TFF: Dhana dhanifu ama halisi?

TFF: Dhana dhanifu ama halisi?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,869
Reaction score
828,380
Ilianza kama utani mitandaoni lakini ni wazi ni kitu kinachojijenga katika uhalisia wake
TFF (Tanganyika Freedom Fighters) Wapigania Uhuru Tanganyika (WAUTA)
Mwansilishi halisi hajulikani mpaka sasa lakini ni wazi ni kundi lenye vinasaba vyote na Gen-Z hasa baada ya yote yaliyotokea 0ctober 29 mpaka Nov 3 na mwendelezo wake
Ni kundi lenye lengo la kuikomboa Tanganyika toka mikononi mwa ccm (kundi la wachache) kupitia njia mbadala badala ya kwenye sanduku la kura kushindikana
Ni kundi linalozidi kujizolea umaarufu lakini lisilo na anuani rasmi mpaka sasa.. Na hata idadi ya wanachama haijulikani

Baadhi wanaliita ni kundi la waasi lakini hilo jina linazidi kukosa nguvu huku kundi la ukombozi likizidi kupata nguvu
Ukifuatilia mitandaoni ni kundi lenye uasisi chini ya Kapteni Tesha anayesemekana yuko hai, yuko salama nje ya Tanganyika, akiwa na support ya wanajeshi kadhaa walioasi jeshi na kwenda kuungana naye kuunda TFF
Inasemekana pia lina support kubwa ndani ya jeshi na ndani ya vyombo vingine vya usalama ambao hawakubaliani na yaliyotokea kwenye uchaguzi mkuu na yanayoendelea kutokea

Ukiacha hao kuna kundi kubwa la vijana wenye mwelekeo wa kulikubali kundi hilo kwa asilimia 100

Je ukweli wa TFF ni upi? Ni halisi au ni dhanifu?

Waswaheli wanasema lisemwalo lipo kama halipo linakuja!
Tuupe muda wakati
downloadfile-2.jpg
 
sipendi yanayotendeka nchi hii, ila zaidi sitaki kuona hili taifa linakua uwanja wa vita, maana athali hazitawapata hao mafisadi bali sisi wananchi wa kima cha chini, wakati huo wao watakua wameshakimbilia oman,

Djs tunaomba utusindikize na ule wimbo uliyoimbwa na wamakonde wawili,
"bora ugali dagaa kwenye amani,kuliko wali nyama vitani".
 
MKuu sjui kama watakuelewa, wahamasishaji ni watu tofauti na wahanga, watu wasipochanganya na za kwao , ndo basi aisee
 
Bahati mbaya watakaoyapata maumivu halisi ya vita wengi ni wananchi wa kawaida wasio na pesa wasio na ulinzi wowote. Kwa hali hiyo waitakayo ndipo wabongo wataanza kulia wakikumbuka old days of peace.
Mungu tuepushie mbali hili janga.
 
Mshana, huwa najiuliza hii haiba ya wewe kuelezea vitu hivi bila woga na identify yako inajulikana, huwa hauna wasiwasi? Ni mambo very complex haya, Mimi hata kuyasikia sometimes nayakwwpa
 
Mshana, huwa najiuliza hii haiba ya wewe kuelezea vitu hivi bila woga na identify yako inajulikana, huwa hauna wasiwasi? Ni mambo very complex haya, Mimi hata kuyasikia sometimes nayakwwpa
Nimeleta kama hoja jadilifu kutokana na yale yanayoendelea mitandaoni. Nmekuwa mwangalifu mno wa kuchagua maneno ya kuandika illi kuepuka kufikiriwa vinginevyo
Ni aina ya mada ambayo inaweza kuamsha mjadala wenye tija utakaolisaidiq taifa kutoingizwa kwenye machafuko
 
Bahati mbaya watakaoyapata maumivu halisi ya vita wengi ni wananchi wa kawaida wasio na pesa wasio na ulinzi wowote. Kwa hali hiyo waitakayo ndipo wabongo wataanza kulia wakikumbuka old days of peace.
Mungu tuepushie mbali hili janga.
Kumbuka hata walioathirika pakubwa na vibaya kabisa October 29 mpaka Nov3 si wengine ni haohao!
 
Nimeleta kama hoja jadilifu kutokana na yale yanayoendelea mitandaoni. Nmekuwa mwangalifu mno wa kuchagua maneno ya kuandika illi kuepuka kufikiriwa vinginevyo
Ni aina ya mada ambayo inaweza kuamsha mjadala wenye tija utakaolisaidiq taifa kutoingizwa kwenye machafuko

Ni sahihi kabisa, mara zote huwa mwangalifu kuwa neutral, however nashauri kidogo uongeze umakini kuleta Hoja kama hizi kabla hazijawa public agenda, delay kidogo, nakuwa mwoga tu, sio vingine!
 
Back
Top Bottom