Kwa nini Yanga inakuwa na wachezaji wanaoamini sana ulozi?

man dunga

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
3,216
5,566
Ukiachana na ile ya kuchoma moto kule Afrika kusini ambao ulikuwa ni upuuzi lakini sijawahi kuona wachezaji wa Simba wakitoa taulo au kufukua kwenye lango la mpinzani hata waattempt mara 30 bila goli.

Kwa Yanga imekuwa kawaida sana kuwa na wachezaji wanaoamini ulozi wazi wazi. Kipindi cha nyuma alikuwepo Kaseke ,huyu alikuwa anatoa na kufukua langoni kwa mpinzani akiona wanashambulia halafu hawapati goli. Sasa hivi wameibuka hawa akina Mzize na Kibwana Shomari wanaamini magoli hayaingii sababu ya uchawi ulio kwenye taulo la kipa.

Vijana wajue tu kuna maisha nje ya yanga na hakuna timu ya maana itakusajili kama unaamini hup upuuzi badala ya kujibidisha.
 
Ukiachana na ile ya kuchoma moto kule Afrika kusini ambao ulikuwa ni upuuzi lakini sijawahi kuona wachezaji wa Simba wakitoa taulo au kufukua kwenye lango la mpinzani hata waattempt mara 30 bila goli.
Mkuu yan unamaanisha kwakua Simba hawafanyi jambo fulani basi haitakiwi na mwingine afanye. Imeprove mara mbili baada ya kutoa mataulo golini na magoli yanaingia.

Kama nyie mmeshaupata ushindi nje ya uwanja wacha sisi tuutafute kwa jasho halali. Nyie mnaumia nini
 
Back
Top Bottom