The Citizen You Can't Be Serious!! Nyie ni Gazeti Makini!!

The Citizen You Can't Be Serious!! Nyie ni Gazeti Makini!!

Wewe ESAM nyie so ndo mloleta uzi hapa ukimsifia Kakobe kwamba kafungua Minisrty huko Mareksni...Maajabu haya leo ndo nimesikia eti Kakobe Yupo tangia 2010.....Maajabu haya khaa...
 
Last edited by a moderator:
Hahaha hata waumini wake wanapumua maana GOLD zao walau zimetulia vifuani na masikioni mwao, wa kuvaa vilemba kama wadoezi wa ubwabwa nao walau nywele zinaonekana sasa na kushine! shit! mxxxiiiiiii

We dada khaaa...Bishara ya dini imekuwa dili sana...Na unapoamua kuifanya lazima uwe makini kweli..
 
Kwa nini watanzania tunakuwa wavivu wa kufikiri kiasi hiki? Kama walivyotangulia kusema wengine kama unataka ukweli wa Kakobe si uende kanisani kwake?umeshaambiwa nenda kanisani kwake Jumapili saa nane wakati wa ibada ukaangalie kama yupo au la, kanisa liko wazi kila jumapili nenda kaangalie kwa macho yako kwa nini usiende kutafiti mwenyewe halafu ndio uje kubwa bwaja huku mtandaoni baada ya kudakia habari za mitaani za watu ambao hawajawahi hata kukanyaga pale kanisani wakati liko hapo Mwenge tu?
 
Nasikia huwa anawaachia dvd muwe mnamwangalia haruhusiwi mtu kupanda pale kuhubiri
 
Ndugu wanaJF,

Nimesikitishwa na kushangazwa na habari iliyochapishwa na kupewa uzito mkubwa sana (lead story) na gazeti la The Citizen toleo la jumapili tarehe 07-04-2013 iliyo na kichwa kifuatacho:
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]"Where on earth is Kakobe? Local church anxious as ‘healer’ bishop skips town".[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Katika habari hiyo mwandishi wake Bwana Mkinga Mkinga alidai kwamba Askofu Kakobe hajaonekana katika miezi sita iliyopita na kwamba kwa mara ya mwisho kuonekana kanisani Mwenge ilikuwa mwezi Januari mwaka huu. Na kwamba sasa hivi yuko Marekani ndiko alikohamia. Pamoja na madai mengine ya kuzushi mwandishi huyo ambaye kwa kweli ninao ujasiri wa naweza kumwita 'uchwara' anadai kuhudhuria ibada ya Pasaka tar 31-03-2013 na kukuta ikiongozwa na aliyemtaja kama Mchungaji Hezron (jina ambalo sijawahi hata kulisikia). Kwa FGBF Dar es Salaam tunaye mchungaji mmoja tu ambaye ni Mchungaji Zakaria Kabobe.

WanaJF kwa ufupi na watu wengine wapenda ukweli habari hizi ni za uzushi na uongo mtupu, na mimi kama mshirika wa kanisa la FGBF Dar es Salaam nasema hivi tangu Jumapili ya Agosti 15, mwaka 2010 alipokuwa Zambia kwa ajili kazi ya Mungu hatujawahi kumkosa kwenye ibada yoyote ya Jumapili. Kwa mfano, jumapili ya Pasaka tulikuwa na baba yetu Askofu Kakobe kama ilivyokuwa jumapili zote zilizotangulia.

Nilikuwa naliheshimu sana gazeti la The Citizen lakini kwa habari hii naanza kutilia shaka umakini wao. Natoa wito kwa Mtendaji Mkuu wa MCL Mzee Tido Mhando, Mhariri wake Mkuu Bwana Machumu na hata mwandishi wa habari hiyo ya kizushi Bwana Mkinga wawe makini vinginevyo wataliharibu gazeti. Nawasilisha

Kwa habari hiyo ya kizushi fuata link hii: http://Where on earth is Kakobe? Local church anxious as ‘healer’ bishop skips town

Nenda mahakamani ama mwandamane kama ni uongo na kwanini kanisa liwe na mchungaji mmoja na akisafiri mnaongozwa na nani kwenye ibada?
 
Niliona recently tv fulani ikionyesha akipewa mapokezi makubwa Lubumbashi, kwani ilikua lini?
 
