The Rise and Fall of Paul Makonda (Dar RC)

The Rise and Fall of Paul Makonda (Dar RC)

If you want to test a man's character give him power

ABRAHAM LINCOLN

Unaccommodated man is no more but such a poor bare,
forked animal
KING LEAR : Act III, scene iv
​

Sipendi kuandika political obituaries lakini kwa huyu mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam (Paul Makonda ) Sidhani kama atamaliza ngwe yake na Magufuli let alone kama atamaliza miezi 12 mayo katika jiji la Dar es salaam kama mkuu wa mkoa kwa sababu naamini kabisa kuwa Rais Magufuli kashaona kuwa Makonda isnt up to the job na mbaya zaidi Magufuli kashashtuka na hataki tena haya mambo ya kusifiwa sifiwa na kupambwa badala yake anataka kuona results baada ya kumpa cheo kuongoza jiji lenye watu karibu milioni 10.

Maguli alimpatia ukuu wa Mkoa wa Dar baada ya Makonda kuonyesha kumpa illusion kuwa ni mchapa kazi lakini ukweli usiopingika ni kuwa Makonda has failed na sasa hivi tumeishia kupewa PR stunts, na maneno mengi yasiyo na substance....
Majungu hayatakufikisha mbali.
 
we we unaponda tu mbona hausemi kuwa anajali watumishi kama mwalimu,kamsaidia yule alotobolewa macho milioni kumi,vipanya road vilianza kuzuka kavidhibiti,mwacheni Mtoto wa watu afanye kazi kama mmeanza lugha za ushawishi kwa Rais wetu kipenzi amtoe hawezi anawafahamu watanzania vizuri Hamna jema.acheni majungu.
Wapo wengi tu waliopata madhara km huyo jamaa.. Kama Angekuwa smart zaid angeanzisha mfuko ajili ya watu wa aina hiyo
 
Bw makonda, kinachomsumbua ni siasa katika kazi vile vile kupenda sifa asizostahili mbele ya wananchi, jiji /nchi linahitaji muongozo na malengo yake bila kujali itikadi za mamea, wakuu wa wilaya na wabunge wa jiji hili. Mambo ni mengi ila namshauri Bw makonda angejiwwekea vipaumbele kwa muda fulani, usafi, usalama, foleni, wafanyabiashara na usafirri, ni mambo ya kila siku yanayogusa wwananchi na yanahitaji mapinduzi. Mambo ya shisha wale asitumie nguvu nyingi kupayuka hadharani badala yake ajipange na timu yake ya usalama/polisi kufanya operation maalumu tena kimya kimya, matendo yake yaongee zaidi kuliko maneno mengi kwny vyombo vya habari. Ushauri wangu kwako Bw. Makonda
 
..tatizo la makonda ni kupingana na wabunge ,mameya, na madiwani wa ukawa.

..mapendekezo yako yangeweza kufanyiwa kazi kukiwa na ushirikiano baina ya wabunge/mameya/ madiwani wa ukawa na mkuu wa mkoa/wakuu wa wilaya toka ccm.

..makonda anataka kuwaonyesha wananchi wa dsm kwamba wabunge mameya na madiwani waliowachagua hawana manufaa yoyote.
naona sasa anapigana na polisi wa dar,kaanza na kamanda wao,hii kwa kweli ni hatari.

unapofanya jambo lolote katika vyombo vya dola vizuri uwe makini sana usije ukavivunja morali.

hawa watu kila siku wanakwepa risasi za majambazi,wananusurika kifo,hata kama wana tatizo,kuna njia za kushughulikia sio kuwadhalilisha hadharani.

pia sasa kahamia kwa wafanyakazi wa ofisi yake,anasema wafanyazi wote ni mzigo ispokuwa wanne tu.Nahisi hao wanne mmoja wapo ni dereva anayempeleka clouds,secretary anayechapa barua za kuxhongea watu na mlinzi wa nyumbani.

Hawa maafisa unawalaumuje kama taarifa za benki kuu zinasema hakuna pesa ya maendeleo iliyotolewa? watembee kwa miguu?watoe mfukoni pesa za kuendeleza jiji?wamfate GSM?

lets go back to the facts

Hii gari ni ya GSM
 
Attachments

  • IMG-20161120-WA0000.jpg
    IMG-20161120-WA0000.jpg
    105.6 KB · Views: 50
..tatizo la makonda ni kupingana na wabunge ,mameya, na madiwani wa ukawa.

..mapendekezo yako yangeweza kufanyiwa kazi kukiwa na ushirikiano baina ya wabunge/mameya/ madiwani wa ukawa na mkuu wa mkoa/wakuu wa wilaya toka ccm.

..makonda anataka kuwaonyesha wananchi wa dsm kwamba wabunge mameya na madiwani waliowachagua hawana manufaa yoyote.
Point noted
 
IMG-20161120-WA0000.jpg
GSM na Dar mpya vina uhusiano gani,ukiangalia kwenye "kichwa" a.k.a cabin ya gari pameandikwa GSM.

je watumishi wa Ofisi ya Mkuu Mkoa wafanye hivi kusaka hela kwa matajiri ili awonekane wanafanya kazi na sio mizigo,halafu mwajiri wao anafanya nini?kwa hiyo gsm wakituchoka? kodi kazi yake nini kama serikali inaendeshwa kwa.hisani ya gsm? kuna mtu atakuwa ana ubavu wa kumkatalia jambo?
 
