The Other Half (Simulizi)

The Other Half (Simulizi)

Heshima kwako Mkuu... Naona bampa to bampa...kazi juu ya kazi! Ebana hii stori dah..by the way naamini kuna watu duniani baadhi yetu wana machale Sana.. Ofcoz pamoja na hii kuwa story lakini kiuhalisia binafsi naamini kwamba population kubwa ya dunia itaangamia.name sababu itakua ni majanga ya kiasili..uko sahihi we are not alone its just the matter of time..let's wait and see!
Shukrani sana kiongozi! Ni mwendo wa kazi juu ya kazi..
 
THE OTHER HALF




EPISODE 3


Ilipoishia Episode 2

Kikosi cha wataalamu kikiongozwa na Afisa wa Usalama wa Taifa Bw. Salim wanagundua kuwa mahali walipo (Wilaya ya Ruangwa) panakaribia kutwaliwa na kugeuka Anabelle.
Wakati huo huo wamepewa taarifa kuwa mji wa Dar Es Salaam ndani ya masaa sita utakuwa umetwaliwa.

Kanali wa kikosi maalumu cha Jeshi kinachowalinda amependekeza kwamba wasafiri kupitia mbuga ya Selous na kutoka Morogoro.

Pia wakati huo huo nchini Marekani katika chumba cha Situation Room Whitehouse kuna kikao kikubwa kinaendelea kikiongozwa na makamu wa Rais David Logan akiongea na washauri wakuu wa Rais.
Pamoja nao yupo mzee kikongwe anayeitwa Bentley Caleb Bentley aliyeletwa na Mkurugenzi wa CIA ili aweze kuwapa siri iliyopo katika mchoro wa George Washington ambao umeibiwa kama wiki mbili zilizopita siku moja baada ya Rais Laura Keith kupotea angani na Airforce One.

Tuendelee..



EPISODE 3

Ipo falsafa ya miaka ya kale inayosema kwamba, nafsi yako inapokuwa na uwezo wa kuona huhitaji macho usoni mwako.
Uwezo mkubwa zaidi binadamu alioumbwa nao si kuona au kusikia au kunusa. Nguvu kubwa zaidi iliyopo ndani ya nafsi ya binadamu ni hisia. Uwezo wa kung'amua kile ambacho hujakiona wala kukisikia.

Pengine kama kila binadamu angetumia uwezo wake wa ndani ya nafsi, uwezo wa hisi aliyoumbwa nayo labda ulimwengu usingeweza kutwaliwa, labda leo hii kusingelikuwa na Anabelle hata moja juu ya uso wa dunia.

Tumefikaje hapa tulipo? Dunia imefikaje hapa?

Labda pengine sisi wote ni wakimbizi hapa duniani, iko sehemu, pako mahala pengine tunapopaswa kuwa.. Sayari nyingine, nyota nyingine.. Pengine, wamiliki halali wa dunia wameamka ili kuitwaa.

Lakini kama tunajua hapa ni kwetu kwanini hatuja fanya lolote muda wote huu. Kwanini tumeishi kama hapa si kwetu?
Kwa karne kadhaa tumeishi juu ya dunia kana kwamba hapa sio kwetu, kana kwamba kuna mahali tunakimbilia kwenda.
Tumeharibu, hatujaboresha
tumeifubaza dunia, hatujaifanya upya!

Ni nani alijua gharama ambayo ulimwengu na vilivyomo vitakuja kulipa siku ambayo wanaohisi dunia ni yao watakapo amka? Ni nani alijua siku moja dunia itatwaliwa kutoka mikononi mwa mwetu?

Lazima kuna waliojua, lazima wapo walioitunza hii siri mioyoni mwao!

Kwanini hawakutuonya? Kwanini walikaa kimya?
Mwisho wa siku kila siri inapaswa kujidhihirisha ili uthamani wake wa kufanywa siri miaka yote upate kuwa bayana.!!



Saa Kumi Alafajiri: Rabat, Morocco

Wale watu sita, waliovalia majoho meusi na miguuni wakiwa peku peku walikuwa wamekaribia kabisa jumba la Kasri ambalo lipo kwenye msitu uliopo kama kilomita tano kutoka baharini.

