The case against MUSTAFA MKULLO

Mwakilishi

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
484
195
Morani75,

When it comes to credibility of these "degrees", your guess is as good as mine! I would like to believe that the powers-that-be are well aware of this problem, but then no one is willing to take the bull by the horns as it were... who knows why?

If nothing is done to stop this shameful trend, we will end up having vihiyos in every profession to our own detriment.
 
MamaParoko

JF-Expert Member
Jan 14, 2008
464
0
hivi wana jf mnaonaje kuhusu huu ushauri kuwa, rais awe anapendekeza jina la waziri mkuu au cabinet yake halafu analeta bungeni kwaajili ya kuwa approved na wawakilishi kwa kuojiwa na kamati ya hearing, hapo waulizwe maswali kuhusu utendaji wao huko walipotoka na maamuzi waliyowahi kufanya huko nyuma kama ni kwa maslahi ya taifa, hizi hearing nishaona huko marekani kama rais akiteua kwa mfano mwanasheria lazima apite kwenye intavyuu ya nguvu mbele ya kamati, ndio anapigiwa kura ya kupitishwa, sio kwenye mjengo wetu kumejaa ushabiki tu, usio na manufaa kwa taifa wanakuwa kama wanamchagua kiranja wa shule ya msingi, kama ilivyotokea wkt wanamchagua mizengwe, angeulizwa tough question kujua ubora wake.
 
Koba

JF-Expert Member
Jul 3, 2007
6,136
1,500
nafikiri ACCA ni qualification tosha ya kumweka katika kundi la wasomi na uwezo wa kuwa waziri,hiyo MBA inaonekana ni halali kaipata kwa kusoma na hiyo shule ina exist ingawaje the school does look like non accredited na mjue its not illegal kutumia non accredited degree in Tanzania maana hakuna hiyo sheria bado,na sio kila non accredited school ni fake maana kuna sheria ya kuomba exemption from accreditation kutokana na mambo ya kodi au kutokubaliana na bodi zinazotoa hizo accreditation
 
Mwakilishi

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
484
195
Koba,

Ni kweli viko vyuo kweli ambavyo sio accredited lakini hii Almeda wala siyo Chuo kabisa, kulikuwa na story on 60minutes kama sikosei walifanya undercover stint, jamaa akawasiliana na Almeda, akalipa hela kataja jina la Mbwa wake na degree anayotaka, tarehe ya graduation akachagua basi wakamtumia in a few days. Hicho sio chuo wala nini ndio ukweli huo!
 
Mbangaizaji

Senior Member
Jul 23, 2007
121
225
Koba,
Mi nakubaliana na wewe kuwa ACCA ni kualification tosha kuwa waziri. Hako kwa MBA kanyanga tunaweza tukaachana nacho. Lakini swali la msingi nin kwamba Mkulo toka 2000- 2005 alikuwa anafanya nini?
Na je alipotoka NSSF, was it by honorable or dishonarable discharge?

Tukijibu hayo maswali ndo tunaweza kusema kweli ndugu yetu huyu anafaa kuwa Minister of Finance. Pale si kuna fedha zetu, na si ndio pale tulipoibiwa? Sasa lazima tupate mtu ambaye his intergrity is not questionable. La sivyo tutakuwa tunaendeleza tu ule "UJASIRI WA KIFISADI"
 
Koba

JF-Expert Member
Jul 3, 2007
6,136
1,500
Koba,

Ni kweli viko vyuo kweli ambavyo sio accredited lakini hii Almeda wala siyo Chuo kabisa, kulikuwa na story on 60minutes kama sikosei walifanya undercover stint, jamaa akawasiliana na Almeda, akalipa hela kataja jina la Mbwa wake na degree anayotaka, tarehe ya graduation akachagua basi wakamtumia in a few days. Hicho sio chuo wala nini ndio ukweli huo!

...mkuu najua story nzima ya Almeda na wala sifagilii non accredited school maana ni upotevu wa resource tuu na kuharibu credibility yako,hapo juu nilikuwa najaribu kutoa maoni yangu tuu na cha maana wanachoweza kufanya ni kuanzisha sheria ya kutotambua hivyo vyeti ili kuondoa shida kama hizi na watu wanaweza question kina mkullo legally lakini sasa hivi is a waste of time!
 
