TFF na TAKUKURU Washughulikie Malalamiko ya Simba

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,578
19,463
Kuna video nyingi sana zinasamaa zikiwaonyesha wafuasi wa Simba wakiilalamikia kampuni ya GSM kushirikiana na timu nyingine za ligi kuu kupanga matokeo ya kuipendelea Yanga. Kama malalamiko hayo ni kweli basi kuna uvunjaji wa sheria za nchi zinazozuia rushwa; hivyo TAKUKURU inatakiwa ilifanyia kazi jambo hilo.

Vile vile kupanga matoke kwenye michezo ni kosa linapigwa vita sana na vyombo vyote vinavyosimamia michezo duniani. Watu kulalamika kuwa Ligi kuu ya Tanzania inaruhusu watu kupanga matokeo ya mpira wa miguu. Malalamiko hayo yanaishushia hadhi ligi yetu ambayo miaka ya vivi karibuyni imekuwa ikipanda ngazi kwa kasi sana Afrika.

Nashauri watu wote wanatoa lawama hizo watafutwe na vyombo husika hivyo watakiwe watoe ushahidi kusudi culprits wakamatwe ili kutunza hadhi ya ligi yettu. Na wakishindwa kutoa ushahdi basi washtakiwe kwa defamation na kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria.
 
Hoja dhaifu kweli! Simba alifungwa 05 na Yanga msimu huu, je kuna kupanga matokeo hapo! Ifike pahala mtambue jitihada zinazofanywa na Uongozi plus wachezaji.

Ni dhahiri kwamba Yanga imeimarika mno! Msisahau kwa haraka, ni Yanga hii iliyomfunga mwarabu goli 4 na kufuzu robo fainali! Ni Yanga hii iliyocheza fainali Shirikisho. Ifike mahali muanze kuiheshimu Yanga please.
 
Waanze na ile mechi simba alikula kono la nyani maana haiwezekani wachezaji na mo waliuza mechi ile.
Mpira ni mchezo wa wazi wazi. Simba wameshindwa kupata ushindi uwanjani, wanatafuta ushindi wa kuchafua biashara zinazodhamini mpira na kuchafua ligi yetu.

Watakiwe watoe ushahidi wa kuthibitisha madai yao na wakishindwa basi waadhibiwe kwa mujibu wa sheria. Tuhuma wanazotoa haziwasaidii Simba au kuwakomoa Yanga ila zinaichafua ligi kuu ya Tanzania na Tanzania yenyewe
 
Hoja dhaifu kweli! Simba alifungwa 05 na Yanga msimu huu, je kuna kupanga matokeo hapo! Ifike pahala mtambue jitihada zinazofanywa na Uongozi plus wachezaji. Ni dhahiri kwamba Yanga imeimarika mno! Msisahau kwa haraka, ni Yanga hii iliyomfunga mwarabu goli 4 na kufuzu robo fainali! Ni Yanga hii iliyocheza fainali Shirikisho. Ifike mahali muanze kuiheshimu Yanga please.
Wafa maji hao utawaweza mkuu , ni haki yao kutapatapa
 
Siku ukimsikia kiongozi wa Simba amesema lolote basi hivyo vyombo vitachukua maamuzi ila kama ni mashabiki wachukuliwe nani waachwe nani?

Hizo kauli ni za mashabiki na wote sio Yanga si Simba kwa nyakati tofauti huwa wanaongea kile wanachoona kinafaa.

Hapa ungesema mashabiki wapewe elimu kuwa kuongea vibaya juu ya ligi yetu hatukomoani wenyewe kwa wenyewe bali tunacchafua taswira ya nchi.

Ila kama hivyo vitendo vinafanywa wachunguze wao kama wao then vikomeshwe...
 
Siku ukimsikia kiongozi wa Simba amesema lolote basi hivyo vyombo vitachukua maamuzi ila kama ni mashabiki wachukuliwe nani waachwe nani? Hizo kauli ni za mashabiki na wote sio Yanga si Simba kwa nyakati tofauti huwa wanaongea kile wanachoona kinafaa...
Hapa ungesema mashabiki wapewe elimu kuwa kuongea vibaya juu ya ligi yetu hatukomoani wenyewe kwa wenyewe bali tunacchafua taswira ya nchi..
Ila kama hivyo vitendo vinafanywa wachunguze wao kama wao then vikomeshwe...
Ni wewe au kuna mtu umempa simu?
 
Back
Top Bottom