Mikono yao ilikuwa imechoka haswa, lile sanduku kama jeneza walilolibeba lilikuwa linaonekana ni zito kweli kweli.
Katika giza hili kilichokuwa kinavuja kwenye viganja mikononi mwao haikuwa rahisi king'amua kama lilikuwa jasho ama ilikuwa damu.

Licha ya kuchoka nyang'anyg'a lakini watu hawa walitembea imara kabisa bila kuyumba wala kupepesuka.

Wakakaribia mpaka kwenye Kasri ndani ya msitu. Kasri hili lilikuwa limetengenezwa katika muundo wa kizamani sana lakini lilikuwa la kifahari haswa. Pia lilionekana kuwa kuu kuu ikiashiria limekuwepo msituni hapo kwa miaka mingi sana labda pengine hata Karne kadhaa.

Kasri hili lilikuwa limezungushiwa ukuta wa mawe na mbele yake kuliwa na geti kubwa.
Jumba hili lilikuwa linaonyesha kwamba halikuwa na kitu chochote chenye kuashiria teknolojia ya kisasa, hata umeme ulionekana kutokuwepo, kwani kwa mbali ndani ya hili jumba vilionekana chemli zikiwa zimenining'inizwa ili kutoa mwanga.

Hawa watu walipofika mbele ya geti la hili Kasri, yule aliyetangulia mbele akagonga geti.

Aligonga geti katika namna ambayo, aligonga mara mbili kisha akatulia. Akarudia tena mara ya pili kugonga tena mara mbili na kisha akagonga tena mara ya Tatu kwa mtindo ule ule wa kugonga mara mbili.

Geti likafunguliwa na kijana mwenye ngozi nyeupe ya kizungu iliyopauka sana. Kijana huyu alikuwa amevalia suti nyeusi na kichwani amenyoa kipara.

Wale watu waliobeba sanduku hawakumsemesha chochote wala kumsalimia na wala yule kijana hakuwauliza chochote.
Wakaelekea mpaka kwenye mlango mkubwa wa kuingia ndani ya lile jumba. Hapa napo wakagonga tena kwa mtindo ule ule. Yule aliyetangilia mbele akagonga mara mbili, kisha akasubiri, akagonga tena mara mbili, akasubiri na kisha akamalizia kugonga tena vivyo hivyo kwa mara ya tatu.

Mlango ukafunguliwa na kijana mwingine wa kizungu mwenye weupe wa kupauka sana na alikuwa amevalia suti nyuesi kama yule wa getini na kichwa amenyoa upara kabisa.

Baada ya huyu kijana kufungua tu mlango, akatamka kwa sauti kubwa,

"SANCTA SEDESSSS..!"

Watu ambao walikuwa ndani ya jumba hilo wakionekana kama walikuwa kwenye kikao wakasimama wote kwa pamoja.

Jumba hili lilikuwa katika namna ambayo, ukiingia tu lango kuu la kuingia ndani, unakutana na ukumbi mpana kama kanisa au msikiti. Kwa ndani juu ya paa la Jengo lilikuwa la umbo la nusu duara likiwa na michoro ya ajabu ya wanyama, binadamu, malaika na kadhalika kufanania kabisa kama Jengo la Basilika lilipo Vatican.

Watu hawa ambao walikuwa wamesimama baada ya hawa waliokuja na sanduku kuingia, walikuwa wamekaa kwenye mtindo kama wakaavyo wabunge wa Uingereza bungeni. Upande huu kuna viti vyenye watu na upande huu kuna viti vingine vyenye watu na katikati kuna meza ya waongoza mjadala.

Tofauti ni kwamba hawa wao meza yao iliyopo katikati ilikuwa kubwa na ndefu ambayo ila upande wa meza kulikuwa na viti vitatu walivyoketi watu na mbeleni kabisa mwisho wa meza kulikuwa na kiti kimoja alichoketi mtu aliyeonekana kama kiongozi wao na mwisho ya upande mwingine wa meza kulikuwa na kiti tupu ambacho hajakaa mtu yeyote.

Pia kwenye vile viti vya pembeni vya kila upande, upande wa kushoto kulikuwa na viti vipatavyo 19 vyote wameketi watu na upande wa kulia kulikuwa na viti 19 vingine lakini ni viti 14 tu ambavyo walikuwa wameketi watu.

