The Rise and Fall of Paul Makonda (Dar RC)

The Rise and Fall of Paul Makonda (Dar RC)

Shige 2 unatumia lugha fulani fulani ambazo huwa naziona kwenye hukumu za kesi za mahakama kuu..malice, innuendo, incomprehensible [emoji2]
Mkuu japo nimependa jibu lako ila si jinsi unavyofikiria!
 
charlotte-bronte-novelist-give-him-enough-rope-and-he-will-hang.jpg

**powerfull words from ancienstral that works"it can work multi purposely .....both ranges...
 
Mkuu katika hili naona umekuwa too personal on the man RC Makonda. Hakuna aliye mkamilifu though, hata wewe uliyetuletea hii mada.
Na nikiangalia IN BETWEEN the lines naona umejaa
MALICE/Fitina!
WIVU
Innuendo na
INCOMPREHENSIBLE narrative kuhusu nini RC Makonda atimize katika jiji letu.

Unaposema atupe HEWA safi, SIKUELEWI Una maana gani ?Eti good Transport system kama ya Ethiopia nakushangaa zaidi!

Hata UNADAI jijini tupewe FREE WIFI kwa ajili ya MITANDAO na raha za watu kama wewe. Mimi si msemaji wake lakini mahali palipo na FITINA na WIVU lazima tuzungumze!
YOU ARE BEING UNFAIR to HIM to say the least!

Ni kweli ana mapungufu yake, hata hivyo si MAKUBWA as you want us to believe! Hayo mambo uliyoyataja yote yanahitaji HELA na kila kitu kina bajeti yake.
Sasa ndugu RC Makonda kama Makonda where will he be able kupata fedha nyingi hivyo na kutimiza hayo yote uliyo ya outline kama FAILURE yake?
Let us be HONEST to ourselves bila prejudice.
This guy Makonda ni MCHAPA KAZI. No question about that!

Na kama unavyosema eti ni ANTI wafanya biashara that is a lie/ si kweli.
Hawezi kuwa kiongozi wa Mkoa huku akipiga vita wafanya biashara. Je waliomba audience naye AKAKATAA kukutana nao?

Mimi naona hii issue ya kuzuia biashara ya UVUTAJI wa SHISHA miongoni mwa mambo mengi mazuri anayoyafanya ndo inamfanya awe na MAADUI wengi ikiwamo wewe uliyeandika mada hii.
Basi nitasema hivi:
This could be but the beginning of the RISE and RISE of RC Makonda to the greater heights! Wivu UNAUWA Achana nao!!
He is not perfect though just like you and me hold your peace!

Kama unakiri hayuko perfect,kwanini hukuonyesha hayo madhaifu yake? what I believe kuna vitu vya ukweli vimeongelewa,na wewe umetumwa kupuliza washa washa ili watu watimke
 
Kama unakiri hayuko perfect,kwanini hukuonyesha hayo madhaifu yake? what I believe kuna vitu vya ukweli vimeongelewa,na wewe umetumwa kupuliza washa washa ili watu watimke
Hakuna washa washa hapa. Jamaa huyu hana mada ni wivu tu umemjaa!!
 
View attachment 437572GSM na Dar mpya vina uhusiano gani,ukiangalia kwenye "kichwa" a.k.a cabin ya gari pameandikwa GSM.

je watumishi wa Ofisi ya Mkuu Mkoa wafanye hivi kusaka hela kwa matajiri ili awonekane wanafanya kazi na sio mizigo,halafu mwajiri wao anafanya nini?kwa hiyo gsm wakituchoka? kodi kazi yake nini kama serikali inaendeshwa kwa.hisani ya gsm? kuna mtu atakuwa ana ubavu wa kumkatalia jambo?

Hizi aibu zingine zimezidi kwa kweli.
 