Morani75

JF-Expert Member
Mar 1, 2007
615
0
Mkuu Koba na wengine.... Heshima mbele.

Ni kwamba sheri ipo na tume ilianzishwa (anagalia post yangu ya nyuma nime refer to the thread) inaitwa Tanzania Council of Universities. So sisemi wale majamaa hawafanyi kazi lakini ninachotaka ni kwamba mwaka 2006 nadhani Julai ilikuwa ni "mstari mfu" wa watu wote kufanya a"accreditation ya vyeti vyote vya nje". Sasa issue kwenye post yangu hapo nyuma ni kwamba, Je ni kweli hawa "maDokta" na "maMBA" yote yemepitishwa pale TCU??

Tukishajibu hilo then tunarudi kwenye main issue ya ile thread yangu kule kwenye "Hoja Mchanganyiko", Is TCU as sucessful and foolproof as one would like/insist it to be??"

Naomba kuwakilisha!!!
 
...kama ulivyoonyesha sheria ipo na council ya kusimamia ipo na deadline ilikuwa 2006,nataka kujua kitu kimoja tuu kama 2006 ni deadline, je waliopata before 2006 ina maana hii sheria haiwahusu na vyeti vyao vitaendelea kuwa valid? in fairness you cant take away from them because of new rules ambazo hazikuwepo wakati wanasoma/kutafuta hivyo vyeti...anyway any diploma mills or whatever it is is just trashy na ni vizuri kuwaelimisha watu kuhusu hii kitu!
 
Pundit

JF-Expert Member
Feb 4, 2007
3,738
1,225
Kumbe mmajua kuwa ni fisadi mbona hamkusema kabla hajachaguliwa? Aliyeficha hili ndiyo fisadi zaidi. Huyu bwana alikuwa Naibu Waziri wa Fedha lakini mkashabikia Zakia ajiuzulu, afukuzwe, hakuna aliyetaja ufisadi wa naibu waziri. Kapandishwa cheo ndiyo mnakuja kusema na huyu naye ni fisadi

Watu tulishamsema Mkullo sana alivyochaguliwa kuwa Naibu Waziri.

Tatizo hapa linaenda zaidi ya Mkullo, tatizo ni uongozi mzima wa CCM pamoja na Rais mwenyewe unanuka rushwa.Na watu tulishasema hata kabla ya uchaguzi kuwa Kikwete ni rais bomu.

That Onion article aside, it probably is objective (The Onion being The Onion) Mkulloa ameshashiriki katika mkopo mwingine usio collateral kama huo, the other time kwa Sumaye.Ameshiriki kufanya maasi na watoto wa shule wa kike ambao ni wadogo kuliko umri unaotakiwa kuwa wa wanawe, amenunua shahada ya uzamili na listi inaendelea.Haya ni yale tunayoyajua kwa bahati tu sisi watu wa mbali.Sijui walio na info za ndani.

usiseme hatujasema, ukitaka kuwapangua Mawaziri wa CCM kwa ubadhirifu na ufisadi hamna hata mmoja atakayebaki maana wote wametumia fedha za ufisadi kupigia kampeni, kuanzia rais mpaka wabunge.

Tuondoe CCM labda tunaweza kuwa na nafasi.
 
Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,281
1,195

Mkulu hili ni sahihi kabisa, ni time bomb waiting to explode....
 
Insurgent

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
469
0
Wametoa fisadi mmoja wametuletea mwingine!!! JK ameweka mtu wa kumchotea mahela 2010. Si unajua tena mambo ya CCM. Lakini nafikiri is better than Meghji!!!

Kumweka Meghji na mafisadi ni ufisadi. Naona kuna haja ya kutoa definition ya ufisadi manake mafisadi sasa wanaitumia hii vocabulary to their advantage.

Nimegundua kitu kimoja hapa JF. Tuna mafisadi wengi sana. Wengi hapa wapo kwenye makundi ambayo yamefanya ufisadi toka enzi za Mwalimu. Huyu Meghji alikuwa tishio kwani baada ya kugundua mafisadi wamemdanganya alirekebisha kosa lake mara moja na kuomba auditing na hii auditing plus kuzidai pesa za import support ndio iliyopelekea wengi kumpiga vita.

Tusidanganyane hapa...mafisadi ni wengi kwani haiingii kumwita Meghji fisadi wakati muhusika mkuu (Basil Mramba and Co.) wakiwa wameachwa.