Wale watu sita walipoingia na sanduku walilobeba, moja kwa moja wakaelekea mpaka karibu kabisa na ile meza kati kati.
Watano kati ya wale sita wakaenda kuketi upande wa kulia kwenye vile viti vilivyowazi na mmoja wao yule ambaye alikuwa anatangulia mbele muda wote alienda kuketi kwenye kiti kimoja kilichobakia pale mezani.

Baada ya hawa waliowasili kuketi na wengine nao wote wakakaeti.

Kisha mzee ambaye alikuwa ameketi mbele kabisa ya meza ambaye alionekana kama kiongozi wa wote waliomo humu ndani, akiwa amevalia suti nyeusi sana na akiwa na upara kichwani, aliinuka na kuanza kuzungumza.

"Viongoziii.!" Akawasalimia

"Kiongoziii.!" Wakamuitikia salamu.

Kisha akaanza kuongea.

"Viongozi wenzangu wa The 46, hatimaye tumeifikia siku ya leo ambayo kwa karne kadhaa tumekuwa tukiitamani.. Siku ambayo tutaweza kurudisha kilicho chetu ambacho binadamu walitudhurumu kwa karne nyingi, siku ambayo tunaenda kuanza kuirudisha dunia kwa ‘The 46"

Akanyamaza kidogo na kuangalia kushoto kisha kulia. Kisha akaendelea.

"Ulimwengu wote ni mchanga.!"

Akachota mchanga uliopo kwenye bakuli pembeni yake pale mezani na kuumwaga juu ya meza. Kisha akaendelea kuongea.

"Ulimwengu wote ni maji!"

Akachota maji kwa kiganja kutoka kwenye bakuli nyingine pembeni yake na kumwaga juu ya meza.

"Ulimwengu wote ni damu"

Akachota damu kutoka kwenye bakuli nyingine pembeni yake na kumwaga juu ya meza. Kisha akamalizia.

"Hatuwezi kusahau, hatuwezi kusamehe udhalimu tuliofanyiwa karne zote hizi.. Leo tunarudisha kilicho chetu kwa halali, tunairudish dunia kwa The 46!! Mleteni hapa.." Akamalizia kuongea.

Wale watu saba wengine walioketi pale mezani wakainuka na kwenda lilipo lile sanduku lililoletwa.

Wakalifungua sanduku, na kutoa kilichomo ndani.
Mzigo ambao ulikuwa umebebwa na watu wale kuileta hapa ulikuwa ni binadamu.

Wakambeba na kumlaza juu ya meza. Kisha wakafunua shuka nyeupe aliyokuwa amefunikiwa.

Binadamu huyu aliyeletwa kutoka maelfu ya kilomita na wale watu sita alikuwa ni Bi. Laura Keith, Rais wa Marekani.
Bado alikuwa hai, japo alionekana alikuwa taabani kutokana na kupumua juu juu kwa shida sana.

Yule mzee kikongwe kiongozi wao akatabasamu na kuwaangalia wenzake.


INAENDELEA POST INAYOFUATA HAPO CHINI..
 

THE OTHER HALF


EPISODE 4




"…katika maisha si lazima kufanya jambo sahihi muda wote. Muhimu zaidi ni kujitahidi kadiri uwezavyo kutimiza unaloliamini… Japokuwa ulimwengu mzima kila upande, kila bara, kila nchi imekuwa na imani yake na kujitahidi kufanya ya kwake wanayoona sahihi na hatimaye kutengeneza utengano, lakini pale ulimwengu mzima unapopambana na adui mmoja, tishio moja, na tunapolia kilio kimoja… huu ndio muda ambao ulimwengu mzima uinuka na kuwa na imani moja, huu ndio muda ambao nguvu iliyopo katika roho ya binadamu udhihirika… tunapopambana wote kwa pamoja, mwishoni mwa vita si sahihi kujiuliza kama tumeshinda au tumeshindwa, jambo la msingi zaidi ni kuhakikisha tunaacha alama juu ya uso wa dunia, ili karne kadhaa zijazo, wataokuwepo wajue sisi tulikuwa ni akina nani, na kwa ushujaa gani tulipambana kutetea Dunia..!"




