Thamani ya daraja la kwanza pointi 7(division 1.7) miaka ya leo

Thamani ya daraja la kwanza pointi 7(division 1.7) miaka ya leo

Mimi nadhani tatizo kuu ni lugha ya kufundishia. Waswahili wanasema mtoto umelavyo ndivyo akuavyo, sasa ngoja nitoe mfano: mtu kazaliwa toka akiwa mdogo anazungumza kiswahili kisha anaanza shule za primary kwa kiswahili, halafu anaenda sekondari kwa kiingereza hapo ndipo majanga yanaanza maana unakuwa unapambana kuelewa kiingereza na kupambana kuelewa somo husika. Baada ya hapo kwa hofu ya kufeli au kuitwa kilaza au kuitwa una akili ndogo sana unaaza kukariri madude na kumeza madude ili ufaulu, mtihani ukija unakuwa unajifaulia vizuri huku unasolve pastpaper na possible za hapa na pale pamoja na solving.

Maana yake hapo unakuwa mtu unayeonekana kwa nje kwamba ni msomi ila kwa.ndani wewe ni chenga tu. Kwa hiyo umekuzwa kukariri ili ufaulu mtihani, kama Mungu akikujalia ukasoma nje hautaweza kubadilika maana toka utoto wako mpaka ujana wako wewe ni mtu wa kukariri, kwa hiyo ukienda kusoma nje maana yake umeenda huko ulaya kumeza madude na kweli utaonekana uko vizuri sana ila kichwani ni empty.


Sasa tatizo linaanza kwenye utekelezaji wa kwa vitendo kwa kile ulichokisoma unakuja kugundua kumbe ulikuwa unameza ufaulu mtihani na maisha halisi sio necta wala vyeti. Ndio maana Tanzania unakuta mtu ni msomi kweli kweli ila ni full chenga (mimiii nikiwemo).
Kwa kuwa shida ni kukariri. Mfano hai ni Mjerumani kajenga reli ya Tanga arusha mwaka 1898, kajenga reli toka Dar mpaka Kigoma ikafika mwaka 1914 na hakutumia kiingereza bali alisoma kwa lugha yake ya asili ya kijerumani na akajenga reli mpaka leo tunaitumia.
Nimefanya field kwa wachina mara kadhaa wao wamesoma kwao kwa kichina tena wengi wao wamesoma wakiwa gerezani ila ndio wanaotujengea barabara,majengo, miradi ya maji na madaraja. Na wanatengeneza vifaa vya ujenzi kwenye nchi yao huku wakilonga kichina tu mwanzo mwisho.
Muda umefika sasa sio kulaumu wasomi wetu wala wanasiasa maana wote ni matunda ya mfumo wa kukariri. Inabidi tufumue elimu ya Tanzania tusome kwa kiswahili na wale wanasoma nje waje nchini kutafsiri walichosoma kwa kiswahili ili kizazi kijacho kisipate mateso tunayopitia kukariri.
Nchi nyingi zilizoendelea duniani husoma kwa lugha zao za asili kuanzia chini mpaka PHD lugha ni kwa ajili ya mawasiliano tu.

NB: Wapo magenious wachache wenye kipaji toka kwa Mungu ambao wamesoma elimu ya Tanzania na wanaweza kufanya kwa ufanisi mzuri kile walichosomea.




Ukiona vyaelea ujue vimeundwa.
Zambia,Kenya,uganda wanasoma kingereza tangu msingi mbona hawana lolote la maana.Tatizo letu sisi sio lugha tu hata mfumo mzima,utamaduni
 
Zambia,Kenya,uganda wanasoma kingereza tangu msingi mbona hawana lolote la maana.Tatizo letu sisi sio lugha tu hata mfumo mzima,utamaduni
Kenya, Uganda na Zambia wanatumia kiingereza ila kiingereza sio lugha zao za asili kwa hiyo na wao wako kwenye mkumbo wa kukariri kwa hiyo lazima wawe weupe kichwani.

Nchi nyingi zilizoendelea duniani wanatumia lugha zao za asili kuanzia ngazi za chini mpaka vyuoni.
 
Katika matokeo ya form 4 2019/2020 sote tumeona Saint Francs watoto 57 wamepata div. Point 7 kati ya wanafunzi 91. Ni jambo jema kuona jinsi vijana wanavyosema kwa bidii na kufanikiwa kufaulu vizuri.

Miaka ya nyuma kidogo ilikuwa nadra sana kwa mwanafunzi kupata div ya saba,na ikitokea ingeweza kujirudia baada ya miaka kadhaa.

Siku hizi si ajabu kwa wanafunzi kupata ufaulu wa div. One pointi 7 kwa zaidi ya nusu ya darasa hasa kwa shule za Mission.

Watu wengi wanahoji je ufaulu huu umetokana na ufundishaji mzuri Au mitihani imelegezwa?

Je, ufaulu huu unaendana na uwezo binafsi wa wanafunzi au wanakaririshwa tu?

Nini thamani ya ufaulu huu ukilinganisha na miaka ya nyuma?
Wote sawa tu hakuna tofauti. Walio soma zamani wameharibu vibaya sana sura ya nchi na maisha ya watanzania. Wasomi wenyewe wakina nani? Wakina Lowasa, Membe au Kikwete? Sahau! Msomi ni mmoja tu katika hii nchi. Rais Magufuli.

Magufuli anatuonyesha sisi wote mafalah jinsi gani mtu anavyo takiwa kuitumia elimu yake kisawasawa kwa maendeleo ya wananchi wote. Sisi wengine wote ni makasuku tu. Watu tulio kariri namba za kiarabu na Symbols za kigiriki, nothing else.

Wengine ndiyo wanajifanya waingereza babu kubwa kama akina Lissu. Wakafie mbali uko! Kiingereza chenyewe hawajui kujidai tu.
Kujua kiingereza sio ndiyo utaalam. Kiingereza ni lugha tu kama lugha yeyote ile nyingine.

Mtu ana jisifu kuwa yeye ni mbobeaji wa sheria wakati anafanya makosa ya kipuuzi namna hiyo, mpaka yana mcost Ubunge wake. Jamaa Falah sana. Watu kama hawa ndiyo tuwape nchi kweli? No way!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom