Kazi ipo tutaona nini ni nini.....mwaka huu.
Wana JF,
Nadhani sasa ni wakati wa kupiga kelele. Hili swala limekaa muda mrefu. Watanzania hatujui kama kuna kitu kinaendelea. Taarifa zinazojitokeza zinazidi kutisha.
a)Taarifa ya SFO ya 21 Machi, 2008 yenye Ref. SPCQ!/D/MC iliyopelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ilikwisha kutoa mwelekeo mkubwa na kuonyesha maeneo yote yanayodhaniwa kuna sura nzito ya Criminal charges. Taarifa hiyo ya SFO ilionyesha wahusika wakubwa kuwa ni BAE Systems, Red Diamonds Trading Ltd and Merlin International Ltd, Envers Ltd, Tanil Kumar Chandulal Somaiya, Shailish Pragji Vithlani, and Andrew Chenge and others.
b) Taarifa hiyo iliweka wazi Kampuni aliyokuwa akitumia Chenge na Mke wake inayoitwa Franton International Ltd ambayo ilikuwa ikipokea fedha kupitia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoka Frankfurt, Lichtenstein, na hatimaye kuingia Jersey, Uingireza. Kwa kitu kinachoonekana kama kupoteza dira.
c) Kampuni ya Franton International imepokea fedha kati ya June 1997 nadi April 1998 katika Akaunti ya US Dollars iliyoko Barclays Bank no 5966999.
d) Inaelekea Chenge mwenyewe alipohojiwa alikuwa akitoa kila mara maelezo ya kujikanganya, ikiwa ni pamoja na " yanatokana na "Professional Earnings", lakini hakuweza kuonyesha ni shughuli zipi za kitaalam zilizomwezesha kulipwa fedha hizo katika kipindi hicho ( ambacho ni kipindi cha ununuzi wa Radar). Katika mazungumzo na J.O. Hambro mawakili wake alieleza kuwa inatokana na "from family savings and Inheritance". Wenye akili watajiuliza hizo family savings ni kutoka wapi na inheritance hiyo ni kutoka wapi na kwa nani.
e) Tarehe 20 September, 1999 Chenge mwenyewe aliidhinisha kuhamisha kiasi cha GBP kutoka kampuni ya Fanton International kweny akaunti iliyoko Barclays kwenda Benki Royal Bank of Scotland International iliyoko Jersey. Mwaka 2006 alikabidhi mamlaka ya uendeshaji wa Akaunti hiyo kwa J.O.Hambro " in his name and his Wife's". Tarehe 13 September, 2006 Fedha zilizokuwepo Benki ikiwa asilimia 75% ikimilikiwa na Andrew Chenge na asilimia 25 ikimilikiwa na "Mrs Chenge".
f) Instruction aliyotoa Chenge ndiyo inayoonyesha sura halisi ya ufisadi mkubwa uliokuwepo. Wapelelezi wanasema,
"We did have a P.O.Box for him in Dar, but... nothing should be sent to that address from Jersey, if Mr. C's government were to be made aware of these assets in London, they may confiscatethem notwithstanding they legally belonged to Chenge and were not obtained via 'brown envolopes..'He asked his financial advisers to send all documentation to C/o 11 Sidmouth, Rd, London."
f) Isitoshe, May 1998 Mr. Chenge alihamisha fedha toka account yake kwenda Langley Investments Ltd (Langley), akaunti iliyokuwa ikisimamiwa (controlled) na Mr. Idrissa Rashid (Rashid) - Itakumbukwa kuwa alikuwa Governor wa BOT kati ya Mwaka 1993 hadi 1998 katika kipindi muhimu cha 'Negotiaton" ya ununuzi wa Radar husika.
Kutokana na hayo yote basi:
i) Ni dhahiri kuwa kuna sheria nyingi za Tanzania zimevunjwa, na hatuoni sababu ya Serikali ya kuwa na kigugumizi katika kumfikisha Mr. Chenge, na Bwana Rashid katika vyombo vya Dola, na hasa Mahakamani ili hatima ya Rasilimali za Taifa zilizotumika vibaya katika ununuzi wa Radar ijulikane. Hatuwezi kuendelea kupiga kelele za nchi maskini wakati rasilimali za Taifa hili zinawaneemesha wachache.
ii) Mhe Chenge ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Uchunguzi umedhihirisha wazi kuwa Mr. Chenge, kama Mbunge hakutangaza Mali zake zilizokuwa Jersey na nje ya Nchi kama anavyotakiwa na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, 1995, kwa Kamishna wa Maadili. Hii inaeleza wazi kwanini Kamishna wa Maadili aliwakataza viongozi wa Vyama vya Siasa kukagua Register ya maadili na kuweka masharti magumu. Kwa kitendo hiki, bila kesi mahakamani, Kamishna anatakiwa kutoa Taarifa kwa Mamlaka husika mara mmoja kuwa Mheshimiwa Chenge amevunja Sheria ya Maadili kwa kutokutangaza mali zake, na hivyo "automatically" amepoteza Sifa ya kuwa Mbunge. Inashangaza kuwa Sheria hiyo nayo imepindishwa kwa makusudi kumlinda Bwana Chenge. Ni nini au kuna nini nyuma ya kulindana huku?
g) Jambo hili la kutochukuliwa hatua stahiki na Kamishna wa Maadili linafanya zoezi la kujaza fomu za mali kuwa kichekesho pale hatua stahiki zinapokuwa hazichukuliwi na sheria zimevunjwa/kukiukwa.
Wana JF nimeona niweke haya hapa ili kuanzisha mjadala kuhusu jambo hili ambalo sasa linajuchukua muda. Mambo haya yanahusu Maslahi ya umma, na hata DPP wala Mwanasheria Mkuu hawawezi kuyanyamazia. Kwanza hadi sasa hakuna anayejua kitu gani kinaendelea. Hatutaki kuingilia kesi, lakini angalau basi Watanzania kama wenye mali wanatakiwa kujulishwa kama kuna uchunguzi wa ndani unaendelea, maandalizi ya kesi yamefikia hatu gani nakadhalika.
Hakuna mwenye hati miliki ya nchi hii, wote tuna haki yakujua kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu. Pili, mjadala husika utaisukuma serikali kuharakisha uchunguzi kama bado haujakamilika. Tatu kama kuna mtu anakuwa "protected" wajue kuwa tunajua mengi na kuwa hakuna tena linaloweza kufichwa. If anything, atakayejaribu kuficha Bomu litamlipukia kwa namna ambayo hajawahi kuiona. Nne mwenye kufahamu details zaidi naye tunaomba atumegee ili wote tusogee mbele kwa pamoja kwa maslahi ya nchi yetu.