Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,406
- 31,387
Nakubaliana nawe 100%. Nakumbuka JK alipotanganza ile Dec kuanza kwa mchakato wa katiba, Wapinzani walimpongeza kwa hatua hiyo. Lile lilikuwa kosa na tuliwatahadharishaKushindikana kuandikwa kwa katiba mpya baada ya kazi za muda mrefu sana iliyofanywa na Tume wa Warioba lilikuwa ni pigo kubwa sana kwa nchi.
Hali hiyo ilitokana na katiba hiyohiyo inayompa rais madaraka ya kuamua lolote, na ndiyo aliyotumia Kikwete kuunda tume hiyo, halafu akayatumia pia kuua muendelezo huo wa kuandikwa kwa katiba mpya.
Swala la kurekebishwa kwa Katiba mpya lilitakiwa lianzie bungeni kusudi liwe na nguvu ya kisheria, siyo kuwa ni utashi wa rais tu.
1. Tuliwaambia ili mchakato ufanikiwe ni lazima uondoke katika mikono ya CCM ambao hawakutaka suala hilo
Niliwaeleza hapa jamvini, hoja ilitakiwa kwenda Bungeni ili ipate uhalali tu wa kisheria na si vinginevyo
Kisha, ilitakiwa mchakato mzima utazamwe na mkutano wa kitaifa ili kuondoa uCCM
Katika hilo Bunge la Katiba lisingehusu CCM kama ilivyokuwa kwa katiba ya 1977 n.k.
2. Kwasababu namba 1 haukizingatiwa, CCM wakatumia nguvu yao kisiasa na si kiuzalendo na nchi kuupiga ngwara mchakato mzima. Na Rais alitishwa na CCM na kwavile alikuwa na nguvu akanywea
Kuharibika kwa mchakato wa katiba kwa sehemu kubwa sana kulichangiwa na Wapinzani kutoelewa mchezo wa siasa za CCM na kuamini kuwa CCM ni Wazalendo wanaoweza kufanya nao kazi, siyo!