Mimi nadhani wakati mwingine siyo vizuri kuwa too emmotional for nothing. Kama gazeti, hakuna kosa kuuliza mahali alipo any public figure, Kakobe akiwa mmoja wapo. Si sahihi pia kuleta emotions zitokanazo na imani binafasi kwa mtu badala ya kuwa na ile imani ya ukweli kwa Mungu. Napata picha kuwa ndugu mleta uzi unamuamini sana Kakobe kuliko hata Mungu wako na ndio maana umejitahidi kuhakikisha kuwa unamponda Bwana Mkinga na huku ukituonyesha waJF kuwa unafahamu The Citizen ni gazeti makini sana likiwa na uongozi thabiti wa Managing Editor Bakari Machumu aliye chini ya Managing Director wa Mwananchi Communications Limited, Tido Mhando. Sidhani kama emotions zako zinaweza kuondoa umakini wa gazeti mbele za wanaJF haswa wale wenye msimamo wa kumwamini Mungu aliyehai kuliko kumwamini mtu.

Mleta uzi unapaswa kukumbuka kuwa Kakobe ni binadamu kama wewe na kuwa naye yuko kama wengine wote so kumuamini kama yeye ni mtu asiye wakaida kunaweza kuathiri uwezo wako wakufikiri kwa kiasi kikubwa. Wote tunatambua kuwa Kakobe huyu huyu anakesi mahakamani akidaiwa na wale ambao katika kanisa lake mumewapa majina ya 'Wabaya wake' eti kwasababu wamehoji matumizi ya Kanisa mahakamani. Wote twajua kuwa kule mahakamani wale 'Wabaya Wake' wameambiwa kesi hiyo itawasumbuwa kwasababu eti kanisa limesajiriwa kama mali yake huyu Baba Yenu Askofu Kakobe (Kumbuka Yesu alikataa watumishi wake kuitwa Baba - Mathayo 23:1 mpaka mwisho) na hivyo kama ni kweli ametumia vibaya zile TSH14bilini basi ametumia pesa zitokanazo na his own investment. Je, huu ndio utukufu unataka kutuonyesha kuwa yeye hana dhambi? Na hata hiyo habari ya umeme wa Tanesco, ikumbukwe kuwa aliwahi kutuambia Watanzania kuwa ule umeme usingewaka baada ya Tanesco kulazimisha upite mbele ya kanisa lake. Mbona unawaka? Ni ule unabii wa kuwa Mrema angekua Rais wa Tanzania mwaka 1995, mbona haikuwa na sisi tunabaki kujifanya hatutaki kuona, kusikia wala kuambiwa kuwa mwaminini Mungu na siyo binadamu.

Kama unachosema wewe ni kweli, basi mpeleke Bwana Mkinga, Bakari Machumu au Tido Mhando kwa Kakobe. Kama kweli yupo nchini, basi aje kwenye ofisi za Mwananchi ili approve the newspaper wrong. Tuache propaganda ndugu zangu. Kama hayupo ni kweli hayupo. Binafsi nawapa hongera sana The Citizen kwani wangekuwa unprofessional, wangeweza hata kuandika mengine mengi ya mitaani yamhusuyo Kakobe. Wewe mwenyewe jiulize tu: Je, idadi ya wale tuliokuwa tukisali pale bado iko pale pale au wengine wameweza kupata kuokolewa na Mungu sasa amezifungua akili zao mpaka wamepata kuanza kufikri vizuri tena? Angalia idadi na utuletee uzi mwingine kwani ni dhahiri idadi imepungua sana na mumebaki wachache mnaod=subiri Mungu aje awaokoe kutokana na kifungo cha kutokusikia, kuona wala kutaka kuambiwa.

Bwaga ya moyoni, hukuwa na haja ya kuandika haya yote, niseme moja tu kwamba kilichonisukuma kuanzisha uzi huu ni madai ya mwandishi wa habari hiyo kuwa jumapili ya Pasaka alikuja kanisani akakuta ibada inaongozwa na Mchungaji anayeitwa Hezron, wakati ibada aliongoza Mchungaji Kakobe mwenyewe tangu saa 3 mpaka 11 jioni. Mengine ningemezea lakni sio hili.

Hapo kwenye red labda wewe waambie wanakaribishwa kanisani jumapili kuanzia mida ya saa 7 mchana na kuendelea watamkuta tayari amepanda madhabahuni akifundisha neno la Mungu.

Hapo kwenye blue, mtumishi wa Mungu yuko na shughuli nyingi hana muda huo, yeye yuko mbele za Bwana kuutafuta uso wake saa zote, wenyewe ndo waje kama nilivyosema awali.
 