Angeweka kwa mhutsari. Bila kuonyesha kuwa ANGEFURAHIA downfall ya mtu mwingine tungemwelewa kuwa ni creativity. Lakini katika hii ni direct attack!!
Mchokoza mada yuko sawa,ni vizuri kuonesha lilipo tatizo na kama halitoshughulikiwa ipasavyo basi kuna anguko mbeleni. Tusipende kusifiwa tu!
 
Uncle anawapenda watu kama makonda awezi kumtoa kwa kuwa na yeye alipata ukuu kama ngekewa ndio maana anasikiliza majungu kuriko hualisia wa mambo yenyewe mwisho anabaki njia panda
 
..tatizo la makonda ni kupingana na wabunge ,mameya, na madiwani wa ukawa.

..mapendekezo yako yangeweza kufanyiwa kazi kukiwa na ushirikiano baina ya wabunge/mameya/ madiwani wa ukawa na mkuu wa mkoa/wakuu wa wilaya toka ccm.

..makonda anataka kuwaonyesha wananchi wa dsm kwamba wabunge mameya na madiwani waliowachagua hawana manufaa yoyote.
The same RC mboga wa chugga. .
 
HNIC nakupongeza kwa kuanzisha mada ambayo kama wachangiaji wangepunguza ushabiki ingesaidia sana kutatua baadhi ya matatizo ya Dar sidhani kama population ya Dar imefika 10m

Naamini kuna changamoto kama kupunguza foleni,usafi wa jiji,usalama wa wananchi mkuu wa mkoa anaweza kutoa msaada mkubwa kutatua hizi changamoto
 
JF kisima cha maarifa! Kuna ile slogan iliyotengenezewa mabango makuubwa ya picha za kutengeneza kwenye Internet! Slogan ya Dar es salaam tuitakayo
Ni mapicha ya miti na minazi pambo nikajiuliza hivi tunataka kutengeneza zoo?
Kuwakuwa naye ni mpitaji huku si mbaya akakualika mkae meza moja pamoja na wataalam kwenye nyanja mbalimbali kama ulivyoainisha! Anaweza kufanya maajabu
Wasije wakamtoboa macho mkuu, kipaumbele chake ni cloudshilawadu, gym, selfies nk
 
Makonda ndio type ya wateule wa Magufuli kwa hiyo haendi popote! Amefanikisha kampeni ya kupanda miti siku ya UKUTA hilo ni muhimu kwa serikali kuliko yote uliyoandika.
Nadhani hili ndilo la muhimu kwa utawala huu.
 
Makonda ndio type ya wateule wa Magufuli kwa hiyo haendi popote! Amefanikisha kampeni ya kupanda miti siku ya UKUTA hilo ni muhimu kwa serikali kuliko yote uliyoandika

It is unfair to expect much from a person of Makonda's caliber ; this is guy who got promoted because he attacked unceremoniously a former Primeminister and not out of any other outstanding contribution to society!!!
 
Makonda anatakiwa aku inspire wewe
If u think he is sinking so low , why dont u try and go deeper man...,!!

Halafu , sio kwavile watu wako free kuongea kuhusu mtu basi nawee cha kwanza unajifananusha nae...!! Jamani! We differ...! Happi , makonda !! They represent offices not u guys mnareprent anger zenu... Dharau zenu na failed characters zenye mna posses....!!!

U should dream to get such recomendable jobs by showing out like them....!!!
Makondaaaaa makondaas makondaa...!!!!

Hayuko level zako man...! Suck it...! Na jikubali kwamba uko chini. U can talk yes lakini not more than that...

Imagine unazo critics against him, unajua utakavo mu address... Ili akusikilize utatakiwa umtafute na ungoje akuruhusu useme au ufanya unachofikiria... Utasema muheshimiwa na kisha kufikisha unachotaka....!!

Truth be told bahna...!!!! Aaaaaggghhh[emoji3][emoji3]
 
kwan unadhan mkuu mwenyewe ana benchmark ya kuwapima wateule hapo ni bora liende tumpotezea miaka mitano kwa sizonje.
 
