The problem of evil and jealousy solved. ( Suluhisho la kuondoa tatizo la wivu na husda duniani)

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,120
27,126
Wakati akina mwenzangu na Mimi bado wapo gizani waki ji stress kutafuta hela za kuwalipia watoto wao ada kwenye shule za English Mediums ili waje wapate ufaulu mzuri secondary ili wafike Chuo kikuu ili wakimaliza Chuo kikuu wawe marketable kwenye soko la ajira ( a very stupid mission), akina Likud tupo busy kuumiza vichwa kutafuta majawabu dhidi ya matatizo halisi yanayo mkabili mwana wa Adam.

Tunaumiza vichwa kutafuta majawabu ya matatizo haya kwa sababu hayafundishwi mashuleni lakini ndio yanayo tuathiri kwenye maisha yetu ya kila siku.

Ndio maana utamsomesha mtoto wako English Medium atafika hadi Chuo kikuu ambako ataenda kusomea POLITICAL SCIENCE ( What is science about politics or rather what is political about science?) halafu akimaliza degree yake anaenda kuishi kwa kufuata maelekezo ya kijana alie ishia darasa la saba Kayumba (Mganga wa kienyeji) Huyu ndio atakuwa anamwambia kijana wako graduate nenda njia panda kavunje Nazi saba saa tisa usiku, mkojo wako wa kwanza kila siku uwe unakojolea baharini blah blah blah. Kinacho weza kumfikisha kote huko kijana wako kinaweza kuwa na mzizi wake kwenye tatizo moja tu " Wivu na Husda"

Yote hii inatokea kwa sababu ya kutokuwa na mfumo wa elimu unao tuwezesha kupata majibu ya vyanzo vya matatizo halisi yanayo tokea katika jamii zetu.

Kwenye Uzi huu nime suggest njia kadha wa kadha ambazo endapo zitafuatwa basi zinaweza kuondoa kabisa tatizo la wivu na husda miongoni mwa wanadamu duniani na zitafanya maisha ya wanadamu hapa duniani yawe yenye furaha kwa sababu kuna idadi kubwa sana ya watu duniani ambao matatizo yao chanzo chake ni chuki na husda..

Uzi wangu huu utasaidia jinsi ya kuwafanya watu wengine wasiwe na chuki au husda dhidi yako. Lakini pia utasaidia kukufanya wewe mwenyewe usiwe na chuki na husda dhidi ya watu wengine. Tatizo la chuki na husda lina wasumbua watu wengi sana duniani. Wewe unae soma Uzi huu kama huwa una struggle ndani ya nafsi yako kukubaliana na taarifa nzuri kuhusu mtu unae mfahamu kama vile kujenga nyumba kununua gari etc basi jua wewe pia una tatizo la husda na wivu. Uzi huu unakuhusu pia.

Kikubwa unacho paswa kufahamu ni kwamba tatizo la chuki na husda ni swali ambalo alie waumba wanadamu amewauliza. How will u deal with this problem? Na majibu yangu nimeyaweka kwenye Uzi huu.

To be continued
 
Back
Top Bottom