Meghji amefanya kazi kubwa ya kugundua wizi uliokuwa unaendelea miaka nenda miaka rudi. Bila ya auditing yake na imani MAFISADI wangekuwa marafiki wake mpaka leo. Haiingii akilini...KUMWACHA MUUAJI NA KUMKOMALIA DAKTARI ALIYEFANYA MAKOSA KWENYE CERTIFICATE OF DEATH (not to mention the certificate was corrected in due process)

Naamini JF ina Mafisadi wengi ambao ni vibaraka wa hawa mafisadi wakubwa....ukisoma humu ndani utaelewa ufisadi wa humu ndani ni more scientific lakini ni ufisadi uleule!
 
Chuma

JF-Expert Member
Dec 25, 2006
1,329
0
Insurgent..sijui ulichokusudia kumpamba Zakia Meghji au kumponda...nilivyoelewa umempamba...Uoni wangu Zakia Meghji alikuwa na unafuu kuliko Huyu kaka aliepewa ujiko hivi sasa. kama kesi ilikuwa kuwatoa wote waliomo ktk Ripoti ya Mwakyembe au ..why Chenge abaki?

Nilichojifunza kwa serikalini Kumejaa ufisadi...basi Meghji alikuwa na unafuu zaidi kuliko Mkullo.

Naweza kukubaliana nawe kuwa kuendelea kwa Zakia Meghi pale wizarani mafisadi wa BOT, EPA etc wangekuwa ktk wakati Mgumu

ila Meghji kama yupo serious basi Bungeni ayaseme akae kidedea...ubunge uliopewa si Fadhila, bali ni Haki yako..SIMAMA na Akina Mwakyembe,Kilango, SLAA na wengineo ili haki ya Mtanzania ipatikane
 
Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,281
1,195
Chuma,

Kwenye hili la Mkulo ninakuhakikisha kila aina ya ufisadi uta unfold pale fedha, kuanzia misamaha, ngono na above all incompetency huyo mtu hana analytical capability atakuwa anasaini tu yaani nipo hoi tumeruka maji tumekanyaga tope sasa tunayatafuta majiili tunawe....
 
Madela Wa- Madilu

JF-Expert Member
Mar 24, 2007
3,065
1,195
Pundit.

Umetaja kuhusu ngono za aibu za Mustafa Mkullo.
Nakwambia hoja ya ngono kwa viongozi wetu siyo maarufu hapa JF kwa sababu wengi inaonekana tunaitetea sana na kusema ngono za ovyo ovyo na aibu ni mambo binafsi.

Tunatetea viongozi wapenda ngono kwa sababu hata sisi wenyewe katia udogo wa madaraka yetu tuna enzi ngono. Hatuzifanyi kwa level ya viongozi hao kwa kukosa uwezo wa kufanya na pengine wasaa lakini kingono mwelekeo wetu ni huo huo.

Ukitaja nguo za ndani tutakuambia uache matusi. Ukieleza kisa cha mzee Mkulo kuopoa vibinti vya miaka 20 na kuvibamiza kwa mtindo wa Sandwich tutakuambia wivu huo, unaona gele.Kwetu mzee mzima kujiweka wazi mbele ya vijuu ni sehemu ya utamaduni, hakuna matusi wala nini.

Tusijue kwamba viongozi wapenda ngono huabudu ngono hiyo kwa gharama za fedha zetu wenyewe.
Wataiba wataharibu watatawanya ili mradi kipatikane chochote cha kulipia uhanga wa ngono usio koma.

Watu wangapi baada ya kuachia ngazi wamejuhuzuru kuvunjari nyumba ndogo na kuvizia vibinti vya watu?

Hivi tunadhani hivyo vibinti vinawependea unene wa mashavu na ukubwa wa mtumbo yao?
Vinaipenda Pochi, pochi tunayo ibiwa kwa kutumia madaraka vibaya na kutufanya wananchi wote wajinga.

Ngono za ovyo ni tatizo kubwa katika kilenge cha utawala wa nchi yeyote Tanzania ikiwemo.
 