If you want to test a man's character give him power

ABRAHAM LINCOLN

Unaccommodated man is no more but such a poor bare,
forked animal
KING LEAR : Act III, scene iv
​




Sipendi kuandika political obituaries lakini kwa huyu mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam (Paul Makonda ) Sidhani kama atamaliza ngwe yake na Magufuli let alone kama atamaliza miezi 12 mayo katika jiji la Dar es salaam kama mkuu wa mkoa kwa sababu naamini kabisa kuwa Rais Magufuli kashaona kuwa Makonda isnt up to the job na mbaya zaidi Magufuli kashashtuka na hataki tena haya mambo ya kusifiwa sifiwa na kupambwa badala yake anataka kuona results baada ya kumpa cheo kuongoza jiji lenye watu karibu milioni 10.

Maguli alimpatia ukuu wa Mkoa wa Dar baada ya Makonda kuonyesha kumpa illusion kuwa ni mchapa kazi lakini ukweli usiopingika ni kuwa Makonda has failed na sasa hivi tumeishia kupewa PR stunts, na maneno mengi yasiyo na substance.

Jiji hili ambalo lina historia na ambalo limetoa vigogo wa kila namna linahitaji mkuu wa mkoa ambaye anaendana na dunia na karne hii tuliyonayo.

So far jiji bado ni chafu, ombaomba wako palepale, foleni na traffic lights zisizofanyakazi, hakuna law wala order, marengo yanajengwa bia mipangilio huko kwenye Central Business District (CBD), kodi zinakusanywa lakini wana Dar es salaam hawaambiwi wala kuonyeshwa mchanganuo wa matumizi wa kodi zao, hakuna transparency, jiji halina strategies wala policies za mambo ya climate change, hakuna strategies za kuongeza nyumba kwa wakazi wa hili jiji (na affordable) na kuondoa ma chaka na slums ya Buguruni, Mwananyamala kinondoni, Ilala, temeke, etc.

Makonda kashindwa kutuletea alternative Transport strategy na policy (kakuta DART) na hajaja na mango wowote wa kuendeleza usafiri walau Dar ikawa na network ya light rail kama walivyofanya Addis au kuongeza na kuboresha barabara zilizopo ili ziendane na ukuwaji wa watu kwenye hili jiji, na usafiri hapa nazungumzia za waenda kwa miguu, baiskeli na magari.

Paul Makonda kashindwa kuja na mikakati yoyote ile ya kusaidia kuwa na Dar es salaam ambayo in hewa safi kwa wakazi wake. Hivi how hard is it for him kushirikiana na January Makamba (waziri wa mazingira) ili kuwepo kwa comprehensive strategies za kutunza mazingira? Mfano jiji la Dar halina power points za ku chat magari ya umeme, hakuna operesheni ya kueleweka ya kupada na kutunza mimi, Makonda kashindwa kuwahizimisha na kutoa incentives ma wajenzi kutumia umeme mbadala wa solar na wind.

Mbali na hayo hana strateges zozote zile kuvuta wawekezaji wa viwanda kama vya ku assemble Solar na vinginevyo kwenye hili jiji wala hana mipango yoyote ile ya kuvutia watalii kwenye hili jiji ambalo watulii hutumia kukaa kwa siku moja kisha wanaenda zao Arusha au Zanzibar. Hili ni jiji ambalo lina historia na vivutio kem kem na linaweza kuongezewa vivutio vingi zaidi ili wall mtalii on average awes ku spend more days hapa Dar na kutumia wastani wa dollar 100 per day hapa. In addition, Makonda amefeli kwenye kuboresha Ulinzi na usalama wa hili jiji kwani sasa hivi wakazi wa Dar hawajiskii salama kutoka nje usiku na hata aliyoko ndani ya gari anaogopa kusimama kwenye traffic lights kwa kuogopa majambazi.

