Mchungaji soma alama za nyakati,Huyu JK una hisa naye ama? Unadhani kuwa yeye ndiye anayekuruhusu kusema haya? Naomba ujue wakati wa bwana umefika, jiulize mbona hapo mwanzo haikuwa hivyo? Mungu wetu kaona atutoe utumwani, si kikwete wala yeyote yule
Kwani ni Mungu "alitupa" Kikwete? Kumshukuru Mungu kwa kufanya kitu ambacho labda hakukifanya haiwezi kuwa kumdhihaki? Wewe Carmalenge ambaye unatangazia dunia "Habeamus Papam" unaamini kweli Mungu angetupa Kikwete? Kwani tumemkosea nini?
Mungu alijua, kabla ya wakati, kwamba JK agekuwa Rais wetu. Alijua hivyo hata kabla baba yake JK hajazaliwa. Lakini unataka kusema ni yeye alichora dili la kuchukua fedha BoT kwa ajili ya takrima za kumfanya JK akubalike? Hapana, Mungu hakutupa JK. Tumejitwalia huyu ndugu wenyewe baada ya kunogewa na takrima.
Kilichobaki ni kumwomba Mungu aendelee kumpa JK ujasiri wa kuruhusu mafisadi wafichuliwe. Ampe hata nguvu ya kuwavaa Mkapa, Yona na Rostam Aziz. Akiwavaa hao basi hata mimi nitaanza kudhani labda ni Mungu ametupa huyu mwenzetu.