Augustine Moshi

JF-Expert Member
Apr 22, 2006
2,528
2,000
Kwa nini tunatawaliwa na wezi? Mtu ambaye miaka ya nyuma alichukua shilingi milioni 250 za walalahoi, kwa nguvu, na kufikisha CCM milioni 10, ni mwizi. Hizo milioni 240 zilizobaki labda aligawana na akina John Kapinga, Marehemu Horace Kolimba, na baadhi ya viongozi wakuu wengine wa CCM, lakini anabaki kuwa ni mwizi, tena wa kutisha.

Ni nchi ya aina gani inachagua watu walioiba fedha za nyuma kuwa Mawaziri wa Fedha? Mwizi wa fedha za umma asimamie fedha za umma?

Inaelekea sehemu kubwa ya viongozi wetu ni watu wenye asili ya wizi, na wameshaiba bila kukamatwa mara kadhaa. Hatutaendelea mpaka tutakapokuwa na uwezo wa kukataa kutawaliwa na wezi.

Kwa sasa nasema hivi: Hatumtaki Mustafa Mkullo awe Waziri wa Mipango na Fedha. Sababu yetu ni kwamba ameshaiba mamilioni ya fedha za uma. Tunataka afunguliwe mashtaka, na sio awe waziri mwandamizi.
 
Sawasawa kabisa mkuu MUSTAFA HAIDI MKULO hafai hafai hafai...
 
Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
6,930
2,000
Ukitaja nguo za ndani tutakuambia uache matusi. Ukieleza kisa cha mzee Mkulo kuopoa vibinti vya miaka 20 na kuvibamiza kwa mtindo wa Sandwich tutakuambia wivu huo, unaona gele.Kwetu mzee mzima kujiweka wazi mbele ya vijuu ni sehemu ya utamaduni, hakuna matusi wala nini.

Astakhafilula wee Madela wee mwana wa Madilu! Sandwich tena? Toba, Mkuu! Ulichosema ni kweli tupu. Jamii yetu bado inaona hao vimwana ni haki yetu. Ni hasusa yetu. Na mbaya zaidi hata hao wakina mama ambao ungedhani wata'sympathize' nao wanaingia mitini. Mpaka yanapowakuta.

Mtu yeyote anayetumia cheti ambacho kina utata katika kujikwaza hastahili uongozi. Mimi Fundi stadi wa Mchundo nikiibuka na cheti feki cha uhandisi hata ujumbe wa nyumba kumi nitakuwa sistahili. Naona huyu bwana hatufai kwa kila hali.
 
Augustine Moshi

JF-Expert Member
Apr 22, 2006
2,528
2,000
Imekuwaje hadi JK akamteua mtu aliyetuhumiwa kuiba kiasi kikubwa za fedha za umma awe Waziri wa Fedha na Mipango? Au JK ana uhusiano wa karibu na wezi wa mali za umma?

Nadhani ilifika mahali viongozi waandamizi wa CCM wakaamua kugawana mali za umma. Wawili wakapewa Kiwira na mkataba wa kulazimisha capacity charge. Mmoja akapewa Kituo cha Mabasi cha Ubungo na parking fees za Dar. Mwingine akapewa parking fees za Arusha. Kabla ya hapo kundi moja lilijikita kwenye kuchota kwa kupitia SUKITA. Yupo aliyepangiwa kuchukua zaidi ya nusu ya royalty ya dhahabu. Wengine wakaunda makampuni mbali mbali yaliyochota BoT, huku wakiidhinishiwa malipo na Waziri wa Fedha. List ni ndefu.

Wote hao ni viongozi wa ngazi za juu wa CCM. Inaelekea wananchi wanaona haya kutaja ukweli kwamba wezi wetu ni viongozi wa ngazi za juu wa CCM. Waswahili husema: "Anayeficha ugonjwa kifo kitamsema".
 
Game Theory

JF-Expert Member
Sep 5, 2006
8,555
0
Mustafa Mkullo pamoja na kuwa na track record mbovu imekuwaje akapewa wizara ya fedha? JK must be jocking kwani kumpa Mukulo wizara ile ni sawa na kumpa fisi kondoo ...

Last edited:

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
123,872
2,000
Mustafa Mkullo pamoja na kuwa na track record mbovu imekuwaje akapewa wizara ya fedha? JK must be jocking kwani kumpa Mukulo wizara ile ni sawa na kumpa fisi kondoo

Huyu si ndiye aliyehusika na kashfa ya NSSF ya kununua magodown ya Yusuf Manji yasiyozidi thamani ya shilingi milioni 100 kwa bilioni 47?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom