Thanks GOD, Thanks JF!

Thanks GOD, Thanks JF!

kwani wewe haujui zawadi za kisasa? Mi sijui kununulia mtoto wa mtu nguo. Ntajuaje uliagiza uingereza quality stuff? Mambo ya kununulia mtu zawadi anaitupa gereji staki. Nakuja na laptop (najua tu atahitaji kujifunzia), mbuzi ya supu na mzinga wa gongo kwa ajili ya baba. Toooppp!

Hahahaha mama nyamtondo huu unaotaka kufanya ndo tunaita ubahili wa kidigiti...!!! anyway karibu bana tumle huyo mbusi...
 
Ndugu wanaJF,
Kwanza kabisa napenda kutumia fursa hii kwa niaba ya familia yangu kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuifikia siku ya leo tukiwa buheri wa afya. Ni rehema zake tu zimetuwezesha kufikia hapa tulipo kwani tunatambua wazi kwamba ni watu wengi sana hawajapata nafasi ya kuuona mwaka 2013 ama kuiona siku ya leo.

Pili ningependa niwashukuru kipekee sana wadau wote wa JF hususan crew nzima ya MMUkwa namna ambavyo mmekuwa nasi tangu Jumatano 02/01/2013 hadi hivi leo wakati huu ninapoandika ujumbe huu.

Mke wangu (Mama Rhobi) ameruhusiwa jana kutoka hospitali, sasa yupo nyumbani akiendelea kujiuguza na papo hapo akimhudumia kijana wetu, kwani maziwa ya mama kwa mtoto ni tosha!

Kwa namna ya kipekee sana niwashukuru wale wote waliotutakia kheri kupitia JF na mitandao mingine ya kijamii, waliotupigia simu na wanaoendelea kutupigia, waliofika hospitali kutuona na wanaoendelea kufika kutuona nyumbani.

Kwa ujumla mama na mtoto wanaendelea vizuri sana, afya zao zimeendelea kuimarika kila siku. Kikubwa muendelee kuwakumbuka katika sala zenu na dua zenu.

Karibuni sana kwetu, kichuri kinapatikana kwa wingi.
Much respect guys, Viva JF. I wish you all the best of lucky in the year 2013!

Mwita Maranya "The blessing of the LORD makes one rich and prosperous and He adds no sorrows with it." Proverbs
 
Last edited by a moderator:
Mimi na wewe hatugombanishiki! Binti yaki si alijitahiidi kutugombanisha akashindwa akaishia kuwa rafiki yangu?Wala usijali unoko wake. Msalimie mama Rhobi.

Hii ndio raha ya kuwa na mpenzi understanding! i'm proud of you... salamu zimefika.
 
Thanks Rutashubanyuma for the words of wisdom from the Holy Bible.

user-online.png
Mwita Maranya Be blessed my brethren............u and family
 
Ni furaha sana mtoto akiongezeka kwenye familia! Nafurahi pamoja nanyi! Mpe pole na hongera mama rhobi!
 
ndio umuulize vizuri huyo Asprin, me nimechoka kumsubiria.
Madame B assuming kwamba Asprin amegoma kabisa kukusindikiza, tunafanyaje sasa ili kukipata hicho kibeseni? manake nshamwambia mama rhobi kwamba kuna mdau kapledge kibeseni, asipokiona si patachimbika!!
 
Last edited by a moderator:
nimefurah sana kwaajili ya afya tele walojaliwa mama Rhobi na kichanga.
Ushauri wangu ni hivi nitakuja kumwon akiwa na miez sita jamani hapo nitakahua anakalia ------ ama mgongo?? nasema ole wako lol!..........................muulize mwenzio Mtambuzi atakwambia ama Jiwe Linaloishii.

BTW Mungu akukuzie na wewe umelee vizuri aje akufae ukubwani.
 
Ndugu wanaJF,
Kwanza kabisa napenda kutumia fursa hii kwa niaba ya familia yangu kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuifikia siku ya leo tukiwa buheri wa afya. Ni rehema zake tu zimetuwezesha kufikia hapa tulipo kwani tunatambua wazi kwamba ni watu wengi sana hawajapata nafasi ya kuuona mwaka 2013 ama kuiona siku ya leo.

Pili ningependa niwashukuru kipekee sana wadau wote wa JF hususan crew nzima ya MMUkwa namna ambavyo mmekuwa nasi tangu Jumatano 02/01/2013 hadi hivi leo wakati huu ninapoandika ujumbe huu.

Mke wangu (Mama Rhobi) ameruhusiwa jana kutoka hospitali, sasa yupo nyumbani akiendelea kujiuguza na papo hapo akimhudumia kijana wetu, kwani maziwa ya mama kwa mtoto ni tosha!

Kwa namna ya kipekee sana niwashukuru wale wote waliotutakia kheri kupitia JF na mitandao mingine ya kijamii, waliotupigia simu na wanaoendelea kutupigia, waliofika hospitali kutuona na wanaoendelea kufika kutuona nyumbani.

Kwa ujumla mama na mtoto wanaendelea vizuri sana, afya zao zimeendelea kuimarika kila siku. Kikubwa muendelee kuwakumbuka katika sala zenu na dua zenu.

Karibuni sana kwetu, kichuri kinapatikana kwa wingi.
Much respect guys, Viva JF. I wish you all the best of lucky in the year 2013!

asante sana mkuu maranya kwa kutujuza zaidi..
 
Back
Top Bottom