Hivi kuna ubaya gani wananchi wakawa organised na kuambiwa wachangie kwenye mambo ya neighbourhood policing? Mrema aliweza na police posts in the 1990's sasa sielewi leo haya mambo yanashindikana. Wananchi kila wakiona polisi ni ama watakamatwa na kusingiziwa kesi na hivyo wananchi wa hili jiji police badala ya kuwa rafiki wa wananchi wanaonekana kuwa wanashirikiana na majambazi.

Hapo zijazungumzia vikosi veytu vya zimamoto ambavyo haviko up to standards. Zimamoto zinatakiwa kuwepo kwenye kila kata ya hili jiji lakini hakuna mipango hiyo na hata habari Mkaonda hana.

Ofisi yake pia imeshindwa kushirikiana na kampuni mbali mbali za teknolojia wakaweka super fast Free Wifi maeneo mbali mbali..

Kuhusu Culture na nisiseme kwani sasa hivi the only cultural thing ambacho ofisi yake inakifanya ni matamasha ya fiesta na nyama choma. Ofisi yake haina habari na vituo vya sanaa na haina mipango ya kuwezesha wawekezaji kujenga Cultural Centres.

Miwsho zaidi Makonda hana habari kama jiji hili indigo walk wawekezaji na walipa kodi wakubwa. Sasa sielewi why mpaka leo hajafanya mkutano awa wafanya biashara wakubwa ambao wanalipa kodi kubwa na kuajiri watu wengi zaidi. If anything Makonda comes across as the most anti business RC kuliko wote ambao jiji hili imewapata. Hivi anashindwa vipi kushirikiana na private sector wenye hizi infrastructure projects kwa njia ya PPP?

Kama kweli anataka kusaidiwa aseme lakini tatizo hasemi. Sisi wana Dar hatupendi kulipa kodi lakini sababu ni hatupewi wala hatuonyeshwi namna kodi zetu zinavyotumika. Tunachokitaka ni kuona tax system ya Dar inakuwa overhauled,increasing taxpayer compliance while pledging that the Local Govt (LG) chini ya ofisi ya RC Makonda will be accountable for how tax money is spent. Naamini kuwa ofisi ya RC Dar wangekuwa honest na transparent, annual tax revenues zitapanda tutu na mana yake ni kuwa hizi pesa za ziada zitatumika kumaintain barabara, kusafisha jiji, kuongeza na kuimarisha ulinzi na usalama, ange weza kuintroduce new public transit options into kwenye hili jiji ambalo watu wanatumia zaidi ya masa 5 kwenye foleni na kwa kuboresha transport systems

Sidhani na siamini kabisa kama Magufuli is impressed na yanayoendelea kwenye hili jiji. Maana huyu Makonda Hana any Strategic Plan ya hili jiji.

Makonda angeweza sana kufanikisha haya mambo kwa kushirikiana na sect binafsi wakafanya kazi kwa njia ya Public Private Partnership (PPP)

In my opinion, its fair to say kuwa Makonda is not up to the job. Tuletewe mtu mwingine,

Mkuu nakuunga mkoni saba mara sabini, kuna jamaa yangu kafika Nairobi kwa mara ya kwanza ameshangaa sana kuhusu jiji la Nairobi, sisi kama kawaida yetu maneno na vijembe tu na majungu Wabongo kazi hakuna. Mwaka umekatika toka awamu ya 5 ianze lakini jiji la Dar sijaona cho chote Zaidi ya barabara ya Mwenge-Morocco na kuanza kwa mwendokasi miradi tulioambiwa kupunguza foleni hakuna hata mmoja ulioanza wachia mbali kumalizika. Foleni za magari bado ni kero sugu Dar hii, barabara zetu bado nyembamba, vituo vya mabasi yaendayo mikoani sijui kama mradi ule umefikia wapi, lakini maneno ya majukwaani kila kukicha wacheni hizo wakina Makonda tunataka matokeo sio mikingamo yenu na Sirro au juhudi za kujisafisha kwa wakubwa zenu hatusaidii sisi walalahoi.
 
Back
Top Bottom