Tetesi za yanayojiri kwenye Vikao vya CCM Dodoma

Status
Not open for further replies.
Mambo ni sivyo-ndivyo. Vikao vinapangwa na kupanguliwa. Makada wanakuja na kuondoka. Mikwara ya kihawara na hela inatawala. Kambi zimewekwa na uadui unatamalaki. Vikao vimeshaanza lakini Wajumbe wameshachimbwa mikwara hadi wamepoteza misimamo yao. Ingawa najua chama hakitishiki na mikwara inayotemwa, najua taswira ya chama inasawajishwa. Chama kinaonekana ni chama cha ubabe na shibe badala ya hoja za haja.

Narudi Dar es Salaam nilikotoka. Hapa mchezo siusomi. Yaani huyu naniliu naye ana uhakika wa kupita na kusikika kweli?!? Pamoja na vihoja na maigizo yake yote bado anatamba kuwa yeye ndiye mwamba. Mambo yamenishinda.Kimbelembele changu kimenifikisha hapa. Ningejua,ningebaki Dar es Salaam na kufuatilia kupitia luninga na redio kama wenzangu.

Viongozi wangu wa CCM, nawatakieni kila la kheri katika vikao vyenu vya leo na kesho. Mchagueni yeyote tu. Hata huyu msanii ambaye ameamua kutumia falsafa ya tishatisha. Sisi tunayemtaka tukimkosa, tutafanya jambo hata kama ni kimya kimya. Mbaki salama!

Mzee Tupatupa (kwasasa Dodoma)
 
Kuenguliwa kwetu sisi ambao siyo wanaccm na ni team lowasa tunatafsiri ni kukatwa kwa Laigwanani wetu. Patachimbika tu hakuna namna nyingine.
 
achani unafiki wenu, mama yetu kila mkutano mkuu wa CCM huwa anaalikwa!!! hata UKAWA tutamwalika ili aje kushuhudia rais mpya wa Tanzania 2015 na OLE wenu mumkataze kuja!!
 
kuna taarifa kuwa huyu mama yuko dodoma,je kaja kumsaidia mwanae kwenye kampeni? mwanae akishindwa atajisikiaje au atamuonaje jk? anahisi ni chama cha mumewe au cha watanzania? mbona mke wa mwinyi na mkapa hawapo dodoma? kunani?
Wakeze mwinyi wawili Sitti na Khadija wapo Dodoma,Wakeze Bilali wawili wapo Dodoma,Wakeze balozi seif Idd wawili wapo Dodoma nk,sio mama Maria tu wengi wapo hapa Dodoma.
 
kuna taarifa kuwa huyu mama yuko dodoma,je kaja kumsaidia mwanae kwenye kampeni? mwanae akishindwa atajisikiaje au atamuonaje jk? anahisi ni chama cha mumewe au cha watanzania? mbona mke wa mwinyi na mkapa hawapo dodoma? kunani?

Wewe ni team lowassa? mnakazi this time kelele zooote zitaisha leo
 
Mambo ni sivyo-ndivyo. Vikao vinapangwa na kupanguliwa. Makada wanakuja na kuondoka. Mikwara ya kihawara na hela inatawala. Kambi zimewekwa na uadui unatamalaki. Vikao vimeshaanza lakini Wajumbe wameshachimbwa mikwara hadi wamepoteza misimamo yao. Ingawa najua chama hakitishiki na mikwara inayotemwa, najua taswira ya chama inasawajishwa. Chama kinaonekana ni chama cha ubabe na shibe badala ya hoja za haja.

Narudi Dar es Salaam nilikotoka. Hapa mchezo siusomi. Yaani huyu naniliu naye ana uhakika wa kupita na kusikika kweli?!? Pamoja na vihoja na maigizo yake yote bado anatamba kuwa yeye ndiye mwamba. Mambo yamenishinda.Kimbelembele changu kimenifikisha hapa. Ningejua,ningebaki Dar es Salaam na kufuatilia kupitia luninga na redio kama wenzangu.

Viongozi wangu wa CCM,nawatakieni kila la kheri katika vikao vyenu vya leo na kesho. Mchagueni yeyote tu. Hata huyu msanii ambaye ameamua kutumia falsafa ya tishatisha.Sisi tunayemtaka tukimkosa, tutafanya jambo hata kama ni kimya kimya. Mbaki salama!

Mzee Tupatupa (kwasasa Dodoma)

Duuuuh! Kazi ipo boss
Kama nakuona umeshika tama hapo kwenye kona! Maana unachotaman kiwe hakiwi ila wanachotaka kiwe ndo hicho
 
CCM wanatangatanga kwasababu wanamgwaya Laigwanan
 
Ufalme uliofitinika....mtakoma na lichama lenu lililozeeka
 
Mkuu mwanzo naona walikuwa na uamuzi tayari lakini baada ya kufika site na kuona vitisho na ubabe ule uamuzi wao mgumu umeyeyuka kama samli kwenye jua.. Jina limeshatoka kwenye chupa.. Inawezekana leo ndo ukawa mwanzo wa mwisho wa chama tawala..

Yaliyotokea 2005 ndo haya yanayotokea leo..
 
Jmosi nitakuwa Tanga Hotel Nyumbani kuna live band kwa pembeni karibu.

Ngongo; tano bora; 1. Mwandosya 2. Ramadhani 3. Billali 4. Pinda 5. Migiro
tatu bora; 1. Mwandosya 2. Ramadhani 4. Migiro
Raisi + Makamu; 1.Ramadhani 2. oMwandosya
Waziri mkuu; Migiro

NB; Karibu Raskazone jpili jioni unizawadie ka - guiness
 
haya hapa chini ni maneno yake mwenyewe...ulitegemea kipenga na kadi alivyopoteza refa vitoke wapi?

Mpambano unaendelea. Katikati ya mchezo,refa anagundua kuwa amepoteza kadi-ya njano na nyekundu pamoja na filimbi. Kutokana na kasi ya mchezo, anauchuna. Haisikiki filimbi wala haionekani kadi hata pale inapohitajika.

Wachezaji wanakatana mitama ya kiama lakini kimya. Wachezaji wanatukana na vikumbo kupigana lakini kimya. Mpira unatoka na kurushwa tena bila filimbi kupigwa.

Wachafu wanacheza rafu na wasafi wanachafuliwa. Wachezaji wanatamba kila namba na kujigamba. Refarii yuko kimya huku akionekana dhahiri shahiri kuwa kasi ya mchezo inamshida.

Anajikaza kisabuni tu. Anaendelea kukimbia hapa na pale akiomba tu mchezo uishe salama. Itasikika filimbi gani goli likifungwa? Atasemaje kuwa ni goli halali au haramu? Mpambano hauna mfano.

Refarii anafanya siri. Hasemi ukweli kama amepoteza filimbi na kadi. Anakufa na tai yake shingoni. Hata mchezaji kibaka naye kajichanganya mpirani na anakaribia kutangazwa 'man of the match'. CCM iko njia panda!

Similar Discussions

Back
Top Bottom