WASHINGTON, D.C: WHITEHOUSE

Watu wote waliokuwepo Whitehouse ndani ya Situation Room walikuwa wamebaki na mshangao baada ya kuyasikia maelezo ya mzee Caleb.
Wate walikuwa wamepigwa na butwaa wasiamini kile ambacho walikuwa wamekisikia. Walichoelezwa kilikuwa kama kisa cha hadithi ya kusadikika ambayo haiwezekani katika maisha halisi.
Lakini kwa kuzingatia jinsi matukio yaliyokuwa yanatokea duniani haikuwa ngumu sana kwao kuamini hiki walichoelezwa.

Mzee Caleb alikuwa amewasimulia kisa cha zaidi ya miaka elfu kumi iliyopita. Kisa kilihusu uwepo wa kisanduku kinachoitwa Pithos ambacho kilitengenezwa na Mungu wa Kigiriki aliyeitwa Zeus.

Hadithi hii karibu kila mtu duniani alikuwa amewahi kuisikia lakini hakuna mtu ambaye aliwahi kuiamini. Watu wote waliichukulia kama simulizi tu za kale za kusadikika. Ni mpaka dakika hii baada ya mzee Caleb kuwapa maelezo ya kutisha kuhusu simulizi hii walau kulikuwa na watu kadhaa ndani ya situation room ambao walianza kuamini uhalisia wa hadithi hiyo.

Mzee Caleb aliwaeleza kwamba, Mungu Huyo wa Kigiriki, Zeus alikuwa amechukizwa sana na wanadamu ambao kwa kipindi hicho wote walikuwa ni wanaume. Ndipo hapa akamtengeneza mwanmke wa kwanza duniani na kumpa jina la Pandora (likimaanisha "aliyejaliwa kila kitu"). Mwanamke huyu alipewa uzuri usio kifani na ushawishi na mvuto wa kipekee kwa wanaume. Pia Mungu Zeus alimpa mwanamke huyu zawadi ya sanduku ambacho alimuamuri kamwe asikifungue. Ssanduku hiki kilikuwa kimejaa chupa ambazo Mungu Zeus alizijaza kila aina ya udhalimu na ufedhuli uliopo duniani. Na kadiri ambavyo sanduku hili litabakia limefungwa basi dunia itabakia kuwa salama pasipo kushuhudia kiwango kikubwa cha tishio, ukatili au ufedhuli.

Akamsisitiza sharti moja muhimu, kamwe asifungie sanduku hili.

Mzee Caleb akawaeleza kuwa baada ya kufariki kwa mwanamke Pandora, sanduku hili limekuwa likirithishwa kwa siri kubwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Kwa zaidi ya miaka elfu mbili sanduku hili lilikaa sehemu ya siri nchini Ugiriki.
Baadae katika kipindi cha utawala wa mfalme Alexander, akalipeleka sanduku hili nchini Misri ambapo lilikaa hapo kwa Karne kadhaa. Baadae yakatolea matukio na sanduku hili likaenda kuhifadhiwa nchini Israel katika hekalu la mfalme Suleiman.

Baada ya hekalu la mfalme Suleiman kubomelewa baada ya kutamalaki kwa dola ya Rumi, sanduku hili likaenda kuhifadhiwa Vatican katika makazi ya Papa wa Kanisa Katoliki ambapo lilikaa hapo kwa karne nyingi mpaka kufikia karne ya 16 miaka ya 1550 mji wa Vatican ulipovamiwa na kubomolewa kwa kuchomwa moto Sanduku hili lilipotea na halikuwa kuonekana tena.

Mzee Caleb akawaeleza kuwa inasemekana kwamba sanduku hili lilikuja kugunduliwa na maharamia wa kimarekani katika bahari ya Atlantiki mahali fulani baharini miaka ya 1780 na waliloligundua baada ya kulijua ni sanduku la Pandora wakaenda kumkabidhi Rais wa kwanza wa Marekani, George Washington.
George Washington akalificha sanduku hili mahali ambapo ni yeye pekee anajua lilipo na akamtumiachoraji kuchora Picha yake na kuiwekea alama kadhaa za mafumbo ambayo yanamuwezesha mtu kung'amua Sanduku lilipo.

