeongea naye sana na kwa muda mrefu sana, nilichomuomba ni kimoja tu kwamba ajaribu ku-define msimamo wake upya, aachane na yaliyopita na aweke chini msingi mpya wa what he stands for, leo nimeona magazeti yenye habari zake ambazo somehow zinatenganisha his old self na Shibuda mpya, lakini sijasoma kwa makini,

Sasa Shibuda akisimama na hoja mpya zinazoeleweka, akaachana na za zamani zisizoeleweka, sina tatizo kum-support tena kwa 100%, sijasoma vizuri hoja zake mpya za kutaka urais, nikishazisoma nitakuja na majibu of what I feel na nitawasiliana naye in personal, I hope umenielewa ndugu yangu!

Simchukii Shibuda, lakini siyakubali matendo yake mengi yaliyopita kisiasa kwa sababu hayajawahi kuwa wananchi, ila yeye tu Shibuda na uongozi tu!
 

Simchukii Shibuda, lakini siyakubali matendo yake mengi yaliyopita kisiasa kwa sababu hayajawahi kuwa wananchi, ila yeye tu Shibuda na uongozi tu!

Sound good and reasonable answer! FMES can you tell us what kind of statements do you think Shibuda should made? Whata is he suppose to say that will make you mind change? By the way do you want him to repeat the very touching and vain words as Kasi mpya, nguvu mpya hali mpya?

I still not get you mkuu! are you in JK's side if you are Shibuda's advisor whta could you advise him?

Englisher

'English is not my mother land'
 
1.
Sound good and reasonable answer! FMES can you tell us what kind of statements do you think Shibuda should made? Whata is he suppose to say that will make you mind change?

Simply kuweka wananchi mbele, kwa sababu it has always been about him na uongozi tu! Huko bungeni ana nafasi nzuri sana kuyafanya haya ya kuwaweka wananchi mbele.

2.
By the way do you want him to repeat the very touching and vain words as Kasi mpya, nguvu mpya hali mpya? I still not get you mkuu! are you in JK's side if you are Shibuda's advisor whta could you advise him?

Englisher

'English is not my mother land'

1. Hayo maneno ya kasi mpya na the rest of story, hayanihusu ni yako mkuu.

2. Jk ni mwenyekiti wa chama changu, na ni rais wa Jamhuri yangu anapofanya mazuri ninasema anapofanya mabaya ninasema tena sana, na kutafuta kila njia kuwafikishia wasaidizi wake, au yeye mwenyewe na anybody can do that sio crime! Wala anything ila ni uchungu na taifa langu au lako pia, au? Na siku zote niko side ya wananchi na taifa, sio viongozi au chama!

3. Shibuda anahitaji kuwa na hoja zinazowajali wananchi kwanza, badala ya yeye binafsi, hilo limekua likimpa taabu kwa muda mrefu saana sasa!

Ahsante Mkuu!
 
Sound good and reasonable answer! FMES can you tell us what kind of statements do you think Shibuda should made? Whata is he suppose to say that will make you mind change? By the way do you want him to repeat the very touching and vain words as Kasi mpya, nguvu mpya hali mpya?

I still not get you mkuu! are you in JK's side if you are Shibuda's advisor whta could you advise him?

Englisher

'English is not my mother land'

Seconded.

Let Shibuda be his own man. Let everyone be their own for that matter.

Times are up for spoon-fed politics. The times are too serious for cheap politics.

For nearly half a century Tanzanians or Tanganyinkans have heard of "CHANGES" and slogans they can't belive in.

Now people are beginning to "BELIEVE" no one is infallible.

We have had mini-gods with their "Zidumu Fikra". Look where they got us: NOWHERE...
 
Shibuda anaishi Upanga. Anapaki gari yake ofisi ya CCM Upanga. Nasikia,from ususally relable sources, anafika pale usiku wa manane amelewa chakari,analala ndani ya gari mpaka asubuhi.

Siyo vizuri mtu kama huyu aseme kwamba anataka kugombea Urais,kwa sababu watu wa kazi nyingi za kufanya,hawataki kusikia mtu anaongea mambo tu yasiyokuwa na maana.

Kwa hiyo, nadhani nimewaokoa wale waliokuwa wanataka kumfadhili huyu. Sasa sijui jambo gani litafuatia, nitapelekwa mahakani kwa kashfa. Kwanza niseme huyu Shibuda simfahamu, akipita mbele yangu sasa hivi, simfahamu.
 
Shibuda anaishi Upanga. Anapaki gari yake ofisi ya CCM Upanga. Nasikia,from ususally relable sources, anafika pale usiku wa manane amelewa chakari,analala ndani ya gari mpaka asubuhi. Siyo vizuri mtu kama huyu aseme kwamba anataka kugombea Urais,kwa sababu watu wa kazi nyingi za kufanya,hawataki kusikia mtu anaongea mambo tu yasiyokuwa na maana. Kwa hiyo,nadhani nimewaokoa wale waliokuwa wanataka kumfadhili huyu. Sasa sijui jambo gani litafuatia,nitapelekwa mahakani kwa kashfa. Kwanza niseme huyu Shibuda simfahamu,akipita mbele yangu sasa hivi,simfahamu.

Kazi kweli kweli.... sasa kama humfahamu hata akipita mbele yako hayo ya kulala ndani ya gari umeyapata wapi?
 
Back
Top Bottom