Thanks God for Giving us Kikwete

Mkandara,

..hili suala la "kila mtu na mzigo wake" mimi naliunga mkono. nadhani ni suala la personal responsibility.

..mimi nilifikiri baada ya ufujaji mkubwa ktk ile semina elekezi kule Ngurdoto, JK na serikali yake watajirudi na kuwa makini ktk matumizi ya serikali.

..umeongelea kuhusu wapinzani kujipanga kwa chaguzi zinazofuata. hilo ni jambo jema na nategemea kuwa na wao wamejifunza kwanini wanashindwa ktk kila uchaguzi.

..kwa mtizamo wangu wapinzani bado hawafahamu wananchi/wapiga kura wa Tanzania wanataka nini.
 
Kuna kitu kimoja muhimu alifanya Kikwete tangu mwanzo wa utawala wake ambacho hajapewa credit anayostahili. Ni kushughulikia mauaji ya watu wanne yaliyofanywa na polisi Sinza kwa kikamilifu.

Kuna kila dalili kwamba Afande Zombe na washirika wake waliwaua raia wema in cold blood. Afande Zombe alidhani hakingekuwa kitu. Labda katika awamu iliyotangulia hakingekuwa kitu. Aliona mafisadi kaka zake kwenye Jeshi la Polisi (Mahita, Chico) walivyofanya maovu wapendavyo wakati wa Mkapa.

Tangu JK aingie madarakani kumekuweko na mafanikio makubwa katika nyanja ya kulinda raia na mali zao. Lazima nimpe credit kwa hilo.

Hata hivyo, iwapo itajagundulika Balali hakufa na ni mazingaombwe tu ya JK, basi nitafuta credit zote ninazompa kwa sasa.
 
Kuna kitu kimoja muhimu alifanya Kikwete tangu mwanzo wa utawala wake ambacho hajapewa credit anayostahili. Ni kushughulikia mauaji ya watu wanne yaliyofanywa na polisi Sinza kwa kikamilifu.

Kuna kila dalili kwamba Afande Zombe na washirika wake waliwaua raia wema in cold blood. Afande Zombe alidhani hakingekuwa kitu. Labda katika awamu iliyotangulia hakingekuwa kitu. Aliona mafisadi kaka zake kwenye Jeshi la Polisi (Mahita, Chico) walivyofanya maovu wapendavyo wakati wa Mkapa.

Tangu JK aingie madarakani kumekuweko na mafanikio makubwa katika nyanja ya kulinda raia na mali zao. Lazima nimpe credit kwa hilo.

Unatania, sio?

Tumeshuhudia mfumuko wa ujambazi ulio kithiri miaka miwili mitatu iliyopita. Sasa hayo mafanikio unayo ongelea sijui ni yapi.

Kuhusu credit ulizompa kwenye mauaji ya Sinza, haujasema alilishughulikia vipi hilo swala.

Na hata hivyo, haitakiwi kuwa kazi ya Rais kuingilia individual issues za jinai. Hizo ni kazi za ma RPC na wakuu wa Polisi wilayani. Hicho kitu Kikwete hakijui, kwa sababu likitokea tukio utasikia anasema amemwagiza Mwanasheria Mkuu au watendaji wengine kuhakikisha haki inatendeka. Muungwana, hizo ndio kazi zao hao law enforcers. Usiwazoeshe kufanya kazi kwa kutegemea Executive Orders!
 
Ndugu wa wafiwa walipolalamika kwamba kuna foul play, JK aliunda kamati iliyofanya kazi kwa haraka na kukusanya ushahidi ulioonyesha kwamba Zombe na wenzake waliwachukua wahusika na kuwaulia kwenye msitu nje ya Dar. Hukusikia hayo?

Kabla ya JK kuingilia Ikulu, Jeshi la Polisi lilishaanza kumtetea Zombe na kudai waliouawa ni majambazi waliokamatwa kwenye wizi Sinza.

Siku za mwisho wa utawala wa Mkapa majambazi walitawala nchi. Umesahau tayari? JK alimwondoa Mahita, na akateua mtu ambaye aliwatupia jicho wahifadhi wa majambazi (yaani akina Mohammed Chico). Hilo limepunguza sana wimbi la ujambazi. Huna shukrani?
 
Mchungaji,
Ingawa si mahala pake, Naam nimepanda grade. Nina mjukuu wa kike ana maneno mengi kama Mahlon! Inatia sana moyo kuona kwamba vijana mnaendelea kuguswa na masuala ya nchi yetu, mama yetu Tanzania. Ni changamoto nzuri kwa viongozi wetu na wananchi kwa ujumla. Bado nina imani ya kizamani kwamba "Tanzania Itajengwa na Wenye Moyo!" Naongoze - Vijana kama ninyi mnaovalia njuja masuala ya Taifa letu kwa faida ya Maendeleo ya wananchi wote kwa ujumla.
 
