Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,565
- 7,996
Ndugu wanaJF,
Kwanza kabisa napenda kutumia fursa hii kwa niaba ya familia yangu kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuifikia siku ya leo tukiwa buheri wa afya. Ni rehema zake tu zimetuwezesha kufikia hapa tulipo kwani tunatambua wazi kwamba ni watu wengi sana hawajapata nafasi ya kuuona mwaka 2013 ama kuiona siku ya leo.
Pili ningependa niwashukuru kipekee sana wadau wote wa JF hususan crew nzima ya MMUkwa namna ambavyo mmekuwa nasi tangu Jumatano 02/01/2013 hadi hivi leo wakati huu ninapoandika ujumbe huu.
Mke wangu (Mama Rhobi) ameruhusiwa jana kutoka hospitali, sasa yupo nyumbani akiendelea kujiuguza na papo hapo akimhudumia kijana wetu, kwani maziwa ya mama kwa mtoto ni tosha!
Kwa namna ya kipekee sana niwashukuru wale wote waliotutakia kheri kupitia JF na mitandao mingine ya kijamii, waliotupigia simu na wanaoendelea kutupigia, waliofika hospitali kutuona na wanaoendelea kufika kutuona nyumbani.
Kwa ujumla mama na mtoto wanaendelea vizuri sana, afya zao zimeendelea kuimarika kila siku. Kikubwa muendelee kuwakumbuka katika sala zenu na dua zenu.
Karibuni sana kwetu, kichuri kinapatikana kwa wingi.
Much respect guys, Viva JF. I wish you all the best of lucky in the year 2013!