Its very difficult kwa watu wa Makonda kuja kujibu hizi hoja

Kitakachofuata ni mleta mada na wengine wataambiwa wako too personal au wataambiwa kuwa hawampendi au wataambiwa wana wivu na makonda

Men lie, women lie numbers don't lie

If makonda really wants to survive this abadilishe team take nzima (wapambe na image consultants) na ikiwezekana amtafute huyu mleta mada na amfanye kuwa mshauri wake otherwise this will spiral out of control
Abadilishe approach yake kwenye issues....siamini katika personal attacks in public spheres. It demoralises instead of encouraging people to work hard
 
Mkuu katika hili naona umekuwa too personal on the man RC Makonda. Hakuna aliye mkamilifu though, hata wewe uliyetuletea hii mada.
Na nikiangalia IN BETWEEN the lines naona umejaa
MALICE/Fitina!
WIVU
Innuendo na
INCOMPREHENSIBLE narrative kuhusu nini RC Makonda atimize katika jiji letu.

Unaposema atupe HEWA safi, SIKUELEWI Una maana gani ?Eti good Transport system kama ya Ethiopia nakushangaa zaidi!

Hata UNADAI jijini tupewe FREE WIFI kwa ajili ya MITANDAO na raha za watu kama wewe. Mimi si msemaji wake lakini mahali palipo na FITINA na WIVU lazima tuzungumze!
YOU ARE BEING UNFAIR to HIM to say the least!

Ni kweli ana mapungufu yake, hata hivyo si MAKUBWA as you want us to believe! Hayo mambo uliyoyataja yote yanahitaji HELA na kila kitu kina bajeti yake.
Sasa ndugu RC Makonda kama Makonda where will he be able kupata fedha nyingi hivyo na kutimiza hayo yote uliyo ya outline kama FAILURE yake?
Let us be HONEST to ourselves bila prejudice.
This guy Makonda ni MCHAPA KAZI. No question about that!

Na kama unavyosema eti ni ANTI wafanya biashara that is a lie/ si kweli.
Hawezi kuwa kiongozi wa Mkoa huku akipiga vita wafanya biashara. Je waliomba audience naye AKAKATAA kukutana nao?

Mimi naona hii issue ya kuzuia biashara ya UVUTAJI wa SHISHA miongoni mwa mambo mengi mazuri anayoyafanya ndo inamfanya awe na MAADUI wengi ikiwamo wewe uliyeandika mada hii.
Basi nitasema hivi:
This could be but the beginning of the RISE and RISE of RC Makonda to the greater heights! Wivu UNAUWA Achana nao!!
He is not perfect though just like you and me hold your peace!
PPP,kinachoandikwa na Mchokoza mada ni creativity katika kutatua challenges za eneo la kiutawala Kwa Mh Makonda. Badala ya kudeal na petty issues.
 
Ni kweli ana mapungufu yake, hata hivyo si MAKUBWA as you want us to believe! Hayo mambo uliyoyataja yote yanahitaji HELA na kila kitu kina bajeti yake.
Sasa ndugu RC Makonda kama Makonda where will he be able kupata fedha nyingi hivyo na kutimiza hayo yote uliyo ya outline kama FAILURE yake?

Mkuu jana RC kamwambia DC Temeke ahakikishe miradi inatekelezwa yote na si kukaa kulalamika kwamba fedha hazipo,sasa kama yeye anashindwa kutekeleza hii miradi kwa sababu ya ufinyu wa bajeti,subordinate wake ataweza wapi?
 
Na akimaliza ngwe/miezi 12 pia uje utueleze kwa nn amemaliza??

Sitakagi unoko.
 
Nnachoona makonda kuna time anafanya vitu kwa show off yaaan

Huwa namuona anamalengo makubwa labda kinachomrudisha nyuma ni kuchanganya siasa na kazi, ushirikiano hakuna kabisa inavoonyesha wazi kabisa kwa tamko lake alivosema wafanyakazi anaowategemea sijui asilimia ngapi sijui ila ni ndogo Sana.

Kingine sijui ni hashauriki au hana washauri wazuri

Hawezi kusimama yeye Kama yeye kutimiza majukumu yake hilo alijue ushirikiano waongee lugha moja otherwise hakuna litakalofanyika zaid ya maneno tu kila siku
 
naona sasa anapigana na polisi wa dar,kaanza na kamanda wao,hii kwa kweli ni hatari.

unapofanya jambo lolote katika vyombo vya dola vizuri uwe makini sana usije ukavivunja morali.

hawa watu kila siku wanakwepa risasi za majambazi,wananusurika kifo,hata kama wana tatizo,kuna njia za kushughulikia sio kuwadhalilisha hadharani.

pia sasa kahamia kwa wafanyakazi wa ofisi yake,anasema wafanyazi wote ni mzigo ispokuwa wanne tu.Nahisi hao wanne mmoja wapo ni dereva anayempeleka clouds,secretary anayechapa barua za kuxhongea watu na mlinzi wa nyumbani.

Hawa maafisa unawalaumuje kama taarifa za benki kuu zinasema hakuna pesa ya maendeleo iliyotolewa? watembee kwa miguu?watoe mfukoni pesa za kuendeleza jiji?wamfate GSM?

lets go back to the facts

Hii gari ni ya GSM
1ca1a38b2d4b371a6f37ca9ee15997b3.jpg
 
We mleta mada, toka lini jiji la Dar lina watu "millioni 10"?

Hizo ni takwimu za Ufipa?
 
na ukiangalia ratio ya askari kwa raia,kwa Tanzania askari ni wachache.

katiba inasema jukumu la ulinzi na usalama ni la kila raia,wakiwamo mgambo cha msingi tu taratibu zifuatwe, Mawilayani kituo kina askari wawili,wanaojazia gepu la upungufu ni mgambo!!

Huyu bwana ni tatizo,bahati nzuri sirro hajamjibu
 
Back
Top Bottom