Tetesi za yanayojiri kwenye Vikao vya CCM Dodoma

Tetesi za yanayojiri kwenye Vikao vya CCM Dodoma

Status
Not open for further replies.
××××SIJAWAHI KUTABIRI NIKAKOSEA×××××
Toka mwaka 1995 sasa huu ni utabiri wangu binafsi.
Utabiri ni makisirio yna kabla yanayojumlisha mambo
mengi(huwa ni close to actual or equivalence). UTABIRI
ni kuwa majina matano ya CC yatapita na wengi
wataondolewa kwa vigezo vi3 ukiacha ushauri wa
baraza la wazeee 1. Kutokuwa na ujuzi wa uongozi
ndani ya chama 2. Kutokuaminika kwa waliowahi kuasi
chama wakahama na kurudi tena 3. Kutokuwa na ujuzi
wa Uongozi na ujuzi wa serikali ya Jamhuri. Watano ni
hawa
1. Lowasa
2. Dr. Bilali
3. Pinda.
4. Membe
5. Asharose
Na kutoka NEC, kwa kuwa NEC ina wajumbe 401 basi
majibu yatakuwa hivi;
1. Lowasa 211
2. Membe 78
3. Pinda 45
4. Asharose 38
5. Bilali 22
Kura 7 zitaharibika.
Mkutano mkuu yataenda majina ma3 Lowasa, Membe
na Pinda na wajumbe wa mkutano mkuu wapo 2600
matokeo yatakua kama ifuatavyo;
1. Lowasa 1678
2. Membe 655
3 Pinda 240
Kura 17 zitaharibika
Lowasa atashinda kwa kishindo(zaidi ya 60%) na
Mgombea mwenza atakua ni Bilali kubalance Muungano,
Pia mamlaka itamtaka ampe Membe uwaziri mkuu
# makubaliano kubalance team# hivyo Membe ataenda
kugombea ubunge hata kama alishaaga.
Narudia: Safari ya Matumaini siipendi ila kwa Busara ya
haraka hakuna Jinsi tunaipenda CCM yetu, wana CCM
tupo mil 6 wapiga kura ni mil 24. # Utabiri Binafsi#
By Banyamulenge Mkwawa.
 
Kura bado NEC tusubiri.Hata hivyo Mwigulu ni opportunist.Hii imejidhihirisha kupitia kwenye tabia yake ya kutokuwa vocal dhidi ya uovu,kuchukuliana na mafisadi na kubadilika badilika kulingana na mazingira ya kiutendaji.Tabia hii imemfanya adharaulike mbele ya macho ya watu makini.Ingawa kweli nimeona mabadiliko makubwa kiutendaji alipokuwa hazina.
Breaking news kutoka Dodoma....

Katika hali ya kushangaza,mwigulu nchemba ameibuka kuwa kinara kati ya watangaza nia wote wa urais...

Ubora wake umechochewa na uadilifu wake ndani ya chama na serikali,ambapo hkn mazingira yyt yanayomzungumzia mwigulu nchemba juu ya ubadhirifu ama utendaji mbovu ktk ngazi alizowahi shikilia.
Mwigulu nchemba amekua bora na wa mfano ktk kujenga hoja makini zenye kujenga taifa na chama kwa ujumla,ni mtu mwenye uthubutu,jasiri anayesimamia maamuzi yake yaliyo makini,ni mkweli,mpenda haki na mtulivu pia mwenye hekima na busara.....

Amejaribu kulinganishwa na wagombea wengine ktk nyanja mbalimbali kama
Uchapakazi,
Uzoefu ktk chama na serikali....hapo ameonekana mwiba haswaa kutokana na nyadhifa kubwa alizotumikia ndn ya chama tena kwa mda mfupi ktk hilo amejikuta akiwapiku mbali wagombea wote...

Uadilifu....bado kete ilionekana ikimwangukia yeye akipambana vikali na jaji ramadhan pmj na mama migiro...

Lingine pia uwezo binafsi wa kisiasa....bado mwigulu alizidi kukimbiza wenzake kutokana na historia yake ya ushiriki wa aina zote za siasa.....

Zaidi ya yote ajenda aliyoibeba imegusa matumaini ya wana ccm wengi kuelekea kwa wananchi ambapo imeonekanika mwigulu nchemba ameeleweka kwa watanzania wengi kwa ajenda yake hivyo ni rahisi kuuzika pasipo na shaka...

Mwigulu nchemba anatafsiriwa kama mtu pekee asiye na makundi ndani ya CCM kiasi ambapo ana uwezo wa kuwaunganisha wana ccm wote kutoka ktk makundi yao...

Kwa ufupi amevishinda vigezo vyote 13 tena kwa kishindo haswaa...

Uhakika wa jambo ulichagizwa na kijembe cha mh rais jana wkt wa hotuba yake bungeni ambapo aliwashukuru viongozi wote aliofanya nao kazi akiwemo Edward lowasa,
Mara tu baada ya kutaja jina la lowasa JK akamalizia kwa kwa kusema mpo wengi sana na wengine ni vigogo.....tusinuniane kwa watakaokatwa....

Hapa Dodoma watu hawaamini kiasi ilianza kusikika jana baadhi ya wagombea wameanza kukata tamaa kutaka kujitoa....
 
Bas sawa acha tusubir ntarud hapa jumapil jion

xxxxxxxxx take my word xxxxxxxxx
 
Confirmed top five are:
1. Ret. Gen/Judge and Pastor August Ramadhan
2. Comrade Bernard Membe
3. Dr Asha-Rose Migiro
4. Uncle Makongoro Nyerere
5. Prof Mwandosya

Mi hapo namba mbili hua pananikosha sana
 
kazi ni ngumu sana tusubiri, walishatabiri wengi sana na wote wanadhani wapo sahihi
 
nyanile

definitely mdau, mwigulu anafaa kabisa kumpokea kijiti kikwete kwa uadilifu wake na uchapakazi wake. watanzania wengi tunamuelewa mwigulu na hatuna shaka nae. Mwigulu atauzika sana kwa wananchii

kayaeleze hayo maneno NEC apa ni kelele tu
 
Last edited by a moderator:
Nenda Premier Meridian bet ukatabiri michezo mbalimbali upate hela kama unajua huwa hukosei..
 
Kwa vile ni utabiri tuu juu ya chama chenu, nami ngoja niweke ndoto yangu ya juzi.
Ni kuwa kutokana na kuvunja kwake sheria ya uchaguzi, Kamati kuu itaamua kukata jina la Edo hivyo katika majina yatakayokwenda NEC halitakuwapo na yeye habari hizo atapewa akiwa anapata Lunch pale Dodoma Hotel. Kitakachofuata ni kuwa atapata mshtuko na hali yake kudhoofika ghafla. Hapo yule daktari wake aliyekuja atashauri apelekwe Ujerumani kule kwenye clinic yake kwa uchunguzi zaidi.
Kwa vile ni kipenzi cha chama na wanachama wengi wameshanufaika naye, chama kitatoa usafiri wa ndege mpaka Dsm na mengine yatafuata. Msinihukumu mie, ni ndoto tuu nimeona niiweke hapa kama huyu "mtabiri" alivyoweka utabiri wake.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom