Abou Saydou
JF-Expert Member
- Dec 1, 2014
- 2,948
- 2,112
Mkuu, miaka ya nyuma NECTA walijuwa hawana grade za marks, mfano sasahivi inajulika kama ifuatavyo
A - 75 -100
B - 74 - 55
C - 54 - 45
Nk
Zamani hii ilikuwa inabadilika sana kutokana na ufaulu & nafasi za kujiunga na elimu ya A-level.
Hasa walikuwa wanalenga nafasi wala sio ufaulu, unakuta wanasema mwaka huu tunanafasi 1000 za kujiunga A-level, kwaiyo kama watu wamefaulu sana watajaribu ku-change grade za ufaulu inaweza kuwa labda
A - 95-100
B- 94-85
C- 84-50
Nk
Hapo watakuwa wamepata hizo nafasi 1000.
Grade zilizokuwa zinatumika mashuleni sio sawa na zile za necta, hata walimu walikuwa hawana uhakika
Pia watu wakifeli sana wana shusha sana hadi utakuta labda A 70 -100.
Lakini sasahivi Grade zinajulikana kabisa hazibadilishwi mara kwa mara. Maana shule ni nyingi sana.
Pia madogo wa sasa wana akili sana
Sent using Jamii Forums mobile app
Unataka tubishane?Siwezi kuamini kwa asilimia 60 ulichoandika, maana kipindi cha 2000yr kurudu nyuma idadi ya shule ilikuwa ya wastani na hakukuwa na shida ya shule, nakumbuka wazazi wengi 1998 walianza kuwatoa watoto uganda kuwapeleka shule za hapa TZ.
Kuhusu nyenzo sijui unazungumzi kipindi gani but nyenzo ni zile zile ila kuna urekebishwaji kwenye matumizi ili kuleta ufanisi.
kumbuka kwenye mtihani hakuna mahabara.
Uwepo wa shule 2000s kurudi nyuma na miaka ya 2005s kuja 2020 wapi kulikua n shule za kutosheleza?
Sio tu za kutosheleza zenye vifaa bora vya kisasa.
Binafsi nilikua mtegaji mzuri shuleni na ningesoma 1998 huko nisingepata hata cheti, ila niliweza kutoboa kwasababu nyenzo zote nazipata hata nisipoenda shule.