Mpaka Kieleweke
JF-Expert Member
- Feb 27, 2007
- 4,132
- 1,580
Basi ni uamuzi mzuri sana.Hata hivyo tufikie mahali tuwe wakweli.Hivi Zitto hilo suala alivumishiwa? ok,yeye nakumbuka alisema aliongea na yule mwamndishi wa habari ila hakufanya press comference lakini mwandishi akaibeba kama alifanya nae press comference.Hata hivyo zitto atafanya jambo la maana sana kama safari hii atafanya press comference atangaze msimamo ili kuondoa comfussion na saije akashabihiana na CCM.Mzee zitto heshima yako mkuu,jaribu tu kuweka mambo clear mapena kwani kwa uzoefu wangu nadhani mabo kama haya yana madhara sana kisiasa
Kuna mambo mawili hapa, maana Zitto alinukuliwa akisema hivyo, na mojawapo ya magazeti yaliyoandika habari ni Daily News (la serikali). Lipo na jingine la Kiswahili silikumbuki.
Hoja zaweza kuwa mbili.
1. Alikuwa akidokeza kwamba jimbo si mali yake, na kwamba anaweza (hata) asigombee ubunge mwaka 2010 ali ajiendeleza kielimu na kujenga chama chake, jambo aliwahi kulisisitiza. Wao wakachukua hiyo, wakasema: "Asema hatagombea." Sensationalism!
2. Ilikuwa dhamira yake kabisa kwamba hagombei 2010 ili akasome au afanye shughuli nyingine. Kwa hiyo atakuwa amebadili msimamo, jambo ambalo ni la kawaida.
Kwa vyovyote vile, kauli yake hii haiwezi kupuuzwa,, lazima iungwe mkono. Hatuwezi kukubali kumpoteza akiwa ndo anahitajika. Agombee tena walau kipindi kimoja tu, aache aende afanye kazi zake.
Huyu chenge ana kitu gani kinamlinda, mbona anasema yeye hajali , hizi tiuhuma ni ukweli mtupu kwani kwa hawa wanasheria wawili kutokutaka kwenda mahakamani kinamaanisha kuwa wanajua kuwa huku ushahidi utaytolewa na wataumvbuka zaidi na hivyo kumlazimisha hata jk awatimue.
Baada ya watu kunivumishia kwamba sitagombea mwaka 2010 kwa sababu ambazo wenyewe walitaka kuzisema natangaza rasmi kwamba nitasimama mwaka 2010.Huu ni uamuzi wangu mwenyewe na pia maombi makubwa toka Jimboni kwangu .Wazee wa Jimbo langu wamenifuta hapa nyumbani kwangu.Haya ni maneno ya Zitto mwenyewe ananieleza haya .Zitto anaendelea kusema kwamba anaamini mwaka 2010 kutakuwa na wabunge wengi zaidi vijana wa Upinzani so nataka kuwapo tuenmdelee kuitetea Tanzania yetu kwa ajili ya watoto wetu na vizazji vijavyo.Zitto anahitimisha kwa kusema mniombee kwa Mungu .
Mimi nasema Homgera Zitto kwa kutoa msimamo wako huo .
Mimi naamini unaweza kuwa kwenye siasa na bado ukawa mkweli, nina wasiwasi kwenye thread hii ukweli ni adimu mno.
Kuna watu walitaka kumlisha Zitto maneno, lakini naona ameshaweka mambo sawa, tena timely. Hiyo ndiyo tunaita responsible politics, kitu ambacho ni adimu sana kukipata kwa wenzetu wa CCM!
Napenda ifahamike kwa uwazi kabisa kuwa maneno ya kutogombea sikusingiziwa. Nilitamka mwenyewe. Ingawa mwandishi alitumia ukaribu wetu na hivyo kupata habari hiyo na akaiona ni scoop, akaandika. Hata hivyo nilisema sitagombea. Sababu za kutogombea nilizitoa.
Ni kweli kuna shinikizo kubwa kutoka katika chama, marafiki na wazee Jimboni kuwa nifute kauli ile. Wazee wa chama chini ya Mzee Mtei wamenikalisha chini na kunisihi kuondoa msimamo huo. Kama kiongozi ni lazima nisikilize. Ingawa sikuombwa na mtu kugombea Ubunge 2005, lakini ndio hivyo tena ukishakuwa Kiongozi si wewe tena. Maamuzi ni lazima yaangalie matakwa ya jamii. Nimeshauriwa na nimesikiliza. Hata hivyo sijatoa kauli rasmi juu ya hilo. Ni lazima nijue yale niliyopanga kufanya after 2010 nitayafanyaje nikiwa bado Mbunge. Kwa kuwa bado sijatoa kauli rasmi, msimamo wangu bado upo palepale.
Jambo la msingini kuzingatia kuwa, sikuwekewa maneno mdomoni. Nilisema sitagombea. Ni rahisi sana wanasiasa kukana maneno yao. Mimi najiepusha na hilo. Wakati mwafaka nitasema!