Jokakuu,
Mkuu kama ungejua maana halisi ya neno KILA MTU NA MZIGO WAKE kwa tafsiri ya walezi wa CCM, usingepongeza hili hata kidogo..
Kwa sababu mzigo wa CCM sio wakati wa kuwajibika kwa wananchibali ni kila mtu abebe kile anachoweza..wamegawana ma deal ambayo yanahusiana na maliza taifa. kila mmoja wao ana mahala amekwisha kamata (mzigo) huwezi kupenyeza.. Ukitaka nyumba za serikali kwanza wana check na mtu huyo maana ndicho kifurushi chake alichoondoka nacho ktk mageuzi..
 
I was right on the money on this! Ukimya wa Kikwete unawaonyesha Watanzania ukweli kuwa CCM ni chama kibovu. Sasa wanaanza kulogana na kutiliana sumu ili kutishana!
 
Rev Kishosha, unanikumbusha story hapa.

Kulikuwa na ndg mmoja aliomba sana Mungu ampe chakula. Alikuwa na udhaifu wa mwili hakuweza kutafuta chakula chake wala kununua nguo. Alisali saaana kwa muda mrefu hakuwa kapata jibu. Siku moja Mungu akamwambia asukume jiwe lililokuwa ndani ya chumba kimojawapo pahala nyumba ilipojengwa. Basi alianza kazi ya kulisukuma. Siku miezi ikapita jiwe hata halikusogea. Siku moja akaja shetani akamkuta anasukuma jiwe. Shetani akamwambia mbona unapoteza muda kwa kusukuma jiwe lisilon'goka? Kijana akamjibu shetani kuwa Mungu kaniambia nisukume. Basi shetani akamwambia kijana usifanye kazi isiyokuwa na matunda achana na wazo la Mungu. Lakini kijana hakuacha kusukuma. Siku ingine akamwendea Mungu akamwambia , Mungu jiwe uliloniambia nilisukume haling'oki wala sentimeta moja halijasogea. Mungu akamwambia kijana , Mimi sikukuambia ulisogeze nilisema ulisukume (push). Lakini sasa naona umesukuma vya kutosha , angalia mikono yakoa na miguu. Kijana alikuwa kajazia mikono na miguu kama bondia. Basi Mungu akamwambia kijana sasa nenda kachape kazi yako maana una nguvu , utalima na kupata chakula na pia ziada utauza na kununua mahitaji mengine.

Inabidi tuelewe Mungu anajibu vipi Sala zetu.
 
As the political spectrum of Tanzania unfolds, a seemingly instability amongst CCM elite and leadership, a confusion of strategies within Chadema and never ending non resolved UFISADI chaos, I still stand tall to declare, Thank God for giving us Kikwete.

If it was not for him, whatever is taking place in Tanzania at this minute and publicly would never had been witnessed or heard, there would have been drastic efforts to silence the open divisions within CCM, a continuous non action from government due to assumption that the mass are not informed.

With Kikwete and his weaknesses, we are seeing the true colors of our leaders, we see who is right for us Wananchi and who is not fit to be trusted to continue to lead.

The nakedness of CCM and its ils would not have ever surfaced in a cristal clear shape had it been "Mzee Ben" time as Mwenyekiti!

We may not like what we see, but I am glad we have front row seat to witness a transition time where perhaps minds to Watanzania will change and stop the traditional habit of giving power to same people who have failed us!
 
Tumshukuru Mungu kwa kuweza kutufumbua macho Watanzania kuwajua viongozi wetu na udhaifu wao!

Wnegi wenu bado mnafikiri hili ni tukuzo, rudieni kusoma tena.

Tushukuru Mungu kuwa Kikwete amekaa madarakani na uozo wa Uongozi wa Tanzania unaonekana wazi na kwa uchi wa mnyama!

Ujuha na Upunguani wao na vikao vyao vya siri vinaonekana katika kazi na maamuzi yao!
 
Mungu anapanga kila kitu na ana makusudi yake.Alimuweka JK kuwa Rais kwa makusudi kabisa sasa tuyasubiri hayo makusudi.Kuna kitu anataka kutuonesha.BWANA ASIFIWE

Makusidi gani? Wala Mungu hajamweka Kikwete madarakani. Kwa nini usiseme shetani katuingilia na majaribu yake yamefikia kiwango cha juu? Tumuombe basi Mungu atunusuru na majaribu haya mabaya .

Kila azaliwapo malaika mmoja huzaliwa mashtani 1000 wa kupamabana nae. Hata wale wachungaji, Mapdre na Masheikh waliotuambia Jk ni chaguo la Mungu walishapigwa kipapai cha shetani.
 
Makusidi gani? Wala Mungu hajamweka Kikwete madarakani. Kwa nini usiseme shetani katuingilia na majaribu yake yamefikia kiwango cha juu? Tumuombe basi Mungu atunusuru na majaribu haya mabaya .