Mimi nimebaki kimya tu.
Lakini kukata mzizi wa Fitna, ingepasa kwa Kakobe kujitokeza hadharani mbele ya waandishi wa habari siku ile ile habari hii ilipotoka(Hata sasa anaweza kujitokeza hadharani) na kukanusha habari hizi kama kweli ni uzushi.

Sidhani kama hili linashindikana Kama kweli Kakobe yupo Tanzania, kwa sababu Kakobe ameshawahi kujitokeza mara kadhaa huko nyuma na kuongea na waandishi wa habari.
Vinginevyo kuna kitu bado kinajifichaficha....

Mimi nadhani tusiandikie mate wakati wino upo, anayetaka kumwona na kuthibitisha uzushi wa habari hii namkaribisha aje kanisani kuanzia saa 7 mchana njoo na kamera mchukue na video muwaletee JF ili wajionee wenyewe uzushi wa Bwana Mkinga wa The Citizen
 
Kinyamana, ukweli unao, ninachokiona kwako ni kujipa moyo. Nilikuwa napindisha sentensi sasa wacha ninyooshe. Kakobe si lolote na mbele ya Mungu ana ya kujibu. Mifano hai ninayo kama hii ligi unaitaka niko tayari. Hakuna aliyemuhukumu, magtendo yake yanaonyesha kwamba siyo.

Pole sana kwa kuishi kwenye ndoto, eti mbele Mungu ana la kujibu lipi hilo!! Na aliyekujulisha hilo unalosema ni nani, Mungu mwema akusamehe na siku moja nuru ikuzukie utubu kwa kumnenea mabaya masihi wa Bwana
 
TANU hakuna uzushi, kakimbia madeni, na kaishaokota sadaka za waumini wake sasa anatanua! God forbide!

Nakuonea huruma kwa kukubali kutumiwa na shetani kusema uongo mchana kweupe, mbona unajidanganya na kudanganya wanaJF. Sasa nasema na kuahidi kuanzisha uzi jumapili wa kuwaita wanaJF ili waje kumwona mchungaji wangu akiwa madhabahuni anachambua gombo
 
Hahaha hata waumini wake wanapumua maana GOLD zao walau zimetulia vifuani na masikioni mwao, wa kuvaa vilemba kama wadoezi wa ubwabwa nao walau nywele zinaonekana sasa na kushine! shit! mxxxiiiiiii

Pole hata hujui usemalo, hayo uloyataja hata hakuna mshirika yeyote wa FGBF anayejishughulisha nayo. Tuna kazi moja tu. Kuhubiri Injili isiyochujwa wala kuchanganywa na mapokeo na kuishi maisha ya usafi na utakatifu ambapo pasipo huo hakuna atakayemwona Mungu (Ebrania 12:14).

Kwa kweli nakukaribisha kanisani jumapili ya tarehe 14 April 2013 ujifunze neno la Mungu Yesu anarudi usikalie kuendekeza uzushi na kuongea vitu usivyo na uhakika navyo
 
Niliona recently tv fulani ikionyesha akipewa mapokezi makubwa Lubumbashi, kwani ilikua lini?

Ziara ya hiyo ya Lubumbashi aliifanya tangu Alhamisi tarehe 6 Mei hadi Jumapili tarehe 9 Mei 2010[FONT=Lucida Grande, Helvetica, Verdana, sans-serif].[/FONT]
 
Nenda mahakamani ama mwandamane kama ni uongo na kwanini kanisa liwe na mchungaji mmoja na akisafiri mnaongozwa na nani kwenye ibada?

Hatuna muda wa kupoteza tunafahamu nyuma ya haya yote yuko shetani na ndio kazi yake hiyo. Na pia hilo linatupa kujua kwamba kazi ya Mungu inasonga mbele bila kuchujwa maana mti wenye matunda ndo hupopolewa kwa mawe.
 
Nasikia huwa anawaachia dvd muwe mnamwangalia haruhusiwi mtu kupanda pale kuhubiri

Usiridhike na kusikia jenga utamaduni wa kutafiti na kujua kitu wewe mwenyewe
 
Kama yupo Bongo mbona hatumuoni?

Anaonekana kanisani kama nilivyotoa mwaliko kwa wengine hapo juu na wewe nakukaribisha. Kama ulitegemea kumwona mtaani au supermarket pole, hutomwona maeneo kama hayo. Yeye amejitoa maisha yake yote kwa ajili ya kazi ya Mungu hana muda wa kurandaranda mitaani
 
Back
Top Bottom