Mafumbo haya ya kwenye mchoro, Rais George Washington alimrithisha siri hii Rais aliyekuja kumrithi John Adams, ambaye naye alipoondoka madarakani akamrithisha siri hii Rais aliyemfuatia Thomas Jefferson, na yeye Jafferson alipoondoka madarakani siri hii akamrithisha Rais James Madison na desturi hii ya kurithishana siri hii imeendelea hivi kwa kila Rais wa Marekani vizazi na vizazi mpaka Rais wa sasa Bi. Laura Keith.

Chumba kizima cha Situation Room kilikuwa kimegubikwa na ukimya wa mshagao na hofu kwa takribani dakika kumi nzima hakuna aliyekohoa wala kujisogeza kwenye kiti. Kila mtu alikuwa kwenye ombwe la mawazo na tafakari kuhusu hiki walichokisikia kutoka kwa mzee Caleb.

"Kwahiyo hayo matukio yanayotokea duniani kote yanahusiana nini na Sanduku hili la Pandora au sijui Pithos… sijaelewa utofauti wake.!" Hatimaye Makamu wa Rais David Logan akavunja ukimya.

"Majina yote mawili ni sawa tu, Jina la 'Sanduku la Pandora' ndilo limezoeleka katika historia, lakini Zeus mwenyewe alivyomtengeneza mwanamke Pandora na kumpa zawadi ya lile sanduku aliliita jina 'Pithos'.! Na nikijibu swali lako sanduku hili linahusiana nini na kinachotokea sasa duniani…. Ni kwamba naamini wale wavuvi nchini Maldives waliookota ile chupa na kuifungua, ile chupa imetoka kwenye sanduku la Pandora… na haikupswa kufunguliwa.. shida imeanzia hapo.!"

Mzee Caleb akajibu.

"Kwahiyo unamaanisha kwamba hiyo sehemu ambayo George Washington alificha hilo sanduku imegunduliwa na sanduku halipo?"

Akauliza Bi. Naomi Cole, mshauri wa Rais kuhusu usalama.

"Hakuna anayeweza kujua ni nini kimetokea na kama sanduku limepota au kuondolewa sehemu iliyohifadhiwa… ila ninachoamini ni kwamba ile chupa imetoka kwenye Pithos, lile sanduku la Pandora.. Na hii inamaanisha kwamba limefunguliwa... Namna pekee tunavyoweza kujinusuru na kinachoendelea duniani kote ni kutafuta mchoro uliopotea wa George Washington ili tuweze kufika sehemu Pithos ilipo na kuirejesha kwenye hali ya kawaida..!" Mzee Caleb akaongea kwa msisitizo mkubwa.


"Ile chupa iliyookotwa na wavuvi kutoka Maldives iko wapi?" Jemedari George Smith akauliza.

"Inafanyiwa utafirti Stanford University idara ya Akiolojia.!" Mkurugenzi wa CIA, James Ruppert akajibu.

"Hii chupa ilikuwa na nini ndani yake?" Mzee Caleb akauliza.

"Ndani ilikuwa na karatasi tu yenye maandishi ya kale mno ya kilatini… neno pekee ambalo tuliweza kulielewa kwenye hiyo karatasi ni 'Novus Ordo Sedorum' ikimaanisha 'The New Order Of Ages'!" Mkurugenzi wa CIA, James Ruppert akaeleza.

Mzee Caleb akashituka kweli kweli.

"Kwanini hamkuiweka hii taarifa kwenye vyombo vya habari, kuhusu hiyo karatasi ni hayo maneno?" Caleb akauliza kwa mshangao mkubwa.

"Ni ngumu kueleza umma kila kitu, taarifa nyingine muhimu ni lazima zibakie kuwa siri… vipi kwani mzee mbona umeshituka sana?" Ruppert akuliza.

"Nahitaji kuiona hiyo karatasi.!!" Mzee Caleb akaongea kwa hofu na kupaniki huku anainuka.

"Oooh samahani mzee! Tueleza nini unafikiria?" Makamu wa Rais akauliza.

"Mheshimiwa, nimesema nahitaji kuiona hiyo karatasi sasa hivi!!" Mzee Caleb akaongea kwa msisitizo huku ametoa macho.

