- Feb 10, 2006
- 4,542
- 16,810
Mheshimiwa Kuongoza ni tofauti na Kukosoa. Kukosoa ni rahisi kuliko kuongoza. Unaweza kuwa bingwa wa kukosoa, lakini tabaan ukawa tobwe katika mkuongoza. Jee una hakika na Waheshimiwa (ma-champion wako) hao ambao umebaini kuwa ni mabingwa wa Kukosoa?
Mac,
Kama ulivyosema ni kweli wengi tumechoshwa sana na mambo yanayoendelea nchini mwetu. Mimi siku zote sipendi kujihusisha na siasa na huona siasa ni kama mchezo mchafu lakini nadhani imefika kikomo sasa. Naamini kabisa ni sisi wenyewe Watanzania ndio tutakaoweza kubadilisha hali inayoendelea nyumbani, Ni sisi wenyewe wenye moyo wa uzalendo na nchi yetu ndio tunaoweza kubadilisha mweleko wa nchi yetu. Tanzania inadidimia kila siku baada ya siku, wananchi wanazidi kuwa masikini, hali ya maisha inazidi kuwa ngumu kila siku ilhali kundi la watu wachache pale nchini linazidi kujitayarisha kwa kutumia migongo ya watanzania wote. Siasa za Tanzania zimekuwa mahali pa kuchumia na kujilimbikizia utajiri, unyonyaji na ufisadi ndio umekithiri. Ni sisi wenyewe ndio tunaoweza kuitoa nchi hii kwenye hili dimbwi la matatizo. Muda ndio huu na hakuna kungoja. CCM Has to Go, Kikwete Has to Go !!
Dr Slaa alikuwa katibu wa Baraza la Maaskofu(TEC) kwa nafasi yake alisimamia vizuri sana mipango na miradi ya kanisa katoliki. Na kwa yoyote anayejua hairakia ya kanisa hilo atajua kwamba huyu jamaa ameshaongoza na kuratibu mtandao karibu sawa na uwaziri mkuu wa nchi ama hata urais. Sasa tumpime kwa ufanisi wake huko. Lakini mimi nina wasiwasi kwamba kutokana na kuwa alikuwa padri wa kanisa katoliki lazima atakuwa Rais mdini anayependelea zaidi wagalatia!
PM
Dr Slaa alikuwa katibu wa Baraza la Maaskofu(TEC) kwa nafasi yake alisimamia vizuri sana mipango na miradi ya kanisa katoliki.
Na kwa yoyote anayejua hairakia ya kanisa hilo atajua kwamba huyu jamaa ameshaongoza na kuratibu mtandao karibu sawa na uwaziri mkuu wa nchi ama hata urais. Sasa tumpime kwa ufanisi wake huko.
Lakini mimi nina wasiwasi kwamba kutokana na kuwa alikuwa padri wa kanisa katoliki lazima atakuwa Rais mdini anayependelea zaidi wagalatia!
PM
Siamini hivyo kuwa kutokana na Upadri wake atakuwa ni Mdini. Dr. Slaa amekuwa akipigania watanzania bila kujali dini zao. Dr. Slaa alisimama kidete kutetea rasilimali zetu bila kujali itikadi za dini zetu. Dr. Slaa amewaumbua MAFISADI na WANYONYAJI wa CCM ilihali viongozi wa Kikristo na Kiislamu walikuwa wamezubaa wakiendelea kumpigia vigelegele na kumkumbatia Rais Kikwete. Viongozi wa dini wamekuwa kimya kwa muda mrefu bila kusimama kidete kutetea haki za watanzania. Naamini Dr. Slaa anaweza na atasimamia haki kwa wote. Dr. Slaa for President.
WAPI PAPAA KADA MPINZANI?
Jamani KADA ametimua kweli nini maana watu wamempamba kwenye hii threads lakini kakaa kimya dah, WE MISS YOU, WE LOVE YOU WE NEED YOUR COMMETS ingawa some times unaboaga lakini bado tunahitaji chalenges zako mheshimiwa sana, pls come on sir...........
Ni vigumu sana kuwashinda hawa Mafisadi kwa sasa katika post ya Upresident, ukizingatia watatumia pesa za BOT kuwadanganya watanzania, na ikibidi za kina Chenge na lowassa.
Ninachoweza kushauri ni kuwa pale ambapo wapinzani wanaweza kufika inabidi wafanye nchini juu kuwaelimisha wananchi wa maeneo hayo na kushinda ubunge, hii itasaidia sana ukikuta sehemu nyingi zina upinzani, itawasaidia pia wao kuweza kupata nguvu pia za kuweza kucompete zaidi next time
Ulivyosema huna habari zake nikaingia kwenye google search kwa kuangika maneno dr Wlbroad Slaa, angalia ana blogspot lakini hajapost kitu,http://www.chadema.net/blogu/slaa/
Google search yangu nimeieneleza kwa jina la manaJF aliyenikuna kwa itikadi yake aliyoipost humu JF,nimesearch kwa jina la kahangwa,nikagundua yawezekana ndio George Kahangwa,naona naye ana blogspot kwa jina hilo hilo.samahani kama sio yeye,but I see something in this JF member by that name
Nimesoma michango yote. Nawatakia mjadala mwema
JJ
JJ unaoppose au unasupport mada ya Dr Slaa kugombea Urais 2010?
Mama
Naunga mkono mada kuendelea kujadiliwa na mawazo ya pande zote kuendelewa kutolewa; ama kuhusu maoni yangu, naomba nisiyatoe kwa sasa.
JJ
Nimekusikia mdogo wangu, Mimi naoppose mada.
Natumaini hupingi mada kujadiliwa; unapinga suala la yeye kugombea. Ni nzuri, hayo ni maoni yako-unaweza kuyakubali kwa upande wako lakini wenzako wasiyakubali kwa upande wao. Ndio maana nikasema naunga mkono huu mjadala uendelee. Mpaka siku, tutakubaliana au tutakubaliana kutokubaliana. Wakati mwafaka ukifika nami nitatoa maoni yangu kama mwanachama.
JJ
Dr Slaa alikuwa katibu wa Baraza la Maaskofu(TEC) kwa nafasi yake alisimamia vizuri sana mipango na miradi ya kanisa katoliki. Na kwa yoyote anayejua hairakia ya kanisa hilo atajua kwamba huyu jamaa ameshaongoza na kuratibu mtandao karibu sawa na uwaziri mkuu wa nchi ama hata urais. Sasa tumpime kwa ufanisi wake huko. Lakini mimi nina wasiwasi kwamba kutokana na kuwa alikuwa padri wa kanisa katoliki lazima atakuwa Rais mdini anayependelea zaidi wagalatia!
PM