Kila azaliwapo malaika mmoja huzaliwa mashtani 1000 wa kupamabana nae. Hata wale wachungaji, Mapdre na Masheikh waliotuambia Jk ni chaguo la Mungu walishapigwa kipapai cha shetani.


..una maana maafa yanakuja?
 
Mungu anapanga kila kitu na ana makusudi yake. Alimuweka JK kuwa Rais kwa makusudi kabisa sasa tuyasubiri hayo makusudi. Kuna kitu anataka kutuonesha. BWANA ASIFIWE



Makusidi gani? Wala Mungu hajamweka Kikwete madarakani. Kwa nini usiseme shetani katuingilia na majaribu yake yamefikia kiwango cha juu? Tumuombe basi Mungu atunusuru na majaribu haya mabaya.

Kila azaliwapo malaika mmoja huzaliwa mashtani 1000 wa kupamabana nae. Hata wale wachungaji, Mapdre na Masheikh waliotuambia Jk ni chaguo la Mungu walishapigwa kipapai cha shetani.



Mfamaji, kinachoandikwa na Rev. Kishoka huwa unakiruka ama? Eti Mungu afanye nini...?!




.
 
Naam Mchungaji umenena!Hata msahafu wa Kikristu unakubaliana na wewe kwa asilimia 100. Hivi ndivyo usemavyo katika kitabu cha Nabii Danieli Sura ya 2 aya ya 21 na 22: " Na lihimidiwe jina la Mungu milele na milele; kwa kuwa hekima na uweza ni wake. Yeye hubadili majira na nyakati; huuzulu wafalme na kuwamilikisha wafalme". Pia msahafu huo unasema hivi katika kitabu cha Mtume Paulo kwa Warumi Sura ya 13 aya ya 1: "hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo imeamriwa na Mungu".

Kumbe kweli wachungaji hamkukosea mliposema Muungwana ni chaguo la Mungu. Yeye Mungu ndio kamweka na yeye ndiyo atakayeridhia ajitoe, atolewe au atoke. Ila mhh nasikia wanasiasa nao wanasema kuwa 'sauti ya watu ni sauti ya Mungu'!Watu walisema nini 2005? Wanasema nini leo? Na watasema nini 2010?
 
JK amemaliza kujenga msingi wa utundaji wa kazi na sasa anaanza kujenga barabara zake kwa urefu wa kms 2300 nchi nzima...nchi sasa inakopesheka...mnataka mabadiliko ya miujiza jambo ambalo ni gumu
 
Mkapa alijisifu sana kutuingiza HIPC! nadhani approach ya jk kututoa HIPC ni hatua muhimu sana. Nchi haiwezi jengwa na Grants tunahitaji Loans tena tujichagulie sio tusukumwe na njaa zetu. Nasema kuwa nakiongozi mwenye ufahamu wa uchumi ni jambo la msingi sana, Bigup jk. Ukweli uchumi hauwezi kuwa kama boga.
 
Ni karibu miaka miwili sasa tangu nitoe "Ushuhuda" huu... na bado naamini nilikuwa sahihi!
 
Tumshukuru pia kwa kutupa
1. JK Nyerere-kwa ujamaa wake na ubaguzi aliokufa nao
2. AH Mwinyi-kwa upole wake na utandawazi wake
3. BW Mkapa-Kwa Ujeuri, kiburi, na ufisadi wake...ndio aliyelianzisha chukua haraka...
4. JM Kikwete-Kwa Upole, Usafiri, Uwoga wake...anaendeleza libenenge
5. Whoever...for good leadership

Tutashukuru kila siku
 
Raisi wangu mpendwa aliyechaguliwa kwa wingi wa kura za kufananishwa na dhoruba la Tsunami hatendewi haki hata kidogo.

Uchumi umeyumba dunia nzima lawama anapewa Kikwete.

Liyumba amekula hela, kafikisha mahakamani anasingiziwa Kikwete kuwa ndio anamshikilia.

Babu Seya kawala witi wa watoto, kahukumiwa kwa mujibu wa sheria halali za nchi hii zilizotungwa na Bunge letu tukufu na kupitishwa na Rais Mkapa mwaka 1998 lakini lawama zinamfikia Kikwete kuwa ndiye aliyemfunga.

Mzee wa vijisenti kapiga dili chafu la rada, hajafikishwa mahakamani wala nini, Kikwete anasemwa eti yeye ndiye ngao.

Jeetu Patel amekula kila senti ya EPA, kafikishwa mahamani na kuachiwa kesho yake..wanasema kaka yangu Mkwere amemuachia.

Wajameni:
Naomba muache kumsakama Raisi wangu JAKAYA MRISHO KIKWETE
 
Back
Top Bottom