Bila maelezo zaidi wote wakainuka na kuanza kutoka nje. Katibu Mkuu kiongozi mara moja akawajulisha watu wa Secret Service kuaandaa chopa ya Rais Marine One kwa ajili ya kuelekea Stanford University.

Dakika kama tano baadae wote walikuwa mbele ya Marine One.

"Mheshimiwa, sidhani kama kuna ulazima wa wewe kuongozana nasi… ni vyema ukiendelea na majukumu mengine hasa zoezi la kumtafuta Rais! Tuache sisi tuendelee na hili na kisha tukueletee mrejesho!" Ruppert akajaribu kumshawishi Makamu wa Rais abaki.

"Acha kupoteza muda.. Let's gooo!" Makamu wa Rais akajibu kana kwamba hajasikia kilichoongelewa na Mkurugenzi wa CIA na akaamuru wengine wote wapande kwenye chopa na kuondoka.

Wote wakapanda, Makamu wa Rais, Mzee Caleb, Katibu Kiongozi Kevin, Bi. Naomi Cole na Mkurugenzi wa CIA James Ruppert.


Muda si mrefu Marine One ilitua chuo Kikuu cha Stanford.

Baada ya kuwasili, moja kwa moja wakaongozwa na Secret Service mpaka kwenye Jengo la Idara ya Akiolojia.

Na walipofika hapa wakaongozwa moja kwa moja mpaka kwenye maabara inayotumia kuhifadhi vitu vya kale.

Makamu wa Rais na msafara wake walipoingia ndani ya maabara hii waliwakuta wenyeji wao, wataalamu wa Akiolojia wanawasubiri, lakini ajabu ni kwamba walikuwa na hofu kubwa kwenye nyuso zao.

Baada ya kusalimiana nao Makamu wa Rais akaanza kuongea.

"OK! Nadhani mnafahamu kwanini tuko hapa?? Tunahitaji kuona chupa ambayo iliokotwa na wavuvi nchini Maldives na hasa hasa tunahitaji kuona karatasi ambayo ilikutwa ndani yake.!" Makamu wa Rais, David Logan akaongea.

"Mr. Vice President nasikitika kukwambia kuwa chupa hiyo wala karatasi yake hatunayo?" Mtaalamu mmoja aliyevalia miwani kubwa ya macho akaongea kwa woga na heshima kubwa.

"Nini??? Imeenda wapi?" Makamu wa Rais akauliza kwa hasira.

"Chupa huwa inahifadhiwa kwenye jokofu hili hapa la chini ya sentigredi za selsiasi -18 ili ibakie kwenye hali yake ya asili… lakini leo tulivyoambiwa kuwa unakuja kwa ajili ya chupa hii.. Tulipoitoa chupa kwenye jokofu ili tuiandae upate kuiona, tukagundua kuwa chupa iliyomo ni feki.. Imebadilishwa.. Na tunaamini ni mmoja kati yetu kwenye idara ndio amefanya hilo!" Yule mtaalamu akajieleza.

"Ni nani? Na amefanya hivyo kwa dhamira ipi?"

"Tunaamini ni Dr. Cindy Wheaton amefanya hivi… yeye ndiye alikuwa in charge kwa chupa hii na kuongoza tafiti.!"

"Yuko wapi?" Makamu wa Rais akauliza kwa hasira.

"Ameenda Tanzania wiki ya Tatu hii sasa… ameenda kufanya tafiti kuna miji mitatu nchini humo imetwaliwa na kuwa Anabelle.!"

Alipoongea sentesi hii mzee Caleb alishituka na kuishiwa nguvu mpaka kukaa chini.

"No no no no.! Siamini kama anataka kufanya ninachokiwaza… no no.! Tafuteni mawasiliano naye haraka niseme naye!!" Mzee Caleb akaongea huku anakaa chini kwa hofu na kunyong'onyea.

"Ni nini mzee?" Ruppert akauliza.





ITAENDELEA JUMNANNE..
 
EPISODE 3 & 4, POST # 154 & 155


Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi @Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM @Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu The Certified DON SINYORI mij adden
bwii ONTARIO Kobe The Vein Mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya Sitaki ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell Toyota escudo mgumu2 troublemaker Linamo shedede kamtu33 SteveMollel ngushi Donald stewart Mshuza2 Glycel mnonje Ochuanilove SingleFather Santi
 
Back
Top Bottom