Mwaka 2010 ni mwaka wa kuongeza vijana bungeni wenye kuweza kukabiliana na mshike mshike wa siasa za kidunia za ushindani. Vijana hao wanaweza kupitia chama chochote makini Tanzania.
Katika ya changamoto inayokwamisha vijana kushinda chaguzi ni ukosefu wa rasilimali. Je, vijana wanaweza kukukabiliana vipi na changamoto zinazokabili? Je mikakati kama huu wa CHADEMA unaweza kusaidia?
Tujadili. Sasa ni Julai 2008, miaka miwili kabla ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Kwa wale wanaowaza kugombea huu ndio wakati wa kuvaa jezi na kuanza kupiga jaramba.
Na kwa wale wanawake wenzangu, safari hii tusisubirie viti maalumu, hebu tujiandae tujitose majimboni. Kama wao wanaweza wananini hata sisi tushindwe tuna nini?
Huu ni mfano tu toka kwa CHADEMA "Nachukua fursa hii kukumbusha tena dhamira ya mfuko wetu. Mfuko wa Vijana na Ubunge ni mfuko unaounganisha wafanyakazi wote wa Tanzania, waliodhamiria kwa dhati kuunganisha uzalendo wao kwa manufaa ya taifa lao, kwa kuchangia raslimali na ustadi wao wa kitaaluma ili kufanikisha azma ya kuongeza Wabunge Vijana kuanzia mwaka 2010 kupitia chama mbadala - CHADEMA. Mfuko huu ni wa jumuia ya siri ya vijana wafanyakazi inayojulikana kama Y4C (Youth for Change) ambayo iko chini ya kurugenzi ya vijana wa CHADEMA. Dira ya mfuko huu ni kuwa na; Bunge lenye uwakilishi mzuri wa vijana, lenye ushindani, na lenye kusimamia kikamilifu utendaji na uadilifu wa serikali kwa manufaa ya umma. Mfuko utatunisha angalau Tsh. Bilioni moja ndani ya kipindi cha miaka 3, kwa kuanzia mwaka 2008 - hadi Septemba Mosi 2010. Wazalendo 4,000 kama wewe watafikiwa nchi nzima na mfuko huu ambapo kila mmoja atachangia walau laki moja kwa mwaka ama elfu kumi kwa mwezi. "
Nimeipata toka:
http://www.chadema.net/mabaraza/bavicha/08/waraka1.php
http://www.chadema.net/mabaraza/bavicha/08/waraka1.php
http://www.chadema.net/mabaraza/bavicha/08/waraka1.php
http://www.chadema.net/mabaraza/bavicha/08/waraka1.php
Lakini CHONDE, vijana hao wawe makini kama wakina Zitto wasiwe kama wakina Peter Serukamba maana watatuabisha zaidi na kulitia hasara taifa.
Je, kuna upekee wa kuwa na wabunge vijana ambao unaweza kupatikana tofauti kuwa na wabunge lilijaa wazee?
Je, sasa hivi- tuna wabunge wangapi vijana kwa maana ya miaka kati ya 18 mpaka 35? Tunaweza kuwataja kwa majina?
Manake nasikia bungeni letu zaidi ya robo tatu ya wabunge ni kati ya miaka 50 na kuendelea. Yaani bunge